Ndondi: Bondia Ibrahim Class "Mawe" amchakaza Said Chino kwa pointi, Dar es Salaam

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Pambano limeanza

Pambano hili la Ibrahim Class ‘Mawe’ dhidi ya Said Chino linaongozwa na Mwamuzi mkongwe, Emmanuel Mlundwa kwenye Ukumbi wa The Warehouse, Masaki, Dar es Salaam.

Wanawania Mkanda wa Super Featherweight Jijini Dar es Salaaam, kabla ya pambano hili kulikuwa na presha kubwa ya kurushiana maneno baina ya mabondia hao ambao waliwahi kuwa marafiki wa muda mrefu

Raundi ya 1: Mabondia wanasomana na kila mmoja anarusha makonde

Raundi ya 2: Imeanza, Ibrahim katawala sehemu kubwa ya mchezo, akimpiga mara kadhaa mpinzani wake, lakini kulekea mwishoni mwa raundi hii Chino naye akaonesha uhai wa kurudisha makonde.

Raundi ya 3: Wamerushiana ngumi na kila mmoja kaonesha umakini, mashabiki wanaongeza shangwe kila wanapoona punch zinarushwa.

Raundi ya 4: Pambano limekuwa kali, Class anapigwa ngumi na kudondoka, lakini anainuka na kulalamika kuwa amekanyagwa mguuni ndio maana amedondoka.

Ushindani ni mkali na Chino anarusha ngumi kadhaa zinamuingia Class lakini baada ya sekunde kadhaa Class anaonesha utulivu.

Raundi ya 5: Kasi ya mchezo imepungua kidogo, Chino anapata wakati mgumu kufikisha makonde usoni kwa Class ambaye anakuwa mjanja katika kuzunguka ulingoni na kupiga pointi kadhaa.

Raundi ya 6: Chino amerusha ngumi nyingi lakini hazijamfikia mpirani wake, Class ameonesha ujanja mwingi wa kukwepa ngumi na kurusha ngumi kadhaa za pointi.

Raundi ya 7: Ushindani umekuwa mkali, Ibra anaendelea kuzunguka ulingoni licha ya Chino kurusha makonde kadhaa lakini hayafafika sehemu stahiki. Class amejaribu mara kadhaa kurusha Upper cut lakini hazijaingia inavyotakiwa.

Raundi ya 8: Chino ni kama anaelekea kufanikiwa kwa kurusha makonda lakini Class anakuwa makini kukwepa makonde huku akirusha ngumu za pointi.

Raundi ya 9: Chino anatumia nguvu nyingi na analazimika kuzunguka kumfuata mpinzani wake anayezunguka na kurusha ngumi

Raundi ya 10: Raundi ya mwisho imekamilika, Class kaonesha uwezo wa juu wa kucheza na mikono yake, amerusha ngumi nyingi zilizotua usoni kwa mpinzani wake ambaye naye alijibu mashambulizi kadhaa

Pambano limekamilika, wanasubiri majibu ya majaji.

Ibrahim Class ameshinda kwa pointi, majaji wote watatu wamempa ushindi wa pointi 98-91, 97-92, 97-92.

TAMBO ZA MABONDIA ZAENDELEA BAADA YA PAMBANO
Akizungumza baada ya pambano hilo la Raundi 10 lililofanyika Masaki, Dar es Salaam, Class amesema “Nilijua nitampiga mpinzani wangu kwa kuwa nilishasema tangu awali kuwa huyu si Bondia bali ni mpiga debe.”

Upande wa Said Chino amesema “Nataka nirudiane naye, Class sio mkali, ameshinda kwa kuwa kuna mambo yametokea lakini uwezo wake bado na ndio maana huwa anapewa mabondia wa mchongo kupigana nao."


FxK05SWagAMLvPf.jpg

FxK0657acAI_wkw.jpg

Class na Chino

Awali, Mtanzania Idd Pialali amemkalisha kwa pointi Bryson Gwayani kutoka Malawi katika pambano la nane usiku huu Pambano kuu ni Ibrahim Class dhidi ya Said Chino

FxKwMKjaAAAs1vA.jpg

FxKsHILaIAAvELV.jpg

Bondia Issa Nampepeche naye ameibuka mshindi kwa pointi dhidi ya Cosmas Cheka kwenye pambano la saba usiku huu.
Cheka.jpg


Bondia Haidar Mchanjo amemkalisha Yohana Mchanja kwa pointi kwenye pambano la sita usiku huu.
Yohana.jpg

Haidar Mchanjo amemkalisha Yohana Mchanja

Bondia Emmanuel Mwakyembe amemchapa Allan Kamote kwa pointi kwenye pambano la tano usiku huu.
Mwakye.jpg

Emmanuel Mwakyembe amemchapa Allan Kamote
 
Aache kukimbia kimbia kama bata. Hadi anampa mgongo mpinzani wake.
Ukipiga ngumi lazima utoke ngumi zinaenda na movement kuanzia miguuni kwaio lazma uingie na kutoka katika basic tu boxing unafundishwa kupiga jab unatoka kiuswazi tunaita "Jab kataa"
 
Ukipiga ngumi lazima utoke ngumi zinaenda na movement kuanzia miguuni kwaio lazma uingie na kutoka katika basic tu boxing unafundishwa kupiga jab unatoka kiuswazi tunaita "Jab kataa"

Kutoka unatoka ila sio kiholela tu. Check watu kama James Toney uone watu wanavyocheza na Shoulder rolling watu wanakwepa hapo hapo na kushambulia
 
Back
Top Bottom