Abakwa baada ya kutoka kanisani kusali misa ya Jumatano ya Majivu

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
JESHI la Polisi mkoani Rukwa linawasaka watu wasiojulikana ambao wanatuhumiwa kumbaka, kumuua kwa kumnyonga Martha Zacharia (40), kisha mwili wake kuutupa pembezoni mwa barabara.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi (ACP) Mayila Mashenene, amesema tukio hilo lilitokea usiku wa Februari 14, mwaka huu, katika Mtaa wa Makutano, Manispaa ya Sumbawanga huku akibainisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Amesema Martha alikuwa mwimbaji wa kwaya ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Epiphania, Jimbo la Katoliki Sumbawanga na inadaiwa kuwa kabla ya kuuawa, alitoka kanisani kusali misa ya Jumatano ya Majivu.

Source - Nipashe
 
Vyombo vya ulinzi na usalama havijawahi kushindwa haswa kwenye kesi kama hizi, watakamatwa tu na case kusikilizwa mpaka hukumu watakuwa jela kama miaka 3 - 4 hivi huko sina shaka na wazee wa Magereza hawana huruma kwa wapuuzi kama hawa. hukumu itatoka wanyongwe mpaka kufa.

Apumzike kwa amani na faraja kwa familia na ndugu zake.
 
Abakwa baada ya kutoka kanisani kusali misa ya Jumatano ya Majivu
Nadhani title ingekuwa Auawa baada ya kutoka kanisani kusali misa ya Jumatano ya Majivu.
Kwa title ilivyo sasa, ni kama vile kubakwa ni tukio kubwa kuliko kuuawa
 
JESHI la Polisi mkoani Rukwa linawasaka watu wasiojulikana ambao wanatuhumiwa kumbaka, kumuua kwa kumnyonga Martha Zacharia (40), kisha mwili wake kuutupa pembezoni mwa barabara.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi (ACP) Mayila Mashenene, amesema tukio hilo lilitokea usiku wa Februari 14, mwaka huu, katika Mtaa wa Makutano, Manispaa ya Sumbawanga huku akibainisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Amesema Martha alikuwa mwimbaji wa kwaya ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Epiphania, Jimbo la Katoliki Sumbawanga na inadaiwa kuwa kabla ya kuuawa, alitoka kanisani kusali misa ya Jumatano ya Majivu.

Source - Nipashe
Misa ya J'tano ya Majivu haimaliziki usiku, ni jioni. Tukio la ubakaji linatajwa kutokea usiku, hapo haiwezi kuwa alifanyiwa tukio hilo akitokea kanisani.

Hapo nadhani PT watuambie ambako marehemu alikokwenda baada ya kutoka kwenye misa kanisani jioni, ili tumjue mhusika wa tukio.

Ila tukio hili limenikumbusha sana tukio la marehemu Betty Ndejembi. Apumzike kwa amani.

Ova
 
Back
Top Bottom