Dr Slaa asitisha operesheni M4C kwa siku 5

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Dr Wilbroad Slaa amesitisha operesheni M4C kwa siku 5.
Dr Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CDM amesema amekubaliana na Serikali kwa maslahi ya nchi kupisha zoezi la sensa liishe ili kuepusha uvurugwaji wa zoezi hilo muhimu kwa Taifa.

Hata hivyo kiongozi huyo kipenzi cha watanzania ametoa onyo kali kwamba kamwe hatakubaliana na visingizio vyovyote vya kuzuia operesheni yao baada ya sensa.

Dr Slaa ameendelea kusema tayari kikosi cha ufundi cha CDM chenye makamanda karibu 100 tayari kimewasili mkoani Iringa kusimamia operesheni M4C inayotikisa nchi kwa sasa...



Source:Habari ITV
 
Bajeti ina utata, mshiko haujaingia bado, anti money laundering wanachunguza vyanzo na nia.
 
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Dr Wilbroad Slaa amesitisha operesheni M4C kwa siku 5
Source:Habari ITV

Sababu za kusutisha? Mbona unatoa habari nusu nusu, unakimbilia wapi?
 
Bajeti ina utata, mshiko haujaingia bado, anti money laundering wanachunguza vyanzo na nia.

Hata kuku kwa kutumia ubongo wake angetambua kuwa kuna maisha ya mtu tena asiye na hatia yamepotea kwa sababu ya kiburi cha CCM na polisi wao. Lazima uhai wa mtu uheshimiwe, mie naamini operesheni imesimamishwa kuomboleza kifo cha kijana aliyepigwa risasi na vilevile kuandaa taratibu za mazishi ya kishujaa.....kumbuka huu ni ukombozi mwingine.
 
Yes ni uamuzi mzuri alioufanya hii itasaidia uchunguzi kwa yaliyotokea
 
jeshi la polisi limewaomba kusimamisha kupisha sensa akasema uwe ni mwisho wa visingizio kwa jesh hilo na baada ya siku tano kwisha watakuwa unstopable
 
Kuahirisha M4C kunatokana na Polisi kusema inaweza kuvuruga shughuli za sensa huko Iringa.

Kwa maana hiyo, Dr Slaa amekubaliana na hoja ya polisi akiahilisha kwa siku tano na kusema baada ya hapo chadema hawatakubali visingizio vingine vyovyote vya polisi na wataendelea na ratiba yao huko iringa kama kawaida.
 
Tena huo ndio wakati wa kuandaa mazingira ya mikutano ya nguvu hasa. God is in our side.
 
Kweli wakati mwingine nakubaliana na maneno ya molemo, kweli bila Mbowe CDM ni history. Busara zake ni muhimu sana, huu upuuzi ulio tokea moro usinge tokea kama angekuwepo nchini.
Slaa,damu ya huyo kijana iko mikononi mwako.
 
Afadhali. Ngoja nipumue kidogo kuvuta siku. Huku nilipo siku wakija sijui itakuwaje, mtatuua jamani na mawazo
 
Back
Top Bottom