Eneo alipotema mate mwana-ubalozi limeanza kutengenezwa

USISAHAU KUWA YANATAKIWA KUTEMWA NA WAZUNGU! Ole wako wewe mbongo ukateme, utakiona cha mot na barabara wala haitengenezwi.Kama vipi tuwakodishe wazungu wengine wafanye hiyo hkazi ya kutemea mate trafiki.

wazo zuri sana.

tunaweza kuanza kampeni sasa hivi tuianzia na wazungu tulionao kwa sasa nchini, ya kumtaka kila mzungu amtemee mate angalau mtendaji mmoja wa serikali kila kwa mwezi ili kuharakisha maendeleo,
 
nafikiri tuunganishe ya kwanza na ya pili halafu tuongeze vkorombwezo kidogo. japo ni ndefu, lain ni comprehensive enough,napendekeza isomeke hivi:

"mate: silaha muhimu ya wanamtandao katika kufanya maamuzi magumu ya kuharakisha maendeleo ya miundombinu bora pamoja na kuimarisha mahusiano ya kimataifa na nchi wahisani ili kuwinda misaada kisawasawa baada ya rasilimali zetu kuwaachia wachukuaji wanaoitwa wawekezaji"

mkuu hii ndefu lazima ifupishwe vinginevyo haitaleta maana, kwa mtazamo wangu kauli mbiu inaleta maana ikiwa fupi n ainayoeleweka
 
wazo zuri sana.

tunaweza kuanza kampeni sasa hivi tuianzia na wazungu tulionao kwa sasa nchini, ya kumtaka kila mzungu amtemee mate angalau mtendaji mmoja wa serikali kila kwa mwezi ili kuharakisha maendeleo,

hahaaa MU mbona kabla ya mwaka mpya tutakuwa tumepiga hatua kimaendeleo
 
Lile eneo la Ukonga Banana ambalo mwana-ubalozi wa Canada alimtemea trafiki mate lilianza kutengenezwa tangu Ijumaa (11.12.2009), siku moja tu baaba ya tukio. Sijui ni kwa sababu ya tukio hilo au ni matengenezo ya kawaida lakini panapotengenezwa ni pale kituoni Banana-ukonga tu (palipokuwa na tukio la kutemea mate). Maaskari pia wameongezwa sehemu ile. Sasa hivi foleni kubwa iliyokuwepo imepungua sana.

Nakumbuka alimtemea pia mwandishi Jeri Muro wakati akimpiga picha kituo cha polisi, vipi nacho wamenza kukikarabati? kama bado ni vema tuwakumbushe waende na huko pia
 
hahahahah hii thread imenifurahisha sana hasa kuadhimisha siku ya wazungu kutemea mate trafiki ili sehemu ziboreshwe hahahaha
 
Nakumbuka alimtemea pia mwandishi Jeri Muro wakati akimpiga picha kituo cha polisi, vipi nacho wamenza kukikarabati? kama bado ni vema tuwakumbushe waende na huko pia

Tuwaonyeshe wazungu ilala na kariakoo wakateme mate na huko ili paboreshwe
 
USISAHAU KUWA YANATAKIWA KUTEMWA NA WAZUNGU! Ole wako wewe mbongo ukateme, utakiona cha mot na barabara wala haitengenezwi.Kama vipi tuwakodishe wazungu wengine wafanye hiyo hkazi ya kutemea mate trafiki.

Hahahaha! Good point!
 
hivi banana ukonga ni mbele ya kule Magereza, hebu nifafanulieni kidogo wakazi wa Dar es salaam.
 
Hii ishu ilikuwa kwenye mpango siku nyingi. lakini kwa namna moja ama nyingine, kuandikwa kwake kutokana na tukio hili kumesababisha wahusika waamke!

Palikuwa na shida sana pale mahala maana parking ni ya shida mno, na ukiunganisha na ile junction ya Kitunda, Pia na rafiki zangu wauza mayai wa Machimbo inakuwa "triple-trouble".
 
Lile eneo la Ukonga Banana ambalo mwana-ubalozi wa Canada alimtemea trafiki mate lilianza kutengenezwa tangu Ijumaa (11.12.2009), siku moja tu baaba ya tukio. Sijui ni kwa sababu ya tukio hilo au ni matengenezo ya kawaida lakini panapotengenezwa ni pale kituoni Banana-ukonga tu (palipokuwa na tukio la kutemea mate). Maaskari pia wameongezwa sehemu ile. Sasa hivi foleni kubwa iliyokuwepo imepungua sana.

Ule msemo wa kinga ni bora kuliko tiba kwa Tanzania haupo kabisaaa!!!!!!.
wao tatizo linapojitokeza ndo wanaamka na kutafuta ufumbuzi.
 
Hii ishu ilikuwa kwenye mpango siku nyingi. lakini kwa namna moja ama nyingine, kuandikwa kwake kutokana na tukio hili kumesababisha wahusika waamke!

Palikuwa na shida sana pale mahala maana parking ni ya shida mno, na ukiunganisha na ile junction ya Kitunda, Pia na rafiki zangu wauza mayai wa Machimbo inakuwa "triple-trouble".

Bwana kati ya mambo ya kuangalia hiyo barabara toka airport kwenda ukonga. Watu wa kupanua hiyo barabara hawaitaji kuvaa miwani kuona adha ya pale. Nadhani ndiyo sehemu mojawapo yenye kero ya foleni dar. Sidhani kuwajaza askari wa barabarani ndiyo suluhisho, wanakazi nyingi na sio kutatua tatizo la barabara finyu. Magari ni mengi hata saa nne usiku kuna foleni, ebu niambie saa kumi mpaka saa tatu inakuwaje? Mi nadhani watu wa mipango wafike mahali waone uhitaji.

Nashauri sijui Halmashauri au Tanroads wapaangalie mahali pale ili trafiki wasitemewe mate tena.
 
hivi banana ukonga ni mbele ya kule Magereza, hebu nifafanulieni kidogo wakazi wa Dar es salaam.

Ukonga-Banana ni kabla ya kupanda ule mwinuko wa kuelekea Gerezani Ukonga. Ukiacha barabara ya Nyerere (inayoishia terminal 2) unaanza Pugu Road, mbele kidogo kuna njia panda ya kwenda Segerea, mbele kidogo ndio kuna hicho kituo cha Banana. Kuna kituo cha mafuta cha GAPCO, na kushoto kuna msururu wa maduka. Hapo kuna biashara mbalimbali. Nyuma ya hayo maduka kuna msururu wa mabaa zaidi ya kumi. Pia kuna njia panda ya kwenda Kitunda. Hapo ndio kuna msongamano wa ajabu.
 
mambo ya bongo bwana!!!!!!!!!!!!

kumbe mate nayo yanasaidia kuzindua wanamtandao?????????!!!!!!!!!

nafikiri mwakani baada ya uchaguzi muu, mate yatemwe kwa wingi sana na yaanze kutemwa mara moja!!!
...Kwani ni kila mate tu mkuu?? Mi nadhani ni mate ya wale wakoloni then watu wanakwenda mbio!!
 
Lile eneo la Ukonga Banana ambalo mwana-ubalozi wa Canada alimtemea trafiki mate lilianza kutengenezwa tangu Ijumaa (11.12.2009), siku moja tu baaba ya tukio. Sijui ni kwa sababu ya tukio hilo au ni matengenezo ya kawaida lakini panapotengenezwa ni pale kituoni Banana-ukonga tu (palipokuwa na tukio la kutemea mate). Maaskari pia wameongezwa sehemu ile. Sasa hivi foleni kubwa iliyokuwepo imepungua sana.

Kifusi kilianza kumwagwa kabla ya Jerry Muro kutemewa mate na traffic police wamekuwepo wakati wote sio kwa ajili ya mate!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom