Dr Slaa Apinga Matokeo Yanayoendelea Kutangazwa na Tume

Makame angaliaaaaaaaaaaaa, iko siku huyo unayemtetea hatakuwa na wewe utajitetea mwenyewe.
 
CCM wanataka washinde kwa 80% ili wapate ruzuku kubwa au? Maana hata ushindi wa 50% si ushindi tuu
 
NADHANI kila mtu atapata kuufahamu ukweli.Lakini kwa maoni yangu sioni kama ni busara kwa Dr SLAA kupinga matokeo na kusema kwamba yamechakachuliwa JE?NIWAPI ANATAKA KUTUPELEKA?:sad:
 
Ndugu zanguni Dr. Slaa ameshindwa tu , asitafute kizingizio. Amachotakiwa nikujipanga upya tu , hivyo visingizio alivyo vitoa si vya kweli . Asiye kubali kushindwa si mshindani, tunajua amepata aibu ila jikaze JK si saizi yake wakuu:yield::yield:
 
Dr. Slaa toa tamko lingine nini watanzania wafanye nini hii kitu haiwezekani...watanzania wanasubiri tamko lianzie kwako wao hawawezi kunza wao...TOA TAMKO lingine
 
Nwachukia mpaka nakosa lugha ya kuelezea Makame na Kiravu wake, MUNGU awalaani kwa kudhulumu haki ya watanzania na vizazi vyao vyote, maisha yao ya uzeeni yawe ya taabu sana na mwisho waishie kuzimu kwa dhambi kubwa waloifanya kwa Taifa la TANZANIA.

Kwa ninavyojua mimi uzee ni hekima lakini huyu makame na kiravo wamekuwa na uzee wenye laana, hii ni bahati mbaya sana kwao,ukiona mzee anashiriki wizi basi jua hiyo ni laana mbaya kuliko zote
 
jamani sisi wengi wetu tupo tz au mpo nje isijekuwa tukatane mapanga wakati yie mpo nje
 
Dr. Slaa toa tamko lingine nini watanzania wafanye nini hii kitu haiwezekani...watanzania wanasubiri tamko lianzie kwako wao hawawezi kunza wao...TOA TAMKO lingine

Liko njiani. Lazima kieleweke tu!! Nguvu ya Umma ni zaidi ya Uchafu (Usalama) wa Taifa
 
Dr Slaa Apinga Matokeo Yanayoendelea Kutangazwa na Tume, akidai kuwa yamechakachuliwa
Source ITV

Nilijua ataanzisha fujo> Kukaa nje ya bunge miaka mitano hawezi. Nadhanu anataka iwe kama Zanzibar
 
MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema, atayakataa matokeo ya urais yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa kumefanyika wizi mkubwa wa kura.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema, kama NEC inaitakia mema nchi hii, ifute matokeo yote ya urais na uchaguzi urudiwe upya.

Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema wamekuwa wakifuatilia matokeo ya nchi nzima kwa umakini mkubwa na wamegundua kuna wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.

"Kuna uchakachuaji mkubwa wa kura na kazi hiyo inafanywa na usalama wa taifa,"alisema Dk Slaa.



Source: Gazeti la Mwananchi
 
Hivi niambieni wana JF...Kuna ulinzi kiasi gani pale wanapotolea uchafu wao hao NEC? Hatuwezi kupinga kwa kufanya maandamano na kushinikiza aache kuendelea na uongo huo? Naombeni mawazo yenu plz
 
Back
Top Bottom