Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

HOJA MBILI KUU ZA WIKI HII

ZUIO LA WIZARA YA MAMBO YA NJE KWA MABALOZI

RAIS NA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA


Tuanze kusema Watanzania wana tatizo la kupambanu kati ya criticism na critic.
Haya maneno yanaonekana sawa kwa maana ingawa ni tofauti.

Kutathmini, kupinga, kukejeli, kudhihaki na kukashifu ni mambo tofauti
Tumejenga utaratibu wa kutoangalia mambo kutoka kona tofauti

Tumekuwa taifa la kumeza tu , na kwasababu hiyo siku zote tunashtukizwa na vitu vilivyohitaji fikra kidogo

Tunapozungumzia uongozi au kiongozi kwa ubaya au uzuri lengo linabaki moja, kujenga taifa na kupanua fikra

WIZARA YA MAMBO YA NJE
Imetoa kauli mabalozi wanadiplomasia kutokutana au kushiriki shughuli bila taarifa kwa wizara ya mambo ya nje. Kwa maneno mengi serikali ijue kila nyendo ya mwanadiplomasia

Yes, kiusalama inaweza onekana ni muafaka, ingawa haiwezi kuwa katika hali iliyoelezwa na wizara

Mataifa hufanya ujajsusi kwa minajili ya usalama yakitumia vitengo bila kukinzana na haki ya mwanadiplomasia

Tanganzo limewashtua wanadiplomasia ambao weledi wa kwanza ni kujua taratibu za kidiplomasia.

Wameshtuka kauli imekuja kukiwa na tuhuma za ubalozi mmoja kuwasiliana na vyama vya siasa

Kwa namna yoyote kauli ya wizara imelenga ''kuzuia'' mawasiliano ya wanadiplomasia na wanasiasa.

Sababu iliyotolewa ni uchanga wa wanasiasa, serikali hofu kama wanajua taratibu za kidiplomasia

Tangazo limezuia wanadplomasia kwenda mikoani au kwingine hata kwa kazi zinazohusu diplomasia

Hapa kuna tatizo. Kwanza, kauli inazidi kutia shaka kwa namna ilivyoletwa na wakati ilipotolewa

Kwa mantiki hiyo, serikali inazidi kuwapa 'habari' watu wa nje kwa kudadisi kwa undani.

Lakini pia serikali inashindwa kuelewa wanadiplomasia wanaweza kukutana na watu nje ya nchi

Pili, nchi yetu inaishi kwa ufadhili , misaada n.k. Kuweka vizuizi kutaumiza wananchi bila sababsababu

Wanadiplomasia wakiona usumbufu katika shughuli zsisizohusiana na siasa wataweza kaa pembeni

Na tatu, hivi kwanini tunafanya mambo kwa 'matukio' na si utaratibu

Hatuna utaratibu unaoongoza shughuli za zetu zikiwemo za wanadiplomasia nchi.

Laiti ungekuwepo, serikali ingeshatoa tangazo mapena pale Katibu mwenezi na katibu mkuu wa CCM waliposimama jukwaani na balozi wa china akiwa na mavazi ya kisiasa kama mwanadiplomasia

Leo nini kimebadilika hadi kauli kama hizi?

Na je, masuala ya kisiasa na migogoro inatatuliwa kwa njia kama hizi?

Hii inaweza kuwa suluhu ya matatizo yetu?

Kwanini tunatafuta suluhu kwa kufunika ''uchafu chini ya kapet'' i?

Inaendele ....Hotuba ya Rais sherehe za mahakama
 
RAIS NA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA
Rais alikuwa mgeni rasmi wa shughuli za kuanza mwaka mpya wa mahakama.
Ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya wanataaluma ya sheria katika kalenda yao

Ni fursa nzuri kwa Rais kuweka mwelekeo wa serikali kwa ushrikiano na mhimili mwingine. Tukio hilo lilikuwa muhimu na muhimu kwa Rais kutoa ujumbe alioukusudia

Tukio halikuwa 'live' kama alivyosema Rais kwavile aliambiwa na Jaji mkuu wasingependa gharama Haieleweki gharama zingebebwa na vyombo vya habari au idara ya mahakama!

Hotuba ya Mh Rais ilikuwa na mambo yanayochanganya ikiangaliwa kwa jicho la pili

Ilikuwa na mambo makuu matatu tunayoyazungumzia kwa uchache katika makundi

KUNDI LA KWANZA
Kama alivyosema Rais, hakusoma hotuba aliyoandikiwa ili kutoa yake ya moyoni

Kila mtu ana namna anayowakilisha ujumbe. Tukijua ni mwanasayansi hotuba haikuwa na mtiririko

KUNDI LA PILI
Hotuba ina mambo mazuri yanayogusa jamii. mfano Ucheleweshaji kesi kwa kisingizio cha uchunguzi

Hili ni tatizo kubwa na Rais amelieleza kwa kumtaja wazi DPP kama kikwazo kwa mahakimu
Haya tumeyaongea sana, kwamba kuchelewesha haki ni kunyima haki

Pili, kama alivyosema kesi zinazohusu wenye uwezo zinacheleweshwa ili kutoa mwanya wa rushwa.

Mifano aliyotoa ni mizuri, ikiwa mtu kakamatwa upo ushahidi,vipi basi kesi iendelee miaka nenda rudi?

Tatu, Rais ameongelea ufinyu wa bajeti na kuamuru kiasi kikubwa kutolewa ndani ya siku tano
Ni kweli mahakama zinaendeshwa katika hali ngumu sana hasa huko vijijini kutokana na bajeti finyu

Nne,akaongelea suala la mafunzo na kwamba wanaotaka mafunzo wakope kama wanafunzi wa HESLB

Hili ni jema kwa kuzingatia hakuna sababu ya kuajiri watu na kuwafunza ikiwa wenye mafunzo wapo

Tano, ameongelea suala la masilahi ya mahakimu. Kwamba, masilahi duni yanachochea ushawishi

MAPUNGUFU
Kwanza, suala la TV kuonyesha 'live' kama alivyoelezwa na Jaji mkuu halikuwa na ulazima kuliongelea

Kama TV ni ghali ni kwanini basi inaonyesha vipindi kwa muda wote? Kwanini isionyeshe kwa muda tu au serikali ijitoe katika shughuli hiyo kuokoa fedha na kuachia watu binafsi?

Pili, takwimu za bilioni 4 alizopewa zinatiliwa shaka na wanahabari na wataalam zilipoletwa na waziri wa habari, zinamweka Rais mahali pagumu. Je, ikithibitika si kiasi hicho umma utamwelewaje?

Tatu, kwanini yap matukio yanyoonyeshwa 'live' ikiwa serikali imekusudia kupunguza gharama?

Pungufu lingine kubwa ni lile la kutoa tamko linaloelekea kuwa ni 'amri' kwa mhimili mwingine
Rais anapokuwepo popote kauli yake ni 'sheria' kama si amri.

Alipotoa amri ya mahakama kupewa fedha ndani ya siku tano, Rais alikuwa anatumia nafasi yake kama Rais hata kama matumizi hayo hayakuidhinshwa na bunge.

Hivyo kauli zake ni muhimu kupimwa kwani zina uzit tuliosema

Rais alipoongelea pesa trilioni moja kutokana na kesi zilizopo na kwamba zilipwe, aikwenda mbali
Kesi zilizopo mahakamni zipo katika kutafuta ukweli

Si lazima shauri lililopo mahakamani mshtakiwa awe na makosa, anaweza kuwa na haki pia

Rais anapoutaka mhimili umsaidie kukusanya trilioni moja ili nao wapewe robo ni jambo la kushtua

Keshawahumu watuhumiwa bila kusikilizwa. Kitendo cha kusema walipe ni hukumu

Na zaidi , napoamuru mahakama iharakishe kesi ili serikali ipate pesa, anawaamba mahakimu wamalize kesi kwa ushindi dhidi ya serikali ili watuhumiwa walipe kiasi anachotaka

Hili lilikuwa kuamuru mahakama na si kuelekeza. Pengine ingalipendeza angesema kesi zilizopo mahakamani zimalizwe haraka bila kutoa masharti au muongozo kwa majaji na mahakama

Leo watuhumiwa wanajua kesi imeshasikilizwa na humu hapo hapo, walipe

Je ikiwa kuna aliyedhulumiwa, haki ataipata wapi ikiwa Rais keshatoa amri pesa zikusanywe?

Hili ni punGufu kubwa, kwani mhimili mmoja umevuka daraja na kuingilia mwingine

Rais pia ametaka DPP amalzie kazi. Hapa panashangaza kidogo DPP anateuliwa na Rais bila kuthibitishwa na chombo chochote.

Uzembe wa DPP hauelezwi kwa wananchi bali yeye ndiye wa kuulizwa.
Wananchi hahitaji kusikia malalamiko, wanataka suluhu. Rais akilalamika Raia wake wafanye nini?

Na mwisho tendo la kwenda kutoa amri katika mhimili mmoja, na kutoa pesa zisizoidhinishwa na mhimili mwingine inaeleza mhimili wa serikali ulivyo na nguvu dhidi ya mingine.
Ile power balance ipo wapi?

Na mwisho, kwanini isiwepo sheia inayotoa bajeti kwa mahakama ili kuuweka mhimili huo huru na si kupewa kwa masharti?

Haya ni kwa uchache mengi yatafuata

Tusemezane
 
RAIS NA KAULI TATA

MIHIMILI YA NCHI , 'KUPOKWA MADARAKA'

JE BADO TUNAAMINI MIHIMILI NI MITATU?


Rais akiongea katika sherehe za mwaka wa mahakama, alisikika akisema 'yeye si dikteta'
Katika siasa za nchi yetu na fikra tofauti kauli tu zinaweza kuleta hisia bila kujali usahihi wa jambo

Rais amesikika mara nyingi akitumia maneno 'nimeamua, mimi ni Rais, ahsanteni kunichagua kuwa Rais) n.k.
Rais ni mtu anayeongoza taasisi ya Urais inayoundwa na vyombo vingi akiwa mkuu wa taasisi

Hotuba za Nyerere, mara chache sana itumia umoja Zaidi ya wingi 'tumeamua, tulikosea, tukapanga' n.k. akionyesha kushirikisha ni taasisi si yeye binafsi

Bandiko la juu, Rais ameagiza mhimili mmoja kupewa pesa na robo kama kesi zitamalizwa ili trilioni ipatikane.

Maagizo ya Rais yanaifunga mahakama mikono kutenda haki katika sheria.
Yanelekeza mahakama zimalize kesi kwa kuhakikisha watuhumiwa wanalipa kodi.

Walioenda mahakamani wanasababu, je hawana haki ya kusikilizwa?

Je mahakama zimeachwa huru kama mhimili usioongozwa na kitu kingine kama ilivyo serikali na Bunge?

Pili, Rais ametoa agizo la pesa kutolewa ndani ya siku tano, na robo ya ya trilioni moja

Utaratibu wa nchi yetu ni mapato na matumizi kupangwa na bunge
Je, hapa Rais hajavuka mpaka wa mhimili wake na kuingilia mhimili wa bunge?

Pesa anazotoa zimetoka fungu gani la bajeti au eneo lolote linaloruhusu hali hiyo?

Tatu, hata katika eno la mhimili wake(serikali) bado kumekuwa na viwango tofauti(double standard)

Waliokwepa kodi walitakiwa warudishe, walipewa muda
Wakati huo huo anamtaka DPP na Mahakama wakusanye trilioni moja kupitia hukumu

Tofauti ya wale waliotakiwa kurudisha kwa majadiliano na hawa wanaotakiwa kurudisha 'kwa hukumu' inatoka wapi?

Nne, Rais ameagiza mahakama ianzishe mahakama ya mafisadi kama alivyokampeni. Mfano aliotoa ni wa mahakama ya ardhi, na kwamba kwanini isiwe rahisi kuanzisha ya mafisadi

Hapa napo lipo tatizo, kwamba Rais anaupa mhimili wa mahakama jukumu lisilo lake.

Kazi ya kutunga sharia ni ya bunge, na kazi ya kuidhinisha sharia hiyo itumike ni ya mhimili wa serikali na kazi ya kutumia sharia hiyo ni ya mahakama.

Inakuwaje jambo la kisheria kama mahakama ya mafisadi lianzishwe kwa njia ya mkato bila kufuata taratibu zetu?

Tumalizie, ni kweli upo uzembe wa kuendesha mashtaka si kwa wakwepa kodi bali eneo zima likiwemo la kesi za chini znazopigwa danadana kwasababu ya 'fedha' hilo lipo wazi

Uharkaishaji wa kesi ni jambo muhimu na hakuna tatizo

Tatizo ni pale mihimili ya nchi inapoingiliana, na kuwa upo mhimili mkubwa kuliko mingine
Ni pale mhimili wa serikali unapohodhi nguvu za mihimili mingine.

Serikali inatoa pesa kwa mahakama badala ya mahakama kuwa na fungu lake.
Serikali inatoa pesa bila kuidhinishwa na mhimili mwingine wa bung

Matumizi ya lugha yanaweza kuleta maana isiyokusudiwa.

Kama alivyosema Rais, yeye si dikteta. Kwa kuangalia tuliyojadili, tutamlaumu vipi atakayesema Rais dikteta?

Sehemu ya matatizo tunayoyaona ni mfumo na hili tumeliongelea sana. Kwamba mihimili si 3 ni mmoja

Lakini pia timu inayofanya kazi na Rais kwa ukaribu, inahitaji kumshauri kuhusu kauli

Tusemezane
 
VYOMBO VYA HABARI NA NGUVU ZA KUJENGA AU KUBOMOA

Vyombo vya habari vina nafasi ya kujenga au kubomoa uongozi

Hli hiyo inaweza kutokea katika njia mbali mbali. Tuangalie chache miongoni mwa hizo

1 Ujenzi: Vyombo vinaweza kujenga uongozi kwa namna vinavyoweza

Uwezo wa wananchi wa nchi kutafuta ukweli nje ya habari ni wa kiwango cha mashaka

Wengi hutegemea habari za magazeti/radio/TV bila kujali jinsi zilivyoandikwa

Mfano ni awamu ya 4 iliyoingia madarakani ikipigiwa upatu na 'vyombo' vya habari.

Hali imeendelea mwisho tunayaona tuliyokuwa tunaishi nayo bila kujua yanatokea.

Nchi ya Tanzania katika karne ya 21 inapima mafuta kwa kijiti!

Vyombo hivyo vilipochoshwa na utendaji na udhaifu ulioonekana, vikaanza kuanika uozo

Tumechelewa, Serikali inakabailiana na mauzauza badala ya kuendeleza agenda zake

2. Vyombo vya habari vinaweza kubomoa uongozi kwa maana ile ile tuliyosema
Kwamba, vinaweza kutoa picha ambayo wananchi wengi hawataweza kuzichuja

3. Vyombo vya habari vinaweza kuujenga uongozi kwa namna tofauti.
Kwanza, vikikosoa , pili vikielekeza na mwisho vikiwakilisha maoni ya umma.

Na hapa vinachukua sura ya kuwa kioo katika jamii ambacho uongozi unapaswa kutumia ili kujua nini kinatokea na nini kinaendelea katika jamii

Katika dunia iliyojaa vyombo binafsi ,mitandao n.k. ni ngumu sana kudhibiti habari.

Lakini pia ni kwa njia hii habari zinawafikia viongozi kutoka katika jamii wanayoongoza.

Kwa mantiki hiyo, hakuna uwezekano wa kukwepa vyombo vya habari

Na wala hakuna namna ya kudhibiti au kuchuja habari kwa matumaini ya kupumbaza

Zile zama za kudhani habari ni kama 'nguzo za ndani' au kundi Fulani lina umiliki hazipo


Inaendelea..
 
VYOMBO VYA HABARI (mwendelezo)

Ni makosa makubwa kwa viongozi kudhani kwamba, kuchuja habari, kudhibiti au kuficha kwa kutoziweka wazi kutasaidia katika jitihada za kuliweka taifa pamoja au kulijenga

Habari hizi mbili ni kwa hisani ya magazeti ya IPP na Habari leo

Home
Muhimbili yang’ara siku 100 za Magufuli

Tunasababu za kuzichukua. Habari ya kwanza inahusu msimamo wa Ulaya kuhus ZNZ.

Ukisoma kwa undani, ni msimamo unaoweza kutuweka sote tusikopendelea

Habari inafuatia tukio lisilo la kawaida la hafla ya mabalozi Ikulu ,mwenyeji akiwa hayupo. Kuna uhusiano kati ya hayo mawili, msimamo na hafla

Hatujui lini ilitokea,sababu zilizotolewa zinatia shaka zaidi ya shaka iliokuwepo.

Habari ya pili inaeleza mafanikio ya siku 100 ya awamu ya tano.

Inanukuu viongozi wakieleza jinsi kmabadiliko yalivyotokea muhimbili hospitali

Habari za magazeti hayo mawili tunaziangalia katika mitazamo ifuatayo

1. Kwanini kuna jitihada za kudhibiti habari kama mzozo wa 'bunge live' ulivyojitokeza

2. Namna vyombo vya habari vinavyoweza kutumika katika propaganda

3. Namna vinavyoweza kutumika kuonyesha, kudokeza, kutahadharisha, kukosoa, kuelekeza

Tutaangalia kwa undani bandiko linalofuata
 
Inaendelea...
Tuangalie mitazamo mitatu kama tulivyoieleza hapo juu

1. Kwanini kuna jitihada za kudhibiti habari kama mzozo wa 'live' ulivyotokea

Kilichoamsha hisia na mzozo bungeni ni ukweli, wananchi hawataki habari zilizochujwa
Kwamba, wasikie kile wanachotakiwa kusikia na si kile wanachotaka kusikia

Ipo dhana mapungufu ya serikali yakiwekwa wazi ni kuiumbua, ni bora kudhibiti habari.
Je, inasaidia serikali inayokabaliana na maouvu?
itakabilianaje ikiwa haijui maouvu yapo wapi?

2. Vyombo vya habari kutumika kwa propaganda
Kwamba, vionyeshe mambo mazuri tu ya serikali.
Kwa mfano, gazeti linaeleza mafanikio yaliyopatikana Muhimbili katika awamu ya tano.

Hakuna uchambuzi au utafiti, kilichofanyika ni kuaminisha umma mambo ni mazuri
Wakati huo huo kuna habari,wodi ya wazazi vichanga na mama zao wanahemea sakafuni

Gazeti haikuandika hayo, linataka wananchi waamini 'mambo poa sana' (propaganda)

Swali la kujiuliza, kama Muhimbili ni 'poa' , je , ni poa mikoani zikiwemo za wilaya na vituo vya afya? Nani amehakiki maeneo mengine ili tuamini 'uzuri' umesambaa?

3.Namna vinavyoweza kutumika kuonyesha, kudokeza , kutahadharisha na kuelekeza

Gazeti jingine limeeleza msimamo wa mabalozi wa nchi za ulaya kwa suala la ZNZ

Ukisoma habari kwa undani gazeti linawianisha habari mbili.
Kwanza hafla ya mabalozi na kisha msimamo wa nchi za Ulaya kuhusu ZNZ.

Gazeti limeonyesha, likadokeza , likatahadhrisha kuhusu utata ZNZ na mwelekeo wake

Kwa haraka, inaweza kuonekana gazeti limetoa habari 'mbaya' dhidi ya serikali.

Katika mizani ,gazeti limeisaidia serikali kuliko lililoandika habari za kuipendeza

Hii ina maana mbili, kati ya magazeti hayo, lililoandika habari nzuri za Muhimbili linabomoa serikali. Haliisaidii kwa kueleza ukweli na hali halisi, linaficha!

Wananchi wanayaona matatizo na hivyo kuamini serikali inaficha matatizo.
Hilo linaondoa kitu kinachoitwa public trust jambo litakaloisumbua sana serikali

Gazeti lililoandika habari za mabalozi linaijenga serikali kwa kuonyesha, kudokeza na kutahadharisha

Hapa tunaona ukweli kuwa lengo la kudhibiti habari ni kutaka kuzichuja.
Swali la kujiuliza, katika zama za leo za teknolojia hilo linaisaidia serikali?

Je, kuficha maouvu au kuyaweka bayana lipi bora?
Na serikali itapambana vipi na maouvu kama haina kioo cha kujitazama?

Vyombo vya habari vya serikali vinaiobomoa serikali kwa jitihada za kuficha uovu na kutunika kwa propaganda

Tusmezane
 
HOTUBA YA RAIS KWA 'WAZEE' WA DAR ES SALAAM

Ilikuwa ni kueleza kazi katika siku 100 za utawala wake.
Kwa mtazamo yakinifu, hotuba ilikuwa na mambo manne makuu aliyoongelea

Kwanza, kuwaaminisha watanzania kazi za 'majipu' zina nia njema kutokana na hisia kuwa zimefanyika katika hali ya 'kutojali' hasa suala la wakazi wa mabondeni.

Rais aliwaambia wakazi 'walioathirika' wa zoezi kuwa nia ni njema hata kama kuna matatizo yanayoonekana. Alitaka kuwahikikishia hatua zinachukuliwa kile eneo sawia

Ingawa hakuzungumza moja kwa moja, kauli yake inaonyesha kueleza kile anachokisema udikteta au ukatili au roho mbaya katika hotuba zake. Na amerudia tena

Pili. Alitaka kuungwa mkono na wananchi kwa hatua ambazo zingine zimelalamikiwa kulenga baadhi ya maeneo au watu na kuhusishwa na mambo ya kisiasa

Tatu, Rais ametambua umuhimu wa kuvileta vyombo vya habari karibu.

Kama tulivyoeleza katika mabandiko #91 na #92 na mengine ya nyuma serikali imeona jinsi inavyoweza kufanikiwa au kukwazwa na suala la vyombo vya habari

Nne, ameliongelea ZNZ ambako lawama zimeelekezwa kwa ukimya akiwa Rais wa JMT

Hayo ni mambo manne yanaonekana katika hotuba yake

Kuna sehemu zenye nguvu 'strength' na zenye udhaifu 'weakness'

Hapo ndipo tutajikita katika bandiko linalofuata

Tusemezane
 
HOTUBA YA RAIS KWA 'WAZEE' WA DAR ES SALAAM
Yaliyojitokeza: nguvu na udahifu wa hoja

Kuongea na 'wazee' wa Dar ni utaratibu wa Nyerere alipotaka kuzungumza na Taifa

Utaratibu umerithiwa kama njia ya kuongea na Taifa kukiwa na hadhira(audience)

Miaka 10 iliyopita utaratibu umepoteza maana.
Limekuwa eneo la propaganda. Ilifika mahali waalikwa kupoteza maana ya 'uzee'

Nyerere aliutumia kufafanua masuala ya Kitaifa na si masuala ya kisera au kiutendaji.

Alipotaka kuongelea mambo ya kisera au kiutendaji, alifanya mikutano na viongozi

Rais kuongea na Taifa ni jambo zito. Kauli anayotoa ni ima 'sheria' au kauli mbiu

Lugha inatakiwa kuwa nyepesi na mpangilio isiyo na utata kueleweka na mtu wa kawaida

Pamoja na ukweli kuwa hakuna lugha ya 'rasmi' iliyokubaliwa kwa maana ya mpangilio. Hatuwezi kukataa ukweli lugha isiyo na mpangilio inachanganya, kubabaisha au kupoteza maana halisi iliyokusudiwa katika hadhra

Rais anapokuwa popote anabeba sura ya Utaifa. Lugha inapaswa kulenga Utaifa hasa kutambua ni alama ya Taifa katika umoja na mshikamano.

Hakuna asiyejua viongozi wetu wanapatikana kwa njia za kisiasa, lakini, kiongozi anapokuwa wa kitaifa inabaki hivyo na utaifa kwanza

Imetokea mara kadhaa Rais Magufuli kuanza maongezi yake iwe ndani ya mikutano ya chama au kitaifa kwa lugha inayotia shaka kidogo.

Amesikika si mara moja au mbili akisalimia umma kwa makabila.
Hilo haliwezi kuwa tatizo ikiwa amelenga kuamsha ari ya hadhira yake

Hata viongozi kama Mwalimu, walipenda utani wa makabila ili kuweka wasikilizaji katika hali laini'easy' kumsikiliza na kumtambua ni mwenzao

Tatizo linajitokeza siku za karibuni tunaposikia salam za kidini.
Mfano asalam alaykumu, bw yesu asifiwe n.k.

Kiongozi wa kitaifa ni yule yule wa waislam, wakristo, wasio na dini, wahindi, magoa n.k.

Kutambua uwepo wa dini mbili, hata kama ni kubwa, kunapalilia hisia za udini na kutenga makundi mengine, Kwa lugha nyingine ni 'discrimination'

Rais wa nchi anaongea na nchi bila kujali itikadi , hili la salamu kwa itikadi halina ladha tukijua Rais anapoapa ni kiongozi wa wote wakiwemo 'wachawi' hata kama hatuwatabui

Tukikumbuka hotuba za Nyerere, alipenda kusema 'Ndugu wananchi.....''
Kama alifanya utani ilikuwa katika mtiririko wa maongezi na si 'alama' ya hotuba.
Na mwalimu alIpomaliza alisema 'ahsanteni kwa kunisikiliza'

Mpangilio wa hotuba za mwalimu ulikuwa unaonyesha vitu vifuatavyo.
Kwanza, lugha rahisi inayoeleweka kwa kila mmoja
Pili. lugha yenye mamlaka 'authority'
Tatu, lugha inayoeleza na kuainisha tatizo na mwisho inayotoa majibu.
Nne, hakutumia umoja (mimi) au lugha za kibabe , zenye ukakasi au hisia mbaya

Haikuwa lugha ya lawama au kulalamika kama inavyojitokeza miaka ya karibuni

Katika kufikia malengo, hotuba za Nyerere ziliishia na kauli mbiu iliyobeba ujumbe.
Mfano, mtu ni afya, uhuru na kazi, punguzeni nundu,hatutageuka minara ya chumvi, matapeli/wahujumu uchumi, sababu /nia na uwezo... n.k .

Kwa uchache hotuba zilikuwa na 'kauli mbiu' iliyoacha ladha midomoni kwa muda mrefu

Alitumia lafudhi laini yenye ukali katika ujumbe.
Mfano, hatukubali, tutaongea , tutashauriana, Amani na usalama.

Nadra kumsikia akitumia lugha ya nguvu za dola kama tutawashughulikia, fyoko, vyombo vya ulinzi na usalama n.k.

Kwa kuangalia hotuba za Rais, kuna tatizo la mwasiliano kwa mtizamo wetu binafsi.

Zipo hoja za'uasili' kutokana na maeneo tunayotoka, fani za elimu n.k.

Hayo yote ni sababu laini zisizo na mashiko kama tutakavyojadili baadaye

Itaendelea....
 
HOTUBA YA RAIS KWA 'WAZEE' WA DAR ES SALAAM
LUGHA

Tunalijadili suala la lugha kwani ni muhimu tukizingatia ndicho chombo kilichobeba maudhui. Haionekani kama lugha ya mh Rais ipo katika hali maridhiwa

Mpangilio wa hotuba haupo katika muktadha mzuri. Mfano akiongea na wazee wa Dar es salaam, neno 'nawashukuru' limerudiwa mara nyingi. Kulikuwa na ulazima ?

Katika lugha kurudia maneno kunaondoa ladha, kuonyesha upungufu au udhaifu wa hoja

Pili, mpangilio unaanza bila kujua unaishia wapi.
Hakuna vifungu na huchukua muda mrefu kujua suala nlimekwisha na lingine limeanza

Tatu, lugha yenye maneno yasiyoweza kueleweka.
Anasema, 'wasiofanya kazi na wasile' kauli hii ina maana gani? Ilikusudia nini?

Nne, matumizi ya lugha kali.
'VYombo vya ulinzi na usalama vitamshughulikia atakayeleta fyoko'

Hii si lugha ya mamlaka au kidiplomasia, ni ya 'ubabe' na ndio maana wapo wanasema kuna aina ya 'udikteta'.

Katika hali ya kawaida, vyombo vya ulinzi na usalama hushUghulikia wavunja sharia.
Hili neno fyoko linaleta ukakasi kwa wasikilizaji

Tunaelewa, alipozungumzia hilo alilenga hali ya visiwani ZNZ.
Hatudhani lugha kali kama hiyo imewapendeza wananchi hasa wa visiwani.

Yes, yeye ni Amir Jeshi mkuu, lakini matumizi ya vyombo alivyopewa yanahitaji hekima na busara. Lugha ya fyoko inaficha hekima au busara zinazotarajiwa

Lugha isiyo ya kidiplomasia, akisema 'Hataingilia suala la ZNZ na atazidi kukaa kimya'

Kulikuwa na namna angeeleza umma uelewe bila kauli hiyo.

Angeweza kueleza kisiasa na kisheria katika lugha nzuri kuliko ubabe unaoonyesha mambo mawili;

kwanza kwamba hana sababu za kushawishi, na pili, anaeleza umma suala ima hana uwezo nalo au limemshinda

Na mengine mengi yanayoonyesha mapungufu katika lugha.

Wanasema Rais anatoka bara,lugha ni tofauti na ya pwani hasa matumizi ya maneno.

Wengine wanasema ni mwanasyansi na hana lugha laini, wenyewe wakisema 'pi ni pi' na kwamba engineers hawana matumizi ya lugha Zaidi ya facts

Hoja zote mbili hazina mashiko kwasababu tuakazo zieleza bandiko linalofuata
 
HOTUBA YA RAIS KWA 'WAZEE' WA DAR ES SALAAM
LUGHA


Rais Nyerere alipokuja Pwani Kiswahili haikuwa lugha irahisi kwake kama walivyo wengi
Hata hivyo,Nyerere alizungumza Kiswahili fasaha kuzidi wenyeji akiondoka madarakani

Mwalimu alijiendeleza, alijifunza na kuwa bingwa wa lugha aliyoikuta
Ndivyo mwanasiasa kama Magale Shibuda alivyojifunza na kuwa na lugha nzuri

Katika dunia ya sasa, fani yoyote haiwezi kutengwa na lugha.
Hakuna msamaha kuwa fani Fulani ina excuse ya kutojua lugha

Hili ni tatizo linaloongezeka nchini.Wataalamu,hawawezi kujieleza au mpangilio wa lugha.

Wanapoachwa hulalamika kuhusu Raia wa nchi nyingine waliojijengea uwezo wa kujieleza hata kama hawana sifa kuzidi wa nyumbani.

Communication skills ni jambo la lazima katika dunia ya leo

Rais amekuwa waziri kwa miaka 20 akifanya kazi na marais wa awamu mbili.
Inatrajiwa uwezo wake wa kuwasiliana utokane na uzoefu wa kufanya kazi na watangulizi

Rais amekaa na kufanya kazi na watu wa kila kona ya nchi.
Inategemewa uwezo wake wa mawasiliano kuwa wa kiwango cha juu.

Hatuoni sababu zozote zinazoweza kuelea mpangilio usioeleweka wa hotuba zake au matumizi ya lugha yanayoonekana kutokuwa sahihi katika hotuba zake

Zipo njia mbili zinaweza kusadia hali. Kwanza, washuri wa mawasiliano watakaomsaidia kabla ya mikutano, na pili, pengine asome hotuba zilizotayarishwa

Tunayasema haya kwani mijadala inayojitokeza katika mitandao inaeleza utata.

Ni vema raia wakamwelewa kiongozi ili kwenda mbele pamoja

Matumizi ya lugha si tu yana athari za haraka, lakini pia za muda mrefu.

Kwa mfano, Rais aliposema ya ZNZ hayamhusu isipokuwa ulinzi na usalama, hili linashadidia hoja ya kundi lilonahitaji muungano wa mkataba (ulinzi na usalama tu)

Hoja ya Rais inaeleza pia umuhimu wa kuwa na serkali 3 kauli zake, tayari yeye ni Rais wa Tanganyika asiye na mamlaka na ZNZ isipokuwa suala la ulinzi na usalama

Hapa Rais anakwenda na sera za chama chake ambacho ni S2.

Kauli yake inatosha kukanusha uwepo wa S2 na mbele ya safari, wananchi watahoji, nini CCM ilichokataa kuhusu maoni ya tume ya Warioba?

Je, alichosema Rais si ukweli uliohitaji ufumbuzi kama ilivyoanishwa na tume?

Lakini pia kauli zingine zinamweka katika wakati mgumu.
Akiwa Singida, alisema watendaji wote wa serikali lazima wasimamie sera za CCM.

Vipi sheria inayokataza baadhi ya watendaji kuwa hata wanachma wa vyama vya siasa?

Kwa hili la mawasiliano tumechukua muda kulijadili, umuhimu wake ni mkubwa kuliko inavyoonekana. Kuna tatizo la mawasiliano na bila mawasilaino tutakwenda vipi pamoja?

Tuangalie hoja zingine kama tulivyoziorodhesha bandiko 93 zikioanishwa na 91 na 92

Tusemazane
 
HOTUBA YA RAIS KWA 'WAZEE' WA DAR ES SALAAM

Ilikuwa ni kueleza kazi katika siku 100 za utawala wake.
Kwa mtazamo yakinifu, hotuba ilikuwa na mambo manne makuu aliyoongelea

Kwanza, kuwaaminisha watanzania kazi za 'majipu' zina nia njema kutokana na hisia kuwa zimefanyika katika hali ya 'kutojali' hasa suala la wakazi wa mabondeni.

Rais aliwaambia wakazi 'walioathirika' wa zoezi kuwa nia ni njema
Alitaka kuwahikikishia hatua zinachukuliwa kile eneo sawia

Ingawa hakuzungumza moja kwa moja, kauli yake inaeleza kile anachokisema udikteta au ukatili au roho mbaya katika hotuba zake. Na amerudia tena

Pili. Alitaka kuungwa mkono na wananchi kwa hatua ambazo zingine zimelalamikiwa kulenga baadhi ya maeneo au watu na kuhusishwa na mambo ya kisiasa

Tatu, Rais ametambua umuhimu wa kuvileta vyombo vya habari karibu.

Kama tulivyoeleza katika mabandiko #91 na #92 na mengine ya nyuma serikali imeona jinsi inavyoweza kufanikiwa au kukwazwa na suala la vyombo vya habari

Nne, ameliongelea ZNZ ambako lawama zimeelekezwa kwa ukimya akiwa Rais wa JMT

Hayo ni mambo manne yanaonekana katika hotuba yake

Kuna sehemu zenye nguvu 'strength' na zenye udhaifu 'weakness'

Hapo ndipo tutajikita katika bandiko linalofuata

Tusemezane
Tuangalie kwa uchache nguvu na udhaifu uliojitokeza katika hotuba yake

Kwanza, tumeeleza kwa urefu kuhusu mpangilio, lugha na mawasiliano aliyotumia
Tumeona udhaifu unaotaka wasaidizi wamsaidie mapema ili aeleweke kwa urahisi na jamii
Itakapofika katika eneo kubwa na hasa diplomasia, hali iliyopo inaweza kuzua utata usiotarajiwa

Pili, nguvu ya hotuba yake ni pale alipouzngumzia kadhia ya akina mama Muhimbili.
Hoja inajengwa na ukweli kuwa bado amefuatilia suala la muhimbili kwa ukaribu

Udhaifu uliojitokeza alipoacha viongozi wa Muhimbili tofauti na ziara ya kwanza alipoondoka na mkurugenzi. Hapa kuna maswali, hawa walifeli vipi ikiwa walikuwa na mwongozo?
Na yule wa kwanza alifeli vipi ikiwa ni mazingira haya haya tena wenzake wakiwa wamewezeshwa?

Udhaifu mwingine ni pale alipomtaja waziri wa afya kushughulikia uhamaji wa wafanyakazi

Endapo alikwenda Muhimbili akiwa hana waziri, na sasa ana timu nzima ya uongozi, je, wasaidizi wake kama waziri wanaelewa dhana nzima ya kile alichokiagiza?

Na kwanini bado wapo kama kweli asiyefaa anapaswa kukaa pembeni? Na kwa muda gani ataendelea kufuatilia Muhimbili? Huko kwingine mikoani na wilayani kuna hali gani na nani wa kufuatilia?

Pili, hotuba ililenga kuwahikikishia 'wazee' hatua zinazochukuliwa ni za lazima kwa manufaa ya umma.

Hapa alijaribu kuelezea manung'uniko yanayotokana na hatua kama za kuhamisha watu wa mabondeni. Hoja ilikuwa na nguvu kwasababu sote tunaelewa, nchi ilipofikia panatisha na hatua zinahitajika. Na kwamba hatua hizo zinaweza kuwa na matatizo yasiyotarajiwa

Udhaifu wa hoja ni kutokana na kuwa na 'double standard' kwamba, vipi watu wa mabondeni wengine wakiwa na vibali na wakilipia huduma za umma pamoja na kodi waondolewe bila wahusika walioruhusu kuchukuliwa hatua?

Inakuwaje serikali ile ile iliyobomoa majengo, inarudi kwa 'mlango' mwingine kuona huruma baada ya kuvunja majengo na watu kulala nje ?

Kulikuwa na uhakiki wa zoezi kabla halijaanza au ilikuwa ni kubomoa tu

Haimanishi hatua ni mbaya, swali ni je zimezingatia haki za waathirika kusikilizwa?

Na kwanini hatua zinachukuliwa nusu nusu. Mfano wa kodi, wapo waliopewa muda, wengine wapo mahakamani. Kwanini kuna viwango tofauti kwa kosa lile lile.

Na yapo manung'uniko kuhusu baadhi ya watu kuonewa haya katika zoezi zima

Udhaifu mwingine ni watu wanaomsaidia. Baadhi wana kashfa kubwa zilizotikisa nchi.
Je, hao wana maadili ya kuchukua hatua dhidi ya watu wengine watakaobainika?

Haya ni baadhi yasiyo na majibu rahisi na kupelekea hofu kwa hatua zinazochukuliwa.

Kuwahakikishia wazee tu hakutoshi bila kuwa na usahihi, usawa na uhakiki wa hatua bila kumuonea mtu au kumuonea haya. Je, wanachi waimwelewa?

Tutaangalia suala la vyombo vya habari na ZNZ

Itaendelea...
 
HOTUBA YA RAIS
Umhuhimu wa vyombo vya habari

Hili tumezlizungumza sana kuanzia bandiko 80 na mkazo katika 91 na 92 hata kabla ya hotuba kwa 'wazee'

Rais alianza uhusiano wenye mashaka, hasa mahojiano ya mwanzo yaliyochukuliwa na waandishi kama 'dharau'

Ametambua kazi ya kupamabana na maouvu haitakuwa na ufanisi ikiwa waandishi watakuwa upande wa pili
Kwa ufupi ameelewa dhana ya waandishi na nguvu yao kama tulivyosema bandiko 91 na 92

Na pia, ametaka kujibu swali muhimu sana baada ya mzozo wa 'Live' ambapo serikali yake ni 'imedhamiria' kuficha maovu yasianikwe. Kuhariri vipindi ni njia ya kuficha maovu

Wengine wanahoji, kama anataka kupambana na maouvu kwanini anataka kudhibiti vyombo vinavyofichua maovu?

Rais ametambua vyombo vya serikali havitamsaidia katika kwa maana tatu
Moja, vitaendelea kumpamba bila kumweleza ukweli
Pili, Vitamficha kuhusu maouvu na uovu ili kusitiri serikali
Tatu, serikali itajitenga na sehemu nyingine ya habari

Vyombo vya umma vimepoteza 'public trust' havisomwi na habari zake hazipewi kipaumbele

Tumesema #92 atakayeiangusha serikali ni vyombo vya umma! havimweleze Rais ukweli uliopo katika jamii na wala haviaminiwi na jamii . Vipo na kuchukuliwa kama mashine za propaganda

Alichokifanya ni kuondoa wingu la kuvitenga vyombo vya habari binafsi na kuvihakikishia vinathaminiwa mchango wake
Ndio maana alitaja habari ya gazeti la Jamhuri

Udhaifu wa hoja hii ni pale aliposema 'vyombo vingine........utajiuliza machafuko yakitokea watakimbilia wapi'

Tunarudi kwenye suala la mawasiliano. Neno machafuko linatisha, na kueleza watakimbilia wapi ina tatizo

Baadhi watatafsiri hali iliyopo inaweza kuwa na matatizo na hivyo kuwaweka 'mguu sawa' bila sababu

Na wapo watakochukulia dhana kuwa likitokea tatizo, ufumbuzi ni kukimbia na si kukaa na kutafuta suluhu

Angeweza kutumia maneno laini kama ' matatizo yakitokea...' na hakukuwa na ulazima wa kuzungumzia kukimbia

Yeye ni 'baba' mwenye nyumba, ni vema kuweka familia katika hali isiyo na mashaka hata kama yapo

Mfano ni Rais Obama, ilipotokea mauaji ya saint Bernadino karibu na mwaka mpya na krismas, alilazimika kutoa hotuba kutoka 'oval office' katika prime time kuwahakikishia wananchi, upo usalama waendelee na shughuli zao

Hata pale alipojua kuna uwezekano wa lolote kutokea baada ya hotuba yake, Obama alielewa jukumu la kuhakikishia wananchi kuwa serikali ipo imara kudhibiti hujuma zozote akiwa 'baba mwenye nyumba'

Hatuelewi wananchi wa Marekani wangekuwa katika hali gani, ikiwa angetumia sentensi za kuonyesha hali ya wasisi badala ya kuwatuliza

Tutaendelea na hoja ya ZNZ
 
HOTUBA KWA ''WAZEE'' WA DAR

Tumalizie na eneo lililohitaji umakini sana na lililofanyika katika hali ya kusgangaza, ZNZ

Tuna kumbu kumbu ya yaliyotokea 2001 kule ZNZ na kupelekea misiba, majeraha na wakimbizi

Katika walioteuliwa kufanyia marejeo ya tatizo alikuwepo Rais mstaafu Kikwete

Kwa uzito na kumbu kumbu, safari hii hakutaka 'kujihusisha' akiwa Rais au mwenyekiti wa CCM

Katika hotuba yake kwa wanadiplomasia kupitia waziri wa mambo ya nje, Rais alilieleza suala la ZNZ kama la sehemu ya Tanzania yenye mamlaka yake.

Na kwamba asingeweza kuliingilia kwavile kuna mamlaka husika

Kama ilivyokawaida tatizo lililosababishwa na mtu likapewa jina la tume
Hakuna anayelieleza kisheria na chanzo chake kwakujua kuwa lipo tatizo na 'hayatapendeza'

Ilitegemewa , Rais angelitolea ufafanuzi tukijua lina mkwamo
Rais akasema, hataliingilia kwasababu ZNZ ina mamlaka yake katika mambo ya uchaguzi
Jukumu lake ni kupeleka ulinzi na usalama na ataendelea kukaa kimya

Kauli ya ataendelea kukaa kimya haikuingia masikioni mwa wasikilizaji vema

Huu ni mzozo wa uchaguzi unaohusisha vyama vya siasa .Msajili anateuliwa na Rais wa JMT

Na katiba ya JMT inaeleza uhusiano wa ZEC na NEC. Uchaguzi mkuu huendeshwa sambamba na sehemu ya waliomchagua Rais wa JMT ni wazanzibar.

Moja ya malalamiko ni wingi wa waiga kura ambao pia unaathiri matokeo ya uchaguzi uliosimamiwa na NEC kwa namna moja au nyingine

ZNZ ni sehemu ya JMT na mbele ya dunia ni Tanzania. Rais wa JMT ni kiongozi na alama ya Taifa kama Tanzania. Hivyo hakuna namna tunaweza kusema hili ni la 'nchi ya ZNZ'

Kupeleka ulinzi ni sehemu ya jukumu lake, lakini je, anapeleka bila msingi 'background'?

Je, anajiridhisha matumizi ya vyombo japo ni ya kikatiba yatazingatia hali iliyopo?
Na kama jibu ni ndiyo, wapi anaweza kusema hahusiki na mzozo au hawezi kuingilia?

Katiba inasema Rais wa JMT ni pamoja na ZNZ. Ikitokea hoja inayolazimu Bunge la JMT kujadili, nani atatoa msimamo wa serikali ikiwa Rais hawezi kuingilia?

Hoja ya tume kuwa huru ina matatizo. 'Inaelezwa' viongozi wa tume waliondolewa wakati wa kuhesabu kura . Hilo lilitokea kwa amri ya nani? Na je, tume ilikuwa huru ?

Muhimu si kurudia yaliyotokea, bali kusema kuwa, matarajio hayakufikiwa katika hotuba. Kilichotokea kitazua matatizo mbele ya safari katika suala la muungano

CCM walisema Serikali 3 zitampunguzia Rais wa JMT mamlaka ya nchi.
Je, kwa kauli ya kukaa kimya, Rais hajajipunguzia mamlaka kama walivyokataa CCM katika Rasimu ya Warioba?

Rasimu ilisema Rais wa JMT atakuwa na mambo machache kama ulinzi na usalama, kipi ambacho CCM inakiona tofauti leo?

Na je haikuwa fursa nzuri endapo Rais wa JMTangesimamia matatizo ya Tanganyika na ZNZ kama Rais wa JMT tofauti na ilivyos sasa ambako Rais wa JMT anaonekana kama wa Tanganyika? Hapa hatuoni mchnganyiko ! Na siku za mbeleni nini nafasi ya Rais wa JMT kwa wazanzibar?

Ilikuwa ni fursa nzuri ya Rais kukutana na wazee na kuwaeleza hali ilivyo, mkwamo, wapi tulipo na nini inaweza kuleta suluhu tukiwa kama Taifa.

Haionekani kama hilo lilifanyika, kauli ya kukaa 'kimya' ilikuwa na udhaifu

Haikufafanunua, ilikuwa ya kisiasa na pengine ikilenga kutia nguvu kundi moja.

Hapa ndipo tatizo litakapoanzia, kwamba walezi wanakimbia majukumu, nani wa kulea Taifa?

Hivi kweli tunaondoka katika heshima ya usuluhishi na sasa tunatafuta wasuluhishi!

Ile hadhi ya Arusha kama Geneva of Africa bado ipo?

Moral authority ya kushughulikia matatizo ya wenzetu bado tunayo?

Tusemezane
 
UONGOZI(LEADERSHIP), MAONO(VISION) NA UTEKELEZAJI (MISSION)

SUALA LA ZANZIBAR ''case study''


Dhana ya uongozi ni pana na si kusonga mbele tu. Inawezakana kuongoza kwa kusimamisha watu walipo, au hata kuwarudisha nyuma kwa makusudi maalumu

Mwaka 1965 Nyerere alipiga marufuku vyama vingi. Kwasababu zozote zinazoweza kutolewa, jambo linaloonekana ilikuwa ni kuliweka Taifa pamoja baada ya uhuru.

Mwalimu alielewa, matamanio ya uhuru yangeweza kuleta mtafaruku zaidi ya faraja

Mwaka 1964 yalipotokea maasi, waasi walidai hali bora baada ya uhuru.
Hakukuwa na madai mengine isipokuwa madaraka na matarajio yaliyokuwa mbali na ukweli

Mwalimu aliturudisha nyuma kwasababu tulitakiwa tuwe na mifumo iliyokuwepo ya vyama vingi kama ilivyokuwa kwa nchi nyingi zilizopata uhuru wakati huo

Mwalimu alitusimamisha kwasababu wenzetu wakijenga demokrasia sisi tulikuwa na mfumo wa chama kimoja. Kwa wengine mwalimu aliturudisha nyuma. Je, kuna ukweli?

Kwa mantiki ya kuliweka Taifa pamoja na kujenga umoja, Mwalimu alikuwa sahihi kwa mtizamo mwingine. Hatukuhitaji vyama vingi tulihitaji umoja wa kitaifa tunaojivunia

Leo suala hili lina mjadala miongoni mwa wasomi. Ksichojadiliwa ni uongozi wa Mwalimu (leadership) kwa maana, alichukua hata zisizofurahisha lakini alisimama nazo

Miaka ya 80 Mwalimu yule yule aliyekataa vyama vingi akakubaliana navyo.
Kwamba wakati ulifika Taifa kwenda mbele zaidi.

Pamoja na hayo, Mwalimu alisimama na yale aliyoamini yalikuwa na thamani katika Taifa. Alisimama na Azimio la Arusha akihoji ubaya wake ulikuwa wapi.

Alisimama with convictions na hakubadili msimamo. Hiyo ni leadership

Yalipotokea matatizo ya hali ya hewa visiwani, Mwalimu aliyakabili mbele ya umma.
Hakujificha nyuma ya chama au kundi.

Hakutoa majukumu kwa watu wengine au kwepa majukumu kwa lugha rahisi.
Hiyo ndiyo leadership

Maamuzi mengi aliyofanya hayakupendeza baadhi yao. Maamuzi yalilenga Taifa si watu. Alisimama na msimamo huo. Hiyo ni leadership

Siku za karibuni tumeona wazanzibar walivyomkejeli na hata kumtakia mabaya huko aliko.

Mwalimu alijua yote, alisimama kama kiongozi kuliweka Taifa pamoja na si kundi la watu

Mengi liyoyakataa akiwa Rais yamebaki mfano 'template' ya maongezi kwa wanasiasa

Mwalimu alichukua hatua hizo kwasababu aliamini katika uongozi(leadership) na aliamini katika maono ya siku za mbeleni (Vision) ambayo tutayajadili bandiko linalofuata

Vision(maono) inaendelea...
 
UONGOZI(LEADERSHIP), MAONO(VISION) NA UTEKELEZAJI (MISSION)

MAONO (VISION)

Mwalimu aliamini katika umoja wa Taifa. Alitumia rasilimali nyingi si kujenga barabara bali umoja

Kwa mfano, wanafunzi kuchanganywa katika mikoa tofauti, wafanyakazi kupelekwa mikoa tofauti na maeno yao n.k.

Haya ni mambo yaliyokuwa na gharama na wapo wanaohoji kama yalikuwa na mantiki.
Mwalimu aliona mbali, kumea kwa nepotism(upendeleo) kunaongezeka baada ya Nyerere

Leo viongozi wanachaguliwa kwa kuangalia uwakilishi wa kanda au dini au makabila.

Haya yalishavunjwa nguvu na Mwalimu kwa gharama kubwa.
Aliongoza kuyatenda(leadership) na kuyatolea maono (vision) tunayokiri leo hii

Nyerere aliamini katika azimio la Arusha kwa maana yapo yaliyotupwa kama miiko na maadili ya uongozi. Alijua ipo siku ''fisi'' watatawala na utakuwa mwisho wa maisha ya matumaini

Leo tunaona hayo kwa kupitia majibu na mengi yaliyochini ya zulia(under the carpet).
Kwa mwalimu, hiyo ni leadership yenye vision

Nyerere alikaririwa akisema, endapo litaundwa shirikisho la Afrika Mashariki ni vema tukienda kama Tanganyika na Zanzibar.

Alijua mbele ya safari majirani watatuangalia vipi na nguvu yetu itakuwa wapi kama watu wa Taifa moja, wenye kura mbili.

Ndiyo yanatotokea EAC . Mwalimu alionyesha leadership yenye vision

Mwaka 1967 alikaririwa na gazeti la Uingereza akisema, endapo Wazanzibar wataamua kuukataa muungano, yeye hatawapiga mabomu.

Hiyo ni leadership na vision na haya ya leo kwa wengine ni marudio ya alichokisema Mwalimu

Orodha ni ndefu, inatosha kusema tu, Nyerere alikuwa na maono juu ya Taifa hili (vision) na hakusita kuweka wazi kile alichoamini ni bora kwa ajili ya Taifa wakati huo na siku za mbeleni

Tukiangalia sasa hivi, viongozi wetu hawana maono. Hili la Zanzibar linaeleza kwa undani zaidi.

Hebu tulijadili bandiko linalofuata kabla ya kujadili 'mission'

La ZNZ na maono ya siku za baadaye

Itaendelea
 
MAONO (VISION)
Ni kuona mbali kwa kuangalia mazingira na kutumia busara
Tatizo la muungano ni la muda mrefu na viongozi walijaribu kulikabili kama tatizo la Taifa.
Hawakuliacha kama la ZNZ na Nyerere ni mfano

Rais wa awamu ya tatu aliingilia mzozo uliomuacha na lawama hadi leo.
Alifanya bila kusingizia mipaka ya kazi yake.

Awamu ya nne, ilikuwa na bahati, vuguvugu la katiba lilipoanza walikwenda mbele'kuliteka'

Kwa tatizo la muungano, CCM ikakataa maoni kwa kisingizio Muungano haukuwa agenda

Hoja ya serikali ya CCM ilikuwa muundo . CCM walitaka serikali 2. Sababu za kukataa maoni ya tume ni kama zifuatazo
1. Kwamba S3 zitaua muungano.
Hoja : Hakuna ushahidi uliotolewa zitaua vipi na S2 zitaimarishaje

2. Kutakuwa na ukubwa wa serikali na kumbebesha gharama mwananchi.
viongozi wastaafu watakuwa wengi na kuongeza gharama za kuwahudumia

Hoja zetu: Serikali ya awamu ya tatu imeongeza mikoa na wilaya na kuongeza gharama

Viongozi wastaafu wanaongezeka,hakuna ushahidi kama wataongezeka au kupungua.
Upo uwezekano wakapungua kwa muda mfupi au pia kuongezeka, ni wanadamu

Katika gharama, tujiulize kwa mkwamo wa kisiasa ZNZ serikali ya muungano inajiendeshaje au imeathirikaje kwa gharama. Na kipi kimekwama kwa ZNZ kutokuwa na suluhu?

Kwa mkwamo wa ZNZ na uchumi wa huduma ulioathirika, gharama za kuendesha SMZ zinatoka wapi. Nani anagharamia bilioni nyingi za marudio ya uchaguzi?

Kwa yoyote anayejua uchumi wa ZNZ hatasita kusema JMT inaendeshwa na Tanganyika na wakati huo huo Tanganyika ikigharamia shughuli za SMZ. Je, walinzi wa Amani na usalama si gharama?

3. Serikali 3 zitampunguzia Rais wa muungano. Kwamba mambo yatakuwa saba, Rais wa JMT hatakuwa na nguvu za kisiasa akitegemea serikali washirika

Hoja yetu: Je, kwasasa nguvu ya Rais wa JMT ipo wapi?
Rais kasema nguvu zake ni za ulinzi na usalama kwavile SMZ ina vyombo vyake.

Kama ni hivyo, CCM walipata wapi hoja ya kupungua nguvu ikitokea S3 zikawepo?

Rais alisema atakaa kimya, je , hapo hajajipunguzia madaraka mwenyewe?

Rais anapokaa kando,umadhbuti wa muungano upo wapi? Na je muungano una nguvu kama CCM wanavyosema?

HILI LA ZNZ KIMAONO LINATUELEZA NINI?

Inaendelea
 
HILI LA ZNZ KIMAONO LINATUELEZA NINI?

Kulikuwa na makundi 3 yaliyokuwa na maoni juu ya muundo wa muungano
1. Waliotaka muungano wa mkataba wakimaanisha uwepo ulinzi na usalama tu
2. Waliotaka S3 wakimaanisha mambo 7 tu na uwepo wa serikali 2 na ya muungano
3. Waliotaka S2 wakiataka muundo uliopo uendelee kama ulivyo

Hoja ya katiba na tatizo la muundo wa muungano lipo pale pale

Rais wa awamu ya 4 alikuta hali ikizorota, akaacha tatizo akitaraji litajimaliza lenyewe
Rais wa awamu ya 5 anasema atakaa kando na kimya isipokuwa ulinzi na usalama

Hapa ndipo tatizo litakapojitokeza kwa kukosa maono ya siku za baadaye

Rais wa awamu ya nne/ tano wanajaribu kuepuka tatizo pengine kwa kulitengeneza zaidi

Hoja ya muungano wa mkataba:
Inaweza kurudi kwa nguvu. Endapo Rais amesema atapeleka ulinzi na usalama kwavile ZNZ ina mamlaka zake, hoja itakataliwa kwa kigezo gani? Si ndicho kinachotokea?

Hoja ya serikali 3:
Nayo itapata nguvu. Kwasasa JMT ni Tanganyika, ZNZ haijakamilisha serikali.
Suala la gharama lina nguvu gani? Tumeona JMT ikiendelea na shughuli bila SMZ

Na SMZ 'inaendesha' shughuli zake za kawaida. Nini kinashindika kwa wawili hawa kuwa na serikali nyingine ikishughulikia mambo machache Zaidi kama ulinzi na usalama?

Hoja S3 zitampunguzia Rais madaraka, ina mashiko gani ikiwa Rais 'amejipunguzia' mamlaka kwa kukaa kimya?

Hoja ya S3 kudhoofisha muungano itakuwa na mashiko gani ikiwa tunaona unavyodhoofika kwa kuwa na pande mbili zisizohusiana zaidi ya ulinzi na usalama?

Hoja ya ukubwa wa S3 ipo wapi ikiwa sasa kila mmoja ana uwezo wake na mambo yake?

Kundi la Serikali 2:
Hoja zote za S2 zimejibiwa katika makundi mawili yaliyotangulia.
CCM watajenga hoja gani tena kuhusiana na muungano wa mkataba au S3?

Zaidi , viongozi wa awamu ya 4/5 ndio wale wale waliokuwa upande wa CCM.

Leo wamekaa pembeni wakiangalia ZNZ.
Siku za mbeleni, watarudi kushawishi vipi wananchi S2 katika kuimarisha muungano?

Na je, baada ya hali kutulia znz nini itakuwa mamlaka ya Rais wa JMT kule visiwani?

Haya ni baadhi ya mambo yanatotakiwa kuangaliwa kwa umbali kabla hayajatokea. Kwanini viongozi hawayaoni? Je, maono(vision) yao juu ya nchi ni yapi?

Matumaini ni kutumia mbinu kama wingi n.k. katika kutengeneza sheria

Ni matumaini ya kutumia nguvu za dola kulinda muungano.

Hivi kwa hali ilivyo, hapo kuna maono ya aina yoyote?

Tutaendelea kuwa na muungano unaolindwa na dola hadi lini?

Na je, hilo ndilo tunaliona urithi kwa vizazi vyetu vya baadaye?

Na wapi duniani muungano umelindwa , badala ya kulindwa na utashi wa wananchi?

kwavile kuna udhaifu wa uongozi(leadership) na upungufu wa maono(vision) kama Taifa hatuna cha kutekeleza (mission). Tunaishi leo iishe ndivyo tunavyoliandaa Taifa letu?

Tusemezane
 
MFUMO WA NCHI NA MFUMO WA 'CHAMA'
KIPI NI KIKWAZO KATIKA KUREKEBISHA MAMBO?

Tumeongelea sana kuhusu mfumo.

Wenye mashaka wanauliza mfumo ni kitu gani pengine kwa kutojua au kwa kujua ilimradi tu kuua hoja nzito tunayoijaribu kuikwepa kwa harakati za muda

Tuseme kwa uchache mfumo (system) jinsi ya mipango, uratibu na utekelezaji ukianisha majukumu kwa kundi au watu mmoja mmoja katika utaratibu unaoonekana.

Kwa mfano , mita za bandarini hazifanyi kazi bila hatua, kuna tatizo

'Wakubwa' wanakurukana bila maelezo mita zipo chini ya wizara, idara au mamlaka gani

Vyombo vya dola vipo kimya muda wote mita zikifungwa.

Hakuna anayejua nani amezifunga na kwa madhumuni gani, ni suala la kurukana

Katika hali hiyo kilichoshindwa si mtu au watu bali mfumo mzima usioelezeka.

Mfumo usioweza kutoa majibu, wala kuzuia mianya ya kutumika vibaya.

Ndivyo ilivyo kwa taasisi na mashirika. Hakuna uratibu si utendaji tu bali usimamizi.

Kuna tatizo kubwa tusiloliona. Chama kama isemwavyo, ni kikubwa kuliko mtu

hakuna mtu maarufu zaidi ya CCM. Na kwamba viongozi wanasimamia sera za chama

Akiwa Singida,Rais alisema watendaji wote lazima wasimamie sera za CCM
Hivyo, Rais anakipa chama nguvu zaidi za kudhibiti serikali

CCM imechukiwa na wananchi, si kwasababu ya jina au sera bali wanaosimamia sera

Kashfa zinafanywa na viongozi -CCM walioteuliwa au Wabunge wenye dhamana serikalini

Hakuna hatua zinazochukuliwa na CCM kwa wahusika.
Sababu ni wahusika kuwa katika 'mfumo' wa chama na kuwa vigumu kuwashughulikia.

Tumesikia hadithi za mgamba na mwisho wa siku kashfa zinazidi kulundikana

Jitihada zinazoitwa kutumbua majipu zinagusa sehemu ya 'mfumo wa CCM'

Kwa bahati mbaya hakuna mwenye uwezo wa kushughulikia '...maarufu zaidi ya CCM''

Hata kama mfumo wa serikali utarekebishwa, huu wa CCM ni mgumu kuurekebisha

Rais atajikuta na wakati mgumu 'sera ni za chama na hakuna maarufu zaidi ya chama'

Tayari jitihada za kulinda mfumo wa chama zimeanza.

Wabunge -CCM wameshindwa changamoto ya waliokichafua kushika madaraka

Haitarajiwi waliotajwa kila kashfa nchi hii wanaweza kuwa sehemu ya uongozi wa bunge

Na sasa hatua zaidi za kujipanga ili kudhibiti chama zinaendelea

CCM itamkabidhi chama Magufuli akiwa ameshapangiwa 'watu' kutoka mfumo ule ule

Inaendelea...
 
MWENYEKITI WA CCM KUPEWA CHAMA NA 'MFUMO ULIOKAMILIKA'

Kama nia ni kusafisha uchafu, nia hiyo ingeanza ndani ya CCM ili kupata watu safi watakaosaidia kusafisha maeneo mengine ikiwemo serikalini. Sivyo inavyotokea sasa!

Pengine mwenyekiti mtarajiwa angependelea asimamie hatua safi za kukisafisha chama
Hilo haliwezekani, si kwa bahati mbaya ni kwa makusudi kabisa

CCM na wenye 'mfumo' wanataka kujipanga wakielewa wazi, kwa wanachokiona ni ngumu kutabiri hatma yao. Hivyo, ni vema wakajipanga ndani ya chama kwanza

Hatua za awali ni kama tunazoziona bungeni kwa wenye mfumo kushika maeneo nyeti

Majuzi ,CCM imetangaza nafasi kwa wagombea katika nafasi tofauti

Inasemekana uenyekiti wa CCM atakabidhiwa mwezi wa sita( hakuna uhakiki)
Hata hivyo, tukubali kuwa tayari kwa muda uliopo wenye chama wanajipanga

Mwenyekiti mpya atapewa chama watu wakiwa wameshajipanga vizuri
Na kwa hatua anazochukua, kasi ya kujipanga ni kubwa kuliko kuimarisha chama

Mwenyekiti mtarajiwa atakumbana na nguvu ya wenye mfumo

Na kwavile chama ni zaidi ya mtu au umaarufu, jitihada zinazoonekana zitakwama

Laiti Magufuli angepewa serikai/chama kwa pamoja pengine mambo yangekuwa tofauti

Kwa hili la kusbiri muda majeruhi wakionekana,hakuna shaka chama kitamdhibiti mbeleni

Na kwavile hakuna maarufu au zaidi ya chama, jitihada zake zitawezekanaje?

Ndio maana tunauliza, kipi kianze, kudhibiti mfumo wa chama uliotufikisha hapa na unaonekana kurithishana kwa miongo kadhaa au kudhibiti serikali kwa majipu?

Tunajua chama ndicho chenye serikali! nani anamfunga paka kengele miongoni mwao?

Hili la znz ni dalili za chama kudhibiti 'shughuli' na woga wa ku deal na wenye chama

CCM ikiwa ni ile ile, mambo yatakuwa ni yale yale,. Ni suala la muda tu

Tusemezane
 
KWANINI WATANZANIA HAWATAKI NA NI WAVIVU WA KUHOJI!
KWANINI KUHOJI IONEKANE NI KOSA AU UTOVU WA NIDHAMU?


Mwandishi wa CNN GPS Farid Zakharia miezi michace iliyopita alima maneno haya ' Siasa za Marekani hazina stara ya kujadili mambo ya kitaifa tofauti na China, mambo hufanyika kwa 'siri'Zakharia akasema, uwazi wa siasa za Marekani ni jambo lenye afya.

Akatolea mfano wa masoko ya dunia yanavyoyumba(stock market volatility) na kupoteza thamani za mabilioni ya dola ya wawekezaji

Hayo yanasabibishwa na kuyumba kwa masoko ya china yenye uchumi namba 2 duniani.

Farid akasema, hakuna aliyejua nini kinaendelea katika uchumi wa China uliokuwa unakua kwa kasi ya kiwango cha asilimia 10.

Hivyo hakuna anayejua nini kinaendelea na kutishia mdororo wa uchumi duniani

Ushahidi wa maneno ya Farid unaonekana katika kampeni za kumrithi Obama.

Wagombe wa Democrat , Hillary Clinton na Bernie Sander wanapingana na sera ya afya (Obamacare) kwa mantiki wakieleza mitazamo tofauti kama ilivyo republican

Marekani wanachama wanapingana hadharani, wanaongozwa na dhana ya Kuhoji

Watanzania kuhoji ni ' utovu wa nidhamu au kosa' Tupo katika fikra za kuaminishwa, anayehoji anapinga, mpinzani, mtovu wa nidhamu n.k.

Hatujifunzi kutokana na makosa. Tuliambiwa uchumi utapaa, hatukohoji kwa njia gani.

Tukaambiwa Tunaenda uchumi wa kati, hatukuhoji. Kukopa ni jambo la kawaida hatukuhoji kwanini tunakopa. Serikali ikaanza kukopa mabenki binafsi, hatukhoji

Serikali haina pesa za mishahara, hatukuhoji. Pesa za bunge la katiba zikapatikana, hatukuhoji kutoka wapi na kwanini hatukuwa nazo.

Orodha inaendelea na leo kila mmoja ameshika kichwa, kumbe tulikuwa tunatia maji katika pakacha linalovuja, tunatahamaki na kauli mbiu na majipu

Sasa yanatokea mengine kuhusu elimu bure,tunapewa sababu rahisi kwa maswali mazito

Hatukuhoji ndio maana tunapelekwa kulia kushoto. Wanajua hatuhoji

Elimu bure..... inaendelea
 
Back
Top Bottom