Dunia bila ya Ukiranja wa Marekani itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana

Tangu Marekani iwe kiranja dunia imekuwa na amani, maendeleo, utangamano na mafanikio zaidi kuliko wakati wowote hii ni pamoja na madhaifu na matatizo yote ambayo Marekani inatuhumiwa nayo.
Kuanzia katikaki Karne ya 19 baada ya WWII hadi karne ya 21 ndicho kipindi dunia imezidi kuboreka zaidi kuliko karne nyingine zozote.
Walikuwa wapi Rwanda mpaka wanachinjana ,DRC kukosa amani ,mauaji ya kutisha vita vya Bosnia mpaka kambi ya wakimbizi iliyokuwa chini ya UN kupigwa bomu na kuua innocent civilians ? tena baada ya tension ya Bosnia kuwa kubwa na mauaji ya kutisha Bill Clinton akajitokeza kupatanisha wakati damu nyingi zishamwagika.
 
Kuchinjana ndio kunakuwa vipi ? fafanua
Dunia isiyo na hofu dhidi ya kuchukua uhai wa wengine na ubaguzi Wa kiimani, rangi, uwezo wa mali kuwa kigezo cha kuua watu.

Umetolea mfano wa Rwanda ambapo wakati wa mauaji ya Kimbari Ile tu mtu kuwa Mtutsi ilitosha kuuawa.

Ukiangalia kwa undani nchi zinazoungana kupambana na ukiranja Wa Marekani nyingi kati yake kumkosoa kiongozi inatosha kuutoa Uhai wa mtu.
 
Huu ndiyo ukweli hata kama ni mchungu.

Siku Urusi au Uchina, au Iran mojawapo ikawa ndiyo inasimamia maslahi ya ulimwengu wetu huu, dunia itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana na mwenye nguvu mpishe apite.
Inaonesha historia ya Dunia huijui ndio maana unaona kama Marekani ndio sululisho la usalama na amani Duniani sio kosa lako but sivyo unavyofikiria ili ujue itabidi utoke kwenye ilo box ulilojifichia ndio utaelewa au tukusaidie kubomoa hili box
 
Huu ndiyo ukweli hata kama ni mchungu.

Siku Urusi au Uchina, au Iran mojawapo ikawa ndiyo inasimamia maslahi ya ulimwengu wetu huu, dunia itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana na mwenye nguvu mpishe apite.
Sasa hivi umefika wakati lazima kuwe na balance of power utake usitake.

Na dola ikiondolewa kwenye mzunguko wa BRICS ndo utaelewa.

Sasa hao unowaona bora ndo walimuua Gaddafi kwa kutaka kuiunganisha Afrika sasa hivi ni Russia, China na Iran zimeamua Duniani kuwe na "Balance of Power".

Ndo Multipolar World hiyo.

Ikifika hapo ndo utapata akili uzuri na utajitambua.
 
BRICS haina ubavu wa kuindoa dollar,hilo sahau.

Sent from my Mi 9T using JamiiForums mobile app
 
Sasa hivi umefika wakati lazima kuwe na balance of power utake usitake.
Hayo mambo ya "Balance of power" ni kati ya nani na nani na ikishatokea dunia itafaidikaje?
Na dola ikiondolewa kwenye mzunguko wa BRICS ndo utaelewa.
Dollar inaondolewaje BRICS. Yaani hizo nchi za BRICS hazitafanya biashara na Marekani?
Sasa hao unowaona bora ndo walimuua Gaddafi kwa kutaka kuiunganisha Afrika
Hivi Gaddafi ni wakati Gani alitaka kuiunganisha Afrika?
Sasa hivi ni Russia, China na Iran zimeamua Duniani kuwe na "Balance of Power".
Wanataka kuwe na "balance of power" au wao wanataka kuwa na "Power monopoly" Kwa nchi masikini zenye rasirimali asilia lakini zisizo na weledi wa kujiongoza?
Ndo Multipolar World hiyo.
Sawa.
 
Hayo mambo ya "Balance of power" ni kati ya nani na nani na ikishatokea dunia itafaidikaje?

Dollar inaondolewaje BRICS. Yaani hizo nchi za BRICS hazitafanya biashara na Marekani?

Hivi Gaddafi ni wakati Gani alitaka kuiunganisha Afrika?

Wanataka kuwe na "balance of power" au wao wanataka kuwa na "Power monopoly" Kwa nchi masikini zenye rasirimali asilia lakini zisizo na weledi wa kujiongoza?

Sawa.
1. Balance of power kwa maana kwamba kila nchi itatumi asarafu yake au commodity yaani bidhaa kama dhahabu au mafuta ghafi au gesi asilia.

2. Ikiwa matumizi hayo yatakuwa ndo yatumiwa na nchi hizi basi Dola itakosa nguvu na nchi nyingi zitakuwa zatumia mali asili kufanya biashara.

3. Gaddafi alitaka Afrika iwe na sarafu moja na pia iwe na uwakilishi mmoja katika vyombo kama UN, World Bank na IMF.

4. Hiyo Power monopoly uisemayo ndo aliyo nayo Marekani kwenye matumizi ya dola na ikiondolewa hiyo hakutakuwa na nchi itayolazimishwa kutumia dola.

Sikatai, kuundwa kwa BRICS na kuimarika kwake kutategemea wanachama wake waandamizi Russia, China, India, Brazil na Afrika Kusini wana misimamo ipi.

Bado njia ni ndefu.
 
Walikuwa wapi Rwanda mpaka wanachinjana ,DRC kukosa amani ,mauaji ya kutisha vita vya Bosnia mpaka kambi ya wakimbizi iliyokuwa chini ya UN kupigwa bomu na kuua innocent civilians ? tena baada ya tension ya Bosnia kuwa kubwa na mauaji ya kutisha Bill Clinton akajitokeza kupatanisha wakati damu nyingi zishamwagika.
Jiongeze, mimi naongelea dunia kwa ujumla na ukubwa wake sio nchi moja moja.

Ukiambiwa Marekani ni tajiri kuliko Tanzania haimaanishi kwa sababu kuna homeless na masikini huko basi haiwi tajiri kuliko Tanzania.
 
Hata wewe pia umeandika kwa hisia sana.

Sikuweka maelezo Kwa kuwa Kwa kufuatilia kinachoendelea kwenye medani za kimataifa inaonesha watu wasiotaka Marekani iwe kiranja wa dunia wanaonesha nia yao Hiyo hadharani.

Kwa kuangalia hao wanaotamani wawe viranja Wa dunia wanavyoendesha nchi zao.

Jibu namba Moja linatosheleza hapa.

Kuna ushahidi wa kutosha tu

Angalau Hitler pekee ndiye aliyetaka uwe uwanja wa kuchinjana. Haijawai Kwa milenia mbili Sasa.

Yap. Hapa sizungumzii Vita.
Majibu yako yapo shallow mno.
Unajibu bora liende tu.

Nimekuuliza kwanini unajibu eti kulingana na yanayoendelea!!!! This is a childish answer. Mtu msomi na GT hawezi akajibu kizembe hivi. Mada umeianzisha imekushinda uwezo.

Ukiulizwa kwanini lazima utoe sababu za:-
1. Kijamii
2. Kiuchumi
3. Kisiasa.

Ueleze kiundani kwanini unasema dunia itakuwa uwanja wa kuchinjana?
Toa mifano kwa kutumia statistical data.

Leta references ku support majibu yako.

Leta mlinganisho kuanzia baada ya vita vya pili vya dunia mpaka sasa nchi zipi zimeua watu wengi ndipo uweze fanya forecast ya future.

Ukianzisha topic nzito usilete majibu mepesi kama mtoto wa chekechea.

Hilo ni swali moja nahitaji elaboration kabla hatujaendelea na maswali mengine.

Karibu ujibu........
 
Kwani Libya, Iraq, Syria, Vietnam na kwingineko USA na washirika wao walipozivamia na kujaribu kuwaondoa na kuwaua viongozi na raia wasio na hatia, walikuwa viranja wa dunia?

Kote USA na washirika wake walipopita wameacha maafa maakubwa, na hizo nchi hakuna amani wala utulivu tena.

Allen Kilewella huo ukiranja unaompamba nao USA ni huo wakumpa uhuru mke wako au kijana wako akaolewe na jinsi yake? Vipi siku mke wako akaomba talaka ili akaolewe na mwanamke mwenzake, utarudi hapo kumsifia?

Hao walikua wakaidi na hawakutaka kutii na kuleta amani,hizo nchi ulizo zitaja viongozi wake walikua wafadhiri wa vikundi vya kigaidi walistahili walichokipata mbwa wale.
 
Huu ndiyo ukweli hata kama ni mchungu.

Siku Urusi au Uchina, au Iran mojawapo ikawa ndiyo inasimamia maslahi ya ulimwengu wetu huu, dunia itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana na mwenye nguvu mpishe apite.
The world is soon going to be under one political government
 
Kwani Ushoga umeanza baada tu ya taifa la Marekani lilipoanzishwa??

Kabla ya Marekani kuwepo kulikuwa hakuna ushoga duniani?

Huwa na shangaa sana,mana hata vitabu vyao vya dini vinautaja ushoga,manake umeanza zamani sana hata kabla ya kufikiriwa kuwepo kwa taifa la marekani,pia wanashindwa kutambua sera za taifa la marekani,its a free world where every one is free kuishi maisha anayoyataka bila kuingiliwa.
 
Chini ya ukiranja wa USA kumetokea mauji ,vifo na vita vingi mno.

Mifano;
Rwanda ,Lebanon,Sudani,Bosnia nk

Mauwaji na vifo vingi yametokea kila empire duniani,hata zenji hapo wanauana kisa madaraka.
 
1. Balance of power kwa maana kwamba kila nchi itatumi asarafu yake au commodity yaani bidhaa kama dhahabu au mafuta ghafi au gesi asilia.

2. Ikiwa matumizi hayo yatakuwa ndo yatumiwa na nchi hizi basi Dola itakosa nguvu na nchi nyingi zitakuwa zatumia mali asili kufanya biashara.

3. Gaddafi alitaka Afrika iwe na sarafu moja na pia iwe na uwakilishi mmoja katika vyombo kama UN, World Bank na IMF.

4. Hiyo Power monopoly uisemayo ndo aliyo nayo Marekani kwenye matumizi ya dola na ikiondolewa hiyo hakutakuwa na nchi itayolazimishwa kutumia dola.

Sikatai, kuundwa kwa BRICS na kuimarika kwake kutategemea wanachama wake waandamizi Russia, China, India, Brazil na Afrika Kusini wana misimamo ipi.

Bado njia ni ndefu.

Gaddafi hakuwahi kuipenda afrika alitaka kuwatumia waafrika kwa manufaa yake ya kisiasa na kiuchumi,ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa vikundi vya kigaidi. Bora alinyongwa mbwa yule.
 
Back
Top Bottom