Dr. Slaa Akamatwe, ahojiwe na ikiwezekana achukuliwe hatua

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Heshima Mbele,

Mhe. Dr. Slaa anahitajika kukamatwa na Vyombo vya sheria hasa baada ya kuwa na Nyaraka ambazo ni siri za Serikali alizozipata kutoka wizara ya Mambo ya Ndani.Tunatambua ni kosa kisheria kwa Mtanzania yeyote kuwa na nyaraka za siri za serikali.

Nchi hii inaongozwa kisheria,na tumekuwa tukipigania hili siku zote .Kwa mtazamamo wangu Naona kuna haja ya Dr. Slaa kuhojiwa hata kukamtwa kwa kumiliki nyaraka za serikali!
 
Last edited:
Kama zinazoitwa "SIRI" zinakuwa na madudu kiasi hiki...Then,there is an immediate need to overhaul our system.
Kama sheria zinasaidia kufunika "maovu" na tukazidi kuzikumbatia blindly(no offence) then its likely that 'we' are retarded!!
 
Mkuu Gembe,

Tungependa sana hii nchi iongozwe kwa sheria lakini tunajua hiyo bado ni ndoto na wahusika wanajua ndio maana Dr. Slaa hajakamatwa kama ambavyo ungependa. Kama tungekuwa tunaongozwa kwa sheria ufisadi ungeshaelekea kuwa sehemu ya historia lakini ndio kwanza...
 
Heshima Mbele,

Mhe. Dr. Slaa nahitaji kukamtwa na Vyombo vya sheria has baada ya kuwa na Nyaraka ambazo ni siri za Serikali alizozipata kutoka wizara ya Mambo ya Ndani.Tunatambua ni kosa kisheria kwa Mtanzania yeyote kuwa na nyaraka za siri za serikali.

Nchi hii inaongozwa kisheria,na tumekuwa tukipigani hili siku zote .Kwa mtazamamo wangu Naona kuna haja ya Dr. Slaa kuhojiwa hata kukamtwa kwa kumiliki nyaraka za serikali!

Mzee mbona ile picha ya handsome boy umeiondoa? Ingekuwepo ile picha na mawazo yako uliyoyatoa ungewakaba sana watu hapa we ujui tu. Hata hivyo siyo mbaya sana tumeanza kuona matunda ya masters yako, Dr Slaa si ni mwajiriwa wa mambo ya ndani lazima akamatwe.
 
Mbona wamechelewa? Mimi nakuunga mkono wa mkamate mapema iwezekanavyo na wamfikishe Kisutu! Siyo kwa hilo tu ulilopendekeza lakini kwa mengine:

a. Kwa kuwataja watu mbalimbali kuhusika na ufisadi na kuwachafulia majina yao katika ile orodha ya ufisadi.

b. Kwa kukubali kupewa nyaraka mbalimbali za "siri" na kuzitumia nyaraka hizo kuibua madai mazito ya ufisadi ambayo yamesababisha watu kadhaa wamtangulie Kisutu.

Hili ndiyo litakuwa funzo kwa Mtanzania yeyote kupokea nyaraka za siri. Siyo yeye tu bali pia itakuwa somo kwa mitandao kama JF kutumika kuweka nyaraka za namna hiyo na watu kuzipata kwa urahisi.

POLISI MKAMATENI DR. SLAA SASA KAMA MHE. GEMBE ANAVYOPENDEKEZA! NAUNGA MKONO HOJA!
 
Hivi siri za serikali ni zipi hasa? huo uozo?!hivi ufisadi wa waziri ukiwa communicated kwenye karatasi zenye nembo ya serikari basi ni siri za serikali? Hii ni hatari kweli. mnanikumbusha ya Mwaibabile(RIP) na Banduka kule Songea
 
Kama zinazoitwa "SIRI" zinakuwa na madudu kiasi hiki...Then,there is an immediate need to overhaul our system.
Kama sheria zinasaidia kufunika "maovu" na tukazidi kuzikumbatia blindly(no offence) then its likely that 'we' are retarded!!

You mean Mataahira kwa kiswahili?

U rock:confused:
 
Nyaraka za siri za sirikali ni zipi hizo?
Huu wizi wizi na ujanja ujanja wanao ufanya ndo nyaraka za siri?
Mkuu sijakwelewa bado Dr.Slaa anakufumbua macho hata wewe ambaye hujui nyaraka za siri na mafamba.Dili chafu viongozi wako wanazo cheza kwa taarifa yako sio siri Dr. zote anazo kama unafikiri ni siri hiyo sahau ndo maana hata UWT wanashindwa kumbana watabania wapi wkt ishu zenyewe ni kimagumashi magumashi viongozi wako wanazicheza.Ndo kwaanza usikute ndo anaepelekewa azilipue.
Ishu ya Mwembe Yanga viongozi wako wangapi waliapa kumfikisha Dr.mbele ya vyombo vya sheria na wameishia wapi wakumbushe basi waende mahakamani wakapambane na Dr.
 
Mbona wamechelewa? Mimi nakuunga mkono wa mkamate mapema iwezekanavyo na wamfikishe Kisutu! Siyo kwa hilo tu ulilopendekeza lakini kwa mengine:

a. Kwa kuwataja watu mbalimbali kuhusika na ufisadi na kuwachafulia majina yao katika ile orodha ya ufisadi.

b. Kwa kukubali kupewa nyaraka mbalimbali za "siri" na kuzitumia nyaraka hizo kuibua madai mazito ya ufisadi ambayo yamesababisha watu kadhaa wamtangulie Kisutu.

Hili ndiyo litakuwa funzo kwa Mtanzania yeyote kupokea nyaraka za siri. Siyo yeye tu bali pia itakuwa somo kwa mitandao kama JF kutumika kuweka nyaraka za namna hiyo na watu kuzipata kwa urahisi.

POLISI MKAMATENI DR. SLAA SASA KAMA MHE. GEMBE ANAVYOPENDEKEZA! NAUNGA MKONO HOJA!

Tatizo siyo kupokea Nyaraka za Siri kama unavyopendekeza Hapo,Ni yeye kumiliki Nyaraka za Siri za serikali.Sheria Zipo na lazima zifuatwe!

Tunataka Utawala wa Kisheria,Kwanini hatuoni hili linahitaji kupewa kipaumbele?
 
Mzee mbona ile picha ya handsome boy umeiondoa? Ingekuwepo ile picha na mawazo yako uliyoyatoa ungewakaba sana watu hapa we ujui tu. Hata hivyo siyo mbaya sana tumeanza kuona matunda ya masters yako, Dr Slaa si ni mwajiriwa wa mambo ya ndani lazima akamatwe.

Mkuu shalom,

Mbona unafanya Personal Atack?Masters yangu inakukera eeh?..tukate ishu,au mkuki kwa nguruwe?wenye kupenda kusifiwa kila siku?
 
Mheshimiwa Gembe hapo ndo huwa nachoka kabisa...unajua hujuma nyingi dhidi ya umma kutoka kwa watawala zimefanywa kupitia hii strategy iliyopitwa na wakati na isiyo na tija kabisa ya kufanya kazi ambazo wala hazihitaji usiri kuwa ni siri za wateule wachache kuzifahamu.
Serikali ni watu...nionavyo mimi, kama Slaa anekutwa anagawa document zenye kuhusu mfumo wa kijeshi au ghala za silaha za nchi etc angekuwa ana maswali ya kujibu. Kwanini mnajidanganya kuwa mnawatumikia watu at the same time mnatumia dhana ya usiri kunufaisha wachache? Usiri huo huo umezaa IPTL,EPA, umezaa Richmond na matakataka mengine mengi katika nchi yetu.
Mindset zetu sasa zibadilike....tutakuwa tunajidanganya sana kama mtindo huu utaendela bila kutuletea madhara ati kwa sababu tuko na vyombo makini vya ulinzi na usalama. Sidhani kama TZ ya leo ina nguvu zaidi ya USSR na eastern block countries zilizo sambaratika in 90's. Sababu kubwa ya kusambaratika ni kuwa watawala waliwasahau watu, wakajitwalia namna ya umungu...wakatishia kila aliyetamka neno wasilolipenda.Matatizo yakawafundisha watu kuwa wakaidi maana walikata tamaa na maisha.Mwisho wa yote hawakulinda tena maslahi ya watawala..wakajitosha kupambana nao, na mfano mzuri ulikuwa Romania na Poland.
Tusilazimishe kufika huko kwa kuandaa mazingira ya watu wachache kuwaibia waliowengi, kwa kigezo cha siri. Mtindo wa kulinda uozo kwa kigezo kuwa ni siri za serikali ukome kabisa kama tunataka tufike tunakotaka kwenda mana watu wanakata tamaa taratibu.Deal zimefanyika za kutosha, tuweke mbele uzalendo sasa...watu wanaelimika...wataendelea kuuliza maswali tu bila kukoma.
Mungu Ibariki Tanzania
 
Gembe hebu tuambie hizo siri za serikali alizonazo Slaa
 
Mbona wamechelewa? Mimi nakuunga mkono wa mkamate mapema iwezekanavyo na wamfikishe Kisutu! Siyo kwa hilo tu ulilopendekeza lakini kwa mengine:

a. Kwa kuwataja watu mbalimbali kuhusika na ufisadi na kuwachafulia majina yao katika ile orodha ya ufisadi.

b. Kwa kukubali kupewa nyaraka mbalimbali za "siri" na kuzitumia nyaraka hizo kuibua madai mazito ya ufisadi ambayo yamesababisha watu kadhaa wamtangulie Kisutu.

Hili ndiyo litakuwa funzo kwa Mtanzania yeyote kupokea nyaraka za siri. Siyo yeye tu bali pia itakuwa somo kwa mitandao kama JF kutumika kuweka nyaraka za namna hiyo na watu kuzipata kwa urahisi.

POLISI MKAMATENI DR. SLAA SASA KAMA MHE. GEMBE ANAVYOPENDEKEZA! NAUNGA MKONO HOJA!

Bwahahahaha, Mwanakijiji Bwana, nakuzimia kwa style yako ya uandishi.
Mi nadhani hata kesi zilizo mahakamani za ufisadi zifutwe kwa sababu zimetokana na nyaraka za siri.
Huu ujinga wa kila kitu kuitwa siri nadhani ni wakati mwafaka kuanza kuipiga vita. Sivyo nchi yetu itauzwa pamoja na mimi na Gembe kwa kigezo cha mkataba wa siri. Na mwisho kila mtanzania akiuliza ataulizwa ulipata wapi hiyo siri? na hatimaye wote tutaishia jela.
 
Gembe hebu tuambie hizo siri za serikali alizonazo Slaa

Huyu Gembe ukijaribu kuangalia ni wale wale yupo against sana kumkoma nyani usoni.....hayo madudu yanayo ibuliwa yeye anaona ni siri haya twendelee.
 
Huyu Gembe ukijaribu kuangalia ni wale wale yupo against sana kumkoma nyani usoni.....hayo madudu yanayo ibuliwa yeye anaona ni siri haya twendelee.

Hapana. Gembe ana haki ya kutoa maoni yake kama anavyoona sheria zinasema.
Sheria zinasema hivyo. Lakini swali nikwamba je sheria zinasemaje ukifichua mpango wa siri wa uhalifu? Je na hilo ni kosa kwa sababu umetoa siri kwa kitu kilichokuwa ni high confidential?
Kwa mfano kuna siri ya kuipindua nchi, je hata kama waraka umeandikwa ni siri nisitoe taarifa?
Na ningependa kumuuliza Gembe tena je ni kweli Dr Slaa anamiliki nyaraka za sirikwa nia gani mbaya?
 
Mie niko ukurasa mmoja wa kumkoma Nyani,ila siku zote sitaki kuw amtumwa wa kumtetea Flani sababu yeye amekuwa ni mtu wa kutetea maslahi ya watanzania wakati kuna mengine anakosea.

Kwa hili siungi Mkono,na natambua kwa dhati jitihada za Dr. Slaa..!Ila akivunja Sheria sitakuwa naye karibu hata kidogo!
 
Heshima Mbele,

Mhe. Dr. Slaa anahitajika kukamatwa na Vyombo vya sheria hasa baada ya kuwa na Nyaraka ambazo ni siri za Serikali alizozipata kutoka wizara ya Mambo ya Ndani.Tunatambua ni kosa kisheria kwa Mtanzania yeyote kuwa na nyaraka za siri za serikali.

Nchi hii inaongozwa kisheria,na tumekuwa tukipigania hili siku zote .Kwa mtazamamo wangu Naona kuna haja ya Dr. Slaa kuhojiwa hata kukamtwa kwa kumiliki nyaraka za serikali!

huwezi kumkatama mkaratu kwa hili kwakuwa alilileta bungeni ambapo hanayo kinga ya kibunge na sio kama angewakilisha hadharani kwenye jukwa kama mwembe yanga hivi, na hili akafikishwe kwenye vyombo vya sheria inabidi idhirishwe wazi na bunge kwamba alikiuka taratibu za bunge,mzee wetu sitta hapangue kinga hiyo,halafu ndio sheria zifwate mkondo wake

ingekuwa tatizo kubwa kwake kama angepeleka nyaraka kwenye magazeti ambazo zina nembo ya '' SIRI SANA'' kama alivyofanya mtoa habari mmoja kwenye Rai la wiki iliyopita,sasa huyo ndio wakushitakiwa,
mhe gembe naomba kuwakilisha hili kukusahihisha
 
Emancipate yourselves from mental slavery;
None but ourselves can free our mind.........
maneno haya aliyasema Bob Marley zamani sana,
leo tumeshindwa kujikwamua kutoka katika utumwa wa fikra,
manabii wachache kama dk. slaa anajitoa mhanga, anafanya kazi kwa maslahi ya sisi wengi tulio wanyonge, leo ndugu yangu unataka apandishwe kizimbani......
gembe, je wewe ni kipi ambacho umekifanya kwa maslahi ya wanyonge wengi wa taifa hili??
kwa nini huna roho ya kizalendo hadi unaona kuwa alichofanya slaa ni udhalimu??
Tanzania haiwezi kamwe kuendelea ikiwa na watu wenye roho mbaya zinazoendana kinyume na matakwa ya wengi.
Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,
Kupingana na sauti ya wengi ni kupingana na Mumgu.
 
Vyama vyetu vya UPINZANI vimeshindwa kuisimamia Serikali ya CCM; Vyombo vyetu vya habari havina waandishi wa habari za UCHUNGUZI; BUNGE letu ndio hilo, kazi yao kupiga za ndio hata pale DHAMIRA zao zinapowasuta; Mahakama zetu haki ni BIDHAA kama zilivyo nyanya sokoni; Watanzania tulio wengi tumelala, hatujui Nchi yetu inatafunwaje; ni lazima tutoe wito kama huu wa Dr Slaa akamatwe.
Anaonekana wa ajabu, mkorofi,...
 
Nimeifurahia hii.

Chanzo cha Mihimili mitatu ya dola kuingiliana.....Wananchi nao,...Dr Slaa nk hawana namna.
 
Back
Top Bottom