DSM: Mwimbaji wa Kwaya ya AICT Chang'ombe, Mariam Charles akutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni ( Guest )

Unaweza ukasema kwa kejeli ukaropoka unavyotaka ila ni vizuri kujua wewe mwisho wako utakuwaje? Najua mariamu hakujua kama yatamkuta hayo.na wazazi wake wangemkatazaje mtu anaekwenda kuonana na mchumba wake.ukiwa bado uko duniani usitoe maneno ya kejeli hujui kesho yako
 
duu hapa kuna maswali mengi ya kujiuliza, twaweza mhukum mchumba wake moja kwa moja kumbe ata hajahusika masikin.
yawezekana kuna njemba mwingine alikuwa anamega mzigo kwa huyo mwimbaji na alikuwa hafurahishwi na huo uchumba ndo kaamua kutumia hiyo tekiniki ili kumwangushia mzigo huyo mchumba wake, la sivyo jamaa ni mafia hatari pamoja na kuwa mwimbaji.
 
wengi mtalaumu wazazi, wengi mtajadili muuaji yote hayo ni matokeo, je chanzo ni nini? hakuna hata mtu humu kajaribu kutafta vyanzo, vipo viashilia vingi kabla ya mauaji, yaweza ikawa usaliti na kudhalauliana, yamkini kijana alijitoa kumuoa lakini akaumizwa, hakuona namna nyingine ya kurevenge, akazani wacha ampige japo makofi, lakini huenda hakuwa na dhamila ya kuua, lakini katika kuzozana ndipo yakatokea ya kanumba shetani akapenya! ushauri Wangu, wachumba jifunzeni kuhemiana ili kuepusha shetani asifanye yake, Ukithaminiwa mthamini na mwenzio mliochumbiana nae
 
Mwimbaji wa Kwaya ya Vijana ya Kanisa la AICT Chang’ombe (CVC), Mariam Charles (22) amekutwa amefariki katika nyumba ya wageni iliyopo Buza anakodaiwa alikuwa na mchumba wake (jina linahifadhiwa kwa sasa).


Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu, Charles Lutonja, mwanaume huyo ambaye pia ni mwimbaji wa kwaya hiyo inayotamba na albamu ya ‘Pazia la Hekalu’, tayari alishatoa posa kwa Mariam Aprili mwaka huu na alikuja jijini hapa kwa ajili ya kutoa mahari.


Akisimulia tukio hilo, Lutonja alisema mchumba wa Mariam alimpigia simu mama wa marehemu, Jumatatu ya Septemba 3 na kumueleza kuwa anakuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa mahari leo Ijumaa.
“Basi mke wangu aliniambia lakini nilishangaa mbona ni ghafla hata hivyo tulikubali,” alisema.



Alisema Jumanne, Septemba 4, mara baada ya kijana huyo kuwasili jijini Dar es Salaam akitokea Dodoma, Mariam aliaga anakwenda kuonana naye katika nyumba ya wageni aliyofikia.
“Aliondoka nyumbani saa 8 mchana, akamuaga mama yake (Ester) kuwa anakwenda kuonana na mchumba wake, lakini jioni alituma ujumbe kuwa atachelewa,” alisema.



Lutonja alisimulia zaidi kuwa usiku huo (Jumanne) hakurudi na ilipofika juzi asubuhi (Jumatano) mama yake Mariam alipokea ujumbe kutoka kwa kijana huyo uliosema: “Mwanao tayari nimemuua.”



Alisema baada ya hapo walianza kumtafuta Mariam na waliporipoti kituo cha polisi Chang’ombe walipewa saa 24 za kusubiri iwapo kuna taarifa zozote.



“Lakini jana (Jumatano), tulienda kituoni tena na tukaambiwa kuna mwili umeletwa umekutwa gesti, tulipoukagua tukagundua ni wa Mariam,” alisema.
Alisema kijana huyo, hakutuma ujumbe huo kwa mama wa marehemu tu, bali alituma pia kwa wanakwaya wengi wa Vijana (CVC) akiwaambia kuwa wanamchonganisha na Mariam.



“Baada ya kutuma huo ujumbe, tulijaribu kupiga simu hiyo lakini haikupatikana na taarifa zote hizi zipo polisi,” alisema. Kwa mujibu wa Lutonja, mwili wa Mariam unaonyesha amenyongwa.



Mariam alikuwa anajishughulisha na biashara ndogondogo huku akihudumu katika kwaya kama mwimbaji. Alikuwa ni mtoto wa sita wa Mzee Lutonja na sasa mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).



Hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke limechukua sampuli kutoka kwenye mwili wa Mariam na kupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi wa chanzo cha kifo hicho.
“Leo (jana) polisi wametuambia kwamba wamechukua sampuli kutoka kwenye mwili wa marehemu na kupeleka ofisi ya Mkemia Mkuu kwa ajili ya vipimo zaidi. Tumeruhusiwa kuendelea na mazishi na sisi tumeamua kuzika Jumamosi katika makaburi ya Temeke,” alisema Lutonja.



Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula alikiri kuwa na taarifa na kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wake. Alisema wanashirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu katika uchunguzi huo.



“Uchunguzi ni jambo pana na linafanyika kwa namna mbalimbali, kwa hiyo siwezi kusema mazingira ya kifo mpaka uchunguzi huo utakapokamilika, ndiyo maana tunachunguza,” alisema kamanda huyo alipoulizwa kuhusu mazingira ya kifo cha msichana huyo.



Akitoa maoni yake kuhusu tukio hilo, Rais wa Mtandao wa Wasanii wa Injili na Maadili ya Utaifa (Tagoane), Dk Godwin Maimu alisema kuna haja ya kutolewa kwa elimu ya urafiki, uchumba na ndoa makanisani ili kuwaepusha vijana na matukio hayo.



Alisema inasikitisha kwa watu wanaomwimbia Mungu kukutwa kwenye maeneo yasiyo ya kimaadili hasa kwa mtoto wa kike. Aliongeza kwa sasa ni wakati wa kuwapa mafunzo ya maadili ili watende yanayowapasa kutenda. “Vyama vya muziki nchini vitoe elimu makanisani juu ya urafiki, uchumba na ndoa. Vijana wakiwa na elimu ya masomo hayo, hawatakumbana na matatizo kama yaliyotokea kwa msichana huyo.”


Usiwaamini na kuwatilia maanani waimbaji kwaya au wachungaji kwani wengi wao ni wasanii tu, wana maisha yao ya asili nyuma ya pazia....wanatumia jina Mungu kuficha asili yao.
 
Lutonja alisimulia zaidi kuwa usiku huo (Jumanne) hakurudi na ilipofika juzi asubuhi (Jumatano) mama yake Mariam alipokea ujumbe kutoka kwa kijana huyo uliosema: “Mwanao tayari nimemuua.”
Alisema baada ya hapo walianza kumtafuta Mariam na waliporipoti kituo cha polisi Chang’ombe walipewa saa 24 za kusubiri iwapo kuna taarifa zozote.

Taarifa zinasema ameuawa, Polisi wanataka kusubiri saa 24, naona kama inatia ukakasi!! Nilidhani Polisi wangeinuka kwenda kwenye eneo la tukio
 
Akitoa maoni yake kuhusu tukio hilo, Rais wa Mtandao wa Wasanii wa Injili na Maadili ya Utaifa (Tagoane), Dk Godwin Maimu alisema kuna haja ya kutolewa kwa elimu ya urafiki, uchumba na ndoa makanisani ili kuwaepusha vijana na matukio hayo.


Elimu hii ipo siku nyingi, na imeandikiwa vitabu vingi, nadhani kinachotakiwa ni kutengeneza mfumo wa kuiboresha iendane na wakati wa sasa.

Enzi zetu, tulifundishwa;
Ukitaka kuonana na mchumba, omba nafasi ukutane naye nyumbani kwa kiongozi wako wa kiimani au mshenga, au kwa ndugu yako wa karibu usiye na shaka naye, hatukuambiwa kuonana na mchumba kwenye hoteli au bar nk
 
Back
Top Bottom