Dr. Slaa alitushauri wa-TZ tukampuuza, sasa kulalama kwanini?

Status
Not open for further replies.
Wakti wa kampeni za urais Dr. Slaa alitushauri waz-tz tusimchague JK. na kama hatumtaki yeye basi angalau tuchague hata Li-PUMBA! na endapo tutamchagua JK basi tutambue tumeingia katika matatizo.
hivi sasa petrol shida, umeme shida, shilingi inaekea kaburini, sukari usiseme,
Je kwa nini tusimwite Dr. Slaa kuwa ni mtume/nabii?

tafadhali ndg yangu, unanikumbusha machungu.
 
yule ni chaguo la NEC na jeshi la polisi na JWT likiongozwa na SHIMBO + Usalama wa Taifa.
 
tuache lawama zisizo na msingi na sifa za kijinga.slaa hawezi kuwa nabii,ana usafi gani wakati amepora/anatembea na mke wa mtu pili hali ya uchumi kuwa mgum inasababishwa zaid na external force,uchumi wa mataifa makubwa km US na UK umeyumba na una direct impact kwetu.kwa hiyo acheni kuhadaa watu.

Wewe ndio unaohadaa watu.
 
wewe umelogwa au kama cyo hivyo basi itakuwa magamba wanaku cameruni.
 
tuache lawama zisizo na msingi na sifa za kijinga.slaa hawezi kuwa nabii,ana usafi gani wakati amepora/anatembea na mke wa mtu pili hali ya uchumi kuwa mgum inasababishwa zaid na external force,uchumi wa mataifa makubwa km US na UK umeyumba na una direct impact kwetu.kwa hiyo acheni kuhadaa watu.

Ama kweli wewe una hoja tete kama jina lako. Unatakiwa kwanza ujiulize ni kwa nini uchumi wa mataifa makubwa ukiyumba na Tanzania inayumba kabla ya kuja hapa na utetezi wako usio na mashiko!
 
tuache lawama zisizo na msingi na sifa za kijinga.slaa hawezi kuwa nabii,ana usafi gani wakati amepora/anatembea na mke wa mtu pili hali ya uchumi kuwa mgum inasababishwa zaid na external force,uchumi wa mataifa makubwa km US na UK umeyumba na una direct impact kwetu.kwa hiyo acheni kuhadaa watu.

MwanaJF Hojatete,

Hizo lawama zisizo na Msingi ni zipi? Hizo sifa za Dr. Slaa zinazohusu kuchukua mke wa mtu zinahusianaje na ugumu wa maisha unaowakabili WaTz kutokana na Serikali kushindwa kutupatia umeme wa hakika kwa ajili ya factories zetu?

Ajira kwa vijana ni finyu kutokana na uzembe wa watawala wetu. Kuyumba kwa uchumi duniani hakukusababisha mabilioni ya TShillings kukwapuliwa toka BoT, ambayo yameingizwa ktk mzunguko wa fedha na kuleta inflation tuliyo nayo sasa.
Dr Slaa na chama chake wameongea tangu wakati wa Mwembe Yanga, kwa ni lazima hatua dhidi mafisadi zichukuliwe kama tunataka kuendesha mambo kwa ufanisi. Mambo haya hayana uhusiano wowote na Slaa kumchukua Josephine kama mke.

Muulize Gavana wa BoT sababu za huu mfumko wa bei. Atakuthibishia kwamba kiini chake kikubwa ni fedha zisizotokana na jasho zinazoingizwa ktk circulation na jamaa za kina Kikwete na mafisadi waliozagaa nchini kwa vile hawajachukuliwa hatua. Zilianzia pale Ballali alipokubali kutoa fedha za EPA kwa claimants feki kama Rostam Aziz na mafisadi wote wanaohusishwa na huo ukwapuaji.

Sababu nyingine za inflation hapa Tz ni uhaba wa chakula hasa ktk sehemu zilizokumbwa na ukame. Tatizo la njaa lingeweza kupunguzwa kama Serikali ilikuwa makini kwa kugawa kwa uadilifu mahindi kutoka Strategic Grain Reserve.

Sehemu ya inflation inayosababishwa na uchumi wa dunia kuyumba, ingeweza kushughulikiwa na Serikali makini kwa kuagiza BoT kutoa fedha za kigeni kwa wingi kuagiza mahitaji na kupunguza au kuondoa kodi ktk bidhaa husika. Serikali makini na adilifu ingewezekana tu, kama Dr. Slaa na Chadema wangechaguliwa.
 
Mimi nakumbuka Dr slaa alipokuwa anafunga anamalizia kampeni kwa mdahalo pale Movenpick 2010 alisema "kuendelea kuichagua ccm ni maafa" naya kumbuka sana maneno yake kila nikisikia watu wakilalamikia ugumu wa maisha na mfumuko wa bei.

The majority of Tanzanians did not vote for Kikwete during the 2010 General elections; the ruling party in collaboration with the National Electoral commission stole the election victory from Dr. Slaa!!
 
Mkuu nina dvd yake ya mdahalo mzima nikirudi jioni nitaiangalia tena nimskia dr wa ukweli akimwaga nondo. Kwenye hiyo Cd alimlipua sana Jk na alibainisha wazi kuwa aliyoyasema yote ya kweli kuwa Jk alikuwemo kwenye ile list of shame.
niwekee hapa vitambu na machapisho ya dr wa ukweli
 
Sikilizeni wadau, Great Thinkers!!! Dr Slaa alishinda uchaguzi 2010! CCM waliiba kura! Naomba msilalamike kuwa mlichagua CCM, muilamu serikali kwa kushirikiana na hiyo CCM na bwana Kivuyo kwa kuiba kura. Ushahidi upo na mtakumbuka maeneo kama mwanza, Arusha n.k
 
JK aliteuliwa na tume ya uchaguzi NEC na si wananchi...watz si vilaza kihivyo!
 
tuache lawama zisizo na msingi na sifa za kijinga.slaa hawezi kuwa nabii,ana usafi gani wakati amepora/anatembea na mke wa mtu pili hali ya uchumi kuwa mgum inasababishwa zaid na external force,uchumi wa mataifa makubwa km US na UK umeyumba na una direct impact kwetu.kwa hiyo acheni kuhadaa watu.

kupora mke hakuna impact kwenye maisha yetu ya kila siku...ila ulegelege wa serekali unasababisha maisha yetu hayatulii......nyie ni kiboko maana mnamsingizia mungu kwa kila jambo..umeme hakuna kwa sababu mvua hainyeshi,ndo majibu yenu hayo kwa maswali magumu
 
Wapi Rejao, MalariaSugu, GiniasBrein na Ritz katika kuchambua maswala nyeti kama haya yanayohusu mustakabali wa taifa letu? Ritz kaibuka na phrase badala ya hoja ya msingi! huyo ndio great thinker anategemewa na magamba kuwakilisha!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom