Dr. Ulimboka azimwa

Katika kuthibitisha kwamba Dk. Ulimboka hayuko tayari kusema chochote, juzi gazeti hili lilikutana nae katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo ambapo alisema kuwa kitendo cha kinyama alichofanyiwa, anamwachia Mungu.

Source: Tanzania Daima

Maskini Mwanahalisi na wanaharakati waliojitolea kuyatetea maisha yake sasa wanasalitiwa!!
 
Nahisi kuna information za muhimu ambayo wanayo na Ulimboka kamegewa kidogo tu na kuachwa aamue mwenyewe kusuka au kunyoa.Zile movement za kabla ya tukio zinanitia wasiwasi kuwa Uli alikuwa anafuatilia dili kubwa la kibinafsi.Kaambiwa mwaga mbga nasi tumwage ugali.
 
Heri kujilipua ukweli ujulikane na wengine wasifanyiwe unyama kama huu!.... Vinginevyo Stella Manyanya ataendelea kuamini Dr. Ulimboka ni Hitler wa Tanzania na Prof. Maji marefu - yule mpiga ramli - witchdoctor na mhishimiwa ngonyani ataendelea kuamini kuwa Dr. Uli ni muuaji!... ACHA NIDHAMU YA WOGA!................ wataje!.... LIWALO NA LIWE!...................
 
teh teh teh..imekaa vibaya, hii bado haijatulia! Sijui ule wimbo aliuimba nani. In short, kutulia ni muhimu sana maana papara na haraka haraka bila kuwa na matayarisho ya kueleweka unaweza kukosea step.

Mkuu anaitwa Kali P....wa Bongo Records kipindi kile
 
mi nadhani ni kuwa na amani ni kulinda usalama wako na ustawi wa familia yako.
Utamu wa ngoma ingia ndani ucheze, asidanganywe na wanaojifanya kum suport wkt hawaathiriki moja kwa moja na kilicho mkuta au kitakacho mkuta.
Dr ni mtu mzima, msomi mwenye akili zake timamu.
Atachagua lili lililobora zaidi kwa maslahi yake na familia yake kwa ujumla.

Nakuunga mkono mkuu....Kuharibiwa kikojoleo sio issue ya mchezo
 
MamaJack, huhitaji kuwa Dr. Ulimboka kutetea maslahi fulani, hata wewe unaweza kutetea unaloamini na kuwa mfano au ukawa role mode wa wengine. Kwa kipindi chote ambacho Dr. alikuwa kwenye matatizo tumefanya nini especially kwa familia yake..... Talking is cheap

siyo tulifanya nn..wewe ulifanya nn? usiwasemee wengine kw sababu hauko kwenye nafsi zao...me nadhani we ni cheap zaidi than talking itself
 
Issue ya Mwakyembe na Ulimboka ni tofauti sana.Mwakyembe hakuwa physically attacked kama ilivyokuwa kwa Dr Uli.Mwakyembe ni mnafiki.

Ulimboka anahitaji sapoti,na kama madaktari wenzake wako kimya,basi lazima atakuwa na wasiwasi na pia faimilia inaweza kumshauri aachane na issue hizo na yeye akakubali.

Pia serikali lazima wana vigogo waliowatuma kupeleka pesa za kumpoza,I can almost bet my life on this.That's how I know bongo...

Cha muhimu nachomshauri,atafute haki hata kama haitahusisha mgogoro wa madaktari dhidi ya serikali.Kama anamwamini Mungu kama anavyodai,basi atakuwa anaelewa kuwa nothing happens for no reason.Kipigo na kunusurika kifo iwe ndo chachu ya kudai haki.Ntashangazwa sana akikaa kimya all the way...


Hatuzungumzii mgogoro wa madaktari hapa,bali unyama na uvunjifu wa haki za binadamu.
 
Nilisema na naendelea kusema " Dr. Ulimboka atafuata nyayo ya nduguye Dr. Mwakyembe" Dr. Mwakyembe nae aliibukia kanisani kutoa sadaka then Akahongwa Uwaziri wa Uchukuzi. Dr. Ulimboka atahongwa Ubalozi soon or later. Tamaa za walengwa wachache toka Mbeya kupenda madaraka, zitaangamiza nguvu za wanaharakati watiifu.
 
You should have asked the bodyguard of Diana princess of wales, who was the sole survivor of the paris subway accident which killed Dodi Alfayed and her lover, who was supposed to be a wife soon, who was supposed pregnant, and who was to be married according to islamic faith. So having an arab baby who his or her brother is king of england. (abomination??????)

the bodyguard, Trevor Rees Jones, promised the britain he will reveals what happened when he recover. But when he recovered, he told them he doesnt remember anything of what happened. Ten yeas later, he still doesnt remember?. Tehe!tehe!

So wadanganyika msishangae. That is what we call, national interest. but whose interest?. If people can course a national black out, and the matter be handled just calmly as it is. Whose interest are we talking about here.

Even if, Ulimboka died, God forbid!. And even if the event was witnessed, by his wife. Still she would not have remembered what happened.

Long live National Interests.
 
Dr. Steven Ulimboka; Karibu naboreka na hizi habari. Oohoo! sema ukweli. Vikao na serikali ni vyanini sasa?
 
Wote tulikua na wasiwasi nae tangu tune Kauli sake zikibadilika. Lakini uamuzi wake itakula kwako, Utakua huna Tofauti na nao waliookufanyia ushenzi huo, lakini how about watanzania wote.waliokupigania wakiamini Utakua chanzo cha,ukombozi wao? How about mwanahalisi lililofungwa kwa kukupigania? Stupid Mtanzania, Mimi ntakuchukia sana kwa ujinga wako, who are you protecting wakati wanaharakati wana taffeta evidence ya,kuwapeleka Wakina Nzoka the Hague?
 
Tutasikia mengi sana kabla dr.ulimboka hajafunguka......funguka dr funguka!!!!!!

daah tuliguswa sana juu ya unyama alio fanyiwa ndugu yetu.ukweli kama hatataja watu husika wa kisa hiki basi usaliti huu juu ya watu wote utamtafuna.

Amekaa ametafakari kwa kina na amejua mchezo wote mwanzo hadi mwisho amesikitika sana ndio maana amesema anamuachia Mungu. ninasikitika kusema "mission failed"

Siku Ullimboka akifunguka na kueleza ukweli kwamba kuna ranks za TISS zikishirikiana na CHADEMA zilifanya mpango mzima wa utekaji ndio watanzania watajua kwa nini aliamua kumuachia mungu. Kwani watu aliowategemea wangemsaidia ndio walitaka kumuua ili kujipatia umaarufu na huruma kutoka kwa Watanzania.
 
Siku Ullimboka akifunguka na kueleza ukweli kwamba kuna ranks za TISS zikishirikiana na CHADEMA zilifanya mpango mzima wa utekaji ndio watanzania watajua kwa nini aliamua kumuachia mungu. Kwani watu aliowategemea wangemsaidia ndio walitaka kumuua ili kujipatia umaarufu na huruma kutoka kwa Watanzania.
Ikiwa hivyo basi wamejitumbukiza kwenye deni, na hili deni litakuja kudaiwa 2015
 
Wote tulikua na wasiwasi nae tangu tune Kauli sake zikibadilika. Lakini uamuzi wake itakula kwako, Utakua huna Tofauti na nao waliookufanyia ushenzi huo, lakini how about watanzania wote.waliokupigania wakiamini Utakua chanzo cha,ukombozi wao? How about mwanahalisi lililofungwa kwa kukupigania? Stupid Mtanzania, Mimi ntakuchukia sana kwa ujinga wako, who are you protecting wakati wanaharakati wana taffeta evidence ya,kuwapeleka Wakina Nzoka the Hague?
Bwana Mkubwa jamaa amebaini ukweli na ameamua kulichukulia hili jambo kama lake binafsi hata hivyo yeye si mwanasiasa
 
Hapa hakuna Siasa UHAI wa mtu na siasa ni vitu tofauti akili yoooooooooooooooooooooote ya watanzania ilikuwa support na Dr,Ulimboka lakini pamoja na woga wa uhai wake bado kukaa kimya ni USALITI kwa Watanzania wapenda amani
 
Madaktari wenzake wakajitolea kufa na kupona, wakahakikisha inapigwa harambee fasta, akapelekwa sauzi tena chini ya ulinzi mkali, yote kwa ajli ya maisha yake, hiyo yote igeuke kuwa bure jamani! hapana haifai hata kidogo, kama unavyosema bila support hiyo saa hizi angekuwa historia, tena ndio kesi ingeisha kiulaini kabisa. post namba 30 hapo juu mohamedi tantawi anasema tumwache apiganie uzima wake, huo uzima angeupata wapi bila support ya hao anaotaka kuwasaliti sasa (kama ni kweli). Halafu kumbuka mohamedi, hili siyo suala la kisiasa tena ni suala la ubakaji wa haki za binadamu,

Pia lazima muelewe kwamba siri haiwezi kufichwa daima, huwa inamkereketa mtu kuisema, kwa hiyo ataitoa kwa mtu wake wa karibu na kumwambia usimwambie mtu, na huyo naye atampata mshikaji wake atamwambia na kumpa masharti kama hayo ya kutomwambia mtu... yani ni kama mtandao wa 'tuko wangapi' unavyokuwa. sasa kwa kuhofia hilo sidhani kama....

Huyu dokta asitake kutuzingua hapa aseme kilichomkuta atakuwa salama zaidi kwa sababu watesi wake hawatakuwa na haja naye tena baada ya ukweli kuwa umewekwa wazi labda kama ni kwa ajili ya kulipa kisasi tu baada ya kuumbuliwa, na sijuji huko alikokuwa anakutana nao kama hawajamwambukiza kitu.
Ameona tatizo kwamba akija akiongea yale mambo ambaye ni kinyume cha wengi wanavyotegemea iwe itakuwa tatizo. kwani ni rahisi sana kusema amepewa kitu kidogo na serikali. kuhusu usalama wake nadhani serikali ndiyo msitari wao wa mwisho wa kujilinda hivyo ni jukumu lao kumlinda. Mkuu alikwisha sema wanamuhitaji mno Dr Uli katika mazungumzo yao na serikali haihusiki katika unyama huo na kama kuna mtu ndani ya serikali alifanya hivyo basi hakufanya kwa niaba ya serikali. Kwahiyo inawezerkana ni watu wa serikali walifanya kwa niaba ya watu fulani na hili ndilo limempa Kamanda Uli tabu kuliongelea hadharani kwani litaleta mkanganyiko mkubwa sana katika jamii
 
Nionavyo namshauri huyu jamaa anaeitwa Ulimboka akimbie nchi na kuomba ukimbizi kokote kule ambako itakuwa rahisi kwake kufika.

Huu si wakati wa yeye kubabaika na kutojua la kufanya ,maisha ndani ya Tanzania kwa upande wake hayatakuwa the same as before ,ataishi maisha ya wasiwasi mkubwa sana na maisha ya hofu na kujifichaficha ,akiwa hana uhakika wa kufika kesho.

Ushauri wa bure akimbie nchi na kuwa mkimbizi nina uhakika nafasi hiyo ipo wazi na ya kukubalika kwa popote pale atakapo elekea.Na naamini itakuwa official ukilinganisha na wengine wanaojiita Wasomali.Yeye atakuwa mkimbizi kama Mtanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom