Ha ha haaa magode, huwaamini wanawake katika mambo makubwa...sawa bwana! Lakini naomba nikuulize, je kuna sababu yoyote nyingie zaidi ya hii?Ngoja kwanza mdahalo baada ya hapo ndo ntasema nilichokuwa nataka kusema..!! Mkuu Mag3 anatuponda sisi team trump. Me nasema ukweli,ntamuunga mkono trump mpaka sekunde ya mwisho kwa sababu sijawahi kuwaamini wanawake ktk mambo makubwa.
Niko nafasi ya mbele kabisa, naisubiri tathmini yako.Mdahalo umekwisha, tathmini inafuata
Duh, huo uliokuwa unauangalia ni mdahalo wa wapi? Kama ni huo huo niliouangalia ukweli ni huu...Trump kam-interrupt Clinton zaidi ya mara 50, kanywa maji zaidi ya mara 10, ka-sniffle zaidi ya mara 20, kasema uongo zaidi ya mara 15, kashindwa kujibu swali zaidi ya mara 12, kafinya uso zaidi ya mara 30...Ha haa haaaa!! Nimeangalia mdahalo mpaka nimejikuta namuonea huruma bi clinton. Trump akiwa anaongea anajiamini sana,anaongea hana pressure kabisa mpaka anavutia..!! Ngoja nisubiri tathimini ya nguruvi3.