Duniani kote usafiri wa reli ndiyo rahisi kuliko wote. SGR tulitegemea kuwa kiama cha usafiri wa mabasi na malori, imeshindikana

Wamekuambia Bei rahisi Ni kiasi gani?
Huko hawatumii treni kama hizi za kwetu zenye spidi hii ya kinyonga inayolingana na spidi ya Vitz au Noah. Za kwao ni ndege za chini zinazo fly over the rail in vacuum at a speed of an aeroplane, my dear. Na hazisimami simami njiani. Ni city to city only. Za kwetu ni za kawaida tu za walala hoi.

Engine na mabehewa yake yanaweza kuwa adjusted upana na kuweza kutembea kwenye reli ya MGR yakitumia dizeli kama ulivyoyaona yakichapa kazi juu ya MGR baada ya kuwasili nchini hivi karibuni.
 
Duniani kote usafiri wa reli ndiyo usafiri wa bei rahisi sana kuliko usafiri mwingine wowote. Malengo makuu ya kuboresha usafiri huu kwa kiwango cha SGR yalikuwa:

~Trip moja ya treni ya mizigo ingaliweza kusafirisha mzigo wa sawa na semi-trailers za malori 500 kwa mara moja, kwa spidi ya 120 kph na kwa bei ya sawa na bure ukilinganisha na malori.

Yaani mzigo wa ukubwa huo wa semi trailer 500 ungeweza kuondolewa kutoka bandari yetu ya Dar es Salaam kila siku na kufikishwa Mwanza au Kigoma ndani ya masaa 10 au 12 tu. Hakungalikuwa tena na mrundikano wa mizigo pale bandari ya Dar es Salaam.

Hata hizo bandari kavu zilizoko mkoa wa Dar es Salaam zingalikosa kazi. Bandari kavu zingalijengwa Mwanza na Kigoma. Uchumi wa nchi ungepaa kwa kasi kubwa na ndani ya muda mfupi tungeifikia Singapore ambayo uchumi wake unategemea bandari tu.

Barabara zetu zingalidumu zaidi kwani usafiri wa malori unalifikia kiama chake. Hata hizo ajali lukuki za barabarani zinazosababishwa na malori haya katika njia hizi kuu zingalifikia tamati. Traffic police wetu wangetafutiwa kazi zingine.

~ Hivyo ndivyo ingalikuwa kwa usafirishaji wa abiria. Trip moja ya passenger train yenye urefu wa si chini ya kilomita 3 ingalikuwa sawa na mabasi yasiyopungua 500 na wangalisafirishwa kwa raha kwa spidi ya 170 kph.

Yaani kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza au Kigoma ni mwendo wa saa 7 tu, kwa bei ya chee ukilinganisha na mabasi ambayo nayo yalikuwa yafikie kiama chake kwa njia hizi kuu za uchumi wa nchi na kuokoa uharibifu wa barabara zetu na ajali lukuki za barabarani. Uchumi wa nchi ungalipaa na wananchi wangalipata furaha.

Bahati mbaya kabisa matarajio hayo ya wananchi yameshindikana kufikiwa. TRC imepanga nauli za train hizo za spidi kubwa kuwa mara tatu ya bei za usafiri wa mabasi. Kwa sasa mtu anasafiri kwa basi kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa nauli ya Sh 55,000 hadi 65,000.

Hii ni nauli ya kupanda kwa mafuta kwa sababu ya Ukraine. Kabla ya hapo ilikuwa Shs 35,000 hadi 45,000 na tunategemea hiyo Ukraine itakapokwisha bei hizi zitarejea. Sasa TRC wamepanga ziwe Sh 150,000 kwani hadi Dodoma tu ni Sh 75,000. Yaani ni karibu sawa na nauli ya ndege. Hawa Waha na Wasukuma wetu kweli watazipanda hizo treni?

Bado TRC hawajatoa nauli za mabehewa ya mizigo. Kwa mantiki hiyo hiyo bei inayotarajiwa ni mara tatu ya bei ya kukodi lori la semi trailer. Hivyo tutegemee mambo kubaki kama kawa. Matajiri wa malori na mabasi wamekataa kufika kiama.

Wameshinda hiyo vita na inasemekana hata hizo treni za SGR zitaendeshwa na wafanya biashara binafsi kwa mtindo wa PPP (private public partnership)! Ni wajanja, wametupokonya SGR yetu tuliyoijenga na tunaendelea kuijenga kwa kodi zetu. Zingine tumekopa lakini tutazirejesha kwa kodi zetu.

Mapendekezo:
1. Nauli ya abiria kutoka Dar had Mwanza isizidi Sh 25,000 kwa economy class. Yaani isizidi nusu ya nauli ya basi. Hayo madaraja mengine mnaweza kuweka mnavyotaka. Hao wanaoishia njiani hususani Dodoma ziende kwa uhusiano huo wa umbali hadi Mwanza.

2. Behewa la mizigo bei yake isizidi theluthi moja ya bei ya kukodi lori.

3. Hakuna mantiki ya kuwa na tofauti ya nauli kati ya MGR inayotumia dizeli na SGR inayotumia umeme. Kwa vyovyote vile uendeshaji (running cost) ya ile ya umeme ni rahisi kuliko ile ya dizeli.

TRC lazima ijue kuwa jukumu lake ni kutoa huduma na si biashara ya kutaka kurejesha kile serikali imewekeza kwenye huo mradi wa SGR. Wanachotakiwa ni kukusanya tu pesa itakayowawezesha kulipa mishahara ya staff wao na mambo mengine ya uendeshaji.
Duniani kote? Si kweli Japan, China na nchi nyingi Ulaya usafiri wa treni si bei rahisi hivyo kama unavyodai!
 
Duniani kote? Si kweli Japan, China na nchi nyingi Ulaya usafiri wa treni si bei rahisi hivyo kama unavyodai!
 
Huko hawatumii treni kama hizi za kwetu zenye spidi hii ya kinyonga inayolingana na spidi ya Vitz au Noah. Za kwao ni ndege za chini zinazo fly over the rail in vacuum at a speed of an aeroplane, my dear. Na hazisimami simami njiani. Ni city to city only. Za kwetu ni za kawaida tu za walala hoi. Engine na mabehewa yake yanaweza kuwa adjusted upana na kuweza kutembea kwenye reli ya MGR yakitumia dizeli kama ulivyoyaona yakichapa kazi juu ya MGR baada ya kuwasili nchini hivi karibuni.
Mtajuana huko huko na ma sgr yenu,kwanza Hilo limradi sijawahi likubali hata siku Moja Ni tembo mweupe Kama Ndege zenu mtumba
 
Umeme lazima uwe ghali zaidi ili kuoffset artificial costs zinazosababishwa na ufisadi ambao bado unaendelea kutendwa TANESCO.
Sio umeme tu, projects zote za Serikali costs zake huwa x3 zaidi ya uhalisia!
 
  • Thanks
Reactions: RMC
Dr Akili,

Tatizo lako kwenye mijadala unasema "Dunia kote" bila kuwa na data. Kwa nchi nyingi za EU bei ya ticket za treni ya mwendo kasi ni zaidi ya ticket za ndege.

Lakini lingine mfano usafiri wa malori sio mbaya inategemea nchi gani hata nchi za wenzetu mfano hapa US usafiri wa malori ni mkubwa sana kiasi kwamba kuna upungufu wa madereva. Hii ni kwasababu ya kuongezeka kwa mitandao na watu kununua vitu mitandaoni. Hivyo sio kweli inabidi tutengeneze barabara zetu vizuri bado na hii reli sana sana itapunguza tu mizigo sio kumaliza
Sasa km nauli ya Treni ni kubwa kuliko ya ndege si Bora kupanda ndege ambayo kwanza nitatumia muda mfupi kufika,km Hali ya nauli itakua ivi ni mtu gani atapanda izo Treni wakati ndege zipo?hapa pesa za wananchi zimepotea bule

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Leo Dr Akili umeamkaje..?

Yaani umetoa hoja mujarabu mpaka nimekupa "like✓"

Yes. Nakubaliana na wewe. Na hili na TRC kupanga nauli hizi limemshangaza kila mtu kiasi cha kuondoa maana kabisa ya ujenzi wa reli ya SGR. Hata kwenye ile reli ya MGR nauli hazikuwa ghali kiasi hiki...

Mimi naanza kupata shaka hata unafuu wa umeme tunaoambiwa kuwa utapatikana baada ya ujenzi wa bwawa la umeme la Stiglers George...

Tusije kushangaa umeme huo ukaja kuwa ghali zaidi ya huu wa sasa..!!
Mkuu Mimi pia nimeshtuka sana sasa km bei ya Treni ni sawa na ndege ivi kuna haja ya kupanda Treni ambayo inatumia masaa 7 wakati nauli yake ni sawa na ndege yenye masaa 2

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Sio kuwa watapinga bali wataelekezana nyinyi fanyeni hiki sisi tunafanya hiki kumbuka wanafanya kwa team work kila fisadi anaplay part yake mwisho wa siku mfumo kamili wa ufisadi unakuwa operational.

Juzi Dr Bashiru amesema katika uchaguzi uliomalizika wa CCM mafisadi walikuwa wanasimika wawakilishi wao NEC na alisemq wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kwa mtindo huu miziz imekomaa na ni ngumu kuikata, hii nchi ni ngumu sana maana uzalendo hakuna,kila mtuanawaza tumbo lake na boss amewapa ruksa ya kula kwa urefu wa kamba zao
 
Tanzania kwa sasa inahitaji treni za kawaida tu, SGR ni anasa zisizo za lazima na white elephant project.
 
Duniani kote usafiri wa reli ndiyo usafiri wa bei rahisi sana kuliko usafiri mwingine wowote. Malengo makuu ya kuboresha usafiri huu kwa kiwango cha SGR yalikuwa:
Kama umewahi kufika huko duniani basi labda India na zile treni zao!

Duniani kwa maana ya duniani, kama unazungumzia treni zenye ubora, nauli ya treni ni very expensive ukilinganisha na nauli za mabasi

Na kama treni zenyewe ni bullets trains, ndo wala usiguse... Kibongo bongo kama unaleta Bullet Trains basi watakaoweza kupanda ni wale tu wenye uwezo wa kupanda ndege!
 
Wapi duniani usafiri wa treni ya haraka bei rahisi? Tupe mfano wa nchi 3 tu duniani?

Mtu uko Chato huko hata Dubai tu hujafika unaleta uongo wako hapa.
Itakuwa anazungumzia India huyu na zile treni zao unazokuta abiria wamejazana juu!!
 
Back
Top Bottom