Elections 2010 Endapo Kampeni ya kumzuia JK kugombea 2010...

Endapo kampeni ya kumzuia JK kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM 2010 itafanikiwa Taifa letu litakuwa matatani kwani itakuwa ni mgawanyiko ambao Taifa haliwezi kustahimili. Kwa ajiili ya amani, umoja, na mshikamano vyovyote vile ni lazima Kikwete awe mgombea wa CCM. Nje ya hapo Nchi yetu itayumba.

Think you are doing that history paper ambapo uliulizwa "discuss how the British used indirect rule in colonial Africa compared to the system of assimilation used in French colonies".

I wonder how the indirect campaigning strategy by mwanakijiji et al ;) will assimilate JF members to destabilize the status quo!!:D

Nimefundishwa hayo hapo juu, reckon!
 
pamoja na hoja nyingi humu ndani kuashiria kutokubaliana na utawaa wa kiujanjaujanja na kisanii wa Jakaya Kikwete, ukweli ulio rahisi kwa utafiti wa kina ni kwamba huyu bwana atashinda tena mwakani na kuendelea kuwa rais wetu kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

watanzania wamejaa ulalamishi juu yake lakini hakuna mkakati mahususi wa kuhakikisha mwakani hashindi uchaguzi. huu ndiyo ukweli kwamba Kikwete ataendelea kuwa Rais wetu kama hatuna mikakati mbinu ya kumzuia kuwa rais wetu kwa mara nyingine tena!
 
pamoja na hoja nyingi humu ndani kuashiria kutokubaliana na utawaa wa kiujanjaujanja na kisanii wa Jakaya Kikwete, ukweli ulio rahisi kwa utafiti wa kina ni kwamba huyu bwana atashinda tena mwakani na kuendelea kuwa rais wetu kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

watanzania wamejaa ulalamishi juu yake lakini hakuna mkakati mahususi wa kuhakikisha mwakani hashindi uchaguzi. huu ndiyo ukweli kwamba Kikwete ataendelea kuwa Rais wetu kama hatuna mikakati mbinu ya kumzuia kuwa rais wetu kwa mara nyingine tena!

...hizo mbinu ziwe za kidemokrasia otherwise (kwa mapenzi ya mw'mungu,) ni "mwendo mdundo" mpaka 2015.
 
Kigarama,
Unayosema yana kaukweli ndani yake lakini safari hii Watanzania wameona waziwazi nchi yao inavyotafunwa na sina wasiwasi kuwa wakamng'oa JK kimya kimya bila kujitambua kama alivyofanyiwa K. Kaunda.

Busanda itakuwa ni kipima joto kizuri sana kuonyesha kama kweli Watanzania wameyasikia makelele ya wazalendo wenzao juu ya nchi kutafunwa au la.

Busanda pia itasaidia kuwafahamisha watanzania kuwa wakati wa kujikomboa kutoka na chama kilichotekwa na mafisadi ni sasa na inawezekana.

Tusivunjike moyo ila tuongeze bidii iwe ni mtandaoni au mitaani. Kelele zetu ndio zilizowapa nguvu akina Mengi na wengineo kujitosa kwenye hii vita ya kuikomboa nchi yetu kutoka kwa mafisadi.
 
Miafrika ndivyo tulivyo

Mwacheni Jakaya a (malaika.. kwa mujibu prince alivotuelekeza kuwa kwenye andiko lamwisho la Balali (RIP) ndivyo aitwavyo ) amalizie vipindi vyake viwili kM ilivyo desturi... Labda hii miaka mitano ya kwanza alikua anajipanga miaka minine mitano itakayokuja ataonesha uwezo wake... Mnajuaje kama alikua na long term plans? Acheni fitna.. maana tukiwaamabi mtutajie ambaye mnaona anafaa hamuwezi.... Nyie watu bana!!!!
 
Jamani ccm kama kweli bado kuna watu wenye uchungu na nchi hii na wananchi wake wamwache huyu kisura aende tu kazi imemshinda atafanya kazi nyingine urais hauwezi. Problem hapa hao ccm wanao huo ujasiri wa kumpiga chini mwenyekiti wao hata kama kachemsha completely? I don't think so. Lakini hivi huyo kikwete naye bado huenda ana nia hiyo ya kugombea? Kama anayo ni kwa faida ya nani jamani mbona noma hivyo? Kama wanamatandao si wamekula hivyo hivyo vinatosha waturudishie nchi yetu.
 
Nitarudia tena na tena kusema kwamba hakuna sababu za msingi ambazo tunaweza kujenga hoja ya kumwondoa Kikwete kama mgombea wa CCM na kumweka mtu mwingine. Hakuna mtu mwingine yeyote ndani ya CCM anayefaa kusimama uchaguzi wa mwaka 2010 kama sababu kubwa tunazojenga ni zitahusiana na Maslahi ya Taifa..

Kwanza kabisa nashindwa sana kuelewa kwa nini tunawalaumu viongozi ambao wanatekeleza sera za chama, hata kama ni kinyume cha matakwa ya wananchi. Nitawakumbusha tena kwamba Mwinyi aliyeteuliwa na Nyerere alikuwa kiongozi kwa mihula miwili pamoja na kwamba aliharibu na uchumi wetu kudodorora bado wananchi tulimchagua Mkapa, mgombea toka chama kilichoshindwa kutusogeza hata hatua moja mbele..

Haya alipoingia Mkapa tulijenga matumaini vile vile lakini akatuacha mataani awamu ya pili, yet bado wananchi tukamchagua Kikwete tena kwa asilimia 80 baada ya chama chake kuboronga Uchumi wetu kwa miaka mitano... Sasa tulitegemea nini hasa Kikwete angeweza kukifanya nje ya sera za chama chake ambazo zimetufikisha hapa tulipo.. Na tunapowachagua watu hawa huwa tuna send message gani kwao?..hakuna zaidi ya kwamba wananchi wanaridhika na Utawala uliopo hivyo Kikwete hawezi kufanya tofauti na kile mlichoridhika nacho kwa miaka 40 iliyopita.

Hatuwezi kumlaumu dereva wa gari kwa kuchelewa kufika trunakokusudia ikiwa tatizo ni utaratibu na ratiba ya shirika la gari hilo ni kusimama kila kituo na kuchukua abiria wengine.. Mtabadilisha kkila dereva lakini kama utaratibu bado ni ule ule sidhani kama mnamtendea haki Kikwete kwa sababu ni nyie wananchi mlomchagua mkijua fika kwamba Mkapa na uongozi wa CCM waliharibu Uchumi wa nchi hii, leo mnataka Kikwete afanye kinyume.. Na nina hakika akifanya hivyo atakuwa Dikteta kwa sababu safari ya CCM ni kutupeleka Tunduma na yeye anahakikisha tunaelekea Tunduma hata kama matakwa yetu wananchi ni kwenda Moshi.. mwenye makosa hapa ni nani?.. na kibaya zaidi gari lilipofika Morogoro tumeisha pita Chalinze watu mnataka Kikwete ageuze gari kurudi njia ya Moshi kinyume cha waajiri wake na wale wote waliomchagua kwa kura asilimia 80 kuwafikisha Tunduma.

Hutaki kwenda Tunduma, panda bus jingine, swala sii dereva jamani hata Mtikila anaweza kuwafikisha Moshi pamoja na kwamba gari lake bovu, at least linaweza wafikisha njia panda Korogwe..Lakini kwa ujinga wetu siosi wenyewe tunaendelea kupanda bus la kwenda kusini tukitegemea somehow pengine tunaweza fika Moshi kwa sababu dereva huyu kijana ana lugha nzuri, bus zuri na kadhalika..

Ukweli utabakia kwamba Kikwete anafanya yote mazuri kulingana na malengo ya chama chake. Ameongeza hesabu za majengo ya shule, barabara zinajengwa, misaada inaongezeka, Ajira nchini zimeongezeka, umaarufu wa Tanzania unazidi (Asha Rose Migiro yuko UN), Mabangusilo wanaanikwa, Vyama vya Upinzani wanapoteza watu muhimu kuhamia CCM. Viongozi wanaoiba wazi wazi wanaachishwa kazi bila kufikisha mahakamani ili kulinda Usalama wa Taifa..Lengo la Tanzania kuwa na Mabillionea 100 karibu inakamilika.. Nini zaidi mnataka?..

Kikwete ktk kampeni zake hakuwaahidi kupambana na Mafisadi, hakuwaahidi kurudisha nyumba za serikali, hakuwaahidi jambo lolote ambalo serikali yake haifanyi kazi na record zote zinaonyesha ongezeko la utenda kazi ktk kila sekta alizowaahidi pamoja na kwamba hazijakamilika...Safari ni kwenda Tunduma na anahakikisha mtafika Tunduma.. Can't U people get it?..Hutaki kwenda Tunduma shuka, toka ktk bus hilo kabla halijakufikisha mbali kwani hizi lawama za kumlaumu dereva haziwezi kukusaidia kitu. Nasema tena Hakuna kiongozi yeyote CCM ambaye atapigana na Ufisadi at the level mnayoitaka, hakuna! kwa sababu kila mmoja wao ana scandal kubwa inayomhusu.. Wewe na mimi hatuifahamu na KULINDANA ndio ILANI ya kwanza ya chama CCM...

People have invested time and money kuhakikisha chama kinakwenda Tunduma, wewe mlalahoi huwezi kubadilisha kitu zaidi ya kutopanda bus hilo. Period!
 
Back
Top Bottom