Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Inaendelea

Kwa kuanzia, tuone namna viongozi wa taasisi tulizotaja hapo juu wanavyopatika

Waziri wa wizara anateuliwa na Mh Rais
Mkuu wa mamlaka ya bandari anateuliwa na Rais
Bodi ya bandari inateuliwa na Rais
Mkuu wa Polisi bandari anafuata ngazi husika na kumfikia IGP anayeteuliwa na Rais
Kitengo cha uslama kina ngazi zake hadi kwa mkuu anayeteuliwa na Rais
Takukuru wana mkuu anayeteuliwa na Rais
Mkuu wa mamlaka ya mapato anateuliwa na Rais
Wapo baadhi ya watendaji wanaoteuliwa na bodi

Katika mfumo wa kiutawala, nani anawajika kwa nani na yupi ni bosi wa nani?

Je mfumo huu tunaouona unatoa fursa ya taasisi kufanya kazi kwa uhuru?

Na endapo mfumo unafanya kazi vizuri, matatizo yanayotokea bandari yanatokeaje?

Je, kwa kuondoa mtu mmoja au wawili hapo juu tunapata jibu la matatizo yaliyopo?

Inaendelea...
 
Kabla hatujajadili maswali katika bandiko hapo juu, tutoke nje kidogo ili kuleta ufahamu Zaidi

Awamu ya nne ilikithiri kuunda tume.Shughuli zinazofanywa na taasisi kama polisi, ziliundiwa tume

Kasi ilianza baada ya sakata la Richmond,ilibainika,tume huru zinaleta 'matatizo' yasiyoarajiwa

Taasisi husika zikawa kama vyombo visivyo na meno au vya kusafisha tu matokeo ya tume.
Tume zikawajibika kwa viongozi na si umma. Hatuwezi kudai taarifa

Mfano,sakata la EPA kama tupo sahihi, iliundwa tume ya mwanasheria mkuu, IGP na mkuu wa PCCB
Hadi leo hatujui matoke au taarifa zilizopatikana kwavile tume inawajibika kwa Rais

Ndani ya serikali wapo wenye nguvu kuliko mamlaka ya umma.wanaziunda kukwepa taasisi husika

Pili, tunakumbuka mgogoro kati ya bodi moja maarufu, waziri na wakurugenzi.
Kila mmoja alitunisha misuli. Bodi i, waziri mkurugenzi wakaendelea na kazi kila mmoja kivyake
Kutunishia misuli kutokana na ukweli kuwa kila mmoja aliwajibika klwa mteule ambaye ni Rais

Hakukuwepo structure iliyoamua nani ni bosi nani anatoa maelekezo na nani anapaswa kuyafuata

Huko nyuma tumesema, kazi ya kiongozi ni kuratibu (coordinate) na si kuamuru (command)

Unapokuwa na vyombo tulivyoonyesha k juu #63 yanatokea afuatayo

1. Vyombo husika si huru kutenda, vinawajibika kwa mtu mmoja vyote kwa pamoja
2. Hakuna uratibu wa shughuli (coordination) anayepaswa kuratibu ni sehemu ya taasisi husika
3 Matokeo ni kuwa na mfumo mfu, yaani usiofanya kazi kama mfumo bali kutegemea amri'command'

Kwa mantiki hiyo, kumuondoa mtu mmoja haijawa suluhu. Kwa mfano, vyombo husika vyaweza kuwa vilifanya kazi vema. Kwavile kila mkuu wa chombo anawajibika kwa Rais hakuna uratibu na kinachotokea ni taarifa kufika eneo moja zikiwa hazina utaratibu,hakuna kazi ya pamoja

Mfano mwingine, kama tatizo ni mkuu wa mamlaka kama TRA, kwanini Polisi, Takukuru, usalama, waziri, bodi hazikugundua tatizo hilo mapema na kuzuia kabla ya athari?

Nini kilizuia vyombo hivyo kufanya kazi kabla Mh Rais haijaingilia kati?
Kwanini kamishna alikuwa na majina hakuchukua hatua?

Na je tunahitaji vyombo visivyoweza kuratibu kazi zake bali kupokea maagizo?

Mfumo mzima umeoza , tunafarijika na viraka vya haraka. Kama mfumo ulifeli ina maana hakukuwa na uratibu na tatizo ni mratibu.Na pia kama vilifeli kwa kutofuata amri kuna tatizo la anaye command

Hatuwezi kumaliza tatizo la TRA au bandari kama tutabaki na mfumo uliopo.

Tatizo si mtu au watu ni mfumo mbaya na hapo ndipo tunatakiwa tubadilike

Tutaangalia maeneo mengine ya shtukiza zikiwemo za mawaziri

Inaendelea...
 
MAWAZIRI NA SHTUKIZA , AMRI NA FUKUZA FUKUZA

BaadA ya baraza kuapishwa, mawaziri wakatawanyika kwa kwa ziara za ghafla
Hata kabla ya kuelewa ukubwa , ugumu au changamoto za ofisi zao, amri zilitawala kila kona

Ni katika mtindo wa kupasua 'majipu' Walifuata 'nyayo' za kiongozi aliyeingia na 'tone' mpya
Tatizo linalojitokeza,maamuzi kutozingatia chanzo cha tatizo.

Haina maana si sahihi, hapana! bali hayaendi mbali kutafuta chanzo na kuzuia

WAZIRI WA ELIMU

Tumeeleza utata wake alipoondoka NECTA kama mkurugenzi mkuu.
Elimu ni suala la kitaalamu. Umuhimu wa elimu kwa taifa hauhitaji kuzungumzwa tena

Miaka 10 iliyopita yalikuwepo maamuzi ya kubadili mwelekeo wa elimu nchini.
Kulikuwa na mradi wa ulioanzishwa na Rais wa awamu ya 4 uliokuwa umeratibiwa japo vizuri

Awamu ya 4 ikaingia na ujenzi wa madarasa ili kuongeza wanafunzi.
Hatua haikuzingatia nini kitatokea baada ya hapo. Je, kuna shule za kutosha kwa masomo ya mbeleni.
Je, kulikuwa na resource za kutosha kwa wakati huo na siku za mbeleni.

Kilichofuata ni ''massive failure'' ya wananfunzi huku CCM na serikali yake wakijivunia namba na idadi

Katika kuficha udhaifu, Seikali ya CCM ikatafuta njia za kisiasa. Kuondoa Divisiob 0 na kwenda GPA ili kuwachanganya wananchi. Muundo wa division ulionekana kuwa wazi zaidi na 'kuharibu' hoja za kisiasa

Katika kukidhi mahitaji ya wingi wa wanafunzi, vyuo vikaota kama uyoga.

Ipo kamisheni ya vyuo vikuu, nayo igageuzwa ya kisiasa na kupokea maagizo badala ya utaalamu

Tukatoa wahitimu hafifu kutoka vyuo vya umma na binafsi vinavyojali faida zaidi ya wa elimu

WAZIRI WA ELIMU ATOA KAULI

Katika mtindo wa Hapakazi, waziri wa elimu ameagiza NECTA kumpa sababu za kufuta division na kutumia GPA. Na ametaka kupata sifa za vyuo vingine vinafundisha na walimu wa viwango vya chini sana

Waziri wa elimu anajua nini kilitokea NECTA na anajua tatizo la Vyuo vilivyoota kama Uyoga.

Hatua anazochukua zinaonyesha weledi wa kitu anachotaka kufanya. Ni hatua za kuungwa mkono

Pamoja na ufuatiliaji na azma njema, kuna tatizo linaloweza kumkwaza!

Tatizo lipo katika utaratibu wa mfumo ambao ndilo tatizo kubwa ingawa tumegoma kuamini hivyo

Tutajadili hili la elimu
 
Ukiona mtu anamshadidia na kumkumbatia Jambazi Sugu, ambaye alikimbia Bungeni baada ya kubadhirika kwamba alikosa maadili ya uongozi na kujitajirisha isivyo halali basi lazima ufahamu ana matatizo sugu (amesheheni peremende kutoka kwa Sugu sasa anajilambalamba tu). Serikali haiendeshwi kutoka mfukoni. Chadema wanaongozwa na majangili ambayo yameiba pesa za walipa kodi walipokuwapo madarakani (EL, S na K). Mbowe ni kuwadi ambaye aliuza chama na kuwaambia wanachama kwamba anawauzia mbuzi kwenye gunia na wao wakakubali tuliokataa tumesepa tumejua ilikuwa janja ya sugura. Wapo waliokubali na ndio hao hao wanalaani Watanzania kwa kumchagua JPM. Walikuwa wanafikiri Watanzania wote ni wajinga kama wao. Inaendelea.
 
WAZIRI WA ELIMU

Bnadiko 65 tumesema Mh Waziri anafanya anachojua.
Matatizo ya NECTA anayajua na kuondoka kwake hakukuwa katika mzingira ya kawaida

Pengine hakukubaliana na utaratibu wa kutumia chombo hicho kuficha uzembe.

Awamu ya nne haikupenda matokeo mabaya. Ndipo ikaamuliwa zitumike GPA ambazo si tu hazina Kiswahili chake, bali hata kwa wasomi zina tatiza kuziipambanua.

Hivi GPA 3.2 kwa mwanafunzi wa kidato cha nne inaeleza nini? Yote ni kufunika uchafu chini ya Zulia

Badala ya kusema sifuri wanatumia 'zero' kama neon. Dvision na GPA hazina maelezo ya kutosha

Kitendo cha Mh waziri kuipa NECTA siku za kueleza kwanini itumie GPA kinaeleza asivyoridhika

Pili, Mh amekwenda shule na vyuo chini ya viwango. Hapa napo inaonekana anapafanhamu vema

Kama tulivyosema, inaonekana anajua anataka kufanya nini. Hakukurupuka , alifanya homework vizuri

MATATIZO
Pamoja na nia njema, Mh Waziri atakumbana na mambo kadhaa yanayoweza kumwakwaza

1. Wakati anaondoka NECTA kulikuwa na shinikizo kutoka sehemu ya jamii.

Ingawa tuhuma dhidi ya NECTA hazikuweza kuelezwa kisayansi na kimantiki, kwa jinsi alivyoondoka ilikuwa ni kama kuna' kuridhia' kutka mamlaka za juu kuhusiana na madai yaliyotolewa.

Hicho kinamuondolea public trust kwa kiasi na pengine kupunguza nguvu ya maamuzi yake.
Yaani anakuwa sensitive na nervous. Kisaikolojia itamsumbua

Anaweza kufanya mabadiliko kuhusu madaraja hilo halina shinda kwa wakati huu,hawapo na si tishio

2. Kuna kundi la 'lobbysit' ,ni kundi masilahi. Lobbyist wapo wa wazi kama tunavyoona makundi ya akina mama, vijana , walemavu n.k.

Kazi yao ni ku influence viongozi wa serikali kuhusiana na masilahi ya makundi yao

Kuna lobbyist wa siri . Kundi hili hutumia sana uwezo wao hasa wa rasilimali bila kutaka kujulikana

Katika nchi za wenzetu lobbyist ni kitu halali na hufanyika kwa uwazi.

Katika nchi yetu ni ngumu kutengenisha lobbyist na mtoa rushwa.
Hatuna utaratibu wa kurasimisha makundi haya

Waziri wa elimu anaweza kukutana na lobbyist wenye masilahi katika sekta ya elimu.
Hawa ni wanamiliki shule na vyuo. Hatua ya Mh kuhoji udhaifu lazima itakutana na kundi hili.

Kitanchoweza kutokea ni lobbyist kumzunguka kwa njia nyingine. Ni hii ya 3 hapa chini

3. Wafanyabishara kuingia katika siasa si kutafuta masilahi au posho.

Ni katika kuhakikisha wana watu, ngazi za maamuzi kulinda masilahi yao

Hapa ndipo CCM inaweza kutumika kulihifadhi kundi hili.

Kwamba, tunaweza kusikia kauli za sera za chama zinakataza kero, ilani inasema ABCD au kufunga vyuo na shue ni kero kwa wananchi n.k. Tunajua Chama kilivyo na nguvu katika maamuzi ya nchi.

Tukumbuke kuwa ni hao hao waliotufikisha katika hali iliyopo ya elimu.

Si kwa bahati mbaya bali kwa sababu maalumu.

Leo wanawezaje kukubaliana na 'sera' tofauti au zinazokinzana na mitazamo yao ya awali tusioijua?

Itaendelea....
 
MFUMO PIA NI TATIZO KATIKA SUALA LA ELIMU

Tumejadili kwa uchache mambo yanayoweza kumkwaza waziri katika azma njema ya kuhakikisha elimu inakuwa kichocheo cha maendeleo

Wengi wanadhani elimu inaishia katika kusoma na kuandika. Kwa uhakika ni sehemu muhimu ya uchumi wa nchi , usalama na ustawi wa jamii. Ni eneo lilisilohitaji mzaha hata kidogo

Ipo kamisheni ya vyuo vya elimu ya juu (TCU) na ipo NECTA inayotahini vyuo vingine, zipo taasisi na mashirika wadau wa elimu lukuki. Ipo wizara husika

Swali la kujiuliza, inakuwaje kuna vyuo visivyofikia viwango? Vilisajiliwa na nani na kwa vigezo gani?

Nani anafanya ukaguzi kuhakiki viwango vinabaki kama vilivyokuwa wakati wa usajili

Je, standards za mazingira, vifaa na Wataalamu vilikidhi haja ya wakati na kuendelea?

Ikiwa chuo hakikidhi haja na kinaendelea kutoa wahitimu kuna tatizo katika system nzima.

Haiwezekani madudu ya vyuo yaonekana wahitimu wanapoingia mitaani
Maana yake hakukuwa na uangalizi au ukaguzi. Na kama ulikuwepo haukuongozwa na weledi

Yote yanatokana na siasa kuwa mbele zaidi ya utaalamu.

Viongozi wa taasisi wanawajibika kwa wanasiasa. Hawana nguvu za 'maamuzi, maono na utendaji' zaidi ya kupokea maagizo.

wanafunzi wanafaulishwa kwa kupunguza viwango vya ufaulu Wanaficha zero na sifuri

Ukisoma Rasimu ya Warioba, kuna kifungu kinachoondoa teuzi nyingi na kuzihamisha kwa tume ya utumishi. Kwamba, kila mmoja angekuwa na 'watch dog' pale panapokuwa na tatizo.

Lakini mwangalizi mkuu ni kiongozi wa nchi na angeweza kusimama na kupokea ushauri wa kitaalam

Leo tunaongelea madudu ya wizara ya elimu. Tunatwisha mzigo kwa vyombo visivyo na uwezo

Tunashindwa kuelewa kuwa mfumo wetu mzima katika mambo mengi ikiwemo hili la elimu ni mbovu

Miezi miwili tu ya kubadili uongozi kila jambo linageuka. Maana yake ni moja, hatuna mfumo unaoongoza haya mambo, kilichopo ni matakwatu.

Hilo linatoa mwanya wa wanasiasa kuchukua sifa badala ya kulisaidia taifa

CCM wanadai miaka 10 tumeshuhudia ongezeko la vyuo vikuu kufikia 50.

Miezi miwili Serikali ile ile iliyotueleza mafanikio inatueleza kufeli kwa vyuo kuwa na viwango duni

Haya ni sehemu ndogo tu ya vikwazo atakavyokumbana navyo waziri

Hatuwezi kufanikiwa katika elimu bila kuwashirikisha wataalamu wa elimu. Hatutafanikiwa ikiwa wanasiasa watabaki kuwa na nguvu za maamuzi katika mambo ya kitaalamu.

Wala hatutegemei mabadiliko ikiwa mfumo uliotufikisha hapa utaendelea kutumika, mfumo unaozingatia maamuzi ya kisiasa zaidi ya kitaalam. Mfumo unaongoza kwa kutumia hoja za kampeni badala ya ustawi wa jamii. Kama hatuoni hili ni tatizo, tuendelee kusubiri

Hatukujifunza kutokana na yale ya UPE, tusubiri kuvuna mabua


Tutaangalia eneo lingine
 
TUANGALIE MAELEZO YA Mh WAZIRI KUHUSU MFUMO

Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi
Serikali yafuta GPA katika elimu, yarejesha divisheni

Waziri wa elimu anaeleza NECTA ilivyoshindwa kuja na majibu ya GPA.
Anasema baadhi ya watahiniwa wa GPA wanaonyesha kiwango kidogo kuliko GPA zinavyoonyesha.

Hoja hii inathibitisha kauli yetu kuwa, GPA iliwekwa kufunika uchafu kwa kutumika kisiasa

Waziri anaendelea , NECTA walimweleza kuingia katika mfumo huo kunatokana na hoja za wadau.
NECTA ikashindwa kuthibitisha ni wadau wapi na katika mikutano au mikusanyiko gani

Hapa inaonyesha NECTA inadanganya. Hiki ni chombo kinachosimamia elimu, moyo wa Taifa lolote

Chombo hiki kinapokuwa cha kibabaishaji inatia hofu na ni hatari kama waziri alivyosema pia.

Waziri ameendele kusema, mfumo huo haukupitia kwa kamishna wa elimu kupata kibali.
Maagizo ya serikali yanasema kila kitu kianze kutumika JUNI 2016

Tunaona ushiriki wa serikali kwa kutoa siku ya kuanza kutumika mfumo.
Wakati kamishna hakutoa kibali, haieleweki serikali ilitoa vipi agizo

Waziri anasema kanuni za mitihani zilipitishwa miaka 2 baada ya kuanza kutumika utaratibu wa GPA

Kanuni zilipitishwa na waziri Oktoba 28,2015 (kipindi cha uchaguzi) na kuingizwa katika gazeti la serikali November 6, siku ambayo Rais Mpya alikuwa na siku 1 tu ofisini

Tunachokiona ni mfumo mbaya, si wa elimu ni wa ujumla. Baraza la mawaziri linapaswa kuvunjwa isipokuwa kwa dharura tu. Waziri anapopitisha kanuni Oktoba 28,2015 kura zikihesabiwa kuna tatizo.
Yaani waziri alikuwa kazini hadi uchaguzi ulipomalizika

Kwa maneno mengine, kuna uwezekanO alifanya hivyo kwa shinikizo la watu.
Elimu na mitaala au mitihani si suala la dharura, kwanini waziri afanye yote akijua huenda asingerudi?

Kitu tunachopaswa kuelewa ni jinsi ambavyo maelezo ya waziri yanavyochanganya.

Kuna maeneo anaitetea serikali, na maeneo mengine serikali ikionekana kushiriki.

Hivyo, tunaweza kusema NECTA walifanya kazi na serikali ina a way, ingawa wadau wakuu kama kamishna wa elimu hawakushirikishwa

Haya yanatokea kwa sababu hatuna mfumo mzuri wa utawala,inaonekana wazi katika sakata la elimu

Mambo yanafanyika gizani kiasi cha waziri kutoweza kuelewa Ilikuwaje, hawezi ku trace nini kilifanyika

Lakini pia waziri aliambatana na Mkurugenzi wa NECTA. Akiwa naye, mh alisema maelezo aliyopewa NECTA kuhusu GPA yalikuwa ya bla bla.

Maana yake maeelezo ya mkurugenzi hayakumridhisha bali ubabaishaji
Laiti waziri angekuwa na nguvu juu wa mkurugenzi, pengine asingetokea naye kwenye mkutano

Mkurugenzi anateuliwa na chombo kingine hivyo waziri hana la kufanya isipOkuwa kushauri tu

Mfumo unakwaza viongozi kiutendaji. Ni kama ule wa Bandari tulioona watu Zaidi ya 4 wanateuliwa na mamlaka moja wakiwajibika kwa mamlaka hiyo na kila mmoja kuwa 'bosi' kivyake

Hili la elimu linaeleza wazi kuhusu mfumo. Tunarudia, kama waziri ambaye alikuwa Mkurugenzi wa NECTA miaka miwili iliyopita haelewi nini kimetokea, nani nje ya system anayeweza?

Je, Watanzania hatuoni tatizo letu kama mfumo na si mtu au watu?

Taasisi zinafanya kazi bila kujua moja infanya nini. Maamuzi yanapitishwa kisiasa, wengine kutoshirikishwa pengine kwa hofu ya 'ukaidi'.

Serikali iliridhia vinginevyo kwanini itangaze jambo isilokubaliana nalo?

Tutaendelea...
 
WIZARA YA AFYA

Wimbi la mawaziri 'kuvamia' maeneo au timua timua linapamba moto. Hii ni kufuatia kauli mbiu ya Hapakazi

Waziri wa Afya alifanya ziara ya Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Waziri alikiri gharama za manunuzi ya dawa ikilinganishwa na bajeti. akamuondoa Mkurugenzi kwa ''mwingiliano wa masilahi''.Haikufafanuliwa ni mwingiliano upi

Hatua ya waziri inafuatia ya Mh Rais aliyemtimua Mkurugenzi wa Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili

Katika mazingira yote mawili ya Muhimbili na Ocean Road tuangalie japo kidogo nini hasa kilitokea

Siku za nyuma Muhimbili iligeuzwa kuwa shirika ili kuwa na bajeti yake kutoka wizarani na kuipa nguvu ya maamuzi kama shirika. Ingawa bado serikali ilikuwa na mkono katika uteuzi wa wakuu na bodi, au bajeti

Muhimbili: Huduma ni hafifu kutokana na ufinyu wa bajeti na Urasimu wa kupata rasilimali

Awamu ya 4, Muhimbili ilidaiwa Bilioni 10 za dawa ambazo zilikwamisha huduma
Katika Awamu hiyo Mabilioni yalitumika kwa mambo mengine yasiyo na tija

Mfano, Bilioni Zaidi ya 100 za bunge la katiba zilitoka wapi ikiwa Muhimbili haikuweza kupewa bilioni 10?

Mbona hatujawahi kusikia Bunge na Wabunge wakikosa pesa kama taasisi hizi za huduma kwa Taifa?

Kwa hali hiyo, kukosekana kwa fedha ni zao la kutojali au kutotoa kipaumbele kwa huduma za jamii

Wagonjwa kukosa dawa au kulala chini au vifaa kutofanya kazi ni zao la uzembe na hujuma

Uzembe: Taasisi husika zina wateuliwa wa Rais wakiwemo wajumbe wa bodi. Kufeli kwa taasisi kunatueleza kufeli kwa Serikali. Si suala la mkurugenzi au wajumbe wa bodi, ni mfumo mzima uliofeli.

Kumuondoa Mkurugenzi kunaweza kuwa kumetokana na uzembe katika utendaji wake na bodi husika
Hata hivyo lazima tujiulize, kama tatizo lilikuwa ni MRI na vitanda, je ni kosa la mkurugenzi?

Mkurugenzi alipewa rasilimali za kutosha katika kuetekeleza majukumu yake?

Mkurugenzi anaomba pesa wizarani, ambako kuna mlolongo kupitia hazina n.k.
Ikiwa hakupewa fungu, kosa lake ni lipi?

Na je waliozembea katika kutoa fungu wakiwemo watu wa wizarani na hazina wamechukuliwa hatua gani?

Tunasema hivyo kwasababu, baada ya uteuzi wa mkurugenzi mpya, kilichofuata ni serikali kuagiza pesa zitoke
Kazi iliyosimamiwa na katibu mkuu kiongozi.

Hapa tu kuna walakini. Katibu mkuu kiongozi ni mkuu wa utumishi serikalini.
Kwanini ahangaike 'kubeba' vitanda ikiwa yupo mkurugenzi mpya, katibu mkuu wizara n.k.?

Ilikuwaje mkurugenzi aliyeteuliwa apewe fungu la kazi na tulitarajia aliyekuwepo angefanya kazi vipi?

Ocean Road: Nako waziri kamtimua Mkurugenzi kwa mwingiliano wa masilahi. Hakubaini uzembe au wizi

Ilipaswa waziri ajiridhishe uwepo wa mwingiliano huo kabla ya kuchukua hatua
Hizi habari za kusikia na kuchukua hatua bila kuwa na ushahidi hazileti sura njema

#Hapa kazi inaweza kutumiwa vibaya kama tunavyoona.

Tulitegemea mtu anaposimamishwa kazi zipo sababu za kujitosheleza, si kumsimamisha halafu sababu zitafutwe

Ocean Road na Muhimbili ni taasisi kubwa zinazopaswa kuangaliwa kwa ukubwa wake na si mtu mmoja mmoja

Kwasababu tuna mfumo dhaifu wenye mapungufu, kinachotokea si kutafuta suluhu, ni kuhangaika katika hali ya mparaganyiko. Tunasukuma matatizo ya mfumo kwa watu tukidhani tunatafuta suluhu

Tutaendelea...
 
MUHIMBILI ,OCEAN ROAD. KWINGINE JE!

ANGALIA 'MVURUGANO' WA NEC/TAMISEMI NA CHAGUZI


Tumeona yalitokea Muhimbili na Ocean Road katika kasi ya Hapakazi.
Wengi wamefurahia hatua hiyo , Kuna sababu za kufarahia, ikiwemo hali mabya iliyokithiri katika maeneo hayo

Hatujiulizi,hatua za kuondoa wakurugenzi zitatoa jibu la tatizo, pengine Wakurugenzi hawana makosa.
Ikiwa hawana rasilimali fedha tunatgemea wangewezaje kutekeleza majukumu?

Hatujiulizi je, hatua hizo zitazaa matunda katika hospitali nyingine za rufaa nchini?

Mtiririko ukiwa mbaya suluhu ni kuangalia wapi tatizo lilipo.
Je, ni wizarani Hazina au uzembe tu wa viongozi kutotumia mafungu kama inavyopaswa?

Ukitaka kuona mfumo wetu ulivyo na matatizo, chukua muda usome hapa

Wabunge Viti Maalumu ruksa udiwani

Mfano huo ni mzuri sana ukiangaliwa kwa upana wa maeneo mengine

Uchaguzi wa serikali za mitaa upo chini ya Wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi)

NEC inashughulikia uchaguzi wa Wabunge na Rais.

Uchaguzi mabaraza ya madiwani baadhi umegubikwa na matatizo ya ushiriki wabunge-viti maalumu.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa uchaguzi NEC, wabunge viti maalumu wanatambuliwa na sheria za Tamiseni kama sehemu ya mabaraza ya madiwani

Hivyo suala la wabunge wa viti maalumu kuwa wajumbe wa mabaraza ya madiwani ni halali

Mkurugenzi anasema, uthibitisho wa makazii unafanywa na NEC,Tamisemi haina uwezo huo

Kwa mtazamo ,chaguzi za Tamisemi zisizohusisha NEC zinaihusisha NEC katika mazingira tatanishi

Tumefanya chaguzi za serikali za mitaa na serikali kuu miaka mingi

Chaguzi zinazosimamiwa na Tamisemi zina searia zake.

Leo tunaambiwa sheria zina mapungufu haziwezi kuthibitisha maeneo ya wabunge wa viti maalumu

Ili kupata suluhu NEC isiyohusika na chaguzi za Tamisemi inaingilia kati

Tunachokina ni kuchanganyana na kuvurugana.Sheria na taratibu zinabadilika kulingana na 'mazingira'

Hakuna uwazi wa mipaka kati ya Tamisemi ya serikali na NEC tume huru

Baadhi ya nyakati NEC hawahusiki, ghafla wanahusika.

Ni kitu gani kinaendelea hapa na kinasababishwa na ni?

Hili tu linaonyesha jinsi mfumo wetu wa kujitawala ulivyo dhaifu na usivyoweza kujisimamia

Mvurugano hauiishi Tamisemi na NEC, ndivyo ilivyo katika taasisi nyingi zikiwemo za afya

Tutaangalia hatua za wizara ya afya kufungia wafanyakazi nje

Inaendelea...
 
Wanajamv
Tulipoanza mabandiko kuhusu awamu ya 5 , tulipitia kwa uchache wizara na mawaziri
Tulifanya hivyo tukijua mbele ya safari na muda mfupi yatatokea tunayoyaona ingawa wengi hawayaoni

Vurugu za bungeni leo tuliwahi kuonya kuhusu waziri Nnauye katika bandiko hili hapa chini
WIZARA YA HABARI ,UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari: Ni eneo linalotumika kwa mawasiliano ya jamii, mtu, watu, taasisi, vyama au serikali. Napo kuna tatizo, wengi wanadhani idara ya habari kazi yake ni kueleza tu au kutoa maelezo tu

Idara inahusisha mawasiliano ya njia mbili (two ways) ya kupata na kutoa habari.
Katika hilo ni pamoja na kueleza, kutafasiri maelezo, kuyafafanua katika kiwango kinachoeleweka na rahisi

Wizara hii ni muhimu katika maeneo yote.. Kwa upande wa serikali, ni chombo kinachoIunganisha wananchii, taasisi za ndani au nje, na serikali na serikali

Kuna nyakati inatumika kama chombo cha 'propaganda' cha serikali., zinazoweza kutetewa kimanti, busara na hoja

Tofauti na propaganda za siasa, habari za serikali zinahitaji umakini.
Tamko la wizara ni tamko la serikali na nchi kwa ujumla.

Ni taarifa zinazoweza kuleta mitafaraku au neema kutegemea zinazvyotolewa

Waziri ni Mh Nape Nanuye(MB) wa Mtama aliyekuwa katibu mwenezi wa idara ya itikadi na uenezaji ya CCM wa serikali ya awamu ya nne.

Akiwa mwanahabari, mh ana uzoefu wa kuongea na vyombo hivyo

Hata hivyo, uzoefu katika siasa za chama ni tofauti na za serikali.
Taarifa au maelezo ya vyama hayana uzito kwa kwavile ni sehemu ya propaganda za kisiasa

Taarifa za serikali au maelezo yake ni habari za nchi bila kujali itikadi za kisiasa.
Ni msimamo wa nchi na Taifa inayoweza kujenga au kubomoa

Kwa mfano, Mh Nape aliwahi kusema CCM itashinda hata kwa bao la mkono.

Kauli ni ya kisiasa na kichama imeendelea kuweka doa juu demokrasia nchini.
Katibu mwenezi anapotoa kauli hiyo inaleta hisia mbaya katika jamiii

Majuzi Mh Nape alikaririwa 'hali ya nchi ilifikia pabaya' kwa kuangalia mambo yaliyoibuliwa na serikali ya leo.

Tofauti ya kauli hizo mbili ni kubwa

Kauli ya chama inachukuliwa na alieleweka anatetea chama licha ya walakini.
Kwa mfano, hajawahi kueleza vita yake na mafisadi kwanini ilikwama

Kwasasa Mh ni waziri,kuelewa tofauti ya kauli za kichama na serikali ni muhimu.

Wizara ni kiungo katika habari na wizara au taasisi nyingine za ndani na nje.
Maelezo yanapaswa kupimwa na kuelezwa kwa ufasaha, linahitaji umakini na mtu makini

Je, tutakuwa na chombo cha uhakika cha habari au ni mwendelezo wa propaganda kama tulizoona awamu ya nne?
Vurugu za bunge ! Inaendelea...
 
Mkuu Nguruvi3

Nape hakupewa ile wizara kwa bahati mbaya, Kawekwa pale kwa makusudi maalum na haya ndio matokeo tunayoyaona sasa. Anatumia vyema nafasi yake ya u-katibu mwenezi wa CCM akiwa waziri anayesimamia sekta ya habari! Magazeti yanayoandika habari zisizoipendeza serikali yanafutwa, TBC inazuiwa kutangaza bunge live... na bado tutaona mengi! Ukichanganya sarakasi hiyo na ile ya Mzee wa VIJISENTI kupewa uenyekiti wa bunge unaweza kupata picha kamili ya nini tukitarajie miaka 5 ijayo. Sina hakika kama haya yote yanafanyika kwa baraka za Bwana Mkubwa wa Jumba Jeupe au Mwenyekiti wa Chama kutoka Lumumba lakini one thing for sure ni kwamba wamejizatiti kuzima mijadala yoyote itakayoumiza chama tawala!
 
Mwalimu pitia kwanza video hiii
TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (LIVE)

Tumeandika kuhusu uteuzi wa Nape. Uzoefu wa chama si uzoefu katika serikali.
Tukaendelea kusema, Awamu ya 5 ipo katika mashaka makubwa katika eneo la habari

Ukisikiliza video , Nape anasema TBC imeondoa baadhi ya vipindi 'live'
Anasema gharama za TBC zinafidiwa na matangazo madogo asilimia 75 ni elimu ya umma na 25 ni burudani
Matangazo yalisitishwa 'live' juzi na jana alishapata habari wananchi wamefurahia
Anadai, kuonyesha 'live' watu wapo katika ujenzi wa Taifa ni tatizo vipindi vitaonyeshwa saa 4-5 usiku , muda watu wengi wanapoangalia TV

Tuzipitie hoja za Waziri wa habari na michezo kama tulivyoziorodhesha hapo juu

1. Kuondoa matangazo 'live' hilo wameondoa kabisa. Hatuna tatizo na kuondoa bali kauli yenye ni hila

2. TBC inajiendesha kwa matangazo madogo Nape hakusema inapata ruzuku asilimia 100 na ''monopoly''

3. Kama asilimia 75 ni vipindi vya elimu kwa umma, maana yake TV ni muhimu na 4 Bilioni si tatizo

4. Eti matangazo yamesitishwa juzi, jana keshafanya tathmini na kubaini watu wengi wamefurahia.

Haya hayawezi kuwa maneno ya serikali. Waziri hana takwimu, hata akiwa nazo masaa 10 hayatoshi kutathmini. Ni propaganda na udanganyifu unaokera na kuudhi umma. Kulifanya Taifa la mabwege

Waziri anasimama bungeni kueleza jambo bila takwimu wala ushahidi

5. Hana takwimu za kuonyesha rating wakati wa 'live' na wakati wa kurekodi.

Akiwa waziri hana mamlaka ya kuelekeza umma ni muda gani watazame TV.

Wapo wanaoangalia TV saa 10 usiku, saa 6 mchana kutegemeana na staili ya maisha na si jukumu la waziri wa habari kujua hilo. TV zinafanyakazi saa 24, Mbona hajauliza usiku wa manane nani anasikiliza radio au TV wakati watu wamelala

Haya ni mambo yasiyo na takwimu/ushahidi wa kutosha bali propaganda za kuufanya umma wajinga

6. Anasema saa 4 had 5 ni muda mzuri wa kuonyesha vipindi vilivyoripotiwa

Waziri hatambui ndio muda watu wanajiandaa kupumzika ili kuamaka Saa 11 kuwahi foleni

Ni muda ambao mzazi anafanya maandalizi ya watoto baada ya wao kupumzika kwa siku inayofuata

Ni wakati wanafamilia wanajadili mambo mengi yanayohusu maisha yaliyotokea au yatakayotokea

Waziri wa habari haelewi utazamaji wa TV unaambatana na masuala mengine ya kijamii.

Ukitazama, alichokifanya ni kuleta propaganda za CCM katika masuala yanayogusa maisha yetu.

Hatudhani 'live au recorded ' ni tatizo. Kinachoudhi/kukera wananchi ni jinsi wanavyofanywa mazezeta

Hili limeamsha hisia na hasira kutoka kwa wananchi

CCM inachukiwa na umma na waziri anafahamu kwa ushaidi.
Serikali tayari ina migogoro na wananchi kwa baadhi ya hatua inazochukua.

Haya yote yanajenga hasira na chuki kwa Rais na CCM

Wananchi wanapomsikiliza katibu mwenezi wa CCM ambaye ni waziri akidanganya, akibadili kauli na kuficha ukweli, akiingilia taratibu za maisha yao, wanaiona serikali kwa jicho la CCM

Tulisema kauli za Nape zitazua matatizo kwa serikali na hilo linaanza kuonekana mapema
Ni vema angebaki katika siasa za chama ambako propaganda zinaishia kwa wanachama wake

Wananchi wanakumbuka '' goli la mkono'' na ile ya majuzi ' serikali ilifikia pabaya sana''
Katika hali ya kawaida, waziri anaamsha chuki na hisia

Kauli zake zinamweka Rais katika mazingira yasiyotarajiwa.
Kwamba, makovu ya uchaguzi hayaponi kama tunavyoona bungeni.

Rais anapata taabu ya kuunganisha taifa kwasababu ya kauli kama za Mh Nape

Mzozo bungeni umesababisha hotuba ya Rais kutopata usikivu na kujadiliwa kwa heshima na kina

Zile propaganda na kauli tulizosema zitaiumiza serikali tulimaanisha haya. Nape anaumiza serikali

Ameanza kuligawa bunge,hotuba ya Rais imekosa heshima stahiki na Taifa limegawanyika

Chuki dhidi ya CCM zinazidi kupanda, makovu ya uchaguzi ''yanavuja damu'' na serikali inadhalilika

Kama Rais angependa utulivu katika kazi zake, kuliunganisha Taifa kama kitu kimoja na kujenga ustawi wa jamii yetu, Waziri wa habari ni JIPU linalohitaji uharaka kulishughulikia.

Vinginevyo tusubiri makubwa zaidi

Tusemezane
 
WAZIRI WA HABARI NA WAZIRI MKUU WANAPOFUKUZA WATEJA
LA TBC LIMEKERA UMMA, LINAFICHUA MENGI


Tangu waziri wa habari alipoleta mzozo bungeni na taifa kwa ujumla , mengi yanazidi kujulikana

Mbunge wa Uzini, Mh Ali Salehe amekaririwa na gazeti Nipashe akisema Nape Nnauye aliandika katika face facebook June 2013 akishauri matangazo ya moja kwa moja yazuiliwe

Kwa vile mfumo wetu haupo sawa, wazo la mtu linaweza kuingia katika maisha ya jamii bila kufanyiwa utafiti, au majadiliano kuangalia umuhimu, hasara, na uzito wajambo.

Leo tunaona kumbe ni wazo la mtu lililogeuzwa kuwa la umma.
Kwa mfumo , vyombo vya umma havina miongozi (guideline). Inashangaza waziri wa habari kuwa msemaji wa TBC.

Shughuli za bunge ni za mhimili mwingine huru, vipi leo serikali inashupalia suala hilo ?

TBC INAPATA RUZUKU NA KUONYESHWA NA TV ZOTE

Sheria ya mamlaka ya utangazaji inalazimisha wenye ving'amuzi waweke channel ya TBC bila malipo.

Kwa maana nyingine TBC inarushwa na vituo vingine bure, ikipata ruzuku na kuendelea na ushindani wa biashara. Katika mazingira haya, hivi TBC inahitaji kubebwa kwa njia zipi kiasi cha kukosa bilioni 4?

TBC inaposhindwa kulipa kiasi cha bilioni 4.2 alizosema Nape ni aibu kwa kituo na Taifa.

Ni aiibu gazeti Nipashe la June 30' 15 linaonyesha serikali kulipa Bilioni 70 za posho za wabunge sitting allowance

Vipi serikali ishindwe bilioni 4 takribani 1/16 ya posho za wabunge?
Kwa maneno mengine watu milioni 45 hawana sababu za kufadika na huduma hiyo muhimu

Wengi wakiwemo wataalamu wa teknolojia ya habari wanahoji namna bilioni 4 zilivyopataikana
Wanahoji kwa nguvu kabisa maelezo yatakayoonyesha jinsi bilioni 4 zilivyofikiwa na waziri wa habari

SERIKALI YAZIDI KUIMALIZA TBC KIBIASHARA
Endapo lengo ni kuhakikisha TBC inajenga uwezo wa kujiendesha(pamoja na monopoly na ruzuku), kauli ya waziri mkuu kuunga mkono kauli ya waziri wa habari inazidi kuimaliza TBC

Wote wanasema vipindi vya mchana havitazamwi na watu kama mama lishe, boda boda n.k. kwavile wapo kazini

Kubadili kauli kunatokana na kubanwa katika suala la gharama. Ni wazi TBC ina 'advantage' kwa kutangaza kupitia ving'amuzi vya watu binafsi na ruzuku ya kodi za watanzania

Hapa ndipo serikali inapobadili mwelekeo unao iumiza TBC kibiashara

Tutafafanua

Inaendelea.......
 
YASIYOTAKIWA KUONEKANA BUNGENI YAONEKANA

'FOCUS' YA KUDHIBITI HABARI YAISHIA NA UMBUKO LA SERIKALI

Umbuko la serikali! wastaafu, wazoefu watia aibu


Tumeangalia hoja zinazopelekea serikali 'kudhibiti' habari za bunge. Hoja za utetezi hazina mashiko

Kwa muda wote serikali kwa kutumia 'mamlaka ' imezuia hoja za wapinzani kupitia miongozo ya kiti
Wapinzani wakiwa na nia njema kujadili suala lenye masilahi kwa taifa. wakatolewa nje

Ikaja hoja ya kawaida ya mpango wa pili wa maendeleo na mweleko wa maendeleo
Kama kawaida kiti kikapuuza hoja za Mh Zitto na Tundu Lisu za kuomba mwongozo

Mwisho wa siku bunge likajikuta likiahirishwa na serikali kuamriwa kuleta mpango wa pili wa maendeleo kama sheria inavyosema. Hoja zilikataliwa na kiti kwasababu tu zimetoka kwa wapinzani

Kilichotokea ni kukiri makosa ya serikali , kwa jambo ambalo halikuhitaji ushabiki wa vyama
Mh Lisu na Zitto walitaka muongozo si kwa masilahi ya kisiasa, bali kusimamia serikali itimize wajibu

Umbuko la serikali linaeleza ni kwanini haitaki shughuli za bunge ziwe wazi

Kilichotokea katika uwasilishaji wa mpango wa maendeleo kinaonyesha hali ya watendaji wa serikali
Siku chache tu, wabunge na mawaziri wa CCM walikuwa 'busy' wakisifia hotuba ya Rais

Waliomba Rais aungwe mkono na kusaidiwa katika jitihada anazoonyesha
Kinyume chake, wanaotakiwa kuonyesha mfano kwa vitendo hawajui nini wanachopaswa kufanya

Mwenyekiti wa bunge ni mwanasheria mkuu wa serikali mstaafu,alizuia mwongozo wa Zitto na Lisu

Pengine angaliwasikiliza bila kuwa na 'prejudice' ya upinzani serikali isingeumbuka kiasi ilichoumbuka

Mwanasheria mkuu wa serikali wajibu wake ni kuiongoza serikali katika mambo ya sheria.
Rais alipoapishwa, naye kumwapisha makamu wa Rais, aliyefuata ni mwanasheria mkuu

Kwanini mwanasheria mkuu? Ni ili aweze kuongoza serikali katika mambo ya sharia

Inapofikia wapinzani wanaelekeza taratibu zilizopaswa kuelekezwa na mwanasheria mkuu, inafikirisha

Waziri wa fedha alikuwa mkuu wa kitengo cha mipango ya maendeleo katika awamu ya nne.
Hakuna shaka anajua taratibu na tofauti za mipango ya maendeleo na mwelekeo wa maendeleo. Ilikuwaje hakuona tatizo katika jambo alililokuwa analifanya miaka michache iliyopita?inafikirisha

Mwenyekiti wa kamati ya bajeti ya bunge alikuwa waziri katika awamu ya nne.
Naye kama wengine anajua taratibu za kuwasilisha hoja za serikali. Akiwa mwenyekiti wa bajetialip aswa kuliona tatizo mapema na kumshauri waziri wa fedha. Mwenyekiti hakuweza, inafikirisha

Waziri mkuu, kiongozi wa serikali bungeni alikuwepo. Ndiye msimamizi wa mawaziri na shughuli zote za serikali . Kama mwenyekiti wa bajeti, alikuwa waziri awamu ya nne. Taratibu anazielewa, ilikuwaje?

Spika wa bunge alikuwa naibu Spika awamu ya nne. Taratibu za kuwasilisha hoja, miswada na anazijua . Ilikuwaje wakati wa kupanga utaratibu wa bunge hakuliona tatizo! inafikirisha

Naibu Spika hakuwahi kuwa mbunge kabla. Hajakaa katika nafasi yoyote bungeni hadi alipoteuliwa na kisha kuchaguliwa kuwa naibu Spika.

Hata hivyo, alikuwa ni mwanasheria mwandamizi katika ofisi ya mwanasheria mkuu.
Ni msomi aliyebobea katika fani ya sheria. Ilikuwaje hakuona tatizo hilo? Inafikirisha

Bunge lina waratiu wa shughuli. Wengi walikuwepo awamu zilizopita,hawakuwa na habari! inafikirisha

Swali la kujiuliza, haya yote yanatokea kwa nini?

Je, tunajifunza nini kuhusiana na mauza uza haya tukiambatanisha na jitihada za nguvu za kuondoa matangazo kwa wakati ili yakahaririwe kwanza?

Kimetokea nini Wabunge wa CCM kuiadhiri serikali mapema kiasi hiki?

Tutajadili
 
MAGUFULI NA MABADILIKO NDANI YA CCM

'ESTABLISHMENT' WA CCM WAANZA KUJIPANGA

NIA IKIWEPO, DHAMIRA IMEZINGIRWA


Rais Magufuli aligombea akiwa na kauli ya mabadiliko ndani ya chama.
Anaamini, CCM inahitaji mabadiliko baada ya kuchokwa . Chuki dhidi ya CCM alikumbana nazo dhahiri

Nia ya mabadiliko 'inaweza'kuwepo, dhamira imeshazingirwa na huenda nia ikatoweka
CCM ina 'wenyewe' ambao hutumia chama katika kudhbiti nyendo zozote zinazotishia masilahi yao

Rais anapotaka maouvu yafichuliwe, wakati wapo wanaojitahid yafichwe, kufanikiwa kuko wapi?

Jitihada zinaendelea kumaliza makali ya bunge. Kamati za bunge ambazo kimsingi zingemsaidia Rais kujua majipu yapo wapi zimeundwa kuhakikisha mambo ya serikali yanaishia ndani ya chama.

Tunakumbuka kauli ya 'watu wanaokiabisha chama' kwa kuibua kashfa

Tunashuhudia jithada za kupanga kamati za bunge.
Viongozi wenye kashfa za kutosha wamechukua sehemu ya uongozi .

Katika kulinda masilahi na kujijenga, nguvu na hoja za kibabe zikitawala na kupoteza uelekeo kwa serikali kuumbukai. Nguvu kubwa inatumika kuhakikisha chama hakiwagusi

Malumbano ya bungeni sehemu kubwa yanachangiwa na 'establishment' wanaotaka nafasi katika chama. Kwamba, waonekane wanamudu bunge kwa 'kuhifadhi' serikali na aibu zisizotakiwa kuanikwa

Kundi la CCM linalojijenga bungeni ni lile liloathirika na maamuzi ya bunge.
Linajijenga likujua muda si mrefu litatwaa uongozi na kudhibiti 'mianya' inayotishia masilahi yao

Katikan kipindi kuelekea mkutano mkuu wa CCM wa kumkabidhi uenyekiti Mh Magufuli, tayari makundi yanayokinzana na 'nia' ya Rais yameshaanza kujijenga.

Ujenzi umeanzia bungeni, kisha mkutano mkuu, NEC na kisha CC ya CCM.
Mwisho wa ujenzi ni Mh Magufuli kujikuta ana chama kinachodhibitiwa na wasio amini nia yake

Ikifika hapo, nia inabaki kama jina kwasababu dhamira itakuwa imezungukwa na kuwekewa uzio

Kama Rais ana nia ya dhati kukabiliana na maouvu kama inayoungwa mkono na wananchi, aanze kuyadhibiti makundi kama hili la bunge.

Ingawa linaonekana kama linatetea serikali ya CCM, dhaimira nyuma ya kundi hili si njema.

Hatua za kuvunja kamati, kubadili majukumu na kuweka watu wanaotiliwa shaka ni njia ya kuficha maovu. Tujiulize, kwani nia ya Rais ni kuficha maovu? Kwanini anatumbua majipu kama hilo ni lengo?

Na majipu atayaonaje ikiwa hakuna wa kumuonyesha au wapo wanaoficha?

Rais aangalie kundi hili la bungeni linalojijenga taratibu.

Siku ''litakapomzingira'' kupitia chama atajikuta ana chama kama jina,wadhibiti ni wengine.

Nia yake nzuri itakuwa imezingirwa na hapo ni kushindwa tu

Kundi la CCM bungeni linataka kuficha nini? Lina nia njema? Lina dhamira njema? Linamsaidia Rais?

Tusemezane
 
Nguruvi3,

Naendelea kufuatilia kwa makini uchambuzi wako, hakika ni darasa kubwa na lamuhimu sana. Ukitaka kushangaa kizazi cha sasa hutaona wengi wakichangia maoni uzi huu, na baadhi kama rafiki yetu kuchangia kwake ni kejeli/matusi nk

Kwa idhini yako Mkuu,naomba nikusanye uchambuzi huu pamoja ili niweze kujisomea/kutafukuri zaidi siku zijazo.
 
Nguruvi3,

Naendelea kufuatilia kwa makini uchambuzi wako, hakika ni darasa kubwa na lamuhimu sana. Ukitaka kushangaa kizazi cha sasa hutaona wengi wakichangia maoni uzi huu, na baadhi kama rafiki yetu kuchangia kwake ni kejeli/matusi nk

Kwa idhini yako Mkuu,naomba nikusanye uchambuzi huu pamoja ili niweze kujisomea/kutafukuri zaidi siku zijazo.
Ahsante na wale wote wanaotutia moyo

Mkuu chochote utakachopata hata kama ni neno moja, tumia popote bila shaka yoyote
 
ZOGO LINALOHUSU ZIARA ZA RAIS NJE YA NCHI

Zogo linaloendelea bungeni na mitandaoni kuhusiana na Rais kutosafiri nje ya nchi
Ni mjaladala mpana unaochuuliwa kirahisi. Kuna makundi 2 yanayopingana bila mantiki au hoja

Kazi za Rais kama mkuu wa nchi pamoja na mengi mengineyo, ni alama ya Taifa.
Hakuna Rais aliyetawala nchi hii bila kusafiri

Mjadala unaanza awamu ya 4 ambayo safari za Rais zinahojiwa , kwanza kwa wingi na pili mantiki

Hapo ndipo mjadala unaposhindwa kuelekezwa sehemu husika, yaani kati ya wingi,mantiki na ubora

Safari za kiongozi wa nchi zina gharama kubwa. Ukubwa wa safara unapoongezeka gharama zinazidi

Msafara wa Rais unaandaliwa katika mambo mengi. Miongoni ni idadi ya msafara kwa kuzingatia umuhimu wa wanamsafara ukiachilia mbali wanaokwenda kwasababu ya majukumu yao ya kawaida

Pili, uratibu wa safari hufanywa ili kiongozi akamilishe majukumu mengi kwa wakati mmoja

Tatu, huandaliwa kwa kulenga kitakachopatikana iwe moja kwa moja au kupitia ziara hizo

Orodha ni ndefu na inaendelea kulingana na taratibu za kidiplomasia

Wakati wa Mwalimu, ziara ziliambatana na mikutano na shughuli nyingi kwa wakati mmoja.

Mathalan, akiwa UN, utasikia kakutana na viongozi wa NAM, viongozi wa Frontline states n.k.

Katika awamu ya nne, Rais aliweza kufanya ziara mbili au tatu eneo moja na zingine zikiwa ni shughuli za zilizoweza kumalizwa na waziri wa mambo ya nje au wanadiplomasia

Waziri wa awamu hiyo aliwahi kusema' Tunapishana angani kama vile Tanzania inawaka moto'

Hilo likamsukuma Rais Magufuli kutoa maagizo baadhi ya shughuli kufanywa na mabalozi.

Pengine kumpa majukumu waziri wa mambo ya nje ambaye ni mzoefu katika diplomasia ya kimataifa

Si lazima Rais asafri kama hakuna ulazimu au kazi maalumu zinazomhitaji nje.

Hilo tu linaokoa pesa nyingi tukizingatia gharama za msafara na muda wa majukumu yake.

Na pia, si lazima Rais asafiri ikiwa majukumu na malengo yanafikiwa kwa mujibu wa masilahi ya nchi

Wingi au uchache wa safari hauwezi kuwa kigezo cha diplomasia au ufanisi wa Rais.

Mantiki na ubora ni kigezo muhimu kupima ufanisi na ubora wa safari husika bila kujali gharama zake

Uratibu mzuri wa safari ukizingatia mantiki, ubora na masilahi ya nchi unaweza kuwekwa katika mizani sawa na gharama, muhimu ni tija na mafanikio yanayotokana na gharama hizo

Yapo masilahi ya nchi yanayolindwa na Rais na wakati ukifika hakuna budi.

Rais kama alama ya Taifa anapewa nyenzo (resources) kutekeleza majukumu muhimu bila kUhojiwa

Rais hawezi kukwepa majukumu yenye masilahi kwa kipimo cha gharama.

Masilahi ni pamoja na ya uchumi, kisiasa na kijamii. Kwa mfano utaongeleaje uchumi kama huhusiani na majirani wa karibu. Utaongelea vipi usalama kama huhusiani na majirani na washirika wa karibu

Inaweza kuwa si muhimu kwa Rais kuhudhuria mkutano wa G7 au G20 tukijua hatuna cha kusema

Tutawezaje kusema si muhimu Rais kuonana na majirani wa EAC au washirika wa SADC au AU ambako tuna masilahi mapana kuliko kule Davos?

Safari ya Dar-Joberg ni masaa 4, Adis Ababa ni 2 , Kampala ni 2 , Nairobi ni 1.

Katika uratibu mzuri i, itachukua siku moja tu(masaa 12) pengine Rais kukamilisha shughuli nyingi zinazohusu maeneo hayo muhimu

Iliwezekanje Nyerere awe Ikulu anaapisha viongozi, mchana Arusha akifungua mkutano , Jioni Lusaka na wenzake wa frontine states , na usiku Msasani kukutana na watu kwa siku moja,leo isiwezekane?

Hatuwezi kuwa kisiwa na kuacha majirani/marafiki kwa kuogopa gharama zinazothibitika(justified)

Hoja muhimu hapa si Rais kusafiri, bali anasafiri kwa lengo gani lenye tija kwa taifa, shughuli zinaratibiwa vipi na je masilahi ya nchi yanazingatiwa?

Suala la gharama linajitokeza panapokuwepo na ziara zisizo na malengo, za hovyo, zisizozingatia masilahi ya nchi na zinazo ratibiwa hovyo kama sehemu ya vacation na shopping

Pengine yapo tusyoyajua,muda ni kitu kinachahitaji subra huenda tukajua haya yanatokea kwanini!

Tusemzane
 
Back
Top Bottom