Dr. Slaa Akamatwe, ahojiwe na ikiwezekana achukuliwe hatua

- Mkulu Gembe, heshima mbele sana, tatizo ni kwamba utafukua mengi sana kwa mfano hii barua ya Masha kwa waziri mkuu, ninajua kuwa imelikishwa kwa makusudi na hao hao tuliowakabidhi dhamana ya kulinda sheria zetu,

- Again huwezi kuwa na maelezo ya kutosha kuhusu ni wapi magazeti ya Mengi yanapata habari nyeti nyingi za uporaji mali wa Mkapa na zingine mbali mbali, sasa tumefikia mpaka mawaziri kurekodiwa kwenye vikao muhimu vya serikali, sasa uta-draw wapi the fine line ya kamata kamata na siri za serikali?

Serikali yetu ya sasa sio siri ina matatizo makubwa sana na utunzaji wa nyaraka za serikali, infact sio vibaya kuiita ni Banana Republic, maana mimi sijawahi kuona mambo ya ajabu kama ya hii serikali, I mean haina siri tena kuna wanazozivujisha wenyewe na ambazo hawana control nazo kabisa,

Sasa ukimkamata Dr. Slaaa then utaishia kuikamata serikali nzima, ndio maaan hawawezi hilo, na besides DR. Slaaa analisaidia taifa zima na hizi nyaraka, na hata sometimes serikali yenyewe, sasa unaona ni kwa nini hii ni Banana Republic?

Mkuu nadhani umeona mbali sana, ukweli ni kuwa kuna kina Slaa wengi ndani ya CCM,Serikali na kwenye upinzani wanaoitakia mema Tanzania. Kwa hiyo kama kamatalamata ikianza basi hakutakuwa na nafas ya kuwaweka waliokamatwa.
ingawa kuvuja kwa siri hizi kunaonesha kuwa watanzania si mabwege tena, na kunaonesha kuwa wazuri serikalini wamechoka na ujinga unaofanyika na kuufanya siri, nakubali ni kama kuiendesha serikali kitoto. Lakini pia it is a blessing in disguise, tunajuaviongozi wetu wanafanya nini. This time hata ukimuuliza mtoto kwanini nchi etu haiendelei atajua sababu, sio kama zamani lawama zooote zilikuwa kwa mwingereza.
Mkuu umenifurahisha sana kuiita nchi yako Jamhuri ya ndizi.
 
Nafikiri huyu Gembe ni fisadi wa mawazo na anafikra finyu. Hakuna nyaraka za siri za serikali hata siku moja nyaraka zote zinazohusu serikali ni mali ya uma .Serikali ni watu sio mafisadi.
 
Watu hapa tumekimbilia kumzungumzia Masha wakati hoja haimhusu Masha. Hoja ipo wazi ni kuhsu Dr. Slaa kumiliki Nyaraka Za serikali, Je tatizo liko wapi na madhara ya kuliki kwa siri za serikali ni yapi?

Sasa tatizo lako ni Dr. Slaa kumiliki hizo unazoita siri za serikali au mtu yeyote kuzimiliki. Kwa kuwa na wewe umemkazania Dr. Slaa tu, na wengine wana haki ya kumtaja Masha kama mhusika katika kinachotafsiriwa kama siri ya serikali. Hoja yako kama ilivyo inakuumbua wewe mwenyewe na obsession yako na Dr. Slaa - shujaa kwa wananchi lakini mwiba kwa watawala - are you there ?

There is apoint ambayo tunamiss hapa, tunatawaliwa na mawazo ya kumzungumzia mtu na siyo kuzungumzia yale ambayo watu wanayataka.

Point ambayo unaimiss hapa ni kuwa umeruhusu kutawaliwa na mawazo ya kumzungumzia Dr. Slaa na si issue ya umilikaji wa unazoita nyaraka za siri na mtu yeyote yule. Kumbuka kuwa zamani yalijulikana kama mabomu lakini yalipoanza kuitikisa serikali sasa yabatizwa nyaraka za siri.

Jiulize kama Barua hiyo ingekuwa inahusu mambo ya kijeshi na nia ya serikali ingekuwaje? Kuna tatizo sehemu na hapa ndipo pahala pa kupata suluhisho lenyewe. Mie nimeanza kuogopa kwa kweli, kama watu wanaweza kupata Barua kutoka kwa Waziri kwenda kwa waziri Mkuu? kuna tatizo hapa

Naamini wanaovujisha unazoita nyaraka za siri za serikali wanatumwa na utiifu wao kwa taifa na dhamira yao ya kutetea maslahi ya Taifa. Ni sababu hii hakuna siri iliyovujishwa mpaka sasa ambayo imehatarisha taifa - naomba utaje angalau moja kama ipo. Kama unaanza kuogopa nyaraka ambazo zimevujishwa mpaka sasa na zikatusaidia kuwajua maadui wa taifa letu, basi hapa mwenye tatizo ni wewe na siyo Dr. Slaa.

Afisa akiandika memo na kusema "Mhe. zile zawadi ulizoagiza zimeshaingizwa kwenye mfuko wako. Kiasi kingine tumeshampatia Katibu x,y na yeye zimepitia UK" halafu akaweka "Siri Sana" je ni haki kuvujisha kitu kama hicho?

Mkuu Gembe kwenye huu mfano wa Mzee Mwanakijiji, wewe kama ofisa serikalini ungefanya nini. Ungeusaliti umma wa Watanzania hapa chini ya mwamvuli wa sheria na kumnyamaza au ungepiga kelele kama za Dr. Slaa. Kwa hoja yako ni kuwa ungenyamaza na mimi naaza kuogopa kama siri hizi za kifisadi haziwezi kuanikwa na wahusika kushughulikiwa.

Basi kama Dr. Salaa akihojiwa itavuruga mambo ya serikali eti kwasababu kuna viongozi wataguswa, ni kheri tuwe na serikali ambayo itaendeshwa kwa usiri na yenye kulinda mambo muhimu ya taifa letu!

Waziri Mkuu mwenyewe mchana kweupe aliuambia umma kuwa mafisadi na wahujumu wa taifa wakikamatwa nchi itayumba - unakumbuka ? Kama mambo yenyewe muhimu ya taifa yanayolindwa ni mikataba mibovu ni hatari ambayo mwisho wake ni kuliangamiza taifa. Je, Gembe hilo ndilo unalolitaka ama kuna ajenda nyingine inayokusukuma kutetea maovu katika jamii. Serikali haiwezi kuendeshwa kwa sheria na hapo hapo ikawa na ubia na wavunja sheria na ikawaogopa.

Ila mpaka sasa wazo langu ni hilo: Naomba Dr. Slaa Akamatwe na ahojiwe na aeleze alitoa wapi vielelezo hivyo, ikiwezekana awataje waliompa ili nao wachukuliwe sheria.

Unarudi pale pale - Dr. Slaa akamatwe - watu wengine bwana. Wakati wengine tunatafuta tuzo gani apewe huyu mpambanaji, Gembe mtetezi wa sheria anataka akamatwe !! Bila shaka ungependa kuona kesi zote zilizofunguliwa kutokana na unazoita nyaraka za siri zifutwe, mafisadi watembee vifua mbele, wezi tupigane nao vikumba mitaani na wenye nguvu ndio watambe - that is called laws of the jungle - wewe unaiita utawala wa sheria.

Tuache uongozi wa kuogopana, haya ndiyo yanaleta mambo ya kuwa nchi itashindwa kutawalika kama jambo flani likitokea. We need to take action.

Hizo unazoziita siri za serikali ndizo zitakazoifanya nchi isitawalike. Je siri alizokuwa nazo marehamu Dr. Balali zingekufikia mezani kwako, ungezikalia kwa kuziita nyaraka za serikali ? Mh. Gembe, siamini kuwa umetumwa na uzalendo wa kutetea utawala wa sheria, bali kwa kutambua "the wall is closing in" na wengi waliomo na wasiokuwamo kuna hatari kubwa ya kuumbuliwa. Swali ninalojiuliza, je aliposimama Gembe ni salama ?

Big up Dr. Slaa, ukiona watu wanaanza kujikuna ujue pilipili inaanza kuwasha.
 
Gembe anatakiwa kukamatwa na vyombo vya sheria hasa baada ya kuweka wazi kuwa nyaraka ambazo Dr Slaa anazo ni siri za Serikali alizozipata kutoka wizara ya Mambo ya Ndani.Tunatambua ni kosa kisheria kwa Mtanzania yeyote kuwa na nyaraka za siri za serikali.

Kwa kuwa Gembe amezitambua nyaraka hizo kuwa ni za serikali, hivyo anathibitisha kwamba anazo na ameshtushwa baada ya kugundua kuwa alizozitaja Dr Slaa ndio hizo hizo za wizara ya Mambo ya Ndani !!
 
Mhe. Dr. Slaa anahitajika kukamatwa na Vyombo vya sheria hasa baada ya kuwa na Nyaraka ambazo ni siri za Serikali alizozipata kutoka wizara ya Mambo ya Ndani.Tunatambua ni kosa kisheria kwa Mtanzania yeyote kuwa na nyaraka za siri za serikali.

Mbona ipo too general Ina maana na wanaziandaa nao hawaruhusiwi au, hebu weka kipengele na section katika sheria zetu inavyoeleza, ni nani anaruhusiwa na nani haruhusiwi kabla ya kuja na maneno ya kufikirika toa reference ya section na quotations.

Mbona wamechelewa? Mimi nakuunga mkono wa mkamate mapema iwezekanavyo na wamfikishe Kisutu! Siyo kwa hilo tu ulilopendekeza lakini kwa mengine:

a. Kwa kuwataja watu mbalimbali kuhusika na ufisadi na kuwachafulia majina yao katika ile orodha ya ufisadi.

b. Kwa kukubali kupewa nyaraka mbalimbali za "siri" na kuzitumia nyaraka hizo kuibua madai mazito ya ufisadi ambayo yamesababisha watu kadhaa wamtangulie Kisutu.

Hili ndiyo litakuwa funzo kwa Mtanzania yeyote kupokea nyaraka za siri. Siyo yeye tu bali pia itakuwa somo kwa mitandao kama JF kutumika kuweka nyaraka za namna hiyo na watu kuzipata kwa urahisi.

POLISI MKAMATENI DR. SLAA SASA KAMA MHE. GEMBE ANAVYOPENDEKEZA! NAUNGA MKONO HOJA!

Hapa Mzee Mkjj nakuunga mkono kwa 100%, kwa nini wanachelewa kumkamata huu si utawala wa kisheria. Wasihofie lolote kwenye hili hapa hakuna siasa hakuna kujuana wamkamate Dr Slaa haraka sana na dhamana yake iwe Shs Billioni 40 cash!
 
Jakaya asidhani mengi ni mtu mzuri kwake kama anavyodhania, wanaodharirika leo ni watu wa kariba yake na kinachofanyika si kuiponya nchi bali ni kuamsha uasi ambao baadae si yeye jk wala mengi watakaoweza kuutuliza, naamini jk anafahamu haya yote kwani ni sehemu ya serikali ya ccm yetu, kilichopaswa kufanywa na wasaidizi wake ktk kumsaidia si kuwavua nguo hao wenzake bali ni kuwanyang'anya vyote kimyakimya huku wakilishwa viapo mbele ya sheria kuwa hawataenda mahakamani kupingana na hayo, uzuri ni kwamba wengi wamehifadhi mapesa yao na mali hapahapa. Wasaidizi wa rais wamekuwa wanasiasa na kufanya ile tafsiri ya sirikali isi exist.

Juzi sitta kalalama sana cha ajabu leo kaishambulia mahakama bungeni kitoto kabisa eti kwa sababu tu mahakama imeonya kutoingiliwa na bunge kiutendaji.

Sasa ktk hali tutegemee nini huko mbeleni.

Naaamini sokoine kama sokoine amekufa leo basi kawawa angelikuwa tayri amehukumiwa juu kifo hicho.
 
Heshima Mbele,

Mhe. Dr. Slaa anahitajika kukamatwa na Vyombo vya sheria hasa baada ya kuwa na Nyaraka ambazo ni siri za Serikali alizozipata kutoka wizara ya Mambo ya Ndani.Tunatambua ni kosa kisheria kwa Mtanzania yeyote kuwa na nyaraka za siri za serikali.

Nchi hii inaongozwa kisheria,na tumekuwa tukipigania hili siku zote .Kwa mtazamamo wangu Naona kuna haja ya Dr. Slaa kuhojiwa hata kukamtwa kwa kumiliki nyaraka za serikali!

ikiwa wengi wenu mnataka Dk slaa akamatwe kwa kisingizio cha kuwa na nyaraka za siri hapa kuna maswali leo hii wengi wenu mgeelewa vipi mamilioni yanayo chotwa kwa maslahi ya watu binafsi au mmeridhika na mwenedo ulivyokuwa ?
 
Heshima Mbele,

Mhe. Dr. Slaa anahitajika kukamatwa na Vyombo vya sheria hasa baada ya kuwa na Nyaraka ambazo ni siri za Serikali alizozipata kutoka wizara ya Mambo ya Ndani.Tunatambua ni kosa kisheria kwa Mtanzania yeyote kuwa na nyaraka za siri za serikali.

Nchi hii inaongozwa kisheria,na tumekuwa tukipigania hili siku zote .Kwa mtazamamo wangu Naona kuna haja ya Dr. Slaa kuhojiwa hata kukamtwa kwa kumiliki nyaraka za serikali!

naamini kwamba dr. slaa kama wabunge wengine wanaruhusiwa kuwa na access na nyaraka za serikali ziwe za siri au vinginevyo. aidha kwa wadhifa wao huo wa ubunge wanakinga inayowalinda kujadili nyaraka hizo bungeni.
na kama nyaraka au suala litakuwa la "siri" sana basi naamini spika anayo mamlaka ya kuelekeza mjadala huo uendeshwe katika mfumo gani. katika hali hii siamini dr. slaa anakosa lolote la kuwa na hiyo nyaraka husika.

naamini dr. slaa anaweza kuwa matatani iwapo itathibitika kwamba yeye
ndio chanzo ya nyaraka hizo kusambaa katika mitandao na magazetini.

kwa hiyo hoja ya dr. slaa kukamatwa haina mshiko. hata waziri mkuu alisema "...umetuwahi. ungesubiri..." na wala hakuomba maelekezo kwa spika hatua inayostahili kuchukuliwa mbunge akiwa na nyaraka za siri za serikali.
 
Tatizo siyo kupokea Nyaraka za Siri kama unavyopendekeza Hapo,Ni yeye kumiliki Nyaraka za Siri za serikali.Sheria Zipo na lazima zifuatwe!

Tunataka Utawala wa Kisheria,Kwanini hatuoni hili linahitaji kupewa kipaumbele?

Wewe nani alikwambia Tanzania inaongozwa kwa utawala wa SHERIA????? mafaili ya Mafisadi Chenge na Idrissa yako tayari tangu Machi 2008 lakini hadi sasa hakuna kati ya hao 2 aliyefikishwa mbele ya sheria. Huu ndiyo utawala wa sheria, aaha
 
Usingehitaji kuwashauri wamkamate, kama wangejua ni wasafi, kwa kukamata huwa hawajambo!! Lakini kwa hili wanaona umma utashtuka,unamkamata anayepiga kelele za mwizi? Bahati mbaya siri zote huwa ni wizi na madudu sasa utamkamata mtu kwa lipi? Ndugu yangu hujawawahi walishaliwaza hilo kabla yako, ukiwaona wameshindwa ujue maji marefu hayo.
 
Heshima Mbele,

Mhe. Dr. Slaa anahitajika kukamatwa na Vyombo vya sheria hasa baada ya kuwa na Nyaraka ambazo ni siri za Serikali alizozipata kutoka wizara ya Mambo ya Ndani.Tunatambua ni kosa kisheria kwa Mtanzania yeyote kuwa na nyaraka za siri za serikali.

Nchi hii inaongozwa kisheria,na tumekuwa tukipigania hili siku zote .Kwa mtazamamo wangu Naona kuna haja ya Dr. Slaa kuhojiwa hata kukamtwa kwa kumiliki nyaraka za serikali!

Fikiria kabla ya kuleta kitu hapa JF. Badala ya kumshukuru unasema akamatwe?.

Anatupa habari za kweli ni jinsi gani serikali inavyofanya madudu na wewe unaleta ujinga wako hapa?.

Unafurahia kuona machafu yanayofanywa na viongozi mafisadi?, hivi unaelewa wametutia hasara kiasi gani na wametufikisha wapi hawa viongozi mafisadi?.

Bila Dr Slaa kumwaga ukweli kuhusu EPA hata hicho kidogo kilichorudishwa kisingerudi na huenda wizi ungekuwa bado unaendelea na wananchi walio wengi wanakufa njaa.

Dr Slaa ni shujaa kuna kila sababu ya kumpongeza.
 
- Kuna wakati waziri Marmo, aliwahi kumtishia Dr. Slaa, kuhusu kuwa kwake na nyaraka za siri za serikali, na DR. Slaa nakumbuka akamjibu wazi kwamba akitaka kusmhika anytime anakaribishwa na atamsaidia kumuelewasha anakozipata, ikawa kimyaa waziri hakujbiu tena.

- Mara ya mwisho nimewahi kusikia mwananchi akishukiwa na sheria kuhusu nyaraka za siri za serikali, ilikuwa ni Muandishi wa habari kwa jina Balinagwe, kule Songea, wakati wa Mwinyi, aliandika habari kwenye gazeti moja kuhusiana na serikali na RC wa huko, akaishia kufungwa miezi sita. Baada ya hapo next alikuwa Mzindakaya, na Mrema, lakini mmoja akapewa "mkopo" wa BOT na mwingine akapewa chochote kwenye dhahabu za airport yakaisha.

- Since then sijawahi kusikia tena, under Mkapa haikuwa rahisi kuzipata hizi siri I mean mnyonge mnyongeni, lakini kuanzia kipindi cha uchaguzi wa rais wa 2005, ndio tukaanza kuziona siri na nyaraka za kambi ya mtandao zikianza kupatikana kwa urahisi sana, na mpaka leo siri na nyaraka za serikali imekuwa ni sawa na kununua Nipashe tu mtaaani.

I mean Arafat na Mandela huenda walikua terrorist kwa US, lakini that was not the case na wananchi wao kama ilivyo kwa DR. Slaaa na sisi wananchi. Kama serikali ina tatizo na kuvuja kwa siri zake, basi ijiangalie kwenye kiooo itamuona mchawi wake. Serikali kumbuka inayo hiyo otpion kwenye table at anytime kumkamata Dr. Slaaa, lakini najua kua inaogopa kwamba Dr. Slaa atasema anakozipata na mstari utakwenda mbali sana na wanaohusika kumpa, tena wananchi watashangaa sana kujua exactly zinatokea wapi mpaka kufikia kwa DR. Slaaa, infact itakuwa aibu ya mwaka, huenda tunaongelea serikali nzima kuondoka!

- The principle hapa ni ile ile kama Msuya na Mwalimu, kwenye EPA like waziri toa millioni 25 za mkutano wa CCM Chimwanga, Msuya anatoa 50 nusu zingine hazijulikani zimekwenda wapi au wala kama zilichukuliwa, mpeni Dr. Slaaa siri fulani ili kumchafua adui flani wa mtandao, zinatolewa zaidi ya zinazotakiwa huwezi kusimamisha huo msululu, in the end tunakua a Banana Republic, ndio maana huwa tunamlamu sana Mkapa, kwa sababu ni urasi wake ndio ulioruhusu makundi ndani ya CCM, na ni makundi haya ndio chanzo cha kuvuja siri za serikali, kwa sababu kuchafuana kwa aina yake kulianzia kwenye uchaguzi wa rais 2005 na Mkapa naye akajiunga na kundi la Mtandao ambao ndio waliokuwa mabingwa wa kuchafua wengine, sasa ukipata utawala kwa kuchafua wengine haina maana kuwa unaacha, no! sasa mtaishia kuchafuana wenyewe kwa wenyewe maana hakuna wa kumchafua kule nje kwani through utawala unajifunza kua kumbe kwenye kutawala unawahitaji wale wengi mliohusika kuwachafua kwenye kampeni,

- Sasa je serikali ya sasa inaweza kuzuia kuvuja kwa habari zake za siri? No way kwa sababu inajua kuwa uchaguzi unakaribia na wanachojua ni one thing only, nacho ni kuchafua wengine ili kutawala maana it worked one time, sasa why not na the next time, popularity ikitaka kushuka tu basi achia nyeti za kiongozi flani maarufu ili wananchi watusahau sisi wengine, it is a Banana Republic na inakwenda miguuni mwa Mkapa ndio maana Masha haendi kokote pamoja na mengine mengi ya kumuokoa, zaidi ameokolewa na hii barua ambayo ipo karibu kila sehemu muhimu ya taifa na hasa penye elimu.

Mkulu wangu sana Gembe kwenye hili la kukamatwa kwa DR. Slaaa hatuko pamoja, ingawa naye DR. Slaaa anahitaji kua muangalifu sana maana one of this days watawala watampata kiongozi mwingine wa upinzani wa kuvujishia habari zao za kuchafuana, kwa sababu I do not care what DR.Slaaa anapata hizi habari toka kwa watawala wenyewe wanaotaka kuchafuana, ingawa wanaweza kua sio wao wanaompa directly mikononi mwake, ni mchezo wa hatari sana ingawa ni a big gain kwetu wananchi.

Thanxs!
 
Last edited by a moderator:
Serikali haiwezi kumshitaki Slaa kwa sababu itakuwa imempa uwanja mzuri wa kui challenge.

Halafu kama alivyosema FMES hapo juu, Slaa alishatoa challenge akamatwe, akataja mpaka vifungu vimavyomlinda kwa logic ya kwamba serikali ikifanya makosa (e.g ufisadi) hata anayekuja kuwa na nyaraka za siri za serikali zinazofichua ufisadi wa serikali anakuwa hana kosa la kuwa na nyaraka za siri za serikali. Ufisadi wa serikali una invalidate uharamu wa kuwa na nyaraka hizo.
 
Mkuu Field Marshall Es,
Shukran mkuu, ama kweli nchi yetu imekwisha kwenda na maji, wadosi wanasema Kushne Karungi..Ndio maana mimi nasimama na kile kinachowezekana kwangu na sisi kukifanya badala ya kuitazama sheria na Katiba butu na mbovu kwa kila jambo wakati haitusaidii kitu kabisa..
Kama Dr. Slaa amevunja sheria, watayajua wao na pengine atakuja waomba samahani huko bungeni au kortini lakini kwangu mimi this guy is my hero!...Kama Mandela mkuu wangu, huyu jamaa ni kiongozi tosha kabisa..

Hii mipango ya siasa na vita ya kisiasa haiwezi kutusaidia kitu kabisa na hakika sipendelei kabisa sisi wana JF kujihusisha na siasa zinazoturudisha nyuma kimawazo..
Tupo vitani sasa hivi na adui yetu ni MAFISADI ambao wanaweza tumia kila hila kutukwaza...Yalimkuta Zitto akaitwa analidanganya Bunge na akafungiwa lakini cha ajabu ukweli ulipobainika huyo Karamagi aliyeonekana mkweli siku ya kwanza imeonyesha wazi yeye ndiye alilidanganya Bunge.. Sijasikia kufungiwa kwake wakati huyu mtu alikataa madai yote ndani ya kiapo, sii mara moja wala mbili na leo hii anapeta ndani ya katiba hiyo hiyo iliyomfungia Zitto..
Kama huu sii ujinga kitu gani jamani twambieni!
 
Invisible,

Naomba ufunge huu mjadala.Nimejifunza jambo moja jingine jipya sana kuhusiana na wapinzani wa Tanzania(silitaji kwa sasa).

Naungana na maneno ya Pinda na Jk kuwa kamwe wapinzani hawatatawala nchi hii,zaidi ya kuisadiaia CCM pindi inapokosea
 
Invisible,

Naomba ufunge huu mjadala.Nimejifunza jambo moja jingine jipya sana kuhusiana na wapinzani wa Tanzania(silitaji kwa sasa).

Kwa nini mjadala ufungwe ? Ulitegemea nini ulipoleta hoja - kuungwa mkono ? Umejifunza lipi jipya - kuwa wote wasiokubaliana na wewe ni wapinzani ? Heri umeamua kutolitaja - hapa tunamkoma nyani bila kumtazama sura.

Naungana na maneno ya Pinda na Jk kuwa kamwe wapinzani hawatatawala nchi hii,zaidi ya kuisadiaia CCM pindi inapokosea

Toka lini umetofautiana na Pinda au Jk ? Kama na wewe unaamini CCM itatawala milele - hauko peke yako. Mafisadi wote lazima wawe na imani kama hiyo - si CCM inawapa hifadhi ? Nje ya CCM watakuwa na usalama gani - kama si yale ya samaki kuvinjari nchi kavu. Kwamba wapinzani hawatatawala nchi hii - nakupa pole ndugu yangu.
 
Gembe anatakiwa kukamatwa na vyombo vya sheria hasa baada ya kuweka wazi kuwa nyaraka ambazo Dr Slaa anazo ni siri za Serikali alizozipata kutoka wizara ya Mambo ya Ndani.Tunatambua ni kosa kisheria kwa Mtanzania yeyote kuwa na nyaraka za siri za serikali.

Kwa kuwa Gembe amezitambua nyaraka hizo kuwa ni za serikali, hivyo anathibitisha kwamba anazo na ameshtushwa baada ya kugundua kuwa alizozitaja Dr Slaa ndio hizo hizo za wizara ya Mambo ya Ndani !!

Naendelea kuhoji Gembe alizitambuaje kuwa hizo alizonazo Slaa ni za siri?
 
Invisible,

Naomba ufunge huu mjadala.Nimejifunza jambo moja jingine jipya sana kuhusiana na wapinzani wa Tanzania(silitaji kwa sasa).

Naungana na maneno ya Pinda na Jk kuwa kamwe wapinzani hawatatawala nchi hii,zaidi ya kuisadiaia CCM pindi inapokosea

Gembe's brain = Tambwe Hiza's brain
 
Naungana na maneno ya Pinda na Jk kuwa kamwe wapinzani hawatatawala nchi hii,zaidi ya kuisadiaia CCM pindi inapokosea

Kauli zingine bana zinaudhi sana.
Mbona hata Mabutu alijua atatawala milele yupo wapi?
Kila lililo na mwanzo halikosi kuwa na mwisho.Siku zenu zinahesabika msije mkaficha nyuso zenu chini ya mchanga kama mbuni.
 
Back
Top Bottom