Eli Cohen
JF-Expert Member
- Jun 19, 2023
- 1,314
- 4,032
View: https://youtu.be/XMvIQexojWo?si=KqoV8KWbaeZDTvA5
Rabies ni virus inayosababishwa mara nyingi na kung'atwa na mbwa, popo, mbwa mwitu, etc
Ndio maana wanashauri mbwa kupewa chanjo mara kwa mara kuziua madhara ya kuwa infected na virus tofauti.
Moja ya madhara ya rabies ni mgonjwa kuwa na hofu ya kunywa maji. Hii ni kwa sababu Rabies huathiri sehemu za ubongo ambazo hudhibiti kuzungumza, kumeza, na kupumua.
Inabadilisha mchakato wa uzalishaji wa mate na husababisha spasms za misuli chungu ambazo zinakatisha tamaa kumeza. Virusi hii hustawi katika mate. Kumeza hupunguza kuenea.
Kwa hiyo, mara moja hufanya kazi ya kumfanya mwathirika wake kuzalisha mate zaidi na kueneza mate hayo kwenye mazingira yake badala ya kumeza.
Rabies inatabika ila ikishakuwa chronic ni changamoto sana.
Ndio maana ukishang'twa na mbwa au popo kimbilia hospitali.
TAKE CARE.