JAYJAY
JF-Expert Member
- Oct 31, 2008
- 7,519
- 7,557
nilikuwa nimefungua email yangu kwenye yahoo, wakati bado niko signed in, ndugu mmoja naye akaomba naye afungue email yake ambayo pia ni yahoo. nikafungua window mpya ya yahoo lakini bado nikakuta email yangu ndiyo iko signed in, nikafungua window nyingine nikakuta ni vile vile. ilibidi mwishoni ni sign out email yangu mimi, kisha ndipo jamaa alipoweza na yeye kufngua email ya kwake. sasa kwa nini hili la kufungua email za watu tofauti wanaotumia mtandao mmoja (mfano yahoo) kwenye computer moja kwa wakati mmoja haliwezekani (au linawezekana?), na je inawezekana mtu akafungua email yake kwa kutumia computer mbili au zaidi kwa wakati mmoja bila tatizo ( mfano mtu huyo yupo na computer nyingi kama kwenye internet cafe)