Dullah Mbabe apoteza kwa pointi dhidi ya Eric Katompa, Arusha, Novemba 25, 2023, Dullah alalamikia Majaji

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Mzaramo Abdallah Pazi maarufu kama Dullah Mbabe anapigana na Mcongo, Erick Katompa katika pambano la Uzito wa Super Middleweight Mkoani Arusha

Wawili hao waliwahi kukutana Oktoba 1, 2021 ndani ya Viwanja vya PTA pale Sabasaba Jijini Dar es Salaam ambapo Katompa alimtwanga Dullah Mbabe.

photo_2023-11-25_23-45-55.jpg

Pambano limeanza kwa kasi ndogo

Raundi ya 1: Mabondia wote wameanza kwa kusomana mdogomdogo
Raundi ya 2: Bado wanapigana ngumi za hapa na pale
Raundi ya 3: Dulla anapeleka makonde kwa Katompa lakini Mcongo anakuwa mvumilivu
Raundi ya 4: Mabondia wote wanarushiana makonde kwa zamu
Raundi ya 5: Katompa anaanza kuchanganya kasi, anarusha makonde mengi na anatawala raundi hii
Raundi ya 6: Katompa anaonekana kuwa imara, Dullah kasi ya kurusha ngumi imepungua
1.JPG

2.JPG

Raundi ya 7: Katompa anaendelea kuonesha uimara japokuwa Dullah naye anajibu mapigo
Raundi ya 8: Katompa anajaribu kulazimisha mambo kwa kupiga ngumu mfululizo
DU.JPG
Raundi ya 9: Ngoma ni moto, Dulla anapambana lakini bado ushindani ni mzito
Raundiya 10: Pambano limetawaliwa na hasira, kuna muda mwamuzi akiwa amesimamisha pambano akitoa maelekezo nje Katompa akamvaa Dullah na kuanza kurusha ngumi.

Dullaha akajibu kwa kumpiga kichwa mwenzake wakati pambano likiendelea.

Pambano limekamilika, yanasubiriwa maamuzi ya Majaji.

Katompa ameshinda kwa pointi baada ya majaji wote watatu kumpa ushindi wa pointi 93-97, 93-7 na 92-98.

Akizungumza baada ya pambano hilo Dullah amesema “Sijui Majaji au Chama cha Ngumi kina nia gani na mimi kwa kuwa nimecheza vizuri na mashabiki wameona kilichotokea.”
 
Mzaramo Abdallah Pazi maarufu kama Dullah Mbabe anapigana na Mcongo, Erick Katompa katika pambano la Uzito wa Super Middleweight Mkoani Arusha

Wawili hao waliwahi kukutana Oktoba 1, 2021 ndani ya Viwanja vya PTA pale Sabasaba Jijini Dar es Salaam ambapo Katompa alimtwanga Dullah Mbabe.

Pambano limeanza kwa kasi ndogo

Raundi ya 1: Mabondia wote wameanza kwa kusomana mdogomdogo
Raundi ya 2: Bado wanapigana ngumi za hapa na pale
Raundi ya 3: Dulla anapeleka makonde kwa Katompa lakini Mcongo anakuwa mvumilivu
Dulla mbabe naona anapelekewa moto, raundi ya tano
 
hua hatukosi upumbavu katompa asipofosi ndio basi tena ila kiukwel Dulla hamuwez uyo jamaa
 
Back
Top Bottom