Dr Slaa: Lowassa ni sehemu ya matatizo yanayoikabili nchi kwa sasa

Mbona Lowasa hajakosea kabisa au mimi ndio sijaelewa?
  1. Mbona serikali inalaumiwa kwa kushindwa kufanya maamuzi magumu ya kumchukulia Lowasa hatua! huu ni uongo jamani?
  2. Serikali imeshindwa kufanya maamuzi magumu ya kufukuzakazi ndugu na marafikize Lowasa waliovurunda katika idara za serikali kumlinda kama Edwardo Heseah wa PCCB, mbona huu sio uongo Lowasa anasema ukweli kabisa.
  3. CCM ili ahidi kumfuka Lowasa, R. Azizi na Chenge lakini Serikali ya Kikwete imeshindwa kufanya maamuzi hayo hata hii mna taka kusema Lowasa kadanganya kweli jamani?
Ebu fakarini maneno ya Lowasa kwa mapana yake, maana kama serikali ya Kiwete hisinge kuwa ni serikali ya kushindwa kuchukuwa hatua leo hii Lowasa hasingelikuwa Bungeni hata siku moja.

Kwa kweli nakubaliana na Slaa kwamba huyu jamaa ni michosho na alidhani atapata pa kutokea ili aonekane shujaa wakati watu wanajua kwamba yeye kwa sehemu kubwa anabeba lawama ya mengi ya mabaya yaliyopo leo serikalini. Asilete unafiki wake kwa ajili ya kupata political mileage.
 
Nafikiri hatumtendei haki Lowasa kwa kumshambulia baada ya kutoa maoni. Inawezekana baada ya kukaa nje ya game, amepata muda mzuri wa kutafakari, kujifunza na , kufanya utafiti. Sasa anajua ni wapi alikosea na anajua ni nini cha kufanya illi kusaidia maendeleo ya nchi.

Swala la richmond hakukosea chochote. Maana richmond ndo ilikuwa iuzie umeme Tanesco kwa bei ya chini kuliko kampuni nyingine yoyote ile. Angeiacha kampuni hii pia asingeeleweka. Kushindwa kwa richmond ni matokeo ya kawaida ya kibiashara. Sidhani katika nchii hii ni mradi pekee wa richmond ulioshindwa kutekelezeka kwa wakati. Richmond walileta mitambo ingawa ilichelewa.

Kuchelewa kwa project kubwa kama hii ni jambo la kawaida. Sakata la Richmond limekuzwa tu kisiasa kwa sababu baada ya mitambo kufika kampuni ya dowans iliichukua na kuanza kuzalisha umeme kwa makubaliano na richmond. Ila kwa ushabiki wa kisiasa mkasitisha mkataba na dowans.

Eti sheria ya manunizi ilikiukwa. Tatizo la watanzania wanafikiri sheria zote ni nzuri. Moja ya sheria mbaya na ambazo zinaliingizia hasara taifa hili ni hii sheria ya manunuzi. Licha ya kuwa na urasimu mkubwa pia hai guarantee anayeitumia kupata kitu bora.

Katika crisis kama ile iliyokuwepo Waziri mkuu yeyote mchapa kazi na asiyeogopa kufanya maamuzi angeenda hata through single source iki umeme upatikane.

Simtetei Lowassa katika mambo mengine, ila katika hili la Richmond.
Hana chochote! Hawa mawaziri anaowalaumu si ndo yeye alishiriki kuwapendekeza wakati awamu hii ilipokuwa inaingia madarakani?
 
Tunamshukuru Slaa kwa kusisitiza unafiki tunaoujua alionao Lowassa. Alidhani hii ni platform ya ku-redeem image yake ambayo imeshasambaratika. It was a suicide mission, very well executed to his detriment.
 
Hii habari tanzania daima iliipotosha nakusema dk slaa alimsifia lowassa!
Absalom kibanda sijui alipewa nini na lowassa!
 
Nimesoma magazeti mawili ya Mwananchi na Tanzania Daima jana (26/06/2011) juu ya kauli ya Dr Slaa kuhusu Lowassa nikajiuliza hivi ni gazeti lipi linasema ukweli au lipi linasimama wapi.

Hebu tushirikiane kwa kusoma hizi habari mbilli:

Habari ya Kwanza toka Mwananchi:
Dk Slaa amponda Lowassa Send to a friend
Sunday, 26 June 2011 08:31
0diggsdigg

ASEMA anawakejili Watanzania, ni sehemu ya matatizo
Hussein Issa na Fidelis Butahe
KATIBU Mkuu wa Chedema Dk Wlibroad Slaa ameunga mkono kauli ya Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa na kumponda kuwa mbunge huyo ni sehemu ya matatizo yanayoikabili Tanzania hivi sasa.
Dk Slaa alisema kuwa Lowassa hakupaswa kutoa kauli hiyo kwa kuwa naye ni mmoja wa viongozi waliokuwa madarakani katika Serikali ya awamu ya nne, ambao hawakufanya vizuri hadi alipoamua kuachia madaraka kwa kujiuzulu.

Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo kikuu cha Ualimu Dar es Salaam (DUCE), katika ukumbi wa TCC Changómbe Dar es Salaam. "Naiunga mkono kauli yake, lakini sio yeye, kwa sababu yeye mwenyewe ni miongoni mwa viongozi waliokuwa madarakani kipindi kile."
Alisema kimsingi ni kweli kuna matatizo ya usafiri wa reli, msongamano na makontena bandarini na ujenzi wa bandari na taifa kukabiliwa na mgawo wa mara kwa mara wa umeme uliodumu tangu mwaka 2006, lakini akasema kuna watu waliotakiwa kuyazungumza siyo Lowassa. Akizungumza katika mahojiano na Mwananchi Jumapili baada ya mkutano huo, Dk Slaa alisema kauli ya Lowassa ni kama kejeli kwa Watanzania na kwa viongozi walioko madarakani kwa sababu na yeye ni miongoni mwa waliokuwa madarakani
Aliongeza kwamba, kauli ya Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli kusema Serikali inasumbuliwa na ugonjwa wa woga katika kutoa uamuzi mgumu ni ya kejeli kwa kuwa hata yeye alikuwa mtendaji mkuu wa serikali. Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza katika utawala wa awamu ya nne, aliitaka Serikali hiyo kubadilika na kuwa na maamuzi magumu alitoa kauli hiyo bungeni wakati akichangia hotuba ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2011/2012.
Alisema kuwa ni bora kulaumiwa kwa kufanya uamuzi mgumu kuliko kulaumiwa kwa kutofanya uamuzi na kwamba, Serikali inapaswa kufanya uamuzi bila kujali matokeo yake. "Ni bora kulaumiwa kwa kufanya maamuzi kuliko kulaumiwa kwa kutofanya maamuzi kabisa," alisema Lowassa.
Aliongeza, "Kuna ugonjwa wa kutokutoa maamuzi hapa na lazima tukubali kubadilike. Ni heri mtu ukosee kutoa maamuzi kuliko kukaa kimya kabisa, heri uhukumiwe kwa kutoa maamuzi mabya kuliko ulaumiwe kwa kushindwa kutoa maamuzi." Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Azaveri Rwaitama alisema kwamba kauli ya Lowassa ni sawa na kiini macho kwa sababu yeye mwenyewe ni wa upande huo wa Serikali. Alisema wakati wa kipindi chake uwaziri mkuu, Lowassa aliyaona matatizo yote ya nchi, lakini alishindwa kuyakabili.

Rwaitama alisisitiza: Anachokisema Lowassa ni kiini macho.” Alisema Watanzania hawataki kuongozwa na watu wanaotaka umaarufu bali wanataka kuongozwa na wachapa kazi na siyo vinginevyo. Alisema kauli ya Lowassa inaonyesha wazi kuwa kuna ushindani unaendelea ndani ya serikali hali aliyodai inaweza kuleta mtafaruku mkubwa baadaye. "Mimi sina chama, awali nilikuwa TANU, lakini niliirudisha kadi baada ya kuona hakuna maelewano mazuri ndani ya chama, hivyo kwa sasa nipo tu bila ya chama'' alifahamisha Aliongeza kwamba haitakiwi kuruhusu vikundi ndani ya tabaka tawala kwani linaweza kuharibu nchi kabisa. Alisema huu sio muda wa kuongozwa na viongozi wanaotaka kuchukua nchi kiujanjaujanja kwani matokeo yake yatakuwa sio mazuri hapo baadae.

Maandamamo
Katika hatua nyingine, Dk Slaa amewaambia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ualimu Chang'ombe (DUCE) kuwa kuandamana ni haki yao na ya kila raia wa Tanzania. Dk Slaa ametoa kauli hiyo huku taifa likiendelea kukabiliwa na migomo na maandamano maeneo mbalimbali. Hata hivyo alisema kwamba ingawa yeye hawezi kuchochea vurugu, lakini wananchi kufanya maandamano si jambo la ajabu, pale wanapoona kuwa haki na amani havifuatwi katika nchi yao. Alisisitiza kwamba kila mtanzania ana haki ya kuishi, kuheshimika, kusema na kushiriki katika maamuzi. “Tatizo sisi tukisema ukweli tunaambiwa tunachochea wanafunzi na wananchi kuandamana…., sasa tusiposema ukweli huu tutausemea wapi; hiyo ndio kazi ya siasa, Serikali na Jeshi la Polisi wanatakiwa kulijua hili.

Hata hivyo aliwaonaya wanafunzi hao akisema: Ukiandamana kwa ushabiki wangu wewe hufai kuitwa mwanachuo.”
Dk Slaa ambaye alikuwa akitoa mifano mbalimbali inayoweza kumsukuma mtu kuandamana alisema kuna upotoshaji mkubwa katika upimaji wa maendeleo ya nchi. Alisema siku zote anayeambiwa ukweli huumia huku akilishukia Jeshi la Polisi nchini kuwa kupiga marufuku maandamano ni upuuzi kwa kuwa kupitia maandamano baadhi ya mambo yamewekwa sawa ikiwa ni pamoja na bei za bidhaa mbalimbali. Huku akitoa mfano wa baadhi ya vitabu vilivyoandikwa na Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1968 vilivyogusia haki, amani na usawa, alisema amani sio ukosefu wa nchi kuwa na mapigano bali ni Watanzania kujitawala wenyewe kuwa na uhuru wa kufanya mambo yao bila kuingiliwa na mtu. Alisema: “Kujenga barabara, nyumba za kifahari na shule sio maendeleo bali hivyo ni vyombo vya kuleta maendeleo tena kama vyombo hivyo vitatumika kweli kuleta maendeleo.”


Habari yaPili toka Tanzania Daima
Dk. Slaa awasha moto
• Asema serikali inawadanganya wananchi kwa takwimu
na Janet Josiah, Dodoma

amka2.gif

SIKU moja baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kuwashambulia viongozi wa serikali ya Rais Kikwete kuwa waoga wa kutochukua maamuzi magumu, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa, amesema serikali inawadanganya wananchi kwa takwimu zisizo na ukweli.
Slaa, alisema serikali ya Rais Kikwete imekosa umakini wa kuchukua maamuzi magumu yenye manufaa kwa taifa na matokeo yake Watanzania wanaendelea kuwa masikini ilhali nchi ina rasilimali lukuki.
Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE), ambapo alisema Watanzania hivi sasa wamekata tamaa kutokana na ugumu wa maisha huku serikali ikishindwa kuchukua maamuzi magumu ya kuboresha hali za wananchi wake.
Alibainisha kuwa serikali imekuwa ikiwadanganya wananchi kwa takwimu mbalimbali kwa lengo la kuwapa imani, matumaini na ahadi ambazo haiwezi kuzitekeleza, kwa sababu ya kutokuwapo kwa kiongozi wenye uwezo wa kusimamia maamuzi magumu.
Alisema katika kampeni za Uchaguzi Mkuu zilizofanyika mwaka jana, alikuwa akizinadi sera za CHADEMA pamoja na kuahidi kusimamia maamuzi magumu juu ya mgawanyo wa rasilimali za taifa ambazo sasa zinawanufaisha watu wachache pamoja na wawekezaji.
“Mara nyingi katika kampeni zangu wakati nilisema CHADEMA ikiingia madarakani itafanya maamuzi magumu ili Watanzania waweze kunufaika …sasa Lowassa juzi katoa kauli kama yangu kwa chama chake na viongozi wa serikali iliyopo madarakani, naungana naye,” alisema.
Alibainisha kuwa maisha hivi sasa yamekuwa magumu zaidi na serikali inayoongozwa na CCM imekuwa kwenye matatizo ya kifedha kwa sababu fedha nyingi za umma ilizitumia kusaka madaraka kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana na kutawaliwa na mizengwe ya hapa na pale.
Alisema mgawo wa umeme kwa nchi nzima uliotangazwa hivi karibuni na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), umesababishwa na ombwe la uongozi uliopo ambao ulitumia fedha nyingi katika uchaguzi na mambo yasiyo na tija kwa taifa.
Aliongeza kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, anapaswa kujiuzulu kutokana na tatizo hilo kujitokeza mara kwa mara huku yeye akiendelea kutoa sababu zisizo na mashiko kwa jamii.
Alisisitiza kuwa Ngeleja, anatakiwa kutoa kauli kwa umma na bungeni kwa mujibu wa kanuni ya 49 ya Bunge kuhusu mgawo mkubwa wa umeme unaoigusa mikoa 18 inayopata nishati hiyo kupitia Gridi ya Taifa.
Alisema kutokana na ombwe la uongozi lililopo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameshindwa kuingilia kati ili kupunguza muda uliotajwa na TANESCO kuhusu mgawo huo unaoathiri uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.
Alisema maelezo ya kwamba mgawo huu umesababishwa na mitambo ya IPTL kuzalisha megawati 10 badala ya 100 kutokana na upungufu wa mafuta mazito (HFO), yanatosha kwa serikali kuwajibika kutokana na uzembe wenye kulitia hasara taifa.
Alisema mahitaji ya mafuta ya mitambo ya IPTL au mingineyo si jambo la dharura, bali lilikuwa linajulikana mapema lakini halikuchukuliwa kwa umakini, kwa sababu ya uongozi mbovu uliopo.
Alibainisha kuwa tatizo kubwa la mgawanyo usiozingatia masilahi ya wananchi ni miongoni mwa mambo yanayowafanya wananchi waendelee kudidimia katika lindi la umaskini ambalo chanzo kikubwa ni mikataba mibovu na viongozi kukwepa kuchukua maamuzi magumu.
Alisema mgawo wa rasilimali za nchi kwa kiasi kikubwa zinashikiliwa na watu wachache na wawekezaji wenye kumiliki uchumi huku idadi kubwa ya Watanzania ikiendelea kuwa mashuhuda wa zinavyowanufaisha wenzao.
“Mgawanyo wa rasilimali kati ya Watanzania na wawekezaji hauko imara na sawa, serikali inadanganya katika takwimu za vitabuni na kuwataka Watanzania waamini hivyo, haya mambo ni lazima yabadilike,” alisema.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alimpongeza Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kwa kuwasema viongozi wa serikali, kwa kuogopa kuchukua maamuzi magumu yenye manufaa kwa taifa.
Alisema Lowassa amefanya jambo la msingi, kwani kama maamuzi magumu hayatachukuliwa na viongozi, Watanzania wataendelea kuwa maskini zaidi na hivyo kutishia mustakabali wa taifa.
“Wananchi wamekata tamaa, viongozi wanaogopa kuchukua maamuzi magumu kama alivyosema Lowassa, mnadhani amani na utulivu vinavyoimbwa hivi sasa vitaendelea kuwapo?” alihoji.
Juzi, Lowassa wakati akichangia hotuba ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2011/2012, alisema serikali inasumbuliwa na na ugonjwa wa woga katika kufanya maamuzi magumu, ndiyo maana mambo mengi hayaendi kama yanavyopaswa na kuitaka ibadilike.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alizindua tawi la CHADEMA katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwataka vijana kutumia elimu watakayoipata kueneza amani na uhuru uliopo kwa masilahi yao na vizazi vilivyopo na vijavyo. “Mwalimu Nyerere alikuwa akizungumza mengi kuhusu amani, utulivu na uhuru tulionao kwamba umepatikana kwa elimu yetu …hivyo kuna kila sababu ya kueneza haya bila woga, kwa kuwa vijana wa chama hiki ndio tegemeo letu kwa kila kitu,” alisema Dk. Slaa

 
mbona lowasa hajakosea kabisa au mimi ndio sijaelewa?
  1. mbona serikali inalaumiwa kwa kushindwa kufanya maamuzi magumu ya kumchukulia lowasa hatua! Huu ni uongo jamani?
  2. serikali imeshindwa kufanya maamuzi magumu ya kufukuzakazi ndugu na marafikize lowasa waliovurunda katika idara za serikali kumlinda kama edwardo heseah wa pccb, mbona huu sio uongo lowasa anasema ukweli kabisa.
  3. ccm ili ahidi kumfuka lowasa, r. Azizi na chenge lakini serikali ya kikwete imeshindwa kufanya maamuzi hayo hata hii mna taka kusema lowasa kadanganya kweli jamani?
ebu fakarini maneno ya lowasa kwa mapana yake, maana kama serikali ya kiwete hisinge kuwa ni serikali ya kushindwa kuchukuwa hatua leo hii lowasa hasingelikuwa bungeni hata siku moja.

nakubaliana na wewe, lakini hata dr. Slaa hajasema anampinga lowasa, alichofanya nikusema lowasa ni mnafiki kwa maneno yake na hilo lipo wazi, dr.slaa asingesema hivyo kuna watu baadhi (non great thinkers) wangesema lowasa hana makosa na wangemchukulia km kiongozi anaefaa.
 
mkubwa,

hata kukubali kuongeza wingi wa vyuo vikuu lowassa alisaidia. sasa hata hawa vijana vilaza ambao zamani wasingegusa lecture theatre sasa wanasoma.
kila siku sasa wanashinda kwenye siasa. wamshukuru lowassa wangekuwa wanalima vijijini.


Aisee unadharau sana! yaelekea una uwezo sana darasani au umesoma havard university au unaumia na wenzio uliotaka wawe na elimu ndogo ili wakunyenyekee sasa na wao wamesoma, umenishangaza sana! kwa hiyo vyuo vikuu hivyo vifutwe tu nafasi zibakie kwa wachache kwa waliopata div one eeeee?
 
-Tanzania kutegemea maji kama chanzo cha nguvu za umeme - Tatizo ni EL?
-Ukame ulioikumba Tanzania miaka ya 2006-2008- Tatizo ni EL?
-Mgao wa umeme unaendelea sasa kutokana na kushuka kwa Kina cha Maji kwenye Mabwawa ya Kuzalisha Umeme na kukosekana kwa Mafuta ya Mitambo ya IPTL-- Tatizo ni EL?

Tumtendee Haki jamani huyu mtu,Ukweli unajulikana wazi.....
 
Hii habari tanzania daima iliipotosha nakusema dk slaa alimsifia lowassa!
Absalom kibanda sijui alipewa nini na lowassa!

Mimi nadhani sura ya KIbanda sasa iko dhahiri na wale waliokuwa na mwashaka na kile ambacho tumekuwa tukikisema kuhusiana na Tanzania Daima na Kibanda sasa wamejionea hadharani. Swali la kujiuliza ni: Je, mmiliki wa gazeti halioni hili? Ana mpango gani? Je, yeye ni sehemu ya tatizo hili?
 
Naona Slaa ananza kumponda mapemaa mpinzani wake kwenye urais 2015!
My take: At least tunafahamu utendaji wa Lowasa, je utendaji wa Slaa tutaupima vip? Hajawahi kushika nyadhifa kubwa serikalini!! Au tukamuulize baba askofu?

Acha udini ndugu!! Kwani huyajua aliyofanya Dr. Slaa Karatu toka alipokuwa mbunge?!!!!
 
Rwaitama alisisitiza: Anachokisema Lowassa ni kiini macho.” Alisema Watanzania hawataki kuongozwa na watu wanaotaka umaarufu bali wanataka kuongozwa na wachapa kazi na siyo vinginevyo. Alisema kauli ya Lowassa inaonyesha wazi kuwa kuna ushindani unaendelea ndani ya serikali hali aliyodai inaweza kuleta mtafaruku mkubwa baadaye. "Mimi sina chama, awali nilikuwa TANU, lakini niliirudisha kadi baada ya kuona hakuna maelewano mazuri ndani ya chama, hivyo kwa sasa nipo tu bila ya chama'' alifahamisha Aliongeza kwamba haitakiwi kuruhusu vikundi ndani ya tabaka tawala kwani linaweza kuharibu nchi kabisa. Alisema huu sio muda wa kuongozwa na viongozi wanaotaka kuchukua nchi kiujanjaujanja kwani matokeo yake yatakuwa sio mazuri hapo baadae.



Dr Rweitama kuwa mkweli na muwazi. Acha kuuhadaa umma wa Watanzania. Nimekaa na wewe zaidi ya miaka mitatu tukiwa chuo Kikuu nakujua sana.

Sema huna kadi ya chama Chochote cha siasa lakini mshabiki wa chama fulani huko Tanzania.

Mimi ni Dr Hamza Yousuf Al Naamani wa Doha
 
Back
Top Bottom