Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Sina hakika kama hii mada ndo mahala pake lakini kwenye hii video Tundu Lisu anazungumzia suala la mfumo.

Jambo ambalo Nguruvi3 amekuwa akilizungumzia sana.
 
Nyani Ngabu video ina error haifunguki iangalie tena
Hakuna shaka ni mahali pake bkabisa

Tunakwenda taratibu tusiachane na kuulizwa tumetoka wapi na tumefikaje

Kwa uchache, wegi wakisikia mfumo wanadhani ni agenda ya UKAWA na ndio maana utaona wanarukia hoja zisizo na mashiko au za mihemuko

Tuwakumbushe watu hoja ya mfumo huenda UKAWA wameichukua kutoka jamvi la JF. Kwa miaka mingi tumezungumzia sana hilo bila kujali itikadi zetu. Ndilo lilileta msukumo wa kuandika katiba mpya.

Watu walihitaji katiba Mpya si kwasababu ya sasa imechakaa karatasi, la hasha!

Wanataka katiba mpya kwavile mahitaji hayalingani na wakati.

Mifumo ya maisha imebadilika na lazima tuangalie mifumo ya kujitawala na kujiongoza

Hii ni concept inayoonekana ngumu lakini ni rahisi sana kuielewa.

Kwamba, tuwe na mpangilio (mfumo) ili tuweze kupanga, kuchagua na kutenda

Tuna vidonda, hatuhitaji bandage tunataka dawa ili vipone, hatutahitaji tena bandage.

Wengine hawaoni hilo wanashangilia bandage zikiletwa, hawatambui vidonda havina dawa, bandage ikianguka vinanuka na tunaendelea kuumwa

Tuatajadili mbeleni
 
Nyani Ngabu umenitafutia ugomvi. Asubuhi hii utasikia watakavyoshuka na hoja za UKAWA, si hoja zinavyozungumzwa.

Tumeyasema sana, bahati nzuri Lissu ameyazungumzia kwa undani na ametuelewa

Tatizo letu hatutaangalia kiini na umakini wa hoja au upotofu, utasikia tu mvua za matusi na kejeli

Nikushukuru sana kwa clip ingawa imekatika wakati wa swali la mkuu wa Wilaya.
Kama una mwendelezo wake tupia hapa tena, ni mahala pake haswa

Lakini pia ninalazimika kuahirisha mjadala wa wizara ya madini na nishati kwasababu Lissu keshayasema ! kwik kwik!

Tulitaka tuonyeshe majukumu ya wizara na inaundwaje na akina nani.

Tuzungumzie mamlaka ya Bunge na jinsi yalivyodharauliwa.
Hilo linaonyesha mfumo ulivyo mbovu

Kwa fikra kidogo, hivi Rais aliyekuwa katika Bunge na Cabinet wakati suala la escrow linazungumzwa, na bunge kutoa maazimio, leo anawezaje kwenda kinyume na yale yaliyotendeka?

Rais aliyeondoka na aliyepo wanatoka chama na baraza lile lile la mawaziri
Tunapata ujumbe gani kuhusu uteuzi uliofanyika wa kurudisha waliotuhumiwa?

Kwamba, walionewa? Au bunge lilikosea? Au Rais aliyepita hakulitazama suala kwa undani! au inakuwaje!

Tatizo ni nini, watu au mfumo?

Endapo mfumo ungekuwa sawa, kuna mawili.
Moja ungejieleza wenyewe, pili, sisi majuha tusingekuwa na maswali.

Mfano aliotoa Lissu wa sheria ya wahujumu kuandikwa baada ya kutekelezwa hata wiki hii umetokea. Kwamba, marufuku ya kwenda matibabu imewekwa baada ya ''mzee''kusema 'ameumwa uchovu''

Uvunjaji nyumba umesitishwa kwasababu mfumo unatoa haki kwa wote, aliyevunjiwa na aliyevunja.

Kwa mfano, lile hekalu Mbezi kumbe kuna afisa aliingia makubaliano kinyemela bila serikali kujua.

Hivi kwa hili hatuoni tatizo kweli. Kwamba mtu anaweza kuingia makubaliano kwa niaba ya nchi na nchi isijue! Real bado hatuoni tatizo hapo, tunashangilia tu!

Watatuelewa siku moja na kujutia nafsi zao! Watatukana, kejeli n.k. hatutabadilisha maono.

Tuna maono ya keshokutwa, itakapowafikia wataungana nasi

Ahsante sana kwa video
 
REJEA BANDIKO #36 (WIZARA YA HABARI, MICHEZO NA UTAMADUNI)

Katika bandiko hilo tumezungumzia Waziri husika katika namna mbili.

Kwanza, kama katibu mwenezi wa CCM ambaye kazi zake ni za kichama
Na pili tumemueleza kama Mh Waziri wa habari , michezo na utamaduni na sanaa

Tulizungumzia umakini unaohitajika kutofautisha kofia mbili, yaani ya chama na ile ya serikali
Tukasema kunahitaji umakini,yapo yanayoweza kuichanganya jamii na kuigawa badala ya kuiunganisha

Tulizungumzia michezo kutumika duniani kote kuwaleta watu wapamoj. Tunakumbuka Rais Mandela alipohudhuria fainali za kombe la Rugby baada tu ya kumalizika kipindi cha ubaguzi.

Mchezo wa Rugby ni wa watu weupe kwa jinsi ulivyo South Afrika. Timu ya SpringBok ni maaruf
Ni mchezo ulioonesha tofauti ya matabaka

Kitendo cha Mandela kuhudhuria mechi ya fainali na kutoa kombe, kilifuta sehemu kubwa sana ya tofauti za kirangi.
Taifa zima likwa nyuma ya timu yao na imebaki kuwa mfano mzuri wa jinsi michezo inavyoweza kuwaunganisha wananchi

Kuna nyakati Brazili ilikabiliwa na hali mbaya ya uchumi. Timu iliposhinda kombe la Dunia, Wabrazil walisahau machungu na kuwa kitu kimoja , jambo lililotoa muda kwa serikali kujipanga

Michezo na wanamichezo wametumika katika shughuli za kijamii kutokana na mivuto na ushawishi wao

Taasisi za dunia ikwemo wa UN zinatumia wana michezo/wasanii kwa majukumu mbali mbali hata kuwapa nyadhifa za ''ubalozi''

Majuzi mwanamichezo Mbwana Samatta ametwaa taji la mchezaji bora wa Afrika kwa timu za ndani.

Hakuna mcheza soka katika ukanda wa A.mashariki aliyewahi kulitwaa,ni heshima kwaTanzania

Mbwana alionekana akiwa na bendera ya Tanzania, si ya chama cha siasa

Tukio la ujio wake nyumbani linatapaswa liwe la kitaifa.
Tofauti, waziri wa habari michezo na sanaa akimkaribisha kukutana na Mwenyekiti wa CCM.

Kwa nyadhifa za uenezi na uwaziri, busara zilipaswa kutumika tukio libebe sura ya Utaifa na si uchama

Kwasasa tukio linaonekana la kichama na kupoteza ile maana ilyokusudiwa.
Tukio hilo lilipaswa kuunganisha wananchi, kinyume chake linawagawa katika misingi ya uchama

Hatudhani Mbwana angependa liwe hivyo,mazoea ambayo ni utamaduni ule ule yanaturudisha nyuma

Waziri anaelekeza nguvu kichama, badala ya kuwa kiungo cha michez/sanaa kama wajibu wa serikali

Kwa hili si tu limegawa Taifa, limepunguza hamasa na linamuondolea waziri muonekano kama waziri

Wengine watatafsiri michezo, utamaduni na sanaa kuwa ni wizara inayoshughulikia mambo ya chama

Kwa hili la Samatta, busara zilitumika?

Tusemezane
 
Last edited:
Nguruvi3

Ngoja nijaribu tena hapo chini.

Ila nikimsikiliza Tundu Lissu nashawishika kusema huenda kajifunza kitu kutoka kwenye hoja zako.

Hebu nawe msikilize kuanzia dakika ya 8:30 na kuendelea.




Nyani

Nimemsikiliza huyo anayejiita Malaika, what a loser yaani anataka kutuletea Jambazi Sugu then anajiita malaika. The guy is bogus. Nitajibu hoja zake baada ya muda there is nothing new ni ulaji tu kama asipokula yeye basi mfumo ni mbovu. Vipi mfumo wa kumpata mgombea wa urais ndani ya Chadema? Huo hauna tatizo ehe! Yaani Mbowe analipwa rushwa na kupeleka nje pesa na bado kuna watanzania kama wewe unaona hilo ni sawa?

Kuna msemo unasema ''Toa mboni kwenye jicho lako kabla ya kutoa mboni kwenye jicho la mwenzako.'' Nitajibu hoja za Tundu Lissu kwa sababu ni mwongo .... ..... .... stay tuned.
 
Nguruvi3

Ngoja nijaribu tena hapo chini.

Ila nikimsikiliza Tundu Lissu nashawishika kusema huenda kajifunza kitu kutoka kwenye hoja zako.

Hebu nawe msikilize kuanzia dakika ya 8:30 na kuendelea.



Tundu Lissu (TL) anasema yaliyopita si ndwele anataka kumdanganya nani? Historia ni mwalimu mzuri sana, leo hii tuna dawa za kutibu magonjwa mbali mbali ni kwa sababu ya historia. Watu wanasoma na kuongeza ufanisi kwa sababu ya historia yeye anataka tusifuate hayo. That I call I d i o t i c . Hatuwezi kuwaamini watu kama Mbowe au Lowasa oops EL ati hao ndio wanafaa kuongoza hii nchi? Walaghai wakubwaa hawa, Mbowe alipokea pesa kutoka kwa Jambazi Sugu ili awe mgombea wa Chadema sasa hiyo ndio demokrasi ambayo nathubutu kusema Wachaga wanataka Watanzania wote tuikubali! Huo ndio ujinga uliopitiliza, hongera yake kwa sababu waliomchagua yeye kwa ujinga bado ndio wajinga, lakini sisi Watanzania tuliomchagua JPM bado tupo wazima na ujinga tulifuta kitambo.

TD anasema marehemu Sokoine alikuwa hafuati sheria? Huu ni upimbi tu unamsumbua, Sokoine ndiye aliyesuluhisha swala la kufungua Mpaka wa Kenya na Tanzania, yeye alikuwa wapi wakati huo? Then anasema watu maelfu walifungwa kwa uhujumu wa uchumi huu ni uongo usio kifani, walifungwa wapi hao maelfu? Anaweza kuweka ushahidi hapa hao maelfu waliofungwa kwa uhujumu wa uchumi? Wengi tu wakati ule waliposikia kwamba serikali ina mpango wa kwenda nyumba hadi nyumba walitupa TVs na vitu vingine viliokotwa sehemu za ufukwe wa bahari nk lakini zoezi lile halikudumu na halikutokea kama anavyodai, kama anakumbuka vizuri kipindi cha Mikingamo ni silaha ya umma kilianza kurushwa RTD. Awadanganye watoto wake, mnafiki mkubwa. BTW TL anafahamu presidential powers? To me TL is just another lunatic.

TD anasema Vyombo kama TRA na taasisi zivunjwe …. .. then iwe nini? Unapovunja taasisi lazima utaunda nyingine huyu jamaa hovyo kabisa hapo kitu kinachotakiwa ni leadership code nzuri tu kwenye hizo sehemu na udhibiti. Tulikuwa na Azimio la Arusha wakabadili na kuweka Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu hawa walafi kufanya biashara na wakati huo huo kukomba pesa za walipa kodi. Mfano mkubwa ni hawa wezi ambao hivi sasa wamejazana Chadema, kuanzia EL, Kingunge na Sumaye ambao hadi sasa wanafaidi pesa za walipa kodi wakati walikuwa wanafanya biashara walipokuwa madarakani . EL alijichukulia bure bure tu shehena za walipa kodi na kujikita kwenye biashara ya simu za mkononi na nyinginezo kwa kutumia pesa za walipa kodi, hii mijitu ni mijangili. Hawa ndio walioeneza corporate grand corruption. TD ana m-support EL ambaye alishindwa kubadili system hii hii ambayo kila siku tuliwaambia waibadili. Leo kwa sababu hawako madarakani ati nao ni vinara wa kusema kitu gani kizuri? Walishindwa nini walipokuwa madarakani?


Ukwepaji wa kodi upo hata kwenye nchi zilizoendelea USA, UK, Japan, China, Sweden, Norway nk. Tatizo ni upinzani ambao wamo humo humo wanachofanya ni kutetea maslahi binafsi na kuwakandamiza walipa kodi na moja wao ni huyu TL. Anapoongela Takukuru analinganisha na taasisi gani? FBI? SOCA? (SOCA ya UK ambayo hivi sasa imebadilishwa na inafanya kazi kwa jina lingine) Au iliyomwingiza Jambazi Sugu kugombea urais? Then anasema watu wanakuwa misinformed ni wajinga etc. Hivi ni nani mjinga kama sio yeye? Organised crime ipo kila nchi, na ukija kwenye nchi masikini kama yetu ndio unaona matatizo tuliyonayo ya kuwa na viongozi ambao sio waadilifu. TL kama una ubavu anza kumshughulikia EL sio kulialia kama nyau wakati adui wa Chadema ni Mbowe aliyewauzia mbuzi kwenye gunia.

Wacha kulalamika ati JPM hajasema au kukwambia lolote, huna sababu ya kumngoja JPM afanye wewe ulikuwa Bungeni tangu kipindi kilichopita ulifanya nini kama sio umangimeza tu? TL analalamika ati rais ana kinga kubwa, sasa unaposema hapa unataka kufanikisha nini? Peleka muswaada bungeni huko ndiko wapo watendaji ambao wameshinda kama wewe kuwa wabunge kuangalia kwamba nchi inakwenda mbele sio kutumia cheap politics.

Kuna mada nilianzisha hapa wakati wa JK, nilisema Tanzania inahitaji kuanzisha taasisi kama SOCA ya UK (now changed) au FBI ya USA, ambayo imejikita zaidi katika organised crime ambayo imepewa nguvu ya kutaifisha mali za wizi nk.

Tatizo sio mfumo, mfumo unaweza kubadilishwa Bungeni kirahisi kabisa pia unaweza kuwa na mfumo ambao hauendani na wakati. Tatizo letu kubwa ni kulindana kwa sababu wezi wote ndio dada, kaka, mjomba shangazi zetu, rafiki nk. Tunaoneana aibu, JK kavurunda wabunge wanamwonea haya, Che-nkapa aliuza benki zetu kwa pesa za peremende tunamwonea soni, Jambazi Sugu oops EL ana utajiri ambao hawezi kusema ameupataje tunamwonea soni TD naye anataka ujiko tu tunamwonea aibu. Shame on TD he needs to grow up.. Kama anashindwa kupata demokrasi kwenye chama cha kikabila ataweza kupata demokrasi ndani ya Tanzania? JPM fanya kazi ambayo uliahidi Watanzania, Wacha-na na hawa mangimeza, na mauza uza yao. Wakiweza kuchagua viongozi wao bila rushwa then wanaweza kuwakosoa CCM .. …Yes I said that!
 
Wacha1 ndugu yangu hapa hakuna sababu za kutukana. Ni majadiliano

Tunakuomba ulipe jukwaa heshima. Unaweza kuandika maneno machache ukaeleweka

Unaweza kujenga hoja zako kistaarabu ukaeleweka. Matusi yanakaraha kwa jamii na hayakufanyi ueleweke tofauti na unavyojieleza. Mkuu inatosha kama ustarrabu huwezi endelea na eneo jingine
 
Wacha1 ndugu yangu hapa hakuna sababu za kutukana. Ni majadiliano

Tunakuomba ulipe jukwaa heshima. Unaweza kuandika maneno machache ukaeleweka

Unaweza kujenga hoja zako kistaarabu ukaeleweka. Matusi yanakaraha kwa jamii na hayakufanyi ueleweke tofauti na unavyojieleza. Mkuu inatosha kama ustarrabu huwezi endelea na eneo jingine


Matusi ambayo nyinyi mnafanya hamuyaoni? Wewe ndio endelea sehemu nyingine kama nyie mnaona hayo ni matusi kwa nini mnatukana wengine. Nyie mnaposema matusi hamuoni mnaona ya wengine. Ndio Upimbi wenyewe huo, TL kaporomosha mitusi hapo wala huoni.

You really make me mad, I told you unawalisha Watanzania matapishi then unakuja oh matusi, what the hell do you think you are? Do you think Tanzania is for chagga people only? Do you think you can only teach democracy to us all? Mmekaa kulaghai laghai watu tu baada ya kupata hizo peremende.
 
Last edited:
WIZARA YA UTALII NA MALI ASILI

Katika eneo tunalotakiwa tujiulize linachangia vipi pato la Taifa ni utalii.
Tuna vyanzo na rasilimali za asili ambavyo vikitumika vema vinaweza kuchangia pato letu. Tatizo ni kuwa hatujajitambua katika eneo hili

Utalii ni sekta kubwa duniani. Kuna nchi zinazostawi kwa utalii tu. Utalii si kuona vivutio bali madhari inayovutia.
Pato la utalii linaweza lisionekane moja kwa moja, hata hivyo athari zake chanya ni kubwa kwa jamii nzima

Tuna bahari na fukwe nzuri, milima yenye sifa na mbuga za wanyama unique duniani.
Kwa bahati mbaya ujangili unatokomeza maliasili kwa kasi inayotisha.

Rais mstaafu JK alisema tatizo la ujangili halikuanza wakati wake , limekuwepo.
Hata hivyo lazima tukiri kuwa katika wakati wake tatizo limeongezeka kwa kiasi kikubwa sana

Ujangili umehusisha watu kutoka nje wanaokuja na pesa kuchukua mazao yanayotokana na wanyama
Hakuna hatua madhubuti za kukabiliana na tatizo.

Operesheni iliyoanzishwa iliishia kushindwa vibaya.
Tunaendelea kusikia makontena yakikamatwa Hong Kong na Uswiss tena yakipita katika bandari na viwanja vyetu vya ndege

Waziri wa wizara ni Mh Prof Maghembe aliyekuwa waziri awamu ya 4. Ni mmoja wa mawaziri waliowahi 'kutuhumiwa' kama mizigo na baadhi ya viongozi wa CCM.

Waziri ni mbunge wa Mwanga, katika mkoa ambao chama tawala hakikupata wabunge wa kutosha

Pengine uwepo wake pamoja na uzoefu kama waziri pia umezingatia utamaduni unaojengwa wa kikanda, utamaduni tunaosema haupendezi

Waziri amepewa msaidizi katika ukatibu mkuu akiwa ni meja jenerali.
Hili linaweza kuwa limelenga kumpata mtu wa kukabiliana na ujangili wenye sura 'mapambano' . Ni uamuzi mzuri

Pamoja na uzuri huo, lazima kuwepo na mfumo utakaohakikisha wizara, idara na taasisi zinafanya kazi kwa pamoja.
Ziwepo sheria zitakazowabana wote kuhakikisha ujangili na uhalifu mwingine unakabiliwa.

Mathalan, sheria kali ya majangili, iwahusishe watu wa forodha, bandari na viwanja vya ndege na ujangili huo, inapotokea

Lakini pia wizara lazima iangalie utalii wa ndani na kutoka nchi jirani ili kukuza pato.
Katika hili, lazima wawepo watu makini wa maamuzi ndani ya wizara, bodi na idar. Watu wabunifu wanaoweza kwenda na wakati

Idara ya misitu nayo itupiwe jicho kali. Hatuwezi kuwa na misitu nchini kisha kuagiza bidhaa za mbao kutoka nje. Haiingia akilini

Uzembe uliofanyika wa huko nyuma ufike mwisho.
Mapato ya utalii nchini hayapaswi kukaribiana na mapato ya wananchi wanaoishi nje ya nchi (Diaspora Remittance) .

Utalii ni sekta kubwa duniani kwanini tusiitumie kuongeza wigo wa mapato?
Utalii si matangazo katika mabasi kule London, ni mbinu za kujenga mazingira yanayojitangaza na kuvutia

Kwanini mtalii apande Mlima Kilimanjaro na kisha kwenda kupumzika Mombasa na si Bagamoyo au kwingineko?

Kuna vishawishi gani katika miji yetu vinavyoweza kuwashawishi watu kuja kutembelea nchi na kuacha Dollar?

Inaendelea....
 
Looking after number one. Yes number ONE, and that number is CCM whether you like it or not because CCM reincarnated itself in JPM.
 
WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA UFUNDI

Katika wizara zenye matatizo hii ni mojawapo. Kwa awamu ya nne, wizara imeendeshwa kisiasa

Ni moja kati ya wizara nyeti na kubwa nchini ikzingatiwa ukubwa wa bajeti na umuhimu wake

Ndiyo inayoratibu mipango ya elimu kwa jamii. Hakuna Taifa lililofanikiwa bila kipaumbele katika elimu
Ushindani wa dunia ya leo ni wa elimu Zaidi ya kitu kingine

Wizara inafanya kazi na vyombo vingine kama mabaraza ya mitihani, shule na vyuo kufikia malengo

Matatizo ya mfumo wa elimu yanajulikana na hakuna ubishi kuhusu hilo.

Mitaala inabadilishwa kwa utashi wa kisiasa na si utaalamu. Mipango inapangwa kisiasa n.k

Ni eneo tunalihitaji kulifanyia kazi. Miaka 10 eneo hili limeoza na kupoteza maana nzima ya uwepo

Tumeshuhudia vituko vya kuficha ukweli kwa kubadilisha tafsiri ya matokeo na madaraja ya mitihani

Haya tutayadili mbeleni

Waziri ni Mh Prof Ndalichako aliyekuwa mkuu wa baraza la mitihani la Taifa NECTA.

Prof ni mzaliwa wa Kigoma na mbunge wa kuteuliwa. Kuondoka kwake NECTA kulikuwa na utata.
Kwanza, zilikuwepo tuhuma dhidi ya baraza kuhusu namna ya kutahini na matokeo ya mitihani

Katika kipindi chake baadhi ya shule zilifutiwa matokeo kwasababu kadhaa ikiwemo udanganyifu
Hayo yaligeuzwa na kuwa hoja yenye hisia za udini

Mh aliondoka ofisini kwa muda mrefu kisha tulisikia ameteatuliwa mtu mwingine.

Ni katika mazingira ya kutatanisha kwani utenguzi wake katika haukuonekane kuwa wazi.

Haieleweki ni utendaji wake au ni kutokana na hisia tu za baadhi ya watu walioweka shinikizo

Hata hivyo, kuteuliwa kwake uwaziri kunatueleza mengi kwa njia nyingine.

Tunafahamu tuliyokuwa hatuyajui kutokana na hatua anazochukua sasa.

Iwe ni ubunifu wake au ametumwa, ni haki kusema aliondoka NECT katika mazingira tatanishi

Baada ya kupitia kwa ufupi kila eneo , tutaanza kujadili hatua zinazochukuliwa kwa upana wake

Inaendelea...
 
NINI SERIKALI YA AWAMU YA 5 INATEKELEZA

KUNA JIPYA AU NI MVINYO WA ZAMANI KATIKA CHUPA MPYA?

HARAKATI ZINAZOENDELEA NI ENDELEVU AU MOTO WA MABUA?


Tumepitia kwa uchache muundo wa serikali ya Magufuli katika ngazi ya washauri (Mawaziri)
Kwa uchache kila eneo limepewa uwakilishi kama awamu ya nne. Kinachoonekana kubadilika kidogo ni uwiano wa kijinsia.

Na wote wametumikia awamu ya 4 katika nafasi mbali mbali ndani ya serikali au chama

Rais alianza kazi tofauti na ilivyodhaniwa. Bila ya baraza la mawaziri, alifanya ziara za kushtukiza katika wizara na taasisi
Alichukua hatua za haraka katika maeneo yaliyoonekana yana matatizo

Ziara na hatua hizo zimeleta msisimko kwa jamii iliyochoshwa na wizi, ufisadi na uzembe uliokithiri kwa miaka kadhaa

Kwa mtazamo wa kiutawala, Rais alitaka kuweka mwelekeo (set a tone) kuhusu utawala anaourajia
Lakini pia ilikuwa ni muhimu kwake kutafuta kuungwa mkono kutokana na hali ya uchaguzi 'tension'
Rais alitaka kuuhakikishia umma , amesikia sauti zao na aungwe mkono katika kutekeleza ahadi zake

Sote tunaijua nchi yetu na matatizo yanayotukabili. Kwa muda mrefu tumeanishwa sababu mbali mbali zikiwemo kutawaliwa
Hakuna marefu yasiyo na ncha, hatimaye ukweli unajitokeza. Matatizo yetu ya leo ni kwasababu ya uzembe wetu

Tumeona nchi zilizotawaliwa kama sisi zikipiga hatua kutoka katika umasikini kwenda dunia ya kwanza
Mfano mzuri ni wa kiongozi wa Singapore Li Kuan Yu (LKY) baba wa Taifa. Nchi hiyo ilijitenga na Malayasia na kujipatiauhuru 1966

Hadi anaacha madaraka mwaka 1990 na anafariki 2015 akiwa mshauri wa serikali, nchi imefikia kiwango cha dunia ya kwanza

Mafanikio ya LKY hayakuja kama mvua, ni zao la kutengeneza jamii inayowajibika ikiongozwa na mifumo iliyojipanga

Hapa ndipo tunalazimika kufafanua kwanini MFUMO ni kauli tunayoisisitiza sana katika kutaka kujiletea maendeleo

Wengi hapa jamvini na kwingineko wanapinga dhana ya kutengeneza mfumo sahihi.
Wanachukulia hoja hiyo kama kupinga hatua zinazochukuliwa.

Hawaeleze kwanini kuengeneza mfumo ni jambo baya, wanamini tu ni jambo baya bila kuwa na sababu.
Hili ni tatizo kubwa sana na kama hatutaweza kufungua vichwa, tutacheza gwaride kama tulilocheza miaka 50

Wasichokielewa ni kwanini tunahitaji mfumo na si hatua nyingine zinazoanza na kuishia njiani baada ya wiki moja
Hwajiulizi kipi kipya, na kama hakuna kwanini kilichotangulia kilishindwa

Inabidi kwanza tuiangalie dhana ya mfumo ili tuweze kujadiliana kwa weledi mbele ya safari.

Tunaposema mfumo tunamaanisha nini?

Tutajaribu kupitia hilo
 
MFUMO
Hapa tunazungumzia utaratibu mzima unaowezesha kitu, chombo, taasisi au serikali kutenda ilivyokusudiwa
Ni utaratibu unaoshirikisha 'units' kufanyakazi tofauti kwa kutegemeana ili kutoa matokeo ya pamoja

Matatizo tunayokumbana nayo yanatokana na mfumo usiokidhi wakati na uliochakaa
Serikali imeshindwa kuweka utaratibu mzuri unaoongoza vyombo na taasisi zake

Kwa nchi za wenzetu kazi ya kiongozi wa nchi ni kuratibu (coordinate) shughuli za vyombo na taasisi
Na vyombo/taasisi humshauri Kiongozi nini kifanyike. Vinakuwa na uhuru wa kushauri na kuelekeza

Kwetu sisi Kiongozi wa nchi anaagiza (command) vyombo na taasisi kutekeleza majukumu yao

Kwa mantiki ya kuwa Kiongozi anapoteza nguvu ya uratibu(coordination) na vyombo au taasisi zinapotea nguvu ya kutekeleza majukumu kwasababu vinasubiri maagizo 'command'

Kwa utaratibu wa maagizo vyombo/taasisi zinakuwa na utiifu 'loyal' si nidhamu 'discipline' ya kutekeleza majukumu.

Katika hali ya kawaida kinachohitajika ni nidhamu(discipline) na uratibu(coordination)

Hapa tutoe mfano uliojitokeza

Serikali ya awamu ya 5 ilifuta sherehe za uhuru kuokoa pesa na kuzitumia kwa usafi wa miji na majiji
Hili ni agizo kutoka juu kwenda kwa vyombo/taasisi za serikali

Tukashuhudia vifaa vya kufanya usafi vikiandaliwa,molization ikafanywa kwa maagizo na si uratibu

Nia nzima ya kufuta sherehe na azma ya kufanya usafi ni nzuri, matokeo ya kazi yote ni mabaya

Soma hapa Home

Zoezi zima limeshindwa kwasababu lilitegemea maagizo ya mtu na si uratibu na vombo/taasisi

Limefanikiwa siku moja, halikuwa endelevu na kushindwa mieizi michache.

Mfano huu mdogo sana unaeleza jinsi tulivofeli mambo mengi na haionekani kama tumejifunza

Tunalalamikia kushindwa hatujiulizi kwanini tushindwe kila siku? Tatizo ni nini?

Wapo watakaohoji kwani zoezi la usafi ilitakiwa nini kifanyike ili zoezi lifanikiwe kwa muda mrefu?

Tuna majibu sehemu inayofuata
 
Last edited:
Huu ndio unafiki wa wapinzani na anayeshabikia Mafisadi ati hao ndio watawaletea neema walipa kodi wa nchi hii baada ya kuiba pesa zao anatakiwa apimwe akili.
 
Katika bandiko 55 tumeseama wapo wana hoji, kwani kilitakiwa kifanyike nini zoezi la usafi lifanikiwe?

Katika yote yanayofanyika hakuna jipya. Kwa mfano, tulikuwa na zoezi la wahujumu uchumi
uwajikaji wakati mwinyi, uwazi na ukweli na sasa Hapakazi yanayoshabihiana

Tofauti na nyuma, hili la sasa lina uzito. Tulitakiwa tujifunze kwanini mazoezi tangulizi yalishindwa

Tuanze kujiuliza, kwanini miji,manispaa, majiji na mitaa yetu ni michafu ikiwa;

-(a)Tuna waziri, naibu waziri, wakurugenzi katika wizara ya afya na watendaji kama katibu mkuu
-(b)Tuna mganga wa jiji au halmashauri na bwana afya wa jiji au halamshari za miji na manispaa
-(c) Mganga mkuu wa mkoa na Wilaya
-(d)Wapo mameya na mabaraza ya madiwani
-(e)Tuna idara za serikali kama za maji, maji machafu, mazingira
-(f)Wapo wakuu wa mikoa na wilaya na kamati zao zikiwemo za afya na mazingira

Kundi a-f linatengeneza sehemu kubwa ya viongozi, watendaji, washauri na wafanyakazi
Wote wana mishahara, pengine na semina , makongamano na kila aina ya masufuru

Swali linabaki, inakuwaje miji yetu ni michafu? Inakuwaje mitaa na vitongoji ni vi chafu?

Je, makundi hayo yanawajibika kama inavyopaswa? Yanafanya kazi kama timu?
Yana mipango endelevu katika suala la afya? Yana uratibu mzuri unaoweza kuelezeka?

Je, upo mgawanyo wa madaraka na majukumu miongoni mwa wakuu na watendaji wa makundi (a-f) hapo juu!

Tutafanya makosa kuwalaumu, kwa lugha nyingine yamepooza 'paralysed' Hayajui yafanye nini, nani mkuu nani msimamizi na ni wajibu wa nani katika wakati gani

Likizuka gonjwa la mlipuko kurugenzi ya maradhi ya mlipuko wizara ya afya ikikimbia katika eneo
Waziri akitoa kauli, mkoa wa mkuu akielekeza hiki au kileachilia wakuu wa Wilaya

Mganga mkuu wa Jiji anakuje na lake, mganga mkuu wa mkoa ana lake
Huku kuna katibu tawala wa mkoa, upande wa pili mkurugenzi wa mji au jiji

Mwisho hakuna anayewajibika, Kama yatakuwepo maagizo, yatakinzana, kitakachotokea ni kutupiana mpira n.k.

Miji, manispaa na majiji yanabaki kuwa machafu. Mfumo uliopo hauna jibu bali 'kiwanda cha ajira'

Tuna rasilimali zote, hatujui tuzitumie vipi, kwa wakati gani na mipango ipi

Ndipo Kiongozi wa nchi anapojikuta akisimamia zoezi la la usafi. Ni kwa nia njema kabisa.

Hata hivyo zoezi halina matokeo ya muda mrefu (sustainable) hakuna mfumo unaosimamia.

Tunarudi kwenye lindi cha uchafu tukisubiri tena siku nyingine itangazwe

Huu ni mfano mdogo wa kuonyesha kwanini kukosekana kwa mfumo ni tatizo la kwanza kabla ya matatizo halisi

Mengine yanayotokea zikkiwemo ziara za kushtukiza , fukuza fukuza yana tofauti?

Tutajadili sehemu inayofuata
 
MVURUGANO WA KUONGOZA
Kwa mfano wa usafi tulioeleza juu, kuna mvurugano mwingine tusiouona kiurahisi

Mkuu wa Mkoa, Afisa tawala, mkurugenzi wa mji au jiji, waziri ni wateuliwa
Ni nani anayeongoza wakikaa pamoja?

Kwa kukosa utaartibu na pangilio wa viongozi, wengine hawajui majukumu yao

Tumeona Mameya wa miji au majjiji wakifanya kazi za vyama vya siasa na si ustawi wa maeneo yao

Unapokuwa na Meya ambaye ni mjumbe wa vikao vya vyama, lini anafanya kazi za eneo lake?

Wamekuwa 'bize' kusimamia shughuli za uenezi wa vyama vya siasa na si kazi zao kama usafi

Wakati uongozi wa nchi ukitafuta suluhu ya uchafu mijini, Mameya wanaeza shughuli za vyama!!!

MFUMO MBAYA UNAVYOPTEZA NGUVU KAZI

Miaka ya nyuma Mabwana/bibi wa afya walikuwa na nguvu kubwa sana katika maeneo
Ilipotokea tatizo la afya, wao walikuwa kimbilio la wananchi

Na kupitia wao, mipango kama ya kutokomeza maradhi na vyanzo iliwezekana japo kwa udogo

Leo nikuulize msomaji, hivi lini uliwahi kusikia au kukutana na bwana Afya wa mtaa au kata yako?
Hata vyuo vyao havijulikani na kazi yao sasa imebaki tajwa 'nominal'

Nguvu za bwana/bibi Afya zimepotea kwasbabu nguvu za kisiasa ndizo zinatawala.

Ni rahisi afisa biashara kusimamia shughuli za hoteli kuliko bwana/.bibi afya

Diwani ana ngvuvu za 'kiutendaji' kuliko bwana afya.

Kuna matukio ya Polisi kutoa maelekezo juu ya magonjwa ya milipuko

Tembelea Hotel za Dar es Salaam au mji mwingine mkubwa au mtaa uone uchafu wa vyoo na majiko

Swali utakalokumbana nalo kichwani ni moja, hivi kuna 'idara' ya afya ? Kama ipo inafanya kazi gani

Kwa mlundikano wa viongozi wanaowajibika kwa mtu, kinachotokea ni mvurugano

Fikiria, Polisi wanaposimamia shughuli za magonjwa ya milipuko, bwana/bibi afya, mganga mkuu wa mkoa,/wilaya , mganga wa jiji au mji wana kazi gani?

Hakuna 'discipline' inayotawala. Kila mmoja amekaa ima kumridhisha mkubwa au funika kombe

Zoezi la usafi limeshindwa. Sababu za kushindwa si azma, nia au makusudio bali kukosa uendelevu
Yaani zoezi zima siyo sustainable, kwa msingi huo limeshindwa

Tumerudi pale pale tulipokuwa miezi miwili iliopita

Ndivyo ilivyo katika kila sekta nchini. Hakuna utaratibu wa kimifumo, kilichopo ni kanyaga twende

Na ushahidi upo kama tunavyouona bandarini

Uongozi wa nchi katika muda mfupi sana ulibaini madudu yanayotia kinyaa katika taasisi zetu

Uongozi ulibaini wizi kupitia kodi katika bandari ya Dar es Salaa.
Bandari kwa umuhimu wake kiuslama na kicuhumi ina vyombo maalumu mbali vya kawaida

Wizi natokeaje miaka nenda bila kubainika na vyombo husika?

Hili nalo tulijadili kwa undani wake

Inaendelea...
 
Last edited:
Unapoongelea awamu ya tano (5) kwa pazia ambalo unalifahamu mwenyewe, ambayo haina hata robo mwaka ni unafiki, kujikweza ili uonekane na wewe umo wakati ni hohehahe wa kutupwa unanunulika kama punda, unapewa peremende na kujilambalamba tu wakati huko kichwani ni boga lililo oza.

Je, tukimuuliza Jambazi Sugu alifanya nini wakati akiwa waziri mkuu anagwaya. Hata huko kungine alikopitia alifanya nini - anagwaya. Je, hawa nguruwe na nyani wameifanyia nini Tanzania? Zero (sifuri) wamekalia majungu, wamekalia ukaskazini, wamekalia ukanda. Ninavyofahamu Jambazi Sugu lilitumia madaraka yake kuwaibia pesa walipa kodi, hatima yake kutoroka yes kutoroka kutoka kuwa waziri kuu maana angejaribu kubaki tu angefukuzwa kama nyani au nguruwe na jela ilikuwa inamngoja. Utajiri wake ni wa mashaka kwa sababu anafahamu yeye ni Jambazi Sugu.
 
BANDARI

Tumeona mfano mdogo sana wa jinsi zoezi la usafi lilivyoshindwa kuwa la kudumu kutokana na mfumo
Hilo si la kipekee, kuna mengi yanayofanana na hilo. Hatuoni, tunafarajika na hatua za haraka

Ndio, hatua za haraka zinahitajika, lakini ziwe za kudumu ili kepuka kurudi myuma
Tumerudi nyuma kwa suala la uhujumu uchumi. Hili lilikuwa zoezi la Hayati Sokoine

Kipindi cha Mwinyi likarudi kwa kasi,Nyerere akasema nchi inanuka rushwa
Kipindi cha Mkapa likatoweka kwa muda, mwish likarudi na nguvu mpya na kasi ya ajabu

Awamu ya nne, stunashuhudia madudu yanayomalzimu Mh Rais kuingilia kati haraka
Ziara ya Bandarini ya waziri mkuu na hatua za Mh Rais kuwawajibisha wateule zinaeleza

Bandari ni eneo la uchumi na usalama wa nchi. Ni 'mpaka' au lango la kuingia na kutoka
Kwa jiografia ya nchi yetu, bandari tu ingekuwa chanzo kikubwa cha mapato

Kwa muda usiojulikana, madudu yameibuliwa yakihusisha makontena na ukwepaji wa kodi wa juu
Kwamba, nchi imepoteza mapato lakini pia linaeleza usalama mzima

Endapo hatujui nini kinaingia au kutoka bandarini na kwingineko, uslama wetu upoje?

Kutokana na umuhimu wa bandari na viwanja vya ndege, kumewekwa ulinzi wa ziada
Kuna kitengo maalumu cha Polisi wa Bandari, kitengo cha mapato TRA n.k

Tuna vitengo kama cha rushwa(PCCB), Polisi na Usalama wa Taifa.
Wapo wakuu wa vyombo vingine kama wizara, bodi n.k vinavyofanya kazi pamoja na hivyo.

Swali la kujiuliza, inakuwaje haya yanatokea na hayakujulikana hadi uongozi mpya?

Tunarudi nyuma kidogo

-Yapo malalamiko ya wananchi kutumia bandari ya Mombasa na si Dar
-Yamekuwepo malalamiko kuhusu 'udalali' uliokuwa unafanyika bandarini

-Yamekuwepo malalamiko ya nchi za jirani kuhusu ubovu wa huduma za bandari

-Vyombo vya habari vilidokeza kuhusu uwepo wa tatizo

-Kitengo cha biashara cha bandari hakikujua na kufuatilia malalamiko haya ya wazi!

Je, tuna ujajsusi wa kibiashara kweli kama haya yanatokea tukiwa na washindani Beira na Mombasa/Lamu

Tiviweke vitengo katika muktadha mzuri. Mamlaka ya bandari, Mkuu wa Bandari, Bodi ya Bandari, kitengo cha biashara, Polisi wa Bandari. Kuna Takukuru,Jeshi la Polisi,TRA, Idara ya usalama, Wizara ya uchukuzi ,n.k

Vitengo vyote vinafanyakazi kila siku, hata hivyo havijui makontena yanaingiaje na yanatokaje kienyeji!!!

Hatuoni tatizo hadi hapo, tunatafuta mchawi

Tuangalie nani anawajibika kwa nani katika hao walioorodheshwa, halafu tujiulize tatizo li wapi na tunayo suluhu?

Inaendelea.....
 
Back
Top Bottom