Msaada kutumia whatsapp kwenye desktop

Mkushi Mbishi

JF-Expert Member
Sep 30, 2018
318
513
Habari zenu ndugu zangu wa Jf,poleni na majukumu ya kutwa nzima.

naombeni msaada ama maelekezo ni jinsi gani naweza kutumia whatsapp kwenye desktop bila kutumia emulator ya aina yoyote kama hili linawezekana.maana nimejaribu kutumia kwenye bluestacks 5 lakini inacrush kila wakati,haifunguki,sometimes inachukua time sana kusend messages na sometimes inakuwa faster yaani inashindwa kunipa burudani vile inavyotakiwa.Ukizingatia now nimefungua kabiashara ambacho kinanihitaji muda mwingi niwe online kujibu customers wangu lakini unaweza ukamjibu mtu saa sita meseji mpaka kesho haifiki na vurugu zingine kibao,kama ipo njia ya kutumia whatsapp kwnye desktop windows 10 ram 4 bila emulators nahitaji sana msaada wenu wa link,maelekezo nk vile utakavyojaaliwa kama hili linawezekana.

na kama haliwezekani je kuna emulator ipi nzuri itakayonifaa bila usumbufu? na pia nawakaribisha kwa ushauri na maoni.

Biashara inasua sua sana bila whatsapp nini nifanye na siwez kuitumia kwenye simu kutokana na mazingira.

msaada wenu unahitajika sana
 
Unaweza kutumia App au Web
Kama ni App kwa Windowa nenda Window store au download kutoka official website ya meta download whatsApp for PC

Kama ni web tumia Opera mini una scan QR code tu kati ya PC na Simu kisha utaweza kutumia vizuri kabisa bila shida
 
bado imekataa wakuu naiona app kwenye ms store lakini nikigusa install haiendelei yaani hakuna kinachoendelea
 

Attachments

  • whatsapp capture.PNG
    whatsapp capture.PNG
    63.7 KB · Views: 9
bado imekataa wakuu naiona app kwenye ms store lakini nikigusa install haiendelei yaani hakuna kinachoendelea
Unaweza kutumia whatsapp web kwenye computer
1. Andika WhatsApp web for PC kwenye browser yyte ile
2. Baada ya kufunguka, utaona maelezo, utaingia kwenye whatsap ya simu yako, utabonyeza vidoti vitatu >> Linked device
3. Utascan QR Code na itaonesha chat zako
4. Utabonyeza mistali 3 kwenye browser yako kisha utabonyeza kwenye Install WhatsApp App
5. Itaonekana kwenye browser computer yako.
Nimefanya jana tu tarehe 16/12/2023 na imekubali
 
Back
Top Bottom