SoC04 Mchango wa Imani, elimu na siasa katika maendeleo ya nchi yetu. Je, inawezekana Tanzania kuwa na sura mpya?

Tanzania Tuitakayo competition threads

Buzi Nene

Senior Member
Feb 10, 2020
142
311
Utangulizi.

Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Mjadala huu si kwaajili ya kuisema vibaya serikali au chama chochote cha siasa, wala kudhalilisha jamii yoyote ya kitanzania bali ni kwa ajili ya kujenga, kama mwanchi wa kawaida nimeona baadhi ya vitu ambavyo ni vikwazo ambayo vinadhorotesha ustawi na mendeleo ya nchi yetu.

Mjadala huu utagawanyika sehemu kuu mbili na kila sehemu itakuwa na vipengele vidogovidogo.

Sehemu ya kwanza nitazungumzia na kuonyesha changamoto ambazo zinadhorotesha maendeleo,sehemu ya pili ni mapendekezo ya namna ya kuboresha.

SEHEMU YA KWANZA

Vizingiti vya mabadiliko.


Ili Taifa lolote liweze kusonga mbele vitu vitatu vina mchango mkubwa katika kufanikisha hilo ,haviwezi kutenganishwa, wala kitu kimoja au viwili haviwezi kuleta matokeo yaliyokusudiwa,ni lazima vyote vitatu vifanye kazi kwa pamoja.Vitu hivyo ni 1.Jamii iliyo staarabika 2. Elimu na maarifa bora 3. Utawala bora.

1. Jamii kama kizingiti cha mabadiliko katika taifa .

Dini na Mila na desturi zetu vina mchango mkubwa sana kwenye maendeleo yetu. Sote lazima tukubaliane kwamba ili jamii iweze kuendelea lazima iweze kutafuta ufumbuzi wa changamoto na matatizo yanayoikabili kwa kutumia njia sahihi kwa wakati husika,hivyo kama jamii inakabiliana matatizo na changamoto kwa kukimbilia kwa waganga,maombi au matambiko ni ngumu kupata utatuzi wa muda mrefu wa matatizo yanayoikabili, hii ni sawa na kusema jamii yetu kwa kiasi kikubwa inakimbia matatizo yaliyopo bila kufahamu.

Ujinga kama kitu cha kawaida katika jamii.

Suala la ujinga Tanzania lipo ndani kwenye mila na desturi zetu. Ujinga ni sehemu ya maisha ya kawaida ya mtanzania,kwenda kwa waganga,mizimu,matambiko, nk..

Ujinga unapelekea watu kutofuata kanuni bora za kuishi na afya,Ujinga na umaskini ndo vinapelekea watu kuamini ushirikina, jamii iliyojaa wasioelimika ni ngumu kuendelea kwasababu hawawezi kutatua matatizo kwa kutumia njia sahihi; kuna wasomi bado wanaamini magonjwa yanaweza kutibiwa kwa waganga wa kienyeji tofauti na hospitaliini, tulishuhudia wasomi wengi walienda Loliondo ,au kupiga vita chanjo kwa visingizio mbalimbali.,rejea taarifa watumishi wa serikali kuchomwa moto kule Dodoma baada ya mchungaji wa kanisa kuwaagiza waumini wafanye hivyo.



Imani za kidini na mila potofu

Sote tunakumbuka ile topic kule Shuleni inayosema (Religion is an opium, kwa kiswahili dini ni ulevi). Watu wengi wameleweshwa na dini kwa kiasi kikubwa na kufanya wawe kama wamefumbwa akili au kuwa kama wajinga. Dini zimelewesha watu wengi kiasi kwamba wamekuwa wakibadili misikiti na makanisa kutafuta majibu ya maswala ya kimaisha ambayo yanatatulika kisayansi,bado wapo wanaoamini kwamba kutokea kwa majanga kama mafuriko ni kudra za Mungu na sio mabadiliko ya tabia ya nchi au sababu za kisayansi.

2. Mchango wa elimu na maarifa katika jamii

Ni ukweli usiopingika kwamba elimu inayotolewa nchini ni elimu ambayo imejikita zaidi kwenye kutoa maarifa ya nadharia zaidi kuliko vitendo,ukiangalia kwa makini hali ni mbaya kwenye shule za ufundi,vifaa vya kujifunzia kwa vitendo ni vichache na vya kizamani,sera za uvumbuzi wa kisayansi hazipewi kipaumbele.Elimu ambayo imejikita zaidi kinadharia kuliko vitendo hawezi kusaidia taifa katika uvumbuzi.Elimu yetu ipo focused kutoa vijana wanaohitaji kajiriwa kuliko kujiajiri,matokeo yake ni kuongezeka kwa idadi ya vijana tegemezi katika taifa.

Vyuo vya ufundi stadi kutopewa kipaumbele namba moja.

Serikali inapaswa kuboresha sana na katika vyuo vya sayansi na ufundi stadi,hii ni sehemu ambayo itasadia vijana wengi kuweza kujiajiri,vyuo vya ufundi,na sayansi kama DIT vinatakiwa kuwa kila wilaya ndani ya nchi yetu ili vijana waweze kusomea ujuzi una uvumbuzi.

Mitaala ya elimu inayotumika mashuleni na vyuoni inasababisha wanaohitimu kukosa uwezo wa kudadavua hoja,au hata kutumia walichokisomea kuleta Mafanikio ndani ya nchi yetu,mitaala mingi imepitwa na wakati na inahitaji kurekebishwa kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

3. Athari za siasa katika maendeleo ya nchi.​

Ili taifa liweze kuendelea linahitaji wanasiasa ambao wana uchungu na Nchi yao,ambao ni wazalendo wa kweli na ambao wa nia ya kweli ya kuwasaidia wananchi,kinyume chake siasa hugeuka kama chombo cha kuwanyonya,kukandamiza;mfano wa siasa mbaya ni kama ifuatavyo

Kuchanganyika kwa siasa na shughuli za kiutendaji za serikali.

Kikatiba serikali yetu ina mihimili mitatu ambayo ni, Bunge, Mahakama na Serikali kuu; lakini ukija kwenye uhalisia wa utendaji wa serikali ya sasa,Mhimili wa serikali kuu una nguvu kuliko mihimili miningine ambayo inaonekana kama matawi ya serikali kuu,kwa sasa serikali kuu ina nguvu ya kuathiri maamuzi ya mahakama na maamuzi ya Bunge.

Rushwa na ulaghai katika miradi

Baadhi ya viongozi waliopo madarakani hufanya maamuzi kwa ajili ya kujinufaisha kisiasa na si kwa nia ya kusaidia wananchi,wakati mwingine wamekuwa wakifanya maamuzi bila kusikiliza ushauri wa wataalamu,mfano mzuri,ni masoko na stendi za mabasi katika miji mbalimbali zilizojegwa sehemu ambazo sio rafiki kwa wananchi,na kupelekea wananchi kususia maeneo hayo.

Watawala kushindwa kuwajibishana.

Tumekuwa tukishuhudia maafisa wengi wa serikali waliofanya makosa kinyume na maadili ya utumishi wa uma wakishindwa kuchuliwa hatua na mamlaka husika, na badala yake huhamishwa kutoka sehemu moja Kwenda sehemu nyingine,vyombo vya ulinzi na usalama kama,tumeona kesi za viongozi zikifutwa,kupewa adhabu ndogo tofauti na ukubwa wa makosa.

SEHEMU YA PILI.

Namna ya kutoka hapa tulipo


Ili Tanzania kama nchi iweze kubadilika na kufanikiwa kufikia matarajio ya wananchi, ni lazima kama taifa tufannye mabadiliko katika sehemu zifuatazo.

Kupata katiba mpya

Kwa kiasi kikubwa matatizo mengi ambayo yanaikabili nchi yetu ni kutokana na ombwe kubwa la kiungozi ambalo limesababishwa na matatizo katika katiba yetu ya sasa;Katiba ya sasa inampa Raisi madaraka makubwa kama Mungu, katiba ya sasa inafanya ile Mihimili ya Bunge na Mahakama isiwe na nguvu yoyote.

Kubadilisha mitaala ya elimu.

Serikali iwekeze nguvu nyingi katika kuviwezesha vyuo vya sayansi na ufundi mabadiliko yanaweza kupatikana,serikali ijenge angalau chuo kimoja kila mkoa mfano wa DIT,na uvumbuzi wa kiteknolojia uwe ni kipaumbele chetu kama taifa.

Mapinduzi mabadiliko ya kifikra,

Kuwe na taifa lenye wananchi ambao wana kiu ya maendeleo,wananchi ambao ni wazalendo,wanachi wanaofanya kazi kwa bidiii, Raisi wa awamu ya tano Mh Pombe Magufuli aliweza kufanya kwa vitendo kwenye kubadilisha fikra za watanzania, kwa kusisitiza wananchi kufanya kazi kwa weledi,kuacha ubabaishaji,unafiki, uongo, na kujenga tabia ya kusema ukweli hata kama ni mchungu.

Mwisho.

 
Ujinga unapelekea watu kutofuata kanuni bora za kuishi na afya,Ujinga na umaskini ndo vinapelekea watu kuamini ushirikina, jamii iliyojaa wasioelimika ni ngumu kuendelea kwasababu hawawezi kutatua matatizo kwa kutumia njia sahihi; kuna wasomi bado wanaamini magonjwa yanaweza kutibiwa kwa waganga wa kienyeji tofauti na hospitaliini, tulishuhudia wasomi wengi walienda Loliondo ,au kupiga vita chanjo kwa visingizio mbalimbali.,rejea taarifa watumishi wa serikali kuchomwa moto kule Dodoma baada ya mchungaji wa kanisa kuwaagiza waumini wafanye hivyo.
Kweli mwanangu, ujinga ni mzigo.

Mapinduzi mabadiliko ya kifikra,

Kuwe na taifa lenye wananchi ambao wana kiu ya maendeleo,wananchi ambao ni wazalendo,wanachi wanaofanya kazi kwa bidiii, Raisi wa awamu ya tano Mh Pombe Magufuli aliweza kufanya kwa vitendo kwenye kubadilisha fikra za watanzania, kwa kusisitiza wananchi kufanya kazi kwa weledi,kuacha ubabaishaji,unafiki, uongo, na kujenga tabia ya kusema ukweli hata kama ni mchungu.
UMepiga penye mzizi wa tatizo. Ahsante.
 
Back
Top Bottom