Dr Slaa Apinga Matokeo Yanayoendelea Kutangazwa na Tume

Yeah! Man it's true,she is out of her mind.(The Good)
Hana na hajui alisemalo huyo mtoto,Dr. Slaa is the right President to be.
Hata ningekuwa mimi ni real Dr. S nisingeyakubali matokeo yaliyochakachuliwa.
Where are the reasons za kuyachelewesha matokeo?
 
you should ask the persons who puts those ideas of pangas and Kenya scenario you bustard...don't come here and comment your non sense read other threads and you will see where i got those quotes and rephrase the subject to reflect what you mean...
 
Watu wenye hulka ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi wanajulikana kwa matendo yao; Buckreef ni mmoja wao. Yawezekana ni mtoto au ndugu wa mafisadi, au fisadi lenyewe. Ucheleweshaji wa matokeo ya ubunge ni dalili tosha ya wizi wa kura. Haiingii akilini nchi ya zanzibar wameshatoa matokeo ya urais huku bara hata ya ubunge ni shida kuyatoa hadi wanachi waandamane. Bila wananchi kuwa macho majimbo kama ubungo, Arusha, Ilemela na Nyamagana kura Zingeibwa. CCM ni wezi wa kura. Kamwe tusikubali matokeo yasiyo halali.

Hivi kwanza umeona lilivyoandika eti viti 30 vya Urais!!! Hivi kumbe kulikuwa na viti 30 vya Urais? Makubwa haya!!!
 
..Dr.Slaa hajasema kwamba ameshinda.

..anachodai ni kwamba kuna uchakachuaji wa kura.

..mimi nadhani hata kama ameshindwa, kuna ulazima wa kumpa kura sahihi alizopata.
 
Watanzania tuliopo Tanzania,
Tuwe makini na michango mingi inayotolewa humu. Posts nyingi ni za wale wanaoishi nje ya nchi.
Hawapotezi lolote iwapo fujo na mauaji yatatokea hapa.
Ole wewe utakayedanganywa uuawe/udhurike/ndugu zako wauawe etc etc.
They have nothing to lose... wao ni kuchochea tu.

Tusubiri 2015 tujaribu tena.
 
Watanzania tuliopo Tanzania,
Tuwe makini na michango mingi inayotolewa humu. Posts nyingi ni za wale wanaoishi nje ya nchi.
Hawapotezi lolote iwapo fujo na mauaji yatatokea hapa.
Ole wewe utakayedanganywa uuawe/udhurike/ndugu zako wauawe etc etc.
They have nothing to lose... wao ni kuchochea tu.

Tusubiri 2015 tujaribu tena.
 
Anachoamanisha Slaa ni kuwa kumekuwa na tofauti kubwa kati ya kura za NEC na zile za majimboni na hii yote ni inaleta fikra kuwa sisiemu wanataka kufikia asilimia 80 mie nadhani kwa jinsi tume yetu ilivyo hakuna budi kushindwa ila nguvu zielekezwe kwenye majimbo yaliyobakia ili wasiibe na pindi upinzani ukiwa na wabunge wengi jamaa hawatapata theluthi mbili which is good for starting kuelekea ukombozi wa kweli.
Frankly speaking and writing nimependa comment yako mkuu, i was always downlooking you but i've come to appreciate you. Thanx but i'm sorry for always having a negative attitude about you. My confessions!
 
Hakuna wizi wowote ulio fanyika , ameisha ona anashindwa na hana la kufanya anawadanganya kuwa ameibiwa. Hana jipya Slaa na hili wala sio jipya kulisikia kutoka kwake, tulilitegemea kabisa.
Kaoshe kwanza ndo uilete hapa tuichakachue ndo utaelewa tunamaanisha nini!~
 
Tumezoea .. wanasiasa wa Africa siku zote wanakataa matokeo " hebu ajifunze toka kwa Maalim seif" aituletee mambo ya kenya hatutaki damu imwagike.. coz mashabiki wenyewe wa chadema ni watu wavurugu
 
Nafikiri uliye uliza swali bado una mawazo mugado, huelewi hali ya dunia inakoelekea na inatakiwa Tanzannia hii ielekee wapi? Utawala wa TZ umerudi nyuma karne moja kwani umeanza utawala wa kisultani baba kumwachia mtoto madaraka kwa nguvu ya dolla wala si ya umma. kulazimisha wajukuu wao kutawala bila kujali jamii inataka nini. Dr S ni shujaa anayesoma nyakati na kutaka kuelekeza umma hisia tunayoiona na tunataka kuondokana nayo. nakushauri usichokoze wana mapinduzi wa JF watakutundika!!!!
 
Kweli watanzania wengi elimu cheche, kuna mijitu mingne haielewi harakati wala haiamini mapinduzi, ndo maana wengne wamerizika na maisha utakuta baba yake alikuwa mjumbe wa nyumba kumi na yeye anataka aje arithi hyo kazi, how come?
 
MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema, atayakataa matokeo ya urais yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa kumefanyika wizi mkubwa wa kura.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema, kama NEC inaitakia mema nchi hii, ifute matokeo yote ya urais na uchaguzi urudiwe upya.

Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema wamekuwa wakifuatilia matokeo ya nchi nzima kwa umakini mkubwa na wamegundua kuna wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.

"Kuna uchakachuaji mkubwa wa kura na kazi hiyo inafanywa na usalama wa taifa,"alisema Dk Slaa.

Source: Gazeti la Mwananchi

Kwani huyu Dr. slaa si ndiye aliyesema usalama wa taifa kawaweka viganjani-vipi wamchakachulie tena-shameful!
 
Sielewi nikitu gani anakitaka huyo DR SLAA haswaa pale anapo dai kwamba wamechakachua matokeo {KWA HIYO ANAMANISHA KWAMBA YEYE NDO ALIPASWA KUSHINDA AU ANAMAANA KITU GANI?}:thinking: jamani asije tupeleka BAGHDAD


Yeye ana maana ya kwamba taratibu hazifuatwi. Hayo mambo ya Baghdad ni hisia zako wewe mwenyewe sababu umekuwa brainwashed (umedanganywa mpaka ukawa mbumbumbu). Tanzania haiwezi kuwa kama Baghdad sababu sisi hatuna Taliban na Osaba Bin Laden pamoja na watu wanaojilipiua mabomu (suicide bombers).
 
Pumba...zenu eti Dr. Slaa anataka kutupeleka wapi? Jiulize CCM/kikwete na mafisadi wake wanataka kutupeleka wapi??? Dr. Slaa anapigania haki ya watanzania wewe nyang'au unayemshangaa kukataa kukubali matokeo ulitaka afanye kama alivyofanya CUF zanzibar??? Hapa mpaka kieleweke kama kukosa tukose wote. CCM NDIYO WANAOICHAFUA NCHI YA TANZANIA SASA KITAELEWEKA MWAKA HUU MBU...............iiiiiiiiiiii HAWA! Mmeshatunyanyasa vya kutosha mbivu na mbichi mtaijua sasa.

Umenena, tatizo makame na kiravu walidhani wanasimamia kura za maoni, walikuwa wanasimamia uchaguzi mkuu wao wakakubali kuendeshwa kama magari mabovu ndio matokeo yake.
 
Kwenye njia sahihi, right path, Kiravu na makame wamewapoteza njia watanzania

Kiravu na Makame wapo pale kama mabuitunge tu. Kuna ''team of experts'' ipo nyuma ya mapazia inacook data kwa fujo na wale vilaza wanaambiwa..haya, tangaza hivi!

Baada ya kumalizia kazi yao kwa ufanisi (wizi), hawa wazee wajiuzuru haraka
 
hawa ni vibaraka wa ccm na sio tume huru,kilichopo tushikamane tumuunge mkono Dk Slaa kupinga uchakachuaji uliofanywa na tume.
 
Dr. Wilbroad Slaa ni rais wa nyoyo za wapiga kura Kikwete ni rais wakuchakachuliwa na NEC
 
Back
Top Bottom