Chapakazi
JF-Expert Member
- Apr 19, 2009
- 2,874
- 310
Katika kusherekea miaka 40 ya Apollo 11, sio mbaya tukaweka picha ambayo nadhani iliweka historia na kutupa sisi wanadamu perspective kidogo ya Ulimwengu na jinsi tulivyo insignificant. Hii picha waliita Earthrise, kufuatia jinsi dunia inavyooneka ikichomoza kama jua, kutoka mwezini.
Ni picha ninayoipenda sana kutokana na jinsi dunia inavyooneka ikiwa 'in it's full glory' ukilinganisha na mwezi uliyo kama jangwa. Picha hii pia ina significance kubwa kutokana na kupigwa wakati wa vita baridi ambapo sisi wanadamu tungeweza kuteketeza hii sayari yetu nzuri na sehemu pekee tuwezayo kuishi ulimwenguni. Ijapokuwa sisi binadamu tuna fikra tofauti na maugomvi kibao, lakini tusikae tukasahau hata siku moja kwamba hakuna nyumbani kwingine kasoro hii dunia yetu ndogo. Hivyo tuitunze na kuipenda.