Dr Slaa amaliza ziara Marekani

Omba omba utamjua tu hata kwa maandishi toka akilini mwake.Fanyeni kazi acheni kutemea kuomba ndiyo CCM imetuuza .

Mkuu Lunyungu huyo mhemea Lumumba alitaka Dr Slaa aende na Bakuli Marekani.Dr Slaa kawaambia hataki pesa zao bali anataka utaalamu wao.

How the greatest Leader in Africa!!
 
Last edited by a moderator:
Kama haitawaliki basi babu alienda Marekani kutafuta hifadhi ya kikimbizi

Slaa ameing'arisha Tanzania. Wanaoenda US kutembeza bakuli kwa kuchekacheka walishaidhalilisha nchi hii. Asante Slaa kwa kurudisha heshma na utu wa Mtanzania
 
Kwa kulifahamu hilo ndio maana babu daily anaweweseka mara utamsikia..."oooh hii nchi haitawaliki","tutaandamana mpaka kieleweke" + matamko mengi yasiyokuwa na tija huku CCM na serikali yake ikizidi kujikita katika mioyo ya watanzania.

Siku bbu atakapoamua kuivalia njuga mahakama ya Kadhi, uwe na uhakika mtaipata ndani ya kipindi kifupi tu. Katiba ndio hiyo....Amewafunga goli akiwa kwenye benchi. Kudadadeki!
cc Mwita Maranya
 
Last edited by a moderator:
Hapo kachemka wasitoe misaada ya pesa na watu wao wakale wapi? Unaipa msaada nchi pesa halafu unaleta watu wako waje kuzibomolea huku kama wasimamizi wa hizo pesa na hayo uliyotolea msaada.Misaada ya pesa haiji kukoma ng`o.Na ambao hataki ikomeshwe kama hajui ni hao wanaotoa wenyewe.Hiyo hotuba aliyotoa ni mwiba kwa CHADEMA.Hawajaangalia wanaowahutubia huwa wanapenda nini.Saa hii watakuwa wamejifungia ndani wanaichambua kama karanga.Take it from me CHADEMA isahau misaada ya fedha toka kwenye nchi hizo walikohutubia.CHADEMA misaada ya fedha toka nje ikipungua wasishangae hotuba zao zimewaponza.

Wewe umekurupuka! Hujaelewa alichokisema Dr Slaa, soma tena na uelewe maana umekurupuka tu na kujibu. Haraka ya nini mkuu! Magamba bhana utawajua tu kwa "kukurukakara" zao...

Mmelogwa na nani jamani?!!!
 
Si ajabu pamoja na matusi haya uliponyeshwa Fistula kwenye hospitali ya CCBRT.Huna hata shukrani.

Slaa ndio hana hata shukrani kwa wafadhili wanaotoa pesa za kuendeshea CCBRT kusema hataki hela za wafadhili wakati anajua kuwa bajeti ya CCBRT inategemea wafadhili ni kwenda kuhutubia uwongo asioufanyia kazi.Slaa kichwa chake hakijatulia au washauri waliomsaidia kuandika hotuba ni mabomu au watunga sera za Chadema mmewachukua watoto wa mwaka wa kwanza vyuo vikuu.
 
daa mtake msitake huy jamaa ni great! bila shaka wazungu wameelewa kuwa tz bado kuna vichwa maana walizoea kuyaona magamba yakitabasamu bila point! bravo sana DR SLAA WA UKWELI!!!
 
Slaa ndio hana hata shukrani kwa wafadhili wanaotoa pesa za kuendeshea CCBRT kusema hataki hela za wafadhili wakati anajua kuwa bajeti ya CCBRT inategemea wafadhili ni kwenda kuhutubia uwongo asioufanyia kazi.Slaa kichwa chake hakijatulia au washauri waliomsaidia kuandika hotuba ni mabomu au watunga sera za Chadema mmewachukua watoto wa mwaka wa kwanza vyuo vikuu.
Shukurani kwa mtu anayechukua dhahabu anakuletea net za mbu, ujinga.

Fuatilia hotuba nyingi za Nyerere UN alikuwa anakiwatukana wazungu na kuwaambia ukweli kwa ubeberu wao, hotuba zake hazina tofauti sana na ya Slaa.
 
Mwongo ni yule aliyekuahidi Mahakama ya Kadhi. Ukachekelea kama zuzu. Ukala pilau lake. Mwishowe kakuchinjia baharini. Hakuna kadhi wala dalili ya kadhi...dadeki!

Mahakama ya kadhi iliondolewa na mkristo itarudishwa na mkristo,LOWASA au MEMBE.ZENJI iliachwa,KENYA iliachwa na Katiba yao mpya imeipa nguvu zaidi.tunajua mupo wengi maofisini na kwanini JK kashindwa,Umoja'TZ ni muhimu zaidi,sisi tunazidisha ibada na subra.kama itapatikana ni kwa maridhiano ya wote isiwe kama fadhila au kuturidhisha.
 
Na ndio sifa ya kiongozi anaefaa kuliongoza taifa la watanzania bila kujali imani ya kidini,rangi,ukanda wala kabila.Na kwa kukosa sifa hizo Chadema hawatokuja kuliongoza taifa la Tanzania milele kwa kuwa tunawafahamu na dhamira waliyoibeba inatambulika.JK ni kiongozi wa taifa la watanzania kwenda kanisani kushiriki na watanzania wenzake katika ibada wala sio tatizo.Lakini jiulize kama ingetokea padri Slaa watanzania wangejaribu kumpa uongozi wa nchi angeshirikiana na watanzania wenzake wenye imani tofauti na yeye?


Ni aibu kwa mtu unayetukana matusi badala ya kujenga hoja kujinasibu kuwa mfuasi wa falsafa za Mwalimu Nyerere.Ndiyo akili kubwa ya kumuenzi Mwalimu Nyerere hii?Na hilo la kusema CHADEMA haiwezi kuchukua Dola linapingana na mtazamo wa mwalimu.Vipi Kumuenzi Nyerere ni kwa kuhudhuria Ibada na kufunga mbio za Mwenge?


Leo ni siku ya wanafiki kumuenzi Nyerere bila dhamira ya dhati.Hata wale waliolizwa kuwa mali walizokuwa nazo mwaka 1995 walizipata wapi hadi leo baada ya kifo cha Mwl.Nyerere bado hawajatoa majibu ila wameona fursa kupitia kifo chake na sasa wanajiandaaa kutekeleza dhamira yao ovu iliyozimwa.Wapo wachache wanaoienzi misingi ya Mwl.Nyerere na fikra zake,yaani yale yaliyokua mazuri.Njia bora ya Kumuenzi sio kujenga sanamu au kufunga na kufungua mbio za Mwenge.Ni kuziishi fikra zake.Njia bora kwetu vijana ya kumfufua Mwalimu Nyerere na kulifuta machozi taifa letu lenye majonzi ni kupigania haki,usawa na kupinga ubaguzi na uonevu popote pale huku tukizifanyia kazi falsafa za Mwalimu
Nimeweka baadhi ya nukuu za Mwalimu Nyerere na za Rais wa Sasa Jakaya Kikwete.Je tunasonga mbele kifikra ama tunarudi nyuma kwa kasi?
Watanzania wanataka mabadiliko,wakiyakosa ndani ya chama hiki watayatafuta nje ya chama-Mwl.Jk Nyerere(1995 Ndani ya Mkutano Mkuu wa CCM)
CCM si mama yangu-J.K Nyerere
Small nations are like indecently dressed women. They tempt the evil-minded. -J.K Nyerere.
Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: taabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni"J.K Nyerere
***********************

'Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya sana' 01/5/1995
***********************

'Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu -ukalikubali, anakudharau!' 01/5/1995
***********************

“Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika” –MwalimuNyerere (Januari, 1966)
***********************

"Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka rais ambaye atalitambua hilo na ataichukia rushwa hata ukimuangalia anaonyesha kweli anaiichukia rushwa, sio rais ambaye anayesema kweli rushwa ni adui wa haki....lakini ukimuangalia usoni unashangaa na kusema.... aaaah kweli huyu?Mwl.J.K Nyerere
***********************

"Poverty is not the real problem of the modern world. For we have the knowledge and resources which could enable us to overcome poverty. The real problem--the thing which causes misery, wars, and hatred among men--is the division of mankind into rich and poor." Mwl.J.K Nyerere
***********************
Source inapatikana kwenye hiki kitabu
Reflections On Leadership in Africa' VUB University Press, 2000.

Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?
***********************
Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii.
***********************
Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga.
***********************

Kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ni wajinga tu.
***********************

Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe....
***********************

Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao (wananchi) na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili.

Kwa mtu msafi kabisa,Ikulu ni Mzigo sio mahali pa kukimbilia- J.K Nyerere

Igeni yale mazuri,yale mabaya muyaache maana katika kipindi cha miaka 25 ni lazima tulifanya makosa,kwani sisi Malaika Tusifanye Makosa?-J.k Nyerere


Tuangalie Nukuu za Rais wa Sasa Jakaya Kikwete





1. Urais wangu hauna ubia.-Jakaya Kikwete

2. Tatizo la umeme ni ukame, mimi siwezi kuilazimisha mvua inyeshe-Jakaya Kikwete.

3. Hawa wanaopata mimba ni kiherehere chao.-Jakaya Kikwete

4. Kama hawa watuhumiwa wa EPA wanasema fedha hizo walizitumia katika uchaguzi, watuenyeshe walizitumiaje(stakabadhi).- Jakaya Kikwete

5. "Mie ndie rais wa kwanza wa Africa kukutana na rais Obama" –Jakaya Kikwete

6.......hili ni panga la zamani, haliishi makali ! – Jakaya kikwete (wakati anamnadi Basil Pesambili Mramba)

7: Ukitaka Kula ni Lazima nawe uliwe-Jakaya Kikwete

8: Mie ndio mwajiri mkuu...... hata mkigoma miaka 8...... mshahara haungozeki ng'o' –Jakaya Kikwete(Akihutubia TUCTA)

10: Uchumi unakua sasa tazama foleni za magari,Maendeleo yana changamoto zake-Jakaya kikwete

11: "Mzee mwinyi alikaa miaka 10 hakuyamalza, mzee Mkapa miaka 10 hakuyamalza, mie miaka 5 sijayamalza na mingne 5 sitayamalza, hvyo basi (kicheko) matatzo hayawezi kwisha" Jakaya Kikwete

12:"Kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi" J. K. (akimtetea mbunge Chitalilo aliyegundulika kuwa kughushi vyeti vya elimu yake. )
***********************

13:"Nafikiri imefika wakati Tuwaombe Rafiki zetu wa Scandinavia,Watufundishe kuandika na Kusoma Mikataba haswa ya MADINI,kwani sie hatuna wataalamu hao" - JK Kikwete May'2007

14:Hata mimi nashangaa kwa nini Tanzania ni masikini-Jakaya Kikwete

15: Sipendi Kusutwa - Jakaya Kikwete(Akiwa Kigoma Mwezi February,2013)
 
Slaa ndio hana hata shukrani kwa wafadhili wanaotoa pesa za kuendeshea CCBRT kusema hataki hela za wafadhili wakati anajua kuwa bajeti ya CCBRT inategemea wafadhili ni kwenda kuhutubia uwongo asioufanyia kazi.Slaa kichwa chake hakijatulia au washauri waliomsaidia kuandika hotuba ni mabomu au watunga sera za Chadema mmewachukua watoto wa mwaka wa kwanza vyuo vikuu.

Hapa simzungumzii Dr Slaa.Nakuzungumzia wewe ulipona Fistula pale CCBRT?
 
Mtoa hoja hii sina wasiwasi dalili zote zinaonyesha kuwa unaumwa Fistula ya kiume na ni mgonjwa wa kiume wa kwanza kumwona.

Mbona unakwepa hoja? Jibu swali kwanza kwamba umeponea Fistula CCBRT lakini bado unakuja hapa kumtusi matusi ya nguoni Dr Slaa mwenye hospitali.

Anzia kujibu hapo mengine yatafuatia....
 
Leo ni siku ya wanafiki kumuenzi Nyerere
Ha ha haaa Ben bana leo wanafiki wako Iringa wanazima msukule wao,

Wanafikiri kuzunguka na msukule nchi nzima ndio kumuenzi Nyerere huku viwanda vyote wamemaliza kuviuza.
 
Back
Top Bottom