Dunia bila ya Ukiranja wa Marekani itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana

Huu ndiyo ukweli hata kama ni mchungu.

Siku Urusi au Uchina, au Iran mojawapo ikawa ndiyo inasimamia maslahi ya ulimwengu wetu huu, dunia itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana na mwenye nguvu mpishe apite.
kiufupi anguko la usa ndo mwanzo wa fujo za karne ya 19 na 20 zitarud tena, ili dunia iwe na amani lzm atokee mmoja awe mkubwa kuliko wengine kwa utofauti mkubwa km usa enzi 1900s , ss nan ataweza ? sio leo lzm tuuane kwanza mpk kieleweke , usa aliifanya dunia itulie imuangalie yeye
 
Walikuwa wapi Rwanda mpaka wanachinjana ,DRC kukosa amani ,mauaji ya kutisha vita vya Bosnia mpaka kambi ya wakimbizi iliyokuwa chini ya UN kupigwa bomu na kuua innocent civilians ? tena baada ya tension ya Bosnia kuwa kubwa na mauaji ya kutisha Bill Clinton akajitokeza kupatanisha wakati damu nyingi zishamwagika.
Wangeingila mapema nyie ndio mngekuwa wa kwanza kusema 'Marekani wanaingilia mambo ya ndani ya nchi zingine'.....wakijivutavuta bado tena mnawatupia lawama.
 
Mtoa mada imebaki kidogo tu uanze kuabudu kuelekea Marekani.
Maana nadhani unaona Marekani ni mbinguni na Rais wake ni Mungu.
 
Aliyehusika na hayo mauaji ni Marekani ?
Yeye si anasifiwa kiranja na mleta amani sasa ameshindwa vipi kuzuia ,kama kiranja haijalishi ameta au hajaleta kazi yake ni kuweka mambo sawa.

Huko Rwanda mfano CIA walikuwa na information kuhusu kila kitu kinachoendelea na kipi kitakuja kutokea lakini hawakufanya lolote la maana mpaka yakatokea yaliyotokea , USA ni kiranja wa mchong.
 
Kuwa kiranja ndio kuingilia mambo ya ndani ya wengine bila utaratibu?....hata hapo Ukraine, Marekani alikuwa na 'Intel' Putin atavamia na akasema ila hakuweza kuifunga mikono Urusi.

Hata yeye (Marekani) ana madhaifu mengi tu mfano vita vya Iraq, ila bado angalau amejitahidi kiasi chake kuwa 'polisi' wa dunia.
 
Jiongeze, mimi naongelea dunia kwa ujumla na ukubwa wake sio nchi moja moja.

Ukiambiwa Marekani ni tajiri kuliko Tanzania haimaanishi kwa sababu kuna homeless na masikini huko basi haiwi tajiri kuliko Tanzania.
Taja sehemu hata 10 ambapo unaweza kusema Marekani kaweka amani .

Tokea WWII dunia imeshuhudia machafuko na mauaji makubwa sehemu nyingi sana.Sifa anazopewa Marekani ni bure labda kama mnaweza kuweka wazi wapi karekebisha au hizo jitihada zake amefanya vipi na baada ya hapo matunda gani yamejitokeza ?
 
1.Marekani ndio alisaidia kumaliza WWII.
2.Bosnia- Herzegovina, Dayton Accords.
3.FARC- Colombia war, Plan Colombia
4. Egypt na Israel, Camp David Accords
5.Korea Kusini.
6.Ujerumani Magharibi na Mashariki 1990.
7.Kuwait dhidi ya uvamizi wa Iraq
8.Panama
9. Uganda, Sudan, CAR dhidi ya LRA
10. Afghanistan dhidi ya uvamizi wa Urusi 1989.
 
Tangu Marekani iwe kiranja dunia imekuwa na amani, maendeleo, utangamano na mafanikio zaidi kuliko wakati wowote hii ni pamoja na madhaifu na matatizo yote ambayo Marekani inatuhumiwa nayo.
Kuanzia katikaki Karne ya 19 baada ya WWII hadi karne ya 21 ndicho kipindi dunia imezidi kuboreka zaidi kuliko karne nyingine zozote.
elaborate more mkuu
 
1.Marekani ndio alisaidia kumaliza WWII.
2.Bosnia- Herzegovina, Dayton Accords.
3.FARC- Colombia war, Plan Colombia
4. Egypt na Israel, Camp David Accords
5.Korea Kusini.
6.Ujerumani Magharibi na Mashariki 1990.
7.Kuwait dhidi ya uvamizi wa Iraq
8.Panama
9. Uganda, Sudan, CAR dhidi ya LRA
10. Afghanistan dhidi ya uvamizi wa Urusi 1989.
Kote huko sehemu nyingi baada ya mauaji ya kutisha , October war alikuwa anatoa msaada kwa Israel mpaka nchi za kiarabu wakakata oil supply .

Case nyingine ni Suez Crisis , Egypt alivamiwa na Israel,France na England kwa wakati mmoja civilians wengi waliuwawa ,wanajeshi ,miundombinu nk kisha US ndio akaja kumaliza mzozo na kuingilia Kati baada ya Egypt kupata hasara kubwa ya mali na uhai.

Mimi point si kusulihisha bali ni kuacha mpaka migogoro inafika violent stage wakati wana intelejensia na uwezo wa kuzuia kabla ya kufika huko.
 
Huu ndiyo ukweli hata kama ni mchungu.

Siku Urusi au Uchina, au Iran mojawapo ikawa ndiyo inasimamia maslahi ya ulimwengu wetu huu, dunia itageuka kuwa uwanja wa kuchinjana na mwenye nguvu mpishe apite.
Sielewi unaumia ukiwa wapi lakini ukweli ni kwamba hakuna jinsi! Hakuna tunachoweza kukusaidia! Hakuna jinsi, USA imeshindwa!
 
Kote huko sehemu nyingi baada ya mauaji ya kutisha , October war alikuwa anatoa msaada kwa Israel mpaka nchi za kiarabu wakakata oil supply .

Case nyingine ni Suez Crisis , Egypt alivamiwa na Israel,France na England kwa wakati mmoja civilians wengi waliuwawa ,wanajeshi ,miundombinu nk kisha US ndio akaja kumaliza mzozo na kuingilia Kati baada ya Egypt kupata hasara kubwa ya mali na uhai.

Mimi point si kusulihisha bali ni kuacha mpaka migogoro inafika violent stage wakati wana intelejensia na uwezo wa kuzuia kabla ya kufika huko.
Wewe kwa nini unafikiri kazi ya kutunza amani ya nchi nyingine zote duniani ni ya Marekani?!
 
elaborate more mkuu
Tangu kuisha kwa vita vya pili vya dunia na Marekani kuibuka kama super power dunia imekuwa na vita vichache na migogoro isiyokuwa mikubwa kulinganisha na kipindi kingine chochote kabla ya mwaka 1945.

Chukulia tu kwa mfano vita kuu mbili za dunia za mwaka 1914 hadi 1918 na 1939 hadi 1945 zilizoanzia Ulaya zilozoua watu karibu million 100, Mwaka 1800 hadi 1900 kulikuwa na vita vya kila aina, revolts, uprisings na mapinduzi karibia kila kona ya dunia. Kabla ya mwaka 1945 kunyang'anyana ardhi na maeneo ya nchi kwa nguvu za kijeshi halikuwa jambo la ajabu wala la kupigiwa sana kelele.

Kuundwa kwa Umoja wa mataifa wazo lilioanza na Woodrow Wilson na msisitizo wa rules based international order kumesaidia sana kuleta amani duniani.

Hapa hatujazungumzia pandemics kama Spanish flu ya mwaka 1918 hadi 25 iliua watu takribani million 25 ambazo zilikuwa zinafagia sana huko nyuma. Mauaji yatokanayo na njaa au ukame ambapo Marekani inawekeza pesa nyingi sana kusaidia kipindi hiki kupambana na mambo kama hayo.
 
Back
Top Bottom