Elections 2010 Endapo Kampeni ya kumzuia JK kugombea 2010...

Na Mwandishi Wetu
Mwanahalisi~Maslahi ya Taifa Mbele

WATUHUMIWA wa ufisadi, wanaolalamika kuwa Rais Jakaya Kikwete amewatelekeza, wanapanga kumhusisha katika baadhi ya tuhuma zinazowakabili ili kumshinikiza kutimiza matakwa yao, MwanaHALISI limeelezwa.

Taarifa za kuaminika kutoka kwa baadhi ya viongozi serikalini na watuhumiwa, zinasema tayari mipango imesukwa ya kumchomeka Kikwete katika sakata la mitambo ya kufua umeme wa dharula inayodaiwa kumilikiwa na kampuni ya Dowans Holding Tanzania Limited.

Aidha, watuhumiwa wa ufisadi wameapa kumhusisha Rais Kikwete katika sakata la ukwapuaji wa Sh. 40 bilioni, uliofanywa na kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mwaka 2005.


Njia mbili zinatumika kufanikisha “mradi” huu. Kwanza, viongozi wa watuhumiwa wanadaiwa kuchochea watendaji serikalini – wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya – kutenda ovyo au kutotenda kazi ili ionekane serikali imeshindwa kutawala.

Pili, wanadaiwa kuchochea madai, lawama na malumbano ndani ya chama, yenye lengo la kupandikiza chuki na uhasama miongoni mwa uongozi, wanachana na wananchi ili ionekane kuwa uongozi wa chama, ambao pia uko chini ya Rais Kikwete unalegalega.

“Sikiliza ndugu yangu; mengine rais atakuwa ameyagundua. Angalia ziara zake mikoani; ni kukemea hapa na pale. Anakuta wakuu wa wilaya na mikoa hawatendi kazi zao kana kwamba wanamsubiri yeye,” kimeeleza chanzo cha habari.


Mfano mwingine uliotolewa ni kwamba miaka miwili iliyopita, watendaji serikalini walipewa elimu elekezi; jinsi ya kutekeleza kazi zao.

Lakini hivi majuzi rais ameonekana akirudia kutembelea wizara na kushiriki katika utoaji mijadala na mahojiano hadi kufikia maazimio juu ya jinsi ya kutenda kazi, kimeeleza chanzo cha habari hizi.

“Yote haya yanalenga kuonyesha kuwa bila wao – watuhumiwa wa ufisadi na wengine ambao wamepoteza nafasi zao serikalini – basi serikali haiwezi kutenda,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi serikalini.

Kiongozi mmoja wa ngazi ya juu katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye tayari aliishaondolewa katika nafasi yake, anadaiwa kuendelea kushikilia madaraka akidai “hakuna mwingine mwenye uwezo kama mimi.”

“Hakuna kitu kilichomuuma sana kiongozi huyu (jina tulalo) kama kuondolewa kwenye nafasi hiyo ya kifedha. Yeye na rafiki yake aliyeng’olewa serikalini (jina tunalo) walikuwa wakijigamba kuwa pekee, wenye uwezo wa kumshawishi na hata kumwamuru rais,” kimeeleza chanzo cha habari.

Habari kutoka Dettroite, Marekani zinasema mpango wa kumhusisha Kikwete katika tuhuma za ufisadi, ikiwemo kushiriki kwake katika mradi wa Dowans sasa unaendeshwa kwa kasi.

Shirika moja la habari la Marekani, KLHN limenukuu vyanzo vya habari vikisema, mara baada ya mwandishi M.M. Mwanakijiji, kufanya mahojiano na anayedaiwa kuwa mmiliki wa Dowans, Bregedia Jenerali Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), wanaodaiwa kuibeba Dowans wameanza kutafuta jinsi ya kumhusisha Kikwete.

Mbunge mmoja wa Kanda ya Ziwa, aliyekuwa nchini Marekani hivi karibuni, amenukuliwa akisema, “Baada ya mradi wetu wa Richmond kushindwa, Rostam aliombwa na “mkuu” – akimaanisha Rais Kikwete – kumfuata Al-Awadi kuona kama angeweza kuleta majenereta ya kufua umeme.


Mbunge huyo alimwambia mwandishi wa KLHN, “Ni Kikwete aliyeahidi mapema kuwa baada ya muda wa mkataba (wa Dowans kufua umeme) kumalizika, majenereta hayo yatanunuliwa na serikali.”

MwanaHALISI inayo mahojiano kamili kati ya mwandishi wa Marekani na mbunge huyo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mara baada ya mahojiano ya kwanza kati ya Mwanakijiji na Jenerali Yahya Al Adawi, ulifanyika mkutano wa faragha, tarehe 8 Machi 2009 huko Dubai, ukiwahusisha baadhi ya wanasiasa wa Tanzania akiwemo mtendaji mmoja wa serikali.

Katika mahojiano hayo ya kwanza, Al Adawi alikana kuifahamu Dowans. Lakini baada ya mkutano wa Dubai, Jenerali huyo alimwambia mwandishi kuwa anaifahamu Dowans na kwamba ndiye anaimiliki.

Makubaliano kwenye mkutano huo yalikuwa ni pamoja na kuelekeza wenye mrengo wa kuitetea Dowans kuendelea kufanya hivyo kwa “gharama yoyote ile” ikiwamo “hata kumtumbikiza Kikwete” katika sakata hili.

Habari kutoka Dubai zinasema watuhumiwa watatu wa ufisadi kutoka Dar es Salaam na ofisa mmoja wa ngazi ya juu serikalini, walihudhuria kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Jenerali Al Adawi.


Kwenye kikao hicho iliamriwa kuwa Jenerali Al Adawi akiri kuifahamu Dowans kampuni hiyo na vilevile kumtuma mmoja wa wanasiasa hao kuhakikisha anawasiliana na Mwanakiji nchini Marekani kwa lengo la “kumuweka sawa.”

Gazeti la Tanzania Daima Jumapili, toleo la 15 Machi 2009 lilimnukuu Al Adawi akisema, aliombwa na Rostam “kuokoa jahazi” baada ya Richmond kushindwa katika kile kilichoitwa “harakati za mwanasiasa huyo” kuvutia wawekezaji.

Katika mahojiano yake na KLHN, Al Adawi anakiri kufahamiana na Rais Kikwete. Anasema ni Rostam aliyemueleza kwamba rais amempa kazi ya kuleta mitambo hiyo nchini.

Taarifa zinasema watuhumiwa wa ufisadi wanataka kutumia madai kuwa Rais Kikwete na Jenerali Al Adawi wanafahamiana kama njia ya kunyamazisha serikali, asasi za kijamii na wananchi, ili hatimaye mitambo ya Dowans iweze kununuliwa.


Katika mahojiano ya awali na mwandsishi wetu Marekani, Al Adawi alisema ana makampuni lakini hakuna hata moja kati yake ambalo linajishughulisha na nishati ya umeme.

Lakini baada 8 Machi, Al Adawi alisema ana kampuni ya Dowans inayofua umeme.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye, aliwaambia waandishi wa habari juzi Jumapili kuwa malumbano yanayoendelea hivi sasa nchini juu ya kununua au kutonunua mitambo ya Dowans, ni ishara kwamba “mafisadi wamejipanga kuifanya nchi isitawalike.”
“Tunakokwenda ni kubaya ila naamini serikali iko imara na CCM tutaomba tulizungumze kwenye vikao vyetu,kwa nia njema ya kuliokoa taifa linalovurugwa na watu wachache wenye fedha,” alisema Nape.


Kupatikana kwa mabilioni ya shilingi mikononi mwa watu wengi, wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara na wapambe wao, kuna uwezekano wa kujenga ubabe miongoni mwa wanaopinga serikali, ameeleza mchumi mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Tatizo ni kwamba kunakuwa na utawala wa kimafia. Kunakuwa na serikali mbili – ya wananchi na ile ya mafisadi. Kila kinachopangwa na serikali kinapingwa na walioko nje ya serikali na kunakuwa hata na hazina mbili. Hii ni hatari, alisema bila kutaka kutajwa jina gazetini.

Hii habari ina mbinu za propaganda za kizamaaaani. Porojo za kujifanya kama wako upand JMK kumba wanampakazia.

Hii mijitu haina hata haya usoni? labda wanawaona waTanzania ni ma mbumbumbu kiasi hawawezi hata kuchuja upuuzi na ukweli? looh poleni sana na njama zenu!

JMK hamumuwezi ng'oo!
 
Hii habari ina mbinu za propaganda za kizamaaaani. Porojo za kujifanya kama wako upand JMK kumba wanampakazia.

Hii mijitu haina hata haya usoni? labda wanawaona waTanzania ni ma mbumbumbu kiasi hawawezi hata kuchuja upuuzi na ukweli? looh poleni sana na njama zenu!

JMK hamumuwezi ng'oo!

Pole pole,...... soma alama za nyakati
 
Hii habari ina mbinu za propaganda za kizamaaaani. Porojo za kujifanya kama wako upand JMK kumba wanampakazia.

Hii mijitu haina hata haya usoni? labda wanawaona waTanzania ni ma mbumbumbu kiasi hawawezi hata kuchuja upuuzi na ukweli? looh poleni sana na njama zenu!

JMK hamumuwezi ng'oo!

Kwa sasa ataonekana mtawala na Rais, vipi siku na yeye atakapokaa benchi sawa na wezi, wala rushwa, waliotumia madaraka yao mabaya kwa kushirikiana na Rostam kufisadi nchi? Inawezekana unaamini siku hiyo haipo.
 
Tukae tukifikiria kwamba wananchi ndio wanaomngoa RAIS kwenye kiti na sio viongozi so kama hiyo itatokea TZ nadhani ndio itakuwa mara ya kwanza.,....Na hapo hapo hao wananchi wanadanganyika kwa tisheti za bure pamoja na kanga...Swali linakuja je viongozi wake kikwete aliowachagua na kuwaweka madarakani watawaweza kumuweka kikwete chini????
 
Uzuri wa nchi yetu, hutakiwi kuwa na sifa na uwezo wa uongozi kuiongoza TZ bali ni kuwa mjanja mjanja. JK alishfanya timing yake sasa imetoka tuandike maumivu mpaka 2015. Mambo ya yeye kuachia ngazi au CCM kumtema ni ndoto ya mchana ambayo haiwezi kutokea. Si ushaona akina Malecela na Msekwa washa anza kumfagilia kuwa hakuna mwingine ni yeye tu. Hawa ni watu waliopaswa kuona na kuelewa uwezo wa mzee wa kaya lakini wao wanajali matumbo yao. Tipical Tanzanian!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Pamoja na yote, kwa vile CCM ni dubwasha la chama ambalo limelewa utamu wa madaraka litajifanya linafata demokrasia na utaratibu wa chama na litampendekeza agombee na atakuwa Rais kwa awamu nyengine.

Kwamba ni Rais failure ni waaaaaaaaaazi mno..solgani ya ARI MPYA, n.k. iliishia wapi, wale mawaziri walotumwa kutetea bajeti walipozomewa na msafara ulipopolewa mawe..jamani kuna haja ya kusema mengi..

Wengi tumechoshwa na haka kaawamu kake ka utawala, ni rais mchovu asiye na maono, na dira wapi taifa linakwenda..tumekaa kusikiliza ya vyombo vya ha habari tuu
 
Endapo kampeni ya kumzuia JK kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM 2010 itafanikiwa Taifa letu litakuwa matatani kwani itakuwa ni mgawanyiko ambao Taifa haliwezi kustahimili. Kwa ajiili ya amani, umoja, na mshikamano vyovyote vile ni lazima Kikwete awe mgombea wa CCM. Nje ya hapo Nchi yetu itayumba.

Think you are doing that history paper ambapo uliulizwa "discuss how the British used indirect rule in colonial Africa compared to the system of assimilation used in French colonies".

MMKJJ,

"Endapo" tu...vinginevyo,

CCM ndio ipo matatani tayari, pamoja na mgawanyiko- Taifa letu Watanzania lipo kidete, atleast I believe, tumeshikamana.

Taifa linaweza kustahamili mgawanyiko wa CCM-ikiwa tutaweza kuwa na imani, umoja na mshikamano;ambayo tunayo kuchagua Chama kingine kishike hatma.


Sio lazima Mh.Kikwete awe mgombea wa CCM. Historia ianjieleza wazi, CCM huwa na mgombea mmoja tu kwa mihula miwili. Hivyo basi, kuepusha mtafaruku(ambao upo) Itakuwa lazima awe mgombea pekee ili kuepusha hayo 'matata' ndani ya CCM na sio Taifa kama ulivyoelezea hapo juu.

Sasa 'endapo' tutayumba, Watanzania kwa umoja na mshikamano thabiti, tutakuwa na haki ya kuwafikisha CCM matatani.-ikiwa ni pamoja ya kutowachagua- au kuwa-'POLISH'


Amani!
 
Sorry kama nitawakwaza watu lakini ku generalize hivi mfano "Watanzania wengi tumekatishwa tamaa na utendaji wake binafsi napenda kupingana nao. hivi hatuwezi kufanya surveys tukapata statistics. wengi maana yake ni 50%, or 70% or what? katika 35+million. Inaweza kuwa 10% hawampendi. mnasemaje wakuu? kuna NGO na hata mashirika mbalimbali, wangeweza kuja na numbers. Hatuwezi kujifananisha na USA lakini tungeweza kuelekea huko kwa kuwa na % wanapendelea nini, ingetusaidia kuwa na Directiion nzuri. otherwise tunajadili tukiwa gizani.

Mkuu kasema watanzania wengi, kuonyesha kuwa hana takwimu sahihi hivyo hajakosea. Nani kakwambia wengi means 50% or 70%???? mwalimu gani huyo aliekufundisha mwenzetu. ukifanya sample size oppiniouns katika mikoa ya Tz ukweli hata bila takwimu inaonyesha waTz tumemchoka JK. Fuatilia ziara zake mfano ile ya Mbeya, Iringa, etc. Hii ni mikoa ambayo JK alikubalika sanaaa wakati wa kampeni lakini sasa mambo yapo kinyume kabisa mpaka kumpiga mawe. Anyway wazo lako ni zuri wamarekani walikuwa na utaratibu wakupata maoni kwa njia ya computer juu ya umaarufu wa Bush, natoa wito wataalam wa mambo hayo watusaidie tujudge popularity ya JK kwa sasa mpaka wakati wa uchaguzi. Challenge ni kwamba watashiriki wale tu wenye access na computer or internet.
 
Why do most members pefer to write in Swahili and not english? we can attract more readers by using english as means of communication.
 
hatuna haja ya kuumiza vichwa vyetu ahadi zake tulizisikia lakini vitendo hatujaviona na muda ndio huo umekwisha. tumweke pembeni tuangalie mwingine atakayetufaa. muda kwetu ni mali kuliko hayo madoido yake anayofanya. hao CCM waache na ujinga wao wa kulindana madarakani. mwaka 2010 tukimpiga chini watajifunza. tuige mifano ya wenzetu raisi akiboronga tu hata miaka 5 hamalizi wanamtoa iweje sisi tubembeleze?? JAMANI 2010 TUWEKE HISTORIA.
 
His time is up, no doubt!! I'm tellin' ya dawgs, this nicca has absolute little or no brain. Time will tell. Kikwete should be stopped and asked to go!! Godamn it, for gods sake tunahitaji angalau DJ.
 
Why do most members pefer to write in Swahili and not english? we can attract more readers by using english as means of communication.

Hata jina pia linaeleza wazi kuwa ni Forums za Jamii yaani JF. Tunaendeleza Kiswahihi.
 
Why do most members pefer to write in Swahili and not english? we can attract more readers by using english as means of communication.

Nadhani ulitaka kusema "other readers". Ukitaka "more readers" huna budi kutumia kiswahili. Thats why
 
Why do most members pefer to write in Swahili and not english? we can attract more readers by using english as means of communication.

The dilemma is, English will probably attract more of the international/ non Tanzanian audience but at the same time alienate many Tanzanians who either cannot communicate in English or are not very comfortable doing so.

On the other hand writing in Swahili will provide a wider audience among Tanzanians but will probably not be accesible to most non-Tanzanians.

It all boils down to who is in the target aimed and which language the writer feels comfortably more fluid writing in.
 
Mtikisiko urais wa Kikwete

Mwandishi Wetu Aprili 15, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Mafisadi kumponza au kumng'oa

KAULI zinazotaka Rais Jakaya Kikwete apingwe kupitia ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani ni matokeo ya kuyumba kiutawala na visasi vya makundi pinzani ndani ya chama hicho wakati wa mchakato wa urais wa mwaka 2005, imefahamika.

Rais Jakaya Kikwete aliingia kwa kishindo kwenye urais mwaka 2005 akiahidi kubadili utendaji na kuzika tofauti zilizokuwa zimeibuka miongoni mwa wana CCM, lakini sasa kinachodhihiri ni aina ya ombwe katika utawala linalosukuma ufufuko wa makundi hayo ambayo yameanza kujadili urais wake hata kabla ya kipindi rasmi kufika, kwa nia ya kuweka watu wa kumpinga katika awamu yake ya pili.

Wanasiasa waliozungumza na Raia Mwema wiki hii wa ndani na nje ya CCM, wameelezea kwamba mjadala unaoendelea sasa unatokana kwa kiasi kikubwa na kuonekana kwa ombwe kubwa la kisiasa katika utawala wa Kikwete na hivyo kuwafanya baadhi ya wanasiasa kuona kwamba wanaweza kuchukua nafasi ya kuiongoza nchi kuanzia mwaka 2010.

Mtu aliyekaribu na mwanasiasa mmoja ambaye mwaka 2005 aliwania Urais kupitia CCM ameliambia Raia Mwema kwamba kwa sasa mjadala unaoendelea wa kuzuia ama kushawishi watu kumpinga Kikwete ndani ya CCM umechochewa na matukio ya kisiasa na kiuchumi yaliyotokea katika miaka mitatu iliyopita.

"Mwaka 2000 hakukuwa na kelele kama hizi hadharani japo zilikuwapo ndani ya vikao vya CCM, wakitaka kujitokeza watu kumpinga Benjamin Mkapa. Katika kipindi chake cha pili cha urais (Mkapa) unaweza kusema hali ilikuwa shwari, lakini sasa unaposikia hizi kelele, tena kabla ya hata muda kufika kuna sababu nzito, si bure," anasema mwanasiasa huyo katika kauli ambayo bila shaka ni ujumbe kutoka kwa mgombea huyo wa urais wa mwaka 2005.

Akielezea yaliyotokea ndani ya vikao vya CCM kabla ya uchaguzi wa mwaka 2000, mjumbe mmoja wa zamani wa Kamati Kuu ya CCM ameliambia Raia Mwema kwamba, mmoja wa watu wazito ndani ya serikali ya sasa alionyesha kukerwa na utamaduni wa chama hicho kumwachia mgombea urais wakati katiba ya chama hicho haizuii mtu mwingine kugombea.

"Ndani ya vikao vyetu vya chama kuna mwenzetu mmoja ambaye kwa sasa ni mtu mzito ndani ya serikali alilalamikia utaratibu wa sasa wa CCM kumwachia mgombea urais kutopingwa katika kipindi cha pili na sasa nadhani wako watu ndani ya vikao vyetu watakumbushia kauli hiyo kama kwa sasa bado inasimama," alisema mjumbe huyo ambaye bado anahudhuria baadhi ya vikao vya juu vya CCM.

Kuwapo kwa mjadala juu ya kuwapo ama kutokuwapo mtu wa kumpinga Rais Kikwete, katika kuwania nafasi ya Urais kupitia CCM mwaka 2010 kumezidishwa na kauli za kupingana kutoka kwa wana CCM wenyewe wakitanguliwa na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, John Malecela. Malecela mbali ya kuwa kiongozi mstaafu wa CCM, alikuwa miongoni mwa waliowania Urais mwaka 2005 kabla ya kuenguliwa na Kamati Kuu.

Baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM wakitanguliwa na Malecela wametangaza uamuzi wa kumuunga mkono Kikwete, huku wakipata upinzani mkali kutoka kwa wanasiasa wengine akiwamo Mbunge wa Maswa, John Shibuda, ambaye yeye ametangaza waziwazi kuwania tena urais kupitia CCM. Shibuda alikuwa miongoni mwa wagombea 17 waliowania na Kikwete mwaka 2005.

Hivi karibuni pia waliibuka baadhi ya wenyeviti wastaafu wa mikoa wa CCM, wakiongozwa na Pancras Ndejembi ambao nao waliungana na maoni ya Malecela, lakini kwa upande wao wakionekana kuchukizwa na mashambulizi dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi wakidai kwamba mafisadi ni wale waliofikishwa mahakamani na si wanaotajwa tajwa tu na vyombo vya habari.

Hayo yakiendelea, uchunguzi wa Raia Mwema kutoka vyanzo vyake ya habari ndani ya CCM na serikalini umebaini kuwa kuna nyendo za kumtenganisha Rais Kikwete na kundi linalotajwa kuwa la wanasiasa maswahiba wake lakini ambao si waadilifu.

Mkakati huo utakuwa ukitekelezwa kwa njia mbalimbali, ikiwamo mikutano ya hadhara utakuwa chini ya usimamizi wa kundi la wanasiasa ambao inaelezwa kuwa msimamo wao dhidi ya ufisadi unaungwa mkono na Watanzania walio wengi katika kila kona ya nchi.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo miongoni mwa wanasiasa ambao inaaminika taswira yao kimaadili si nzuri mbele ya jamii na ambao kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani ni lazima watenganishwe na Kikwete kwa hoja, ni pamoja na mawaziri kadhaa waliojizulu mwaka jana.

Mantiki iliyopo katika kumtenganisha Kikwete na kundi hilo kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani ni kuithibitishia jamii kuwa Kikwete hayuko pamoja na watu walioporomoka kimaadili katika jamii.

"Sasa ni lazima kuanza kumtenganisha Rais Kikwete na magenge ya wanasiasa ambao maadili yao yanatiliwa shaka na jamii tena kwa kurejea mifano iliyo hai na wazi kabisa," kinasema chanzo komoja cha habari.

Wanasiasa wanaotajwa kutenganishwa na Kikwete katika masuala yanayohusu kuporomoka kwa maadili yao mbele ya umma ni pamoja na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, Rostam Aziz na Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha baadhi yao wakiwa watu ambao Rais alikubali kujiuzulu kwao baada ya kutajwa katika kashfa ya Richmond.

Wamo pia watuhumiwa wazito wa wizi wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao baadhi ni wafanyabiashara na viongozi au wanachama wa CCM.

Itakumbukwa kuwa katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa, aliwahi kumkingia kifua aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Iddi Simba, asijiuzulu.

Hata pale ambapo shinikizo la kumtaka ajiuzulu lilipokuwa kubwa, Mkapa alikubali kujiuzulu kwa kiongozi huyo lakini katika mazingira ya kushangaza, akimtaka awasilishe kwanza nchi katika mkutano wa kimataifa nje ya Afrika.

Taarifa zaidi zinabainisha kuwa mkakati huo mpya uliosukwa unaweza kuwakera baadhi ya wanasiasa walio karibu na viongozi hao watakaotumiwa kama mifano katika kumjenga Kikwete.

Inaelezwa kuwa utekelezwaji wa mkakati huo utahusisha viongozi mbalimbali wa kisiasa na baadhi ya wanaharakati walio msitari wa mbele kupinga ufisadi kwa ushirikiano mahsusi na baadhi ya mawaziri na sehemu ya watendaji serikalini.

Hatua hiyo inatajwa kulenga kufungua ukurasa mpya baada ya juhudi za awali za Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na wenzake ambao wanaaminika kuwa karibu na wanasiasa ambao maadili yao mbele ya jamii yamehojiwa kushindwa kukisafisha chama chao na ufisadi.

Juhudi hizo za awali za akina Makamba zililenga kukitenganisha chama hicho na watuhumiwa wa ufisadi majukwaani kwa hoja kuwa "chama kisihusishwe na ufisadi. Ufisadi ni wa mtu mmoja mmoja si chama," hoja ambayo imekuwa ikipata upinzani mkali na kupuuzwa na sehemu kubwa ya jamii kwa kuongozwa na kambi ya wanasiasa wa upinzani, akiwamo Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa.

Hata hivyo, mpango huu unaweza kukiweka katika shinikizo jipya CCM kwa kulazimika kuwasimamisha nyadhifa za uongozi watu ambao maadili yao yameporomoka mbele ya jamii.

"Itategemea na namna jamii ilivyopokea mpango huo. Kama mambo yatakwenda vizuri maana yake jamii itakuwa inatoa ujumbe kwa CCM kwamba ni lazima watuhumiwa wa ufisadi wenye nyadhifa katika chama wasimamishwe hadi uchunguzi dhidi yao ukamilike au vinginevyo," kilidokeza chanzo chetu cha habari. Kati ya majukwaa yatakayotumika kujenga hoja hizo ni ya mikutano ya hadhara katika baadhi ya majimbo.

Uchunguzi zaidi wa Raia Mwema umebaini kuwa mkakati huo unaweza kupata changamoto hata kutoka kwa sekretariati ya CCM, inayoongozwa na Yusuf Makamba.

Dalili hizo za kujitokeza kwa changamoto na hata kukwamishwa kwa mpango huu zinajengeka katika hoja kwamba wahusika watakuwa wanazidi kupotezwa kwenye ramani ya siasa nchini, hoja ambayo inajidhihirisha kuwatetea zaidi wahusika hao.

Lakini pia kama sekretariati hiyo ya CCM inaweza kuminya mpango huo ambao bado haijawekwa wazi kama mfumo rasmi (system) serikalini umetoa baraka zake chama hicho huenda kikazidi kujisogeza mbali na wananchi wanaoamini kuwa ufisadi umechangia umasikini wao na nchi yao.

Tayari baadhi ya viongozi ndani ya CCM wameelezwa kuwa na mashabiki ndani ya chama hicho na hata ndani ya serikali katika kutimiza dhamira yao ya kuwania urais mwaka 2010 na kama ikishindikana basi mwaka 2015.

Lakini yote haya yakizungumzwa, kwa utamaduni ndani ya CCM, Rais Kikwete ataendelea kuwa mgombea pekee ndani ya chama hicho mwakani hii ikiwa na maana kwamba kama kuna watu wanaitaka nafasi hiyo itabidi wasubiri hadi mwaka 2015.

Uchunguzi wetu ndani ya CCM umethibitisha kwamba wote wenye malengo ya kuwania urais mwaka 2010 ama 2015 wamekuwa wakijizatiti katika chaguzi ndani ya CCM katika ngazi zote kuanzia wajumbe wa mkutano mkuu hadi nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na hata Kamati Kuu ili kuhakikisha wanakuwa na wafuasi wengi katika nafasi zote muhimu ndani ya chama.

"Watu hawalali wanafanya kampeni na zaidi kuna wanaojaribu kuhakikisha kwamba wanapunguza upinzani mkali walionao Kanda ya Ziwa ili kuhakikisha kwamba mambo yanakwenda vizuri katika mkutano mkuu wa CCM," anaeleza kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM.

Baadhi walijaribu kudhibitiwa wasiingie hata katika nafasi ya NEC lakini walijizatiti, huku wengine wakiwa wanajijenga kwa kuwasimika watu wao ndani ya Jumuiya za chama hicho, ambazo wenyeviti wake wanakuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho moja kwa moja.

Kiongozi mwingine mwandamizi wa CCM aliliambia Raia Mwema kwamba, ni vyema Watanzania wakaanza kujadili wanaotaka urais ili kama wanafaa wasaidiwe na kama hawafai ijulikane mapema badala ya kushitukizwa na kukabidhiwa viongozi wasiofaa.

"Si lazima wanaotajwa wagombee lakini si vyema Watanzania washitukizwe. Wajadiliwe ili kama hawafai basi tuanze taratibu kuangalia nani atafaa na tujenge hoja kulingana na usafi wao na uwezo wao kiutendaji.," alisema mwana CCM huyo.

Pamoja na kuwapo kundi kubwa linalotaka kuwania urais "ikibidi mwaka 2010", ni Mbunge wa Maswa pekee, John Shibuda, aliyejitokeza na kuwashangaa wenzake kuogopa nafasi hiyo.

Shibuda anasema kitendo kinachofanywa wenzake kupinga wanaotaka kuwania urais ni kuwa na, "mawazo mgando na maoni yaliyopauka kwani mwana demokrasia hawezi kuthubutu kukandamiza katiba kwa kiasi hicho."

Anasema ya kuwa demokrasia bila utii ni wendawazimu kwani kitendo cha kumtisha kwa jinsi hiyo haitabadili utashi wake wa kugombea urais kwani anaamini kile anachokisimamia.

Shibuda alisema tamko la CCM linasema milango iko wazi kwa mwanachama mwenye sifa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho lakini tamko la wenzake linasema mtu akijitokeza atafukuzwa.

"Viongozi ndani ya chama na nje ya chama wanahitaji kufundishwa haki elimu za kiraia ili wajue na kuisemea demokrasia na si kukurupuka kwa kujikosha kwa kiasi hicho," alinukuriwa akisema Shibuda hivi karibuni katika vyombo vya habari.

Alifafanua kuwa kitendo chake cha kuonyesha nia ya kugombea hakina maana kwamba Rais Kikwete hafai na wala hajafanya kazi, ila anatambua kazi yake, hivyo kugombea kwake ni jambo la kikatiba na kidemokrasia na kuwaonya wanaojaribu kuvunja katiba kwa kiasi hicho.

Hata hivyo baadhi ya wanasiasa wameelezea kuwa hatua ya sasa ni ukomavu wa kisiasa na kwamba, "wanaosema apite Kikwete bila kupingwa waacheni waendelee na wale wanaotaka kugombea kama akina Shibuda na wenyewe waendelee. Yote ni ukomavu wa demokrasia."

Dalili hata hivyo zinaonyesha ya kuwa uwezekano wa kumng'oa Kikwete katika kinyanganyiro cha ndani ya CCM mwaka 2010 ni mdogo. Hata hivyo, hali inaweza kubadilika kama Kikwete hatachukua hatua za makusudi kukabiliana na hali ya sasa ya kuyumba kwa serikali yake na hata chama chake cha CCM.

Magazeti kadhaa, hivi karibuni yalimtaja Profesa Mark Mwandosya kama mgombea anayetajwa kuweza kumkabili Rais Kikwete ikifika mwaka 2010. Mwandosya alikuwamo katika hatua za mwisho za mbio za urais mwaka 2005.

Wengine wanaotajwa kwa sasa kwa upande wa CCM kujiandaa ama kuandaliwa kumrithi Kikwete, iwe 2010 au 2015, ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na hata wengine wanamtaja Lowassa.

Kumekuwapo pia na mijadala ya Watanzania, na hasa walioko nje, inayotaka Dk. Salim Ahmed Salim agombee ama kupitia CCM au kupitia muungano wa vyama vya upinzani. Yeye na Profesa Mwandosya walishindwa na Kikwete 2005, wote wakiwa wamefikia hatua ya mwisho kabisa.

Baadhi ya wananchi wamekuwa wakizungumzia utawala wa sasa wakilalamikia kuyumba kwa hali ya utaifa na kuwapo kwa taarifa za nchi kutekwa na watuhumiwa wa ufisadi huku uchumi ukielezwa kuwa mikononi mwa wageni.

Kutokana na hali ya kisiasa kuwa tete, kuna habari kwamba vikao muhimu vya CCM vinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii kwa kuanzia na Sekretarieti ya chama hicho inayotarajiwa kukutana Ijumaa na Jumamosi ya wiki hii.

Baada ya kikao cha Sekretarieti, imeelezwa kwamba kunaweza kukawa na kikao cha Kamati ya Maadili ya chama hicho Jumapili kabla ya kikao cha Kamati Kuu Jumatatu ijayo.

Vikao hivyo vinaelezwa kuweza kuweka mambo sawa kama si kuwasha moto mpya wa kisiasa kutokana na makundi yaliyoibuka sasa ndani ya chama hicho kuwindana kila kukicha.
 
Taifa letu litakuwa matatani kwani itakuwa ni mgawanyiko ambao Taifa haliwezi kustahimili. Kwa ajiili ya amani, umoja, na mshikamano vyovyote vile ni lazima Kikwete awe mgombea wa CCM. Nje ya hapo Nchi yetu itayumba...
-----------------------------------------------------------------

NANI ATAIYUMBISHWA WAKATI SHERIA ZA UHAINI ZIPO...?
KAMA NI KIKWETE HATA YEYE ATAKUMBWA TU NA SHERIA HIZO ZA UHAINI KWA KULISABABISHIA TAIFA HALI YA HATARI...

HAYO NI MAWAZO YA WATOTO WA CHEKECHEA AMBAO HUTEGEMA CHAKULA KWA KIJIKO...
 
Back
Top Bottom