Dkt. Slaa: Niliwahi kusema Lowassa ni fisadi lakini mimi ni Padre, katika umauti ni lazima niiombee Roho yake iingie mbinguni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,035
Dkt. Slaa amesema iko kwenye rekodi kwamba pale Mwembe Yanga alisema Lowassa ni fisadi Lakini yeye ni Padre anayetakiwa kuiponya roho ya Lowasa hivyo hana Tatizo lolote na Lowasa

Dkt. Slaa amesema Yesu mwenyewe pale Msalabani akimwambia yule Jambazi " hakika Leo hii utakuwa nami peponi"

Sasa mimi ni nani hadi nimuhukumu Edward Lowassa ikiwa Yesu Kristo mwenyewe alitangaza msamaha, amesisitiza Dr. Slaa

Chanzo: Jambo TV

Mlale Unono 😃😃
 
Atengue kauli.

Yeye si Padre. Bali alikuwa.

Baada ya kuasi na kuondoka hana uhalali wa kuendelea kujisemea yeye ni padri.

Si hivyo tu, Padre hana uwezo wowote wa kuiponya nafsi au roho ya mtu. Kwa hiyo kwa vyovyote vile matamshi yake hayasadiki chochote katika maisha ya Edward.

Akalaze mbupu zake.
 
Tukiacha siasa Uchwara. Na zakuzushiana Na kuchafuana nchi yetu itaendelea sana.

Mzee lowassa Alizulumiwa ndoto Yake Na wahuni wakishirikiana Na wapinzani kumchafua.

Taifa tunapoteza viongozi wazuri Ambao wanamaono Na uchungu Na Ali za watanzania lakini wanapakwa Matope Na wahuni.
 
Dkt. Slaa amesema iko Kwenye rekodi kwamba pale Mwembe Yanga alisema Lowasa ni Fisadi Lakini yeye ni Padre anayetakiwa kuiponya roho ya Lowasa hivyo hana Tatizo lolote na Lowasa

Dkt. Slaa amesema Yesu mwenyewe pale Msalabani akimwambia yule Jambazi " hakika Leo hii utakuwa nami peponi"

Sasa mimi ni nani hadi nimuhukumu Edward Lowasa ikiwa Yesu Kristo mwenyewe alitangaza msamaha, amesisitiza Dr Slaa

Source Jambo TV

Mlale Unono 😃😃
Na ukaongeza nyingine ya chadema wamechukua choo wamekiweka chumbani!
 
Atengue kauli.

Yeye si Padre. Bali alikuwa.

Baada ya kuasi na kuondoka hana uhalali wa kuendelea kujisemea yeye ni padri.

Si hivyo tu, Padre hana uwezo wowote wa kuiponya nafsi au roho ya mtu. Kwa hiyo kwa vyovyote vile matamshi yake hayasadiki chochote katika maisha ya Edward.

Akalaze mbupu zake.
Upadre hauishi kwa kuondoka altareni.Na haiponyi nafsi bali kuiombea kheri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom