Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

MPANGILIO WA MADARAKA
Mabandiko ya nyuma tumeeleza wajibu wa Congress na Senate katika uchaguzi baada ya electoral college kumaliza kazi. Ni January 6 Congress na Senate zinakutana

Watakapokutana kutakuwa na makundi mawili kila eneo. Wapo Congressmen and women wanaoendelea na mwaka wa 3 ambao waliochaguliwa katika midterm election 2014.
Wapo wapya wataingia kwa kurudi au mara ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa Senate

Hawa watamchagua Spika na Senate majority Leader. Tunasema hivi kwasababu kipindi cha January 6 hadi linaweza kutokea jambo lisilo tarajiwa Rais na VP wakawa incapacitated, yaani hawamudu majukumu.

Kuelekea Janury 20 ikitokea hivyo, Spika ndiye anayefuata kwa madaraka

Kwa Marekani, madaraka yana ngazi zifuatazo
Rais, VP, Spika, Secretary of states, Sec of treasury, Sec of defence na kuendelea

Mpangilio wao upo wazi kwa kila dharura inayotegemewa isiyotegemewa, inayotokana na mambo ya kisiasa au vinginevyo

Hili ni kuhakikisha kuwa kwa wakati wote hakuna ombwe la uongozi (Power vacuum) na taratibu za kujaza nafasi zimeainishwa kisheria si suala la kubuni tu au kuvunja katiba

KWANINI TUMEELEZA HAYA
Tumeyaeleza kutokana na hoja kama ilivyoletwa na mwenzetu magode ambayo imefungua sana upana wa mjadala wetu

Muhimu sana ni kuonyesha jinsi wenzetu walivyo na mipangilio katika mambo yanayowahusu ya kisisasa , kijamii na kiuchumi hasa upatikanaji wa viongozi

Tukiri kuwa pamoja na kujaribu kuyaweka katika lugha rahisi ya kwetu, mchakato mzima ni mgumu kueleweka kiurahisi hata kwa sehemu kubwa ya Wamarekani wenyewe.

Sheria na taratibu zao zingine zinahitaji weledi wa mambo ya kisheria

Tukiangalia na sisi hapa, kuna tatizo kubwa sana. Tuchukulie mfano mmoja rahisi.

Tatizo la ZNZ limechagizwa na sheria zilizowazi zinazotoa ruhusa ya kukiukwa na viongozi kutofuata sharia hizo. Kulikuwa na ombwe la uongozi baada ya matokeo kufutwa

Hakuna anayeeleza sheria iliyofuta matokeo, hakuna anayeeleza nani alikuwa Rais baada ya mgogoro kwakuwa sharia inasema muda wake ulikwisha.

Hakuna sheria inayoeleza katika hali hiyo nini kinafuata.
Hakuna sheria iliyoziba mianya ya ombwe la uongozi inapotokea

Hatuna chaguzi zinazobakiza wajumbe wa baraza la kutunga sharia(Bunge au wawakilishi) kama ilivyo vipindi viwili vya US.

Hivyo, kulikuwa na mhimili mmoja tu wa Sheria ZNZ , hakukuwa na BLW wala Serikali.

Utaratibu wa US umetengenezwa miaka Zaidi ya 200 iliyopita na watu walioiangalia Marekani kama Taifa na wala si Democrat au Republican.

Hili ndilo tunatakiwa tujifunze,kwamba tunapoandika katiba uroho na ulafi wa masilahi yetu usiweke vizazi vijavyo katika wahka usio na ulazima

Ni lazima waafrika tujifunze kuangalia mbele, kuheshimu sheria, kuziandika kutokana na makosa au matukio na kuzisimamia kama zilivyo.

Bila hivyo tutabaki kuwa bara la giza kila karne

Tusemezane
 
MPANGILIO WA MADARAKA
Mabandiko ya nyuma tumeeleza wajibu wa Congress na Senate katika uchaguzi baada ya electoral college kumaliza kazi. Ni January 6 Congress na Senate zinakutana

Watakapokutana kutakuwa na makundi mawili kila eneo. Wapo Congressmen and women wanaoendelea na mwaka wa 3 ambao waliochaguliwa katika midterm election 2014.
Wapo wapya wataingia kwa kurudi au mara ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa Senate

Hawa watamchagua Spika na Senate majority Leader. Tunasema hivi kwasababu kipindi cha January 6 hadi linaweza kutokea jambo lisilo tarajiwa Rais na VP wakawa incapacitated, yaani hawamudu majukumu.

Kuelekea Janury 20 ikitokea hivyo, Spika ndiye anayefuata kwa madaraka

Kwa Marekani, madaraka yana ngazi zifuatazo
Rais, VP, Spika, Secretary of states, Sec of treasury, Sec of defence na kuendelea

Mpangilio wao upo wazi kwa kila dharura inayotegemewa isiyotegemewa, inayotokana na mambo ya kisiasa au vinginevyo

Hili ni kuhakikisha kuwa kwa wakati wote hakuna ombwe la uongozi (Power vacuum) na taratibu za kujaza nafasi zimeainishwa kisheria si suala la kubuni tu au kuvunja katiba

KWANINI TUMEELEZA HAYA
Tumeyaeleza kutokana na hoja kama ilivyoletwa na mwenzetu magode ambayo imefungua sana upana wa mjadala wetu

Muhimu sana ni kuonyesha jinsi wenzetu walivyo na mipangilio katika mambo yanayowahusu ya kisisasa , kijamii na kiuchumi hasa upatikanaji wa viongozi

Tukiri kuwa pamoja na kujaribu kuyaweka katika lugha rahisi ya kwetu, mchakato mzima ni mgumu kueleweka kiurahisi hata kwa sehemu kubwa ya Wamarekani wenyewe.

Sheria na taratibu zao zingine zinahitaji weledi wa mambo ya kisheria

Tukiangalia na sisi hapa, kuna tatizo kubwa sana. Tuchukulie mfano mmoja rahisi.

Tatizo la ZNZ limechagizwa na sheria zilizowazi zinazotoa ruhusa ya kukiukwa na viongozi kutofuata sharia hizo. Kulikuwa na ombwe la uongozi baada ya matokeo kufutwa

Hakuna anayeeleza sheria iliyofuta matokeo, hakuna anayeeleza nani alikuwa Rais baada ya mgogoro kwakuwa sharia inasema muda wake ulikwisha.

Hakuna sheria inayoeleza katika hali hiyo nini kinafuata.
Hakuna sheria iliyoziba mianya ya ombwe la uongozi inapotokea

Hatuna chaguzi zinazobakiza wajumbe wa baraza la kutunga sharia(Bunge au wawakilishi) kama ilivyo vipindi viwili vya US.

Hivyo, kulikuwa na mhimili mmoja tu wa Sheria ZNZ , hakukuwa na BLW wala Serikali.

Utaratibu wa US umetengenezwa miaka Zaidi ya 200 iliyopita na watu walioiangalia Marekani kama Taifa na wala si Democrat au Republican.

Hili ndilo tunatakiwa tujifunze,kwamba tunapoandika katiba uroho na ulafi wa masilahi yetu usiweke vizazi vijavyo katika wahka usio na ulazima

Ni lazima waafrika tujifunze kuangalia mbele, kuheshimu sheria, kuziandika kutokana na makosa au matukio na kuzisimamia kama zilivyo.

Bila hivyo tutabaki kuwa bara la giza kila karne

Tusemezane
Mkuu nguruvi3 nakushukuru sana kwa ufafanuzi ulioutoa. Binafsi nimekuelewa kwa sehemu kubwa..!! Napata shida moja tu pale unapojaribu kulinganisha uongozi wa Tanzania na wamarekani.

Kiukweli sisi hatufanani hata kidogo,ndo maana sisi wengine tunaona bora achaguliwr Donald Trump ambae anaamini waafrica hawajawa na uwezo wa kujisimamia na kwa misingi hiyo bado wanastahili kutawaliwa..!

Tuendelee kufuatilia uchaguzi wa wenzetu ambao hata wakiwa wanafanya mkutano mkuu wa chama lkn bendera ya marekani ndo inapambwa eneo la mkutano. Hapa kwetu bendera za ccm,chadema,cuf na act ndo zinazoonekana mitaani halafu ile ya Taifa ipo km tambiko tu,maana kuna watu bado wanataka tuwe tunasimama bendera inaposhushwa..!

Yaani binadamu atumikishwe na kitambaa alichokitengeneza mwenyewe. Huu ni upuuzi uliopitiliza. Tuachane ya nchi yetu.

Kura za maoni zilioendeshwa na wikileaks zinaonyesha Trump anaongoza kwa mbali sana vp kura za vyombo vingine kwa mwezi huu!!?? 1471768528332.jpg
 
Napata shida moja tu pale unapojaribu kulinganisha uongozi wa Tanzania na wamarekani.

Kiukweli sisi hatufanani hata kidogo,ndo maana sisi wengine tunaona bora achaguliwr Donald Trump ambae anaamini waafrica hawajawa na uwezo wa kujisimamia na kwa misingi hiyo bado wanastahili kutawaliwa..!

Kura za maoni zilioendeshwa na wikileaks zinaonyesha Trump anaongoza kwa mbali sana vp kura za vyombo vingine kwa mwezi huu!!??
Mkuu natumaini uliona hoja za mwenzetu TUJITEGEMEE hapo nyuma aliyekosoa demokrasia ya US kwa kusema yao ni mbovu na hawawezi kutueleza lolote kuhusu yetu

Hoja za ufafanano wa hii ya Jitegemee zinatumiwa na watawala kufunika ukweli na wapo wengi wanaoamini hivyo. Kwamba, wakitaka kufanya 'yao' wanasema tusifundishwe demokrasia na nchi za magharibi

Wakisifiwa na nchi za magharibi wanageuka na kusema 'tunasifiwa na demokrasia kubwa'

Lengo ni kuwaonyesha jinsi demokrasia ya wenzetu ilivyosonga mbele. Inaweza kuwa si perfect 100% lakini ukiitazama na madudu yetu , wana kila sababu za kutusota vidole

Pili, ni katika kusaidia jamii ione ni umbali kiasi gani sisi tupo kutoka mstari wa mwisho wa mbio

Kuhusu kura za maoni, kura nyingi zilizofanywa na mashirika ya ndani ya Marekani zinaonyesha Trump akiwa nyuma katika battle states ikiwemo red states
Hilo ndilo limemfanya Trump ku reset tone ya kampeni yake ikiwemo kufukuza kampeni meneja

Nitatafuta info Zaidi inatosha kusema tu, Trump ana trail kwa Clinton in double digit kwa baadhi ya sehemu
 
Nimekutana na hii ktk chanzo kingine! Kampeni ya mama ni km imepoa sana baada ya mkutano mkuu!!??

Breaking! Trump now winning in key battleground state


Trump finally takes a lead in PA!

CBS8.com reported: Republican presidential nominee Donald Trump has surged to a 5-point lead over democratic rival Hillary Clinton in the key battleground state of Pennsylvania as per the poll conducted by CEPEX Center for Excellence in Project Execution, on Friday (19th Aug 2016).

Trump leads Clinton 41.9 percent to 36.5 percent, with 21.5 percent voters undecided. Trump’s lead is just inside the margin of error and marks the first time that the Republican candidate is catching up in the traditional stronghold state of the democratic party.

The survey contacted around 1,000 registered voters. Results are estimated to be accurate within 7.1 percentage points, 19 times out of 20. According to CEPEX analysis, the error percentage is high due to the results obtained from just one day of polling. Subsequent polling would be required to reduce the error percentage.

Full article @ (Link: www.cbs8.com)
 
magode

Habari za mitandaoni nyingine si latest.
Hiyo habari ni kabla ya DNC convention na post GOP convention.

Wakati huo kampeni meneja wa Trump alikuwa Landowiski aliyejiuzulu. Nafasi yake ilichukuliwa na Manifort aliyejiuzulu wiki iliyopita.

Nadhani umefuatilia shake up ya kampeni ya Trump na inaeleza kwa undani hali ipoje.
 
Ndugu yangu magode, are you really serious? Ha ha haaa...! Hata polls za Fox News zinampa Clinton ushindi!

1470254754722.jpg
 
WIKI HII

Tunaendelea na habari za uchaguzi mkuu wa Marekani ambako wiki hii mengi yametokea

Kwa upande wa Bi Clinton suala la emails limeendelea kuitesa kampeni yake.

FBI kwa shinikizo la Republican wametoa taairfa ya mahojiano yao na Bi Clinton
Hakuna kinachooenekana pengine kitabadilisha hali ya mambo

Kinachojitokeza ni kampeni ya Clinton kufunikwa na suala hilo kwa kiwango kikubwa
Takribani wiki nzima, kampeni imekuwa na harakati za kujisafisha na sakata

GOP wanafufua kila mara kama mbinu ya kudhoofisha kampeni ya Clinton.
Wanalihusisha suala na hatari ya usalama wa Taifa na kutoaminika kwa Bi Clinton

Lengo la GOP wanaopata msaada mkubwa wa Sanders ni kuhakikisha kampeni haitulii bali kuhangaika na suala la damage control.

Kama mtakumbuka tulisema kuwa Sanders atakuwa tatizo mbele ya safari ya Democrats, ndilo linaendelea sasa. Mbinu wanazotumia GOP wameazima kitabu kutoka kwa Sanders

Kuelekea mdahalo wa mwanzo wiki hii, suala emails litaendelea kumtesa sana Bi Clinton

TRUMP
Takribani wiki mbili, Trump ameyafikia makundi ya watu wa rangi (Black na Latinos)
Amefanya ziara hata kubadili kauli zake katika lafudhi laini 'low tone'

Trump amefanya Ziara nchini Mexico iliyozua maswali mengi kuliko majibu yaliyopatikana
Leo alikuwa katika makanisa ya watu weusi akijaribu kuwafikia

Kabaini maeneo ambayo ni lazima ashinde, kuna idadi nzuri ya watu wa rangi.

Kwa kuangalia kura za maoni, Trump anaongoza kwa kura za watu weupe.
Kwa upande mwingine Clinton anaongoza kura za watu wa rangi

Hapa kuna hesabu zake na si suala la rangi tu. Kwamba, electoral college zinaamua na si popular vote. Mfano, hakuna Rais aliyetoka Republican bila kushinda jimbo la Ohio

Ingawa idadi ya weupe ni kubwa, idadi ya watu wa rangi ni kubwa ya kutosha katika mantiki ifuatayo

Ikiwa Trump atashinda kwa idadi ya weupe katika asilimia 45 kwa 30 dhidi ya Clinton, idadi ya watu wa rangi inatosha kubadilisha hesabu hizo.
Hadi sasa watu wa rangi wanaomuunga mkono Trump ni aslimia 1

Hivyo disadvantage ni kuwa na kundi pungufu akigawana kundi la weupe na Clinton

Kundi la weupe si lazima lote limpe kura zote. Kuna suala la vyama dem na Gop na hatari kubwa Zaidi inayomnyemelea ni uwepo wa wagombea wa wengine wanaokula eneo lake Zaidi

Tutaendelea
 
KAMPENI ZAENDELEA

MDAHALO WA KWANZA UNAKUJA

Kampeni zimeendelea pande zote zikikumbwa na masahibu kadhaa

CLINTON
Suala la emails limezidi kujirudia mara kwa mara. Hili limedhoofisha kwa kiasi fulani kampeni. Muda mwingi umetumika kuzuia uharibifu kuliko kushambulia.
Emails zimefungamanishwa na suala la ulinzi na usalama

Trump kila anapoongelea ulinzi na usalama, suala la emails linakuwa katikati

Hii ni kutokana na kauli kuwa 'Clinton' haaminiki. Ndivyo Sanders alivyolitumia

TRUMP
Baada ya jaribio la kuungwa mkono na watu wa rangi, amerejea ratiba za kawaida. Hakuna takwimu za kuonyesha matokeo ya jitihada hizo

Kampeni imekumbwa na suala la wahamiaji(immigration), Trump amebadili msimamo mara 3.Nii katika kutafuta kuungwa mkono na Latinos

ULINZI NA USALAMA

Kuelekea sept 11, Trump ameliingiza suala hilo makusudi.
Kwanza kama nguvu ya Republican na pili kuoanisha kumbukumbu na hoja zake.

Ni njia nzuri, ujumbe unasikika hasa anapoongelea ISIS na matishio ya ugaidi

Kwa bahati mbaya kauli tata zinamweka mahali pagumu bila kutarajia.

Trump alikaririwa akisema 'Obama amewafanya majenerali vifusi' (Reduced to ruble) na kwamba hakuunga mkono vita ya Iraq kama Clinton

Clinton kampnei wametumia fursa hiyo kumrudi Trump.
Wanasema kama Obama hakuwajali iliwezekanje watu kama Osama kuondolewa?

Wamerudisha kauli za Trump alizosema anajua namna ya kushinda ISSI kuliko Majenerali wa jeshi la Marekani

Kuhusu vita ya Iraq, ipo video ikionyesha Trump aliunga mkono uvamizi,imerudi

Kwamba, ISIS wasingekuwepo kama US wangeenda kupora mafuta.

Hoja nyingine ni kulisuka upya jeshi la Marekani kama asemavyo Trump

Anatoa takwimu kulinganisha jeshi la sasa kwa ukubwa na yale ya miaka ya 1946/1915 Anaonyesha kusinyaa kwa ukubwa wa jeshi na vifaa

Hili linampa tatizo, ukubwa wa jeshi la 1946 hauwezi kulinganishwa na 2020.

Teknolojia imeabadilisha mambo. Kazi iliyofanywa na vifaru au askari 500 mwaka 1946, inaweza kufanya na askari 20 leo hii

Hivyo, kwa kiasi fulani anajikuta 'vulnerable' bila sababu.
Wapinzani (Clinton) wanalitumia kuonyesha udhaifu wa Trump na ufahamu

Kuelekea mdahalo wa kwanza, pande zote zina ' mashtaka' ya kujibu

Tutafafanua .... inaendelea
 
WIKI HII KATIKA KAMPENI

MDAHALO WA KWANZA

AFYA YA CLINTON

Kama tulivyosema hapo juu mdahalo wa kwanza wa wagombea upo karibuni
Kwa kawaida kura za maoni hubadilika kila wakati na hakika hutegemea sana zimechukuliwaje

Kuna sehemu kubwa ya watu haisikiki lakini ina impact kubwa sana katika kura
Hili ni kundi la independents ambao husema 'bado hawajafanya maamuzi'

Kuelekea mdahalo wa kwanza, sura ya uchaguzi itaanza kuonekana.
Kutakuwa na panic za wagombea kutokana na matokeo ya mdahalo.

Hata hivyo, mdahalo hauwezi kuwa conclusion ya uchaguzi.
Mwaka 2012 mdahalo wa kwanza Mitt Romney alionekana kufanya vema dhidi ya Obama.

Mdahalo wa Pili Obama akafanya vema hasa eneo la uhusiano wa kimataifa
Kinachoonekana ni Clinton kupewa nafasi ya kufanya vema kuliko Trump

Hili lina sehemu mbili, endapo atafanya vema litamjenga, kinyume,litamjenga Trump

Trump ana advantage kama underdog kizuri hata kama ni kidogo kinafaida kwake

Clinton atakuwa na wakati mgumu kuhusu suala la emails linaloweza kugusa maeneo kama Benghaz na kujenga picha ya uzembe katika mambo ya ulinzi na usalama

Trump ana advantage, hajawahi kuwa katika maamuzi ya serikali kama kiongozi.
Historia ya utendaji wake ambayo ni limited itamweupusha na maswali ya kiutendaji

Tatizo la Trump ambalo itabidi akabiliane nalo ni kubadilisha nafasi 'position' katika masuala kama uhamiaji na ulinzi na usalama.

Mfano, hadi leo ana position 4 kuhusu wahamiaji.

Kwa waandishi kama Anderson Cooper, wawili watakuwa na wakati mgumu

Kura za maoni ni 'survey' tu inayoashiria na wala si kuonyesha uhalisia ni ni kinaendelea
Clinton anaonekana kuongoza Florida, kuna baadhi ya kura za maoni zinaonyesha tie

Ndivyo ilivyo kwingine kama Ohio na North Carolina ambayo ni battle ground states

CLINTON
Leo Clinton 'aliugua' ghafla na kukimbizwa hospitali katika maazimisho ya 9/11.
Baada ya masaa 4 akionekana mzima, Dr kasema alianza kugua pneumonia,Ijumaa

Hili ni mazungumzo ikizingatia afya yake inatiliwa shaka. Kwanza, aliwahi kufanyiwa operesheni ya 'deep vein thrombosis' na kisha kuwa na concussion iliyosababisha mgando wa damu katika ubongo.

Hadi sasa inaelezwa anatumia dawa za kulainisha damu 'blood thinner'

Trump alishawahi kuongelea afya ya Clinton akisema siyo fit 'physically and mentally'

Hili kuingia wakati huu linaiweka afya ya Clinton on spot na kampeni kuwa na kazi ya ziada. Litaendelea kuwa mjadala wa wiki kama halitatokea jingine.

Anayeweza kumsaidia katika kupunguza nguvu ya hoja ni Trump, huenda akaja na jipya na ku- divert attention ya mazungumzo yaliyopo

Tusemezane
 
HILLARY CLINTON NA MARADHI
Ndiyo iliyokuwa habari kubwa baada ya kuondoka katika maadhimisho ya 9/11
Aliondoka akiwa amedhoofu na kukaribia kuangauka

Muda baadaye alijitokeza akionekana mzima wa afya
Kampeni yake ilikaa kimya kwa muda hadi ilipotoka video ikonyesha kudhoofu

Siku zilizofuata kampeni ilisema alikuwa na pneumonia.
Kabla ya siku hiyo, Ijuma Bi clinton alikuwa na kikohozi katika moja ya mikutano yake

Juzi ameeleza namna kampeni ilivyoshindwa kuli 'handle' tatizo lake

KISIASA
Kwa muda, Trump amesema Clinton hana stamina 'kimwili na kifikra'

Hili lilisababisha Clinton kampeni kutoa nyaraka za Daktari kuonyesha dawa anazotumia. Kwa upande mwingine Trump alitoa taarifa kupitia Daktari wake iliyotiliwa shaka kwa kutoandikwa kitaalam

Tukio la juzi , kampeni ya Trump imekaa kimya huku wandishi wakiendelea kulifuatilia. Kwa haraka inaweza kuonekana kampeni imetumia 'utu'

Hili lina tatizo na kampeni iliona ni vema ikae pembeni

TATIZO
Kwamba zitakapohitaji rekodi,kampeni ya Trump itabidi itoe nyaraka zote kuonyesha hali ya afya yake.

Ni sehemu ya utamaduni wa Marekani kujua afya ya Rais Mtarajiwa

Hata hivyo, Clinton kampeni inataka kulitumia kumbana Trump.
Iwapo wote watalazimika kutoa taarifa zingine wazi na hapa na kodi

Trump kampeni haijaonyesha kodi kwa miaka kadhaa
Clinton kampeni wanasema, kama rekodi zitawekwa wazi zile za kodi ziwe wazi

Ni kwa msingi huo suala la Clinton limebaki kwa waandishi zaidi kuliko Trump Kwa hoja ya 'mwaga mboga namwaga ugali''

Kwa ujumla wiki haikuwa nzuri kwa Clinton kampeni ikiunganishwa na kauli yake ya 'wafuasi wa Trump nusu ni deplorable'

Kauli haina tatizo kwa maana aliyokusudia, ina tatizo pale inapotumiwa na Trump kuondoa sehemu ya wapiga kura hasa weupe

Kutokana na ombwe la Clinton kutowepo mumewe ameendelea na kampeni huku Obama akimsaidia kule Philadephia

Trump na charity, achunguzwa. Hili tutalijadili bandiko lijalo

Tusemezane
 
TRUMP KATIKA UCHUNGUZI

Mwanasheria wa NY anachunguza taasisi ya misaada ya Trump

Hii ni baada ya habari za matumizi mabaya ya fedha za michango' donation'

Tuliwahieleza,GOP wanatumia 'kitabu' cha Sanders kujenga hoja.
Hili la Clinton foundation ni mojawapo

Zipo tuhuma za foundation kupokea michango kutoka maeneno yasiyo sahihi
Mfano, nchi zenye ukandamizaji wa wananawake

Yapo madai taasisi ilitumia ofisi ya mkewe 'kufanikisha' shughuli jambo linalosemwa na Trump halikuwa sahihi kwa usalama wa Taifa

Trump ametumia hoja hizo katika kampeni bila kujua zinaweza kumrudi

Zipo habari za Trump kutumia pesa za foundation kununua mivinyo

Kwa ujumla tuhuma ni juu ya matumizi mabaya ya fedha za mfuko

Sasa anachunguzwa na mwanasheria wa NY kama kulikuwa na ndivyo sivyo

MATATIZO YA FOUNDATION

Bill Clinton itabaidi ajibu swali hilo katika mdahalo kama kulikuwa na matumizi mabaya ya ofisi. Hili ni swali litakalokuja likiambatana na emails

Taarifa ya AG wa NY inaweza kumweka Trump pagumu kama inathibitisha tuhuma. Hili lina maana kampeni yake itakuwa imekatwa makali ya hoja

Tatizo la kuchunguzwa kuhusu foundation litaunganishwa na ulipaji wa kodi

Pesa za foundation hutoa misamaha ya kodi,
Ili kujua kama zilitumika sahihi lazima 'tax return' ionekane

Hoja ya Trump kuwa anafanyiwa uchunguzi na idara ya kodi 'IRS' kupoteza nguvu. Waandishi wana hoji,kwanini hatoi ya miaka 5 au 10 iliyopita?

Advantage ya Trump ni kutokuwa katika utumishi wa umma na hivyo hana mengi anayoambatanishwa nayo ukilinganisha na Clinton

Disadvantage ni mdomo wake unaobeba hoja bila kuangalia madhara

Hoja nyingi anazotumia, zinamfunga kamba mwenyewe badala ya kuwa silaha

Kwanini suala la uchumi halijabeba uzito?

Tutajadili
 
WIKI HII KATIKA KAMPENI

CLINTON NA UGONJWA

TRUMP NA 'VIDONDA'

Hillary Clinton amerudi \peni baada ya ugonjwa. Daktari alitoa taarifa ikionyesha yupo fit kwa kazi. Trump katoa taarifa ya Daktari na kuitangaza kupitia kipindi Dr Oz

Kwa kiasi waandishi hawajaridhishwa na taarifa wakitaka kujua wakimelnga Hillary ambaye alipata concussion na blood clot katika brain huko nyuma

Habari ilifunikwa ghafla na matukio mengine. Kama tulivyosema bandiko lililotangulia, kuna nyakati Trump anaweza kuwa katika nafasi nzuri lakini mdomo wake humponza

Kwa wiki kadhaa kampeni ya Trump imekuwa na nidhamu.
Hilo linatokana na ukweli mara nyingi ametumia hotuba zilizoandaliwa 'teleprompter'

Tatizo lilianza juzi akiwa katika mahojiano na gazeti la Washington post.

Trump aliulizwa iwapo Rais Obama alizaliwa Marekani.
Hii ni hoja ameisimamia kwa muda mrefu hata pale birth certificate ilipotolewa.

Trump hakukiri wala kukataa jambo hilo likaamsha hisia kwa wengi hasa wa rangi wanaoamini Trump ni racist na alilitumia suala hilo kubagua.

Hali katika vyombo vya habari ilikuwa ni nzito kwani issue hiyo iliamsha hisia upya

Trump akalazimika kutoa kauli fupi 'Obama amezaliwa Marekani' kauli iliyoonekana ni ya shinikizo la kampeni pengine hakupenda kuitoa.

Ilikuwa kama kudhalilika na kampeni ilimwambia wakati anajitahidi kufikia makundi ya weusi na walatino hakukuwa na njia bali kukubali

Kauli ya kukubali ikaongeza mafuta kwenye moto , kwamba alitakiwa amwombe Obama radhi kwa kueneza uongo kwa miaka mingi sana.

Wabunge weusi 'black congressional caucus ' walichachamaa, Obama alidhalilishwa

Kulikuwa na Latino caucus, mgeni alikuwa Obama na Clinton. Suala la birth cert lilirudi

Katika kubadili topic Trump akazungumzia suala la silaha akiwa Miami. Akasema, kama Clinton hataki wamiliki silaha, secret service waache silaha aone nini kitatokea''

Pengine si suala zito kama inavyoonekana, hata hivyo huko nyuma alliongelea akisema '2nd amendment people can do something'. Nalo limeamsha vidonda tena

Wiki hii ilikuwa nzuri kwa Trump na mbaya kwa Clinton,haieleweki kwanini Trump anaingiza hoja zinazosababisha matatizo kwake. Kwa mfano hoja ya kodi inarindima

Kuelekea mdahalo, haya yatajirudia

Tusemezane
 
MLIPUKO NEW YORK
SIASA ZAINGIA KABLA YA UCHUNGUZI

Leo kulikuwa na 'dinner' ya congressional black caucus Washington ambako Rais Obama aliongea kama Rais kwa mara ya mwisho. Alikuwepo Hillary Clinton aliyepewa tuzo na CBC

Rais Obama alifantya kazi ya kuamsha hamasa kwa wapiga kura weusi akieleza mafanikio ya serikali yake na hatua alizochukua katika miaka ya uongozi.

Katika aliyosema, Obama alizungumzia bima ya afya 'Obamacare' iliyogusa watu milioni 21 wakiwemo weusi, ajira zilizotengenezwa takribani milioni 15, ongezeko la pato la mwananchi na kupunguza umasikini kwa watu milioni 3 wengi wakiwa weusi

Obama inaelekea alimjibu Trump ambaye akiwa Michigan aliwaambia watu weusi, wata lose nini wakimchagua. Hii maana yake hawajanufaika na serikali ya Rais mweusi

MLIPUKO NEW YORK
Rais Obama akiwa katika mkutano, majira ya 2.45 usiku kumetokea mlipuko katika mtaa wa Chelsea Jijini New York. Huu ni mtaa tu na jina halina uhusiano na mtoto wa Clinton

Mapema leo asubuhi kulikuwa na IED (Improvised explosive device) katika Jiji la New Jersey

Mlipuko wa New York umeathiri watu 29 lakini hakuna matarajio ya kupoteza maisha
Mtu mmoja inaelezwa yupo critical

Inaendelea....
 
MLIPUKO NEW YORK (II)

Baada ya mlipuko Rais alifahamishwa kuhusu tukio. Kama kawaida, wagombea wote wawili Trump na Clinton walipewa taarifa (security briefing). Huo ni utaratibu wa Marekani kwa kujua mmoja kati yao atakuwa Rais wa nchi

Rais
Hadi sasa Rais hajatoa kauli kuhusiana na tukio hilo uchunguzi ukiendelea

Clinton
Hajatoa kauli kuhusiana na tukio

Trump
Akiteremka katika ndege kule Colarado, Trump amesema 'amepewa taarifa ya mlipuko New wa mabomu New York, na kusema Fox we'r living in time, we must get very very tough'

Kauli hii kaitoa kabla ya chombo chochote hakijatoa taarifa rasmi kuhusu tukio

10.30pm
Meya wa New York, Bill De Blasio amezungumza na vyombo vya habari. Alichosema
1. Kumetokea tukio katika Jiji la New York
2. Hawana taarifa kama tukio ni la kigaida
3. Hawana taarifa za connections kati ya tukio la New York na New Jersey
4. Hakuna credible threat kwa jiji la New York
5. Ni tukio la kukusudia na wanachunguza

Kasema taarifa Zaidi itatolewa uchunguzi ukiendelea

Duputy Director FBI
Wana video inayoonyesha tukio na wanaomba mwenye taarifa Zaidi awafikie.
Anasema tukio ni intentional lakini hawaoni kama kuna connections na terrorism

Update 10.45pm
Clinton anasema uchgunguzi unaendelea taarifa zikikamilika atatoa kauli kamili

Tathmini
Katika hali ya uchaguzi hili ni tukio pengine 'likisubiriwa' ili kujenga hoja. Tulisema katika mabandiko ya nyuma, nguvu ya Republican ipo katika masuala kama haya.

Trump atapata mahali pa kzungumzia hoja yake ya ISIS na Immigration. Kwa bahati mbaya, kitendo cha kuongea kabla ya taarifa yoyote kitamweka mahali pagumu

Tayari vyombo vinahoji kama alikuwa sahihi kutumia maneno bomu na kuashiria hatari hata vyombo husika havijatoa taarifa. Lina pande mbili, litamsaidia lakini lita expose weakness zake

Mkanganyiko
Kitendo cha Meya kusema ni tukio la kukusudia linazidi kuongeza maswali.
Kama watu wameumia kwa tukio la kukusudia kwanini lisiwe la kigaidi?

Na je, waliposema wana video, hilo limewapa nguvu gani hadi kusema si la kigaidi?

Tunafahamu vyombo vyote vinafanya kazi na huenda taarifa zikabadilika kila muda

Hata hivyo, tukio litachukua sura ya kisiasa na limefunika mambo mengi ya uchaguzi

Tutaendelea...
 
MLIPUKO NEW YORK

Taarifa zinasema mlipuko ultokea katika jaa za taka 'dumpster' Uchunguzi unaendelea kujua kama ulitokea ndani au nje. Bado wanasema uchunguzi unaendelea

Timu za FBI, counter terrorism, Explosion expert katika federal, state and local level

Ingawa uchunguzi unaendelea, kuna jambo moja la kutazama nje ya siasa
1. Rais na Wagombea Urais wamepewa Taarifa
2. Meya akiwa mkuu wa kikosi cha zimamoto, FBI na uokozi walikuwepo

Ilibidi taarifa ya awali itolewe na viongozi hao. Hili lina maana
1. Kwamba viongozi wa kitaifa wanajua hali iliyopo
2. Kuwahakikishia wananchi kuwa vyombo husika vipo katika eneo
3. Kuwatahadhrisha wananchi hali iliyopo au lolote linaloweza kutokea

Kwa ufupi, kuna organization katika kushugulikia tukio ikiwemo kutoa taarifa, update the majeruhi n.k. Kwamba, vyomboo katika level zote vipo tayari kwa matukio

Tutaendelea
 
UPDATE

Katika avenue 27 New York kumepatikana kifaa kama pressure cooker kikiwa na nyaya zilizoungwa na cellphone na kipande cha karatasi kikiwa na maandishi. Hakuna ajuaye maandishi yanasema nini

Polisi wanasema kuna second device imepatikana eneo hilo na hakuna maelezo Zaidi

Kupatikana kwa pressure cooker kinakumbusha tukio la Boston wakati wa mbio za marathon

Tukio la leo linakuja kukiwa na mkutano mkuu wa umoja wa mataifa (UN GA)
Hili linaongeza pressure kuhusu uchunguzi

Update zitaendelea kila habari mpya ikipatikana
 
SHAMBULIO LA MIINNESOTA

Baada ya matukio ya jana NY na NJ jana usiku kuna mtu mwenye asili ya kisomali aliyecharanga watu kwa visu katika mall. Hakuna anayetarajiwa kupoteza maisha.

Mtandao wa ISIS umekiri kuwa mtu huyo ni askari wao. Mshambulaiji aliuawa na Polisi ambaye wakati huo alikuwa off duty.

Jumuiya ya wasomali na ile ya waislam wa America zimelaani tukio hilo

KWANINI TUNAELEZA HAYA KATIKA UZI HUU
Matokeo haya yana uhusiano sana na uchaguzi wa Marekani. Kama mtakumbuka hoja ya ulinzi na usalama, ilihusishwa na ISIS na Wahamiaji. Ndiyo hoja iliyomweka Trump katika matatizo na Waislam na wahamiaji kutoka Latino country.

Jana Trump bila kusubiri taarifa yoyote tayari alishaingiza suala la uchaguzi na siasa

Matukio haya yanabadilisha mtazamo wa Wapiga kura kwa kiasi kikubwa sana. Trump ametumia 'scare monger' kuwatisha Wamerekani kuhusu matukio ya kigaidi akilaumu serikali, kumhusisha Clinton n.k.

Katika kitu alichokuwa anasubiri ni kutokea matukio kama haya.
Katika mambo Democrat waliyoombea yasitokea ni haya. Hili ni suala leye masilahi na pande zote

TRUMP
Kwa Trump matukio haya yataongeza kuungwa mkono kwake. Kura za maoni tu wiki zijazo zitaonyesha akiongoza. Tatizo kubwa la Trump ni jinsi atakavyounga ujumbe wake na matukio.

Kuna uwezekano mkubwa sana matukio kama haya yanayotarajiwa kumjenga, yakambomoa kutokana na mdomo wake usio na stara

CLINTON
Mjadala au mdahalo unaokuja itabidi afanye kazi mbili.
Kwanza kueleza nini kitakuwa tofauti na sasa, na pili maelezo ya kina kuhusu hilo.

Trump atatakiwa aeleze kwa uyakinifu ni njia zipi atakazotumia kuzuia matukio kama haya ambayo yanaitwa' lone wolf' yaani vijibwa vinavyoshambulia vyenyewe bila msaada wa mitandao

Kwa namna yoyote matukio haya yatatumiwa sana kubadili siasa za uchaguzi

Kwanini yanatokea nyakati hizi?

Tuitafafanua
 
KWANINI YANATOKEA?

Uchaguzi wa Marekani una influency kubwa katika siasa za dunia.

Tunaweza kuona siasa za Reagan, Bill Clinton, Bush na Obama zinavyobadilisha mitazamo ya Taifa hilo kwa siasa za nje

Zipo kila jitihada za makundi kuhakikisha anayeingia oval office 'analinda masilahi' yao

Hizi ni kama nchi za Uingereza, Israel, Uarabuni, Korea , Japan kwa uchache wa kuzitaja

Zipo zinazoangalia masilahi yao kama China, Urusi n.k

Hivyo kuna mapambano au kampeni zinazoendelea ambazo si rasmi.

Kazi za Snowden aliyehifadhiwa Urusi zinaingilia sana siasa za Marekani.

Nyaraka anazomwaga kupitia WikiLeaks zinakuwa na mijadala inayobadilisha siasa za uchaguzi. Snowden analindwa na Urusi ambayo inatuhumiwa kufanya 'hacking'

Kinachoonekana sasa ni kidogo, kukaribia uchaguzi zinaweza kuwekwa nyaraka nyingine ili kubadilisha upepo wa Wagombea. Katika hili mwathirika mkubwa ni Hillary Clinton

Hii ni kwasababu ya utumishi wake katika umma ukimlinganisha na Trump
Na pia harakati zake za kutaka Snowden akamatwe akiwa secretary of state

Lakini pia ikumbukwe nchi kama Israel kwa kutumia Raia wao wanaomiliki mali nyingi ikiwemo vyombo vya habari ina ushawishi sana.

Tunajua Uhusiano wa Marekani na Israel umezorota, kati ya Obama BB Nyahu

Jaribio la kumweka Bernie Sanders ambaye ni Raia wao kwa asili limeshindwa.

Swali la kujiuliza, nguvu kubwa aliyoipata Sanders ilitoka wapi akiwa hana ushawishi katika siasa za Marekani?Halafu iangalie timu yake inaundwa na kundi la namna gani

Kundi la pili ni la waha wanaofanya mashambulizi ya kudhuru wanadamu

Hawa si wendawazimu kwa maana ya kufikiri. Ni wendawazimu kwa kutenda

Lengo lao siku zote si kupiga tu, bali kupiga kwa kuhakikisha inauma haswa!

Na hapa tutoe mifano michache sana ya siku za karibun
i
Shambulio la Madrid (wakati wa uchaguzi) na kubadili siasa za uchaguzi nyuzi 180
Shambulio la London, baada ya kushinda uenyeji wa Olympic
Shambulio la Paris, wakati wa shughuli za muziki na starehe katika kiini cha utalii uropa
Shambulio la venice, wakati wa sherehe za ufukweni
Shambulio la Boston, marathon ikifika mwisho

Orodha ni ndefu na inaendelea

Haya ya NY au NJ na MN ni sehemu tu ya mambo ya siasa za uchaguzi

Kwanza, wiki hii UN GA inaanza,na ugeni mkubwa wa Marais wa Dunia unatarajiwa!

Pili, suala la uchaguzi wa Marekani ambalo suala hili litabadilisha upepo na kuwa mjadala

Litabadilisha upepo lakini upepo unaweza vuma tofauti na matarajio! Kwanini? Tutajadili

Tusemezane
 
WAKAMATWA

Kabla hatujaendelea na hoja ya kwanini matukio ya NY, NJ,MN yanaweza kubadilisha hali ya mtazamo wa uchaguzi, kuna habari za sasa hivi

Mtuhumiwa mmoja ambaye picha yake iliwekwa hadharani amekamatwa NJ baada ya mapambano na Polisi na kujeruhiwa bega

Mtuhumiwa ni Raia wa Pakistan Ahmada Khan Rahim.

Uchunguzi wa simu iliyokuwa ilipue pressure cooker pale 27th street Manhattan na alama za video zimetoa maelezo zaidi ya mtuhumiwa

Video zinaonyesha ni mtu huyo huyo alionekana kule New Jersey

Imefahamika pia aliyecharanga watu visu Minnesota ni Dahir A Adan(22)
Huyu ni Raia kutoka Somalia

Wachunguzi wanaendelea kuwatafuta 5 wanaosema ni 'people of interest' wanaohusiana na Ahmada Khan

Wakati tunasubiri habari zaidi, kuna mambo matatu yanajitokeza
1. Kwamba tukio lililenga Ugaidi tofauti na taarifa za awali
2. Waliofanya hivyo ni immigrant
3. Ni immigrant ''Waislam', Dahir wa Somalia amethibitishwa na ISIS

Mambo hayo yatabadilisha mazungumzo na siasa za uchaguzi wa Marekani.

Yatanufaisha upande mmoja na kudhoofisha mwingine kutegemeana na jinsi gani hoja zitajengwa. Lakini pia yanaweza kuwa shubiri yakitumiwa vibaya

Tusemezane
 
ULINZI NA USALAMA LACHUKUA NAFASI

Kama tulivyojadili, suala la ulinzi na usalama sasa limechukua sura kubwa
Wagombea hawakusubiri muda bali kuonyeshana nani ni mjuvi

Kuna nadharia mbili kuhusu suala hili lililochagizwa na tishio la ugaidi
Kura za maoni za CNN zinaonyesha ifuatavyo

Nani anaweza kukabliana na ugaidi kwa nguvu?
Trump 50% na Clinton 45%

Nani mwenye 'uthubutu' mzuri wa kuwa commander in Chief?
Clinton 50% na Trump 45%

Hili maana yake wapo wanaoamini katika matumizi ya nguvu kukabiliana na Ugaidi na wanakubaliana na hoja za Trump

Wapo wanaoamini matumizi na utulivu wa akili,wanakubaliana na Clinton.

Hoja ya Trump ni kuwa wanaofanya hivyo ni ''Waislam''.

Hili wamelitumia sana akina Rudi Guliani ambaye ni mshauri wa Trump. Kwamba, kukabiliana na ugaidi ni vema kutaja neno 'Islamic terrorist''

Hoja hii iliwahi kujibiwa na Obama kuwa kutaja neno hilo kunabadili vipi mwelekeo wa mapambano dhidi ya Ugaidi?

Hillary anasema, si vema kutuhumu jumuiya nzima ya Waislam

Kwamba, kufanya hivyo ni kukidhi haja ya ISIS na magaidi wengine wanaotaka iwe vita kati ya Waislam na Marekani

Hoja yake ni kuwa hilo litaitenga Marekani na washirika wa nchi za kiislam na kukosa ushirikiano wanaouhitaji kupambana na Magaidi

Swali litakalo wakabili katika mdahalo ni hili
Kila mmoja aeleze kwa undani atakabailianaje na tatizo hilo

Hoja hiyo inagusa eneo la immigration na hapo kuna thin line

Trump anahitaji kura za Latinos/Balck na Immigrant.
Je, atathbutu kusema tofauti na siku za nyuma?

Clinton anahitaji kura za weupe , je ataweza kuwashawishi kuhusu mkakati wake?

Inaendelea...
 
Back
Top Bottom