Enzi zetu za utoto..........

kule kwetu mikahawani tangu napata akili hadi nilipoenda mara ya mwisho sijaona mwembe!!

Kuna nini?
Sisi kwanzia maembe, machungwa, mapera, maparachichi, elimu, zambarau, malimao tunayo. Kazi kusubiria msimu tu.
 
Hahahahahaaa ilikuwa Mikocheni kaka, dah Cine Club nadhani ni ya zamani hii naongelea early 90s nilikuwa ndo naanza anza primary school enzi hizo ila ilikuwa kama club ya kawaida kabisa not the way ilivyo sasa

Haya niamkie haraka vinginevyo bakora ni halali yako. Kidongo chekundu ninachokisema ni pale karibu na shule ya Kisarawe jirani na mnazi mmoja. Na hapo palikuwa maarufu enzi ya miaka ya 80
 
sie wa kijini kombolela ilikuwa usiku tena kipindi cha mbalamwezi

Afu unachagua katoto kazuri ka kike unakaelekeza tujifiche huku ebwana mnajificha hd mnapitiliza, mkija kutokea wenzenu wamkekasirika ile mby!
 
yeah kuna ile mnajificha hadi wengine wanaenda kulala maana mchezo hauwezi kuendelea kama hampo. ila tulikuwa na hatari maana tulikuwa tunajificha kwenye shamba la mpunga bila kung'atwa na mdudu nyoka ama wengineo. sana sana siku moja tu tulikosea tukajificha kwa mama siafu, hapo ndo balaa lilipoanza kutoka kwa askari wake
 
Enzi za utoto........Nakumbuka kila mchezo ulikuja na msimu wake wakati wa mbalamwezi kombolela kwenda mbele...kipindi cha kaskazi tulikuwa tunarusha vishada kila mmoja akijaribu kurusha kishada chake kiende mbali kuliko cha mwenzie.....kuna wakati wa kuogelelea lakini ukirudi nyumbani umepauka mkong'oto wa nani huo-halafu unatishwa eti shauri yako utachukuliwa na chunusi!...DAH KWELI KILA JAMBO NI WAKATI.
 
Haya niamkie haraka vinginevyo bakora ni halali yako. Kidongo chekundu ninachokisema ni pale karibu na shule ya Kisarawe jirani na mnazi mmoja. Na hapo palikuwa maarufu enzi ya miaka ya 80
Dah hiyo miaka ya 80 inabidi uwe specific maana mi ndio kuna wakati nazaliwa kwenye miaka hiyo........ Haya SHIKAMOOOOOO
 
Afu unachagua katoto kazuri ka kike unakaelekeza tujifiche huku ebwana mnajificha hd mnapitiliza, mkija kutokea wenzenu wamkekasirika ile mby!
Hahahahaa sio mnaibuka wakati kombolela lenyewe limeisha!?
 
Kama mtihani wa geography o'level miaka ileee ungepoteza 30marks za photograph and Map reading,upande unaouona vizuri ndio aliokua mphotoaji
Hebu eleza picha hii imepigwa saa ngapi? na Taja vitu vinavyoonekana katika picha...........Hahahahahaa Geography ya zamani
 
yeah kuna ile mnajificha hadi wengine wanaenda kulala maana mchezo hauwezi kuendelea kama hampo. ila tulikuwa na hatari maana tulikuwa tunajificha kwenye shamba la mpunga bila kung'atwa na mdudu nyoka ama wengineo. sana sana siku moja tu tulikosea tukajificha kwa mama siafu, hapo ndo balaa lilipoanza kutoka kwa askari wake
Hahahahahaaa sipati picha mlivyosaula..........
 
Enzi za utoto........Nakumbuka kila mchezo ulikuja na msimu wake wakati wa mbalamwezi kombolela kwenda mbele...kipindi cha kaskazi tulikuwa tunarusha vishada kila mmoja akijaribu kurusha kishada chake kiende mbali kuliko cha mwenzie.....kuna wakati wa kuogelelea lakini ukirudi nyumbani umepauka mkong'oto wa nani huo-halafu unatishwa eti shauri yako utachukuliwa na chunusi!...DAH KWELI KILA JAMBO NI WAKATI.
Dah kweli stori za chunusi siziskii siku hizi, mara walikuwa wanadai chunusi akitaka kukuchukua popote ulipo utaenda tu mwenyewe baharini na ukifika ukigusa maji tu unapotea
 
Back
Top Bottom