Enzi zile za wazazi wetu...............

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,301
Hapo zamani kabla na baada ya mwalimu na hata wakati wa mwinyi ilikuwa mtoto akizaliwa mvua inanyesha anaitwa "mwamvua" akitanguliza miguu wakati wa kuzaliwa ataitwa "sikitu" akizaliwa ijumaa ataitwa "juma au mwajuma" akizaliwa jumapili ataitwa "pili" akizaliwa jumatatu ataitwa "tatu"

Kuna kipindi kukazuka watoto kuitwa majina ya watawala wa zama husika, hii ilitawala hasa kipindi cha kuanzia mwinyi ila sina uhakika kama bado kuna watoto wanazaliwa wanapewa majina kama Slaa, Mbowe, Kikwete n.k.

Ingekuwa enzi zile za mwalimu tungeshuhudia watoto wanaozaliwa katika kipindi hiki wakiwa wanamajina kama Dowans, Mbagala, Gongo la Mboto, Al adawi, Rostam,google, JF, You tube,hi5,IPTL, Songas, Mwakyembe na kadhalika kutokana na wakati wenyewe.

Jana nimesoma news sehemu nikaona kuwa nchini Misri kuna jamaa amemwita mtoto wake wa kike "facebook" kuapriciate mchango uliofanywa na facebook kwenye maandamano yaliyopelekea HM kuangushwa. Wapashaji habari wanasema mtoto huyo amepokea zawadi kem kem kutoka kwa vijana wengi wa kimisri. Nadhani hapa kwetu katika waliozaliwa kwenye mkesha wa tukio la gongo la mboto angepewa jina la gongo la mboto si ajabu watu wangemiminia mizawadi.
 
Kaka, hayo majina ya ajabu ajabu ndi yanaharibu hata future za watoto husika. Mfano unamuita mtoto SIKITU yaani anakuwa sio kitu kweli. Unamuita mtoto GONGO LA MBOTO basi anakuwa anaandamwa na mikosi kila kukicha. Nadhani hiyo fasheni ya kizamani sijui wazazi nao walikuwa wanatoa majina kujifurahisha wao tu bila kuangalia kwa mapana hata maana ya jina lenyewe
 
Hapo zamani kabla na baada ya mwalimu na hata wakati wa mwinyi ilikuwa mtoto akizaliwa mvua inanyesha anaitwa "mwamvua" akitanguliza miguu wakati wa kuzaliwa ataitwa "sikitu" akizaliwa ijumaa ataitwa "juma au mwajuma" akizaliwa jumapili ataitwa "pili" akizaliwa jumatatu ataitwa "tatu"

Kuna kipindi kukazuka watoto kuitwa majina ya watawala wa zama husika, hii ilitawala hasa kipindi cha kuanzia mwinyi ila sina uhakika kama bado kuna watoto wanazaliwa wanapewa majina kama Slaa, Mbowe, Kikwete n.k.

.
Shosi hebu nipe ufafanuzi hapo kwenye red.kutanguliza miguu na sikitu inauhusiano gani?au inamaanisha nini.
btw,usharudi jf?maana ulikuwa unaaga na kufunga mizigo..
 
Hapa wenye majina ya kiswahili tutasemwa mpaka tuchoke...!!
Ndo maana mnasema mende wa kizungu..lol
 
Shosi hebu nipe ufafanuzi hapo kwenye red.kutanguliza miguu na sikitu inauhusiano gani?au inamaanisha nini.
btw,usharudi jf?maana ulikuwa unaaga na kufunga mizigo..

Zion daughter habari yako bibie.......ndio waswahili wenyewe mila zao mtoto akitanguliza miguu wakati wa kuzalia anaitwa sikitu. Nimerudi au hunitaki niwepo?
 
Sipati picha unamwita mtoto Rostam. Watamchukia huyo mtoto watanzania wote!!!
 
Nadhani ni kasumba tu LD mie nadhani kuna jambo kwenye kumchukia Rostam nina amini hata kama ni fisadi basi hayupo peke yake kwanini basi asakamwe na kuchikiwa peke yake? Mbona wapo wengi?.................
 
Tabu
Shida
Mwamvua
Sikitiko
Sikujali
Sikudhani
Mwajabu

Endelea

Hilo la kwanza nimeshuhudia huyo mdada na alipata taabu za maisha mpaka umauti ulipompata hakupata raha hata kidogo ya maisha yake na mwisho wakati karibu anafariki aliwaambia watu wake wa karibu hapendi kabisa mtoto yeyote arithishwe jina lake hilo
 
Waafrika tunatawaliwa mno kimawazo.
Tupo tayari kumwita mtoto Happy lakini ukiita Furaha mm ni tatizo.
Tupo tayari kumwita mtoto Peace lakini ukiita Amani mm tatizo.
Tupo tayari kumwita Gift ila kumwita Zawadi ni tatizo.
Cloud ni jina, ila Mawingu waswahili tutalikataa.
Hakuna uhusiano wa Jina na matukio. Ni psychological perception ya mtu tu ndio inafanya watu wafikiri namna hiyo. Mbona wazungu wao hawasiti kumwita mtu Swain, Copymore, Bean etc. Kuna hata makanisa ya kikristo ukimwita mtoto say Tabu watakataa kumbatiza ati sio la Kikristu! Yani akili zetu zimekuwa colonized too much! No wonder wajanja wanatuendesha tu jinsi wanavyotaka wao.
 
Hapo zamani kabla na baada ya mwalimu na hata wakati wa mwinyi ilikuwa mtoto akizaliwa mvua inanyesha anaitwa "mwamvua" akitanguliza miguu wakati wa kuzaliwa ataitwa "sikitu" akizaliwa ijumaa ataitwa "juma au mwajuma" akizaliwa jumapili ataitwa "pili" akizaliwa jumatatu ataitwa "tatu"

Kuna kipindi kukazuka watoto kuitwa majina ya watawala wa zama husika, hii ilitawala hasa kipindi cha kuanzia mwinyi ila sina uhakika kama bado kuna watoto wanazaliwa wanapewa majina kama Slaa, Mbowe, Kikwete n.k.

Ingekuwa enzi zile za mwalimu tungeshuhudia watoto wanaozaliwa katika kipindi hiki wakiwa wanamajina kama Dowans, Mbagala, Gongo la Mboto, Al adawi, Rostam,google, JF, You tube,hi5,IPTL, Songas, Mwakyembe na kadhalika kutokana na wakati wenyewe.

Jana nimesoma news sehemu nikaona kuwa nchini Misri kuna jamaa amemwita mtoto wake wa kike "facebook" kuapriciate mchango uliofanywa na facebook kwenye maandamano yaliyopelekea HM kuangushwa. Wapashaji habari wanasema mtoto huyo amepokea zawadi kem kem kutoka kwa vijana wengi wa kimisri. Nadhani hapa kwetu katika waliozaliwa kwenye mkesha wa tukio la gongo la mboto angepewa jina la gongo la mboto si ajabu watu wangemiminia mizawadi.

Sijakuona jana kwenye harambee ya kakudo au ulikuwa tanga
 
Kumbe dili eeh!
Mwanangu nitamuita JF INVISIBLE BAN PM.
Baba yake sijui atakuwa anaitwa nani.
 
Kuna mdada hivi alijifungua mtoto wa kiume enzi za Mullah Omar, akakaita katoto kake ka kiume Mullah Omar, sikumoja, wakati anijishugulisha na kazi ndogo ndogo, alikalaza mkekani kwenye kivuli cha miti. Kulikuwa na mti wa mpapai amongst other trees by the shde. Upepo mkali ukavuma na kuangusha majani ya mpapai, masikini baby Mullah Omar akaangukiwa na jani la mpapai na kufariki. Hii taarifa iliandikwa hata kwenye magazeti wakati ule, lilitokea Dar.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom