Elimu nzuri kwa wote TZ inawezekana!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,608
8,748
Watanzania wenzangu kuna jambo linaniumiza sana kwenye nchi yetu Tanzania. Mimi ni Mtanzania kama vijana wengine wengi niliojaliwa kupata elimu lakini ina niuma kuona hakuna jitihada za kuboresha elimu kwa vijana wadogo Tanzania. Mimi nina maswali machache.

1. Je kwa nini sisi kama Watanzania tuna ruhusu shule ambazo zinafelisha wanafuzni hasa za private kila mwaka ziendele kupokea watowo wa Kitanzania.Shule ambazo zina division 4 na 0 nyingi kuliko 1,2 na 3.

2. Je ni kwa nini wazazi wanaendelea kupeleka shule Watoto , shule ambazo hazifaulishi?

3.
Je serikali inautaratibu gani wa kuweka viwango vya shule? Ni kwa nini shule zinazofelisha mwaka nenda rudi zinaruhusiwa kuendelea kufundisha.

Imefikia wakati watoto masikini ni lazima wawe na kipaji cha juu kufanikiwa. Tunafahamu fika kwamba kama umetoka kwenye familia yenye uwezo hata kama una kipaji cha wastani unaweza kufika hadi PHD. Mimi inaniuma sana kwasababu hili ni Tatizo ambalo linaweza kutatuliwa na nina shangaa sana wanasiasa wanapuuza hili hasa ukizingatia wengi wao wametokea vijijini na wamefika walipo kwa bahati. Nchi yetu haitaendelea kama elimu itaendea kupuuzwa. Mimi ningezaliwa kwenye familia masikini ya kijijini sijui ningekuwa wapi sasa hivi?

Je ndugu zangu tujiulize nchi yetu inaenda wapi?
 
Mimi inaniuma sana kwasababu hili ni Tatizo ambalo linaweza kutatuliwa na nina shangaa sana wanasiasa wanapuuza hili hasa ukizingatia wengi wao wametokea vijijini na wamefika walipo kwa bahati.

Kukuuma sana na usifanye kitu hakutaleta mabadiliko yoyote.
IT BEGINS WITH YOU.WHAT HAVE U DONE?
Maswali uliyouliza yana majibu. Kwa mfabo..Wazazi kuendelea kupeleka watoto wao shule zinazofelisha, huwezi kuilaumu serikali.
 
Mimi inaniuma sana kwasababu hili ni Tatizo ambalo linaweza kutatuliwa na nina shangaa sana wanasiasa wanapuuza hili hasa ukizingatia wengi wao wametokea vijijini na wamefika walipo kwa bahati.

Mjomba hao wanasiasa unaowasema, elimu duni kwa watanzania walio wengi ni mtaji wao mkubwa sana wa kisiasa........! So don't expect anything good from them.....labda muing'oe sisiem!
 
Kukuuma sana na usifanye kitu hakutaleta mabadiliko yoyote.
IT BEGINS WITH YOU.WHAT HAVE U DONE?
Maswali uliyouliza yana majibu. Kwa mfabo..Wazazi kuendelea kupeleka watoto wao shule zinazofelisha, huwezi kuilaumu serikali.

Unaweza kuilaumu kwa kushindwa kuingilia kati ada kubwa wanazotoza hao wenye shule zinazofaulisha. Ada kubwa imekuwa sababu ya wazazi wasio na kipato kuwapeleka watoto kwenye hizo shule mbovu kwa kuwa ada zao ni za chini. Wanachoamini ni bahati inaweza kutokea watoto wao wakafaulu kwa Mapenzi ya Mungu.
 
VeraCity nashukuru kuchangia hoja yangu. Naomba nijubu swali lako nilicho fanya ni nini?

1. Kufikiria kwangu kuwa hili ni tatizo ni hatua ya muhimu.
2. Mimi kuongelea hili swala hapa na kulijadili na Watanzania wenzangu pia ni muhimu kwani naamini mawazo yanatoka kwa watu.
3. Nimefanya uamuzi wa kuwa Mtanzania ambaye nitapigania elimu bora kwa watoto wetu. Huu ni mwanzo tu hivyo nitajitahidi kufanya kila niwezalo kusaidia. Vilevile ningeomba Watanzania wenzangu kulichukulia hili swala umuhimu kwani nchi yetu haitakuwa bora kama watoto wetu hawatakuwa na elimu nzuri.
 
Back
Top Bottom