Dr.Slaa ajibu hoja mbalimbali na kueleza Sera za CHADEMA hapa JF

Dk W Slaa naomba utuwekee Muswada wa Baraza la Usalama wa Taifa ili tujue abc zake! Pia mshaurini Spika aweke Miswada na Acts mapema kwenye Parliamentary Website kama wanavyofanya kwa upande wa Order Papers na Hansards! Please, help us, thanks in advance!
Buchanan,
This is a genuine request. Niliko kwa bahati mbaya sina access kwa scanner. Kesho nitaangalia katika ofisi za Bunge inaweza kupatikana Scanner. Tutawaambia wahusike wawe wepesi wa kuweka miswada kwenye website. Am very sorry, there cannot be an informed debate bila kupata information sahihi. Very sorry.
 
Dr Slaa,mie sina swali bali nina maombi/ushauri

Kwanza,kwa vile jitihada zenu za kuwafichua mafisadi zimekuwa zikikazwa na taasisi kama TAKUKURU,DPP,nk ushauri wangu kwenu ni kuhamasisha wanasheria/taasisi za kisheria (na mna mwanasheria mahiri Ndg Lissu) kufungua kesi dhidi ya watuhumiwa.Japo mie si mwanasheria lakini nadhani upo uwezekano wa kisheria wa kufanya hivyo.Vinginevyo,kazi nzuri mnayoifanya itaishia kuwa kazi nzuri tu pasipo matunda yanayokusudiwa.Na wazo la kutarajia hukumu ya wapiga kura (japo natambua kuwa the court of public opinion is more puwerful than "the usual court") lakini kwa vile idadi ya wapiga kura wengi ni maskini,ni rahisi kwao kununuliwa kwa tsheti,kilo za mchele na sukari,na trkima kama hizo na kusahau "hukumu" wanayopaswa kutoa kwa mafisadi.

Pili,nashauri mhamasishe recruitment drive ya wanachama nje ya Tanzania kama ilivyo ndani ya nchi yetu.Kuna umuhimu wa the likes of operesheni Sangara kutanuliwa hadi nje ya mipaka ya nchi.Correct me if I'm wrong,like kwa takriban muongo mzima niliokaa hapa Uingereza sijawahi kusikia kiongozi wa Chadema amekuja na kufanya maongezi na Watanzania.CCM wanafungua matawi yao hadi huku (sana sana kwa wanaotarajia kuingia kwenye mfumo fisadi),CUF pia walikuwa active sana siku za nyuma (pengine kutokana na idadi ya kutosha ya Wazanzibari waliokuja hapa kama "wakimbizi").It's high time kwa Chadema kuangalia umuhimu wa ku-consolidate support nje ya mipaka ya nchi kama ilivyo kwa ndani ya mipaka.

Ni hayo tu.
Mlalahoi,
Concerns zako kuhusu ufunguzi wa Matawi Nje tumeipokea. Thanks a lot.
 
Mheshimiwa Slaa naomba kutofautiana nawe hapa. Suala la shughuli za kimaendeleo sio suala la kusubiri kushinda uchaguzi tu. Hata chama kisichokua na uwezo wa kukusanya kodi kinaweza kuwa na mikakati ya kuanzisha, kutekeleza na hata kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo. Ama iwe ni ile ya kuanzishwa na wananchi wenyewe, ama inayoanzishwa na serikali ili madarakani ama itakayoanzishwa na wanachama wa vyama hivi ama chama chenyewe.

Tatizo linakuja pale vyama vinapochukulia FEDHA kuwa msingi mkuu wa maendeleo hivyo kupima uzito wa jukumu hilo kwa mizania ya uwezo wa kifedha. Kuna miradi mingi ya maendeleo ambayo inaweza kutekelezeka kwa kiasi kidogo cha fedha ambacho mnaweza kuchangishana wanachama ama hata vongozi tu wa chama na kushirikiana na wananchi kutekeleza miradi hiyo haswa ile inayoweza kutatua changamoto ndogondogo zinazowakumba wananchi katika maeneo yao.

Hili ni muhimu kwa chama chochote kuweza kujenga imani ya kuwa ni mbadala makini machoni mwa watanzania. Lakini pia ni nafasi muhimu ya wanachama wenu kujijengea uwezo wa kuongoza miradi ya maendeleo kama matayarisho ya kuingia madarakani.

Mheshimiwa Slaa kutolea mfano kauli mbiu ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA kama moja ya ahadi zisizoweza kutekelezeka sidhani kama unakuwa sawa. Ina maana kwako wewe ama kwa chama chako hamuamini kuwa MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA yanawezekana? Kwa upande wangu nadhani kuwa ahadi hiyo sio kuwa ni ahadi isiyoweza kutekelezeka bali ni ahadi inayohitaji maandalizi makini yenye kuhakikisha kujenga taifa na uongozi wenye nidhamu na unaojali ufanisi na kuweka mbele maslahi ya watu, yaani watanzania.

Tatizo linakuja pale ambapo ahadi hizo zinatolewa wakati kunakosekana niathabiti ya kujenga mazingira muhimu ya utekelezji wake. Kwa utawala huu naamini ahadi hiyo imeshindwa kutekelezeka kutokana na mazingira hasi yaliyojengwa na wagombea na makundi yao ndani ya chama tawala wakati wa kinyang'anyiro cha uteuzi wa ndani wa Urais na Ubunge. Harakati zile na hali ya ndani ya chama tawala, imelazimisha serikali iliyopaswa kutekeleza ahadi hiyo kutumia muda mwingi hivi sasa kushughulikia masuala mengi yasiyotowa tija katika juhudi za kujenga maisha bora kwa kila mtanzania.

Makosa yaliyofanyika na yanayoendela kufanyika ili kupata/kulinda hadhi ya Chama Tawala na uhodhi wa MADARAKA YA SERIKALI ndio yamekuwa kikwazo cha kutekeleza ahadi ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA na sio kuwa hiyo ni ahadi isiyotekelezeka.

Naamini mkiliangalia suala hilo kwa mtazamo huo na mkawa tayari kujisahihisha nanyi hamtaendelea kuiga makosa waliyoyafanya na wanayoendelea kuyafanya wapinzani wenu katika harakati zenu za kuchukua madaraka, hasa katika suala la DEMOKRASIA NA UWAJIBIKAJI..Na hata mkaweza kutekeleza ahadi ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ambayo wenzenu wanaelekea kushindwa kuitekeleza.

omarilyas
Omarilyas,
Nadhani tumetofautiana katika approach. We seem to be saying the same thing. That is exactly what I meant. Nakubaliana na ushauri wa kujifunza kutoka kwa makosa ya wenzetu. We dont have to "re-invent the wheel".
 
Dr. Slaa issue ya mabadiliko ya katiba, tume ya uchaguzi na serikali ya umoja wa kitaifa CHADEMA ina msimamo gani? mmefikia wapi kudai hayo mambo na je kuna tumaini lolote, what about timeline??just imagine mnapata kura 50% ya urais mnafikiri ni vyema kupoteza nafasi ya angalau hata ya kuwa na wizara 5!!
Waberoya,

Tunaendelea na tutaendelea kudai, Katiba mpya, japo Serikali haitaki kusikia Kabisa jambo hilo. Lakini pia tubaki kulalamika kusubiri Katiba mpya ipatikane. Wakiendelea kukataa, tunaendelea na maandalizi ya kushinda na Katiba hiyo hiyo Mbaya. Serikali ya Mseto ni ngumu hadi Katiba mpya itakapopatikana.

Tuelimishe Watanzania tupate katika uchaguzi Mkuu, 2010 wapatikane Wabunge wengi, significant enough if not to win outright, to be able to effect major changes. Tusitegemee major changes iwapo Watanzania bado wataendelea na msemo wa " Zimwi likujualo....". We need change of attitude, na kutumia nguvu ya umma kupitia Sanduku la Kura. Ndiyo njia pekee.

Hatua nyingine zote zinafia kwenye Ukumbi wa Bunge, au na kwenye Caucus ya Wabunge wa CCM. Kuna Hoja hazifiki hata kwenye ukumbi (iwapo haina maslahi kwao au inawaumiza kwa namna mmoja au nyingine).

Nakubali inauma unapopata kura nyingi za kutosha, na kura hizo zote kwa system ya " First Past the Post" zinaachwa kupotea bure.

Mfumo mzuri katika hali hiyo ingelikuwa full Proportional Representation (Tanzania tunatumia partial- kwa upande wa viti maalum-Wanawake).
 
asante sana kwanza kwa kuchukua mda wako Mh W.Slaa. Swali langu moja ambalo linanisumbua akili kwani najua bila upinzani kuungana ni sawa sawa na kutwanga maji kwenye kinu inavyofika kwenye uchaguzi.Utengano wa upinzani anaye faidi sana ni CCM.

Swali langu je kuna mpango wowote wa kujaribu kuunganisha vyama upinzani vyote hili mueze kushindana na ccm kwa nguvu zaidi? Kama mkiweza kuungana nadhani itasaidia sana kuwezakupata wabunge wengi zaidi na ndio hapo watanzania nasi tutapata moyo zaidi kwenu kwani tutawaona jinsi gani mnavyo tetea maslahi ya nchi.

Utengano wa upinzani unatukatisha tamaa tunaona kama kila mtu anaangalia zaidi maslahi yake binafsi kuliko ya nchi yetu,kama wote mnaitakia mema nchi yetu na mna nia safi ya uongozi bora kwanini mnashindwa kuungana?

kuna juhudi zozote chama chako kinafanya kuweza hili kufanyika? kama wabunge wachache wa upinzani wanaweza kusumbua akili ccm inamaanisha mkiongeza nguvu pamoja basi nchi yetu itapata mabadiriko makubwa sana.
 
Buchanan,
This is a genuine request. Niliko kwa bahati mbaya sina access kwa scanner. Kesho nitaangalia katika ofisi za Bunge inaweza kupatikana Scanner. Tutawaambia wahusike wawe wepesi wa kuweka miswada kwenye website. Am very sorry, there cannot be an informed debate bila kupata information sahihi. Very sorry.

Nashukuru sana kwa kuona umuhimu wa kutuletea Muswada huo Muhimu! Pia kuna zile Sheria zaidi ya 10, mojawapo CPA, Cap. 20 zilizofanyiwa marekebisho tunaomba utuwekee! Hapa JF watu wengi wako concerned mno na kinachoendelea Bungeni na inasikitisha kwamba tunapata "vipande" vya Miswada kupitia magazeti ambayo mara nyingi hayaendi kwenye detail zaidi na mara nyingine yana-misquote vifungu husika! Narudia tena kuomba ufikishe ujumbe kwa Mh Spika Sita ili tovuti ya Bunge iwe updated! Thanks once again for your promise to help, I sincerely appreciate!
 
Waberoya,

Tunaendelea na tutaendelea kudai, Katiba mpya, japo Serikali haitaki kusikia Kabisa jambo hilo. Lakini pia tubaki kulalamika kusubiri Katiba mpya ipatikane. Wakiendelea kukataa, tunaendelea na maandalizi ya kushinda na Katiba hiyo hiyo Mbaya.

Dr. Slaa, huoni kuwa kwa kukubali kinadharia kuwa hata kama CCM haitabadilisha Katiba mko tayari kujaribu kushinda kwa kutumia "Katiba Mbaya" mnaondoa kabisa umaana wa Katiba Mbaya? Kama Katiba ni mbaya na haitengenezi mazingira huru na ya usawa kushindana unaweza vipi kushiriki kushindana? Kwa kukubali kushindana kwa kutumia katiba mbaya si kwamba mnaikubali kwamba katiba hiyo mbaya inaweza kutumika kushinda kitu ambacho kimsingi mnakubali ni KATIBU NZURI?

We need change of attitude, na kutumia nguvu ya umma kupitia Sanduku la Kura. Ndiyo njia pekee.

Hivi hii ndiyo imani kwamba njia pekee ya kusababisha mabadiliko ni kutumia sanduku la kura tu? Je hiyo ndiyo njia pekee ya kisiasa ya kulazimisha watawala kubadili mfumo wa utawala wao?

Karibu nchi zote duniani ambazo ziliamua kulazimisha mabadiliko makubwa ya kisiasa zimetumia muunganiko wa njia mbalimbali ambazo kilele chake ni kufanyika kwa uchaguzi huru zaidi na wa haki zaidi. Miongoni mwa njia hizo ni pamoja na maandamano, migomo, civil disobedience (kama kukaa chini mbele majengo ya serikali) n.k

Kwanini Chadema hadi leo hii haijafikiri, kujaribu, wala kutumia njia za kulazimisha serikali na chama tawala kuja kwenye mazungumzo. Hamuoni kuwa Zanzibar wameamka zaidi katika kutumia njia mbalimbali kiasi cha kulazimisha serikali ya mseto sasa?

Kweli kwa kuendelea kujenga hoja kwenye mikutano ya hadhara, na vyombo vya habari tunaweza kweli kuwashawishi CCM waone uzuri wa hoja hizi na hatimaye kutokana na hisani na uungwana wao wakubali kubadilisha mfumo unaowalisha?

Kwanini Chadema isifanye vigumu sana kwa CCM kutawala wapendavyo kwa kutumia njia nyingine za kidemokrasia za kulazimisha kama migomo, maandamano, n.k Yawezekana kwamba uongozi wa Chadema hauko tayari kulala rumande na kutiwa pingu kwa kusababisha vurugu? Yawezekana wengi wao wanaogopa kwenda kukaa mbali na familia zao na kumwagiwa maji ya kuwashwa?

labda kama mkiwapa wananchi uongozi wa kupinga ufisadi kwa maandamano na migomo, kudai Katiba mpya kwa kugomea vikao vya Bunge na hata kufanya sitins, kukataa hoja za serikali kwa kutoka kwenye vikao vya bunge in protest (CUF wamefanya hivyo) na hata ikibidi kugoma kuitambua serikali iliyopo; labda wananchi watabadili fikra zao..na kupata matumaini ya kuchagua wapinzani wengi zaidi?
 
Dr. Slaa,

Ni nini maana halisi ya "demokrasia" ndani ya Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) pale ambapo tumekiona chama hicho pamoja na shinikizo lako wewe mwenyewe kumkatalia mwanachama mahiri asithubutu kugombea uenyekiti wa Taifa wa chama kinyume cha nia na matakwa yake? Kama hatua hii ambayo ni ya msingi ki demokrasia inanyongwa kwa nguvu zote vipi chama hiki kijigambe kuwa kinaheshimu demokrasia na vipi kitailinda demokrasia kama kikibahatika kuongoza nchi? Tueleza tafadhali na usibabaishe.
 
Generation-Y,

1) Ni kweli mengi uliyosema, nakubaliana nayo. Lakini, nadhani tukubaliane kuwa kwa wale walioenda vijijini kabla ya 2004 na wale wanoenda leo mabadiliko ni makubwa sana na ninatoa mfano:-

a) Inawezekana wengi wanaandika hapa hawajui mapambano tuliyonayo kama wapinzani. Tulipoanza awamu ya pili ya mzunguko wa vijijini (Mzee Mtei na Timu yake walifanya awamu ya kwanza na wakati ule msukumo ulikuwa zaidi katika kupata wanachama 200 kwa kila mkoa na baadaye kuanzisha matawi. Zoezi hilo kwa bahati mbaya halikuendelea hadi 2004).

CCM ilipogundua kuwa sasa tuko makini na tunaenda vijijini ambako ndio nguzo zao, kila mbinu ya kutuhujumu ilifanyika. Guest hatukupokelewa( nakumbuka Kilwa tulilala kwenye nyumba ambayo haijaezekwa), chakula hatukuweza kupatiwa kwenye hoteli na migahawa tukawajibika kutembea na vyakula vyetu kwenye magari. Ilikuwa kipindi kigumu sana. Wananchi nao walikuwa wanatishiwa sana na hawakuwa wakijitokeza kwenye mikutano ( mfano extreme ni Mufindi ambapo jioni tuliingia wananchi wakatushangilia. Asubuhi tulipoamka kila nyumba imetundikwa bendera mpya ya ccm-mtindo wa zile zinazowekwa kwa mabalozi wao). Tulipoweka uwanjani Sound system na kuweka muziki hata watoto hawakutokea. Tukaamua kujihutubia wenyewe (tulikuwa na msafara wa watu kama 30), ndipo kwa nguvu za Spika tulizokuwa nazo tukawahutubia manyumbani mwao na kuwaondoa hofu. Saa 12 jioni uwanja ukafurika na kuishia kugawa kadi za Chadema kwa wanachama wapya zaidi ya 1,500 kazi iliyoendelea hadi saa 5 usiku. Hivyo, niliweka mkazo kwenye uhuru wa habari na uhuru wa wananchi kwa kuwa wengi inawezekana hawafahamu kabisa vikwazo tulivyokumbana navyo. Unafika jukwaani, hata VEO au WEO tu anakuwa na ujasiri wa kuja kukushusha Jukwaani. Hali hii pole pole imeondoka. Nakumbuka Chunya tulizuiwa kufanya mkutano kwa kisingizio cha mwenyekiti wa Halmashauri kuwa na mkutano wa maendeleo siku hiyo( ulitangazwa usiku kama mbinu ya kuzuia wa kwetu). Tulifika mahali tukamwambia DC na OCD wake watupeleke kwenye Cello(Lupango) yao ndipo tukiona siyo hadhi yetu tutaacha kufanya mkutano. Wakadhani utani wakatupeleka kweli. Tulipopaona tukawaambia mkutano utafanyika na wakitaka watupeleke lupango kwani ni size yetu ndipo wakaogopa kutushusha jukwaani.

Hivyo, kazi kubwa ilikuwa kujenga imani kwa wananchi lakini pia kwa viongozi mbalimbali waliojigeuza kuwa makada kwelikweli wa ccm kuwa na sisi tumesajiliwa kama CCM na hivyo tuna hadhi sawa. Kwa mtu ambaye hajapitia haya, ni vigumu kuelewa hatua tuliyopiga katika eneo hilo, hatua ambayo ilikuwa muhimu kabla hujafanya lolote. Demokrasia mliyokuwa mnasikia ilikuwa zaidi ya vitabuni, na wote mnajua Agustino Lyatonga alivyokuwa anapiga mabomu misafara ya Upinzani, alikuja kugundua ubaya wake baada ya yeye mwenyewe kujikuta upinzani.

b) Ziara nilizoeleza katika a) zilifanya kazi ya kuelimisha umma, kuondoa hofu kwa umma, kuanzisha matawi, lakini hata tulipoondoka bado walitishwa na viongozi wetu wengi siyo tu walinunuliwa, bali walibambikizwa kesi za mauaji, na au ujambazi ambazo nyingi hazikuwa na mdhamana. Mtu yeyote anayehukumu kama upinzani umeleta maendeleo yeyote, ni vyema akawa na msingi huu, ndipo akafanya judgment fair. Swala la Fair Play Ground tunalolilia hadi leo lilikuwa baya zaidi huko nyuma. Mimi mwenyewe, hadi 2000 Wilayani Karatu ambako mimi ni mbunge nilikuwa naachwa Ofisini na DED na wakuu wake wa Idara, sasa kama Mimi Mbunge nilikuwa ninahujumiwa kiasi hicho, je kwa viongozi wetu wengi ambao kwa wakati huo walikuwa ni watu wa kawaida kwa vile wasomi wote walizuiwa kabisa kujiunga na upinzani (japo walikuwa wakigombea kupitia ccm bila kuathiriwa) wasingeliweza kuhimili mikiki ya kudhibiti mapato na matumizi kama unavyosema. Ndiyo maana nimeona ni vema kueleza historia hii kwa kina ili wana JF muelewe mnayosoma kwenye vitabu na hali halisi havifanani sana on the ground. Hayo yamenitokea mimi kama mbunge, kama Katibu Mkuu wa chama katika ziara ya kuzunguka wilaya mbalimbali, na siyo nadharia. Ni mapambano tu ndiyo yametuwezesha kufikia hapa, na wengi mtakumbuka Karatu, tulimpomfungia Mkurugenzi Mtendaji(W) nje ya Ofisi yake kwa siku saba hadi masharti yetu yalipotimizwa na Serikali, jambo ambalo katika Historia ya Tanzania lilikuwa halijawahi kutokea. Unachokisema ni sawa na kumtaka mtoto wa siku 7 aanze kukimbia, political growth is a process and at times a very slow and tedious one. Tusione kuwa CCM imejikita leo, mazingira ya kukua ccm na ya vyama vya upinzani 1992 ni tofauti sana.

c) Kwa hatua tuliyofikia leo, ndiyo maana unasikia kila kona ya nchi kuna kelele za ubadhirifu, ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za wananchi. Juzi nilikuwa na Kamati yangu ya LAAC. Tukapelekwa kwenye nyumba ya Daktari, tukadanganywa na maofisa wa Serikali. Lakini wananchi walisema kidete na kusema " hata senti mmoja ya Serikali haiko katika jengo hilo, imejengwa kwa nguvu ya wananchi". Huu ndio mchango mkubwa kuwa watu leo wako huru. Ingelikuwa miaka ya nyuma wangeliswekwa ndani au kufanyiwa hujuma ya aina yeyote ile. Na ndio maana hata Wenyeviti wa Oversight Committees ni kutoka Upinzani ( kama ilivyo kwa kamati yangu ya LAAC). Wananchi wakielewa majukumu yao vizuri, wakasaidiwa kusimamia maendeleo yatakwenda haraka kwa vile hakutakuwa na uwezekano wa kuficha tena. Serikali ya kijiji itakuwa na Matawi ya vyama ambayo nayo yataa act kama Shadow government katika level hiyo ( jambo ambalo tayari linafanyika maeneo mengi).

2) Generation-Y inawezekana hujafuatilia vizuri chimbuko la Hoja ya Ufisadi. Ukitaka rudi nyuma, 2007 wakati naibua hoja hiyo. Nilizuiliwa(kwa kupigwa point of order wakati nawasilisha hoja ya Upinzani kwa ofisi ya Waziri Mkuu) na mawaziri, wabunge wa ccm kati yao wakiwemo kati yao hao hao ambao leo wanaonekana kinara wa kupiga vita ufisadi. Nadhani umekwisha kuona kauli zetu mara nyingi tukiwaita "wanafiki" kwa kuwa wako wepesi kupiga kelele kama sisis. Wabunge wa ccm hawatakiwi kupiga kelele. Kwa uwingi wao wanayoturufu ndani ya Bunge, na wangelikuwa na ujasiri hoja zote leo zingelikuwa zimefungwa, kwa sababu Bunge linauwezo kwa kupitisha "Azimio". Mara ngapi tukifika kwenye maazimio wanarudi nyuma na kuunga hoja ya upande wa Serikali. Nadhani mnahitaji kufanya utafiti wa kina kujua hoja hii imechumbuka wapi, kwanini iko hai hadi leo. Kama si kwenda kwa Wananchi Hoja zote zingelikuwa zimekwisha kufungwa. Ni baada ya kuona wanazomewa katika majimbo yao ndio wamerudi kuungana nasi hasa baada ya kuona pia kuwa hii ndiyo hoja yenye mshiko.

Hivyo, nadhani kimsingi maelezo yangu, yakichukuliwa pamoja na haya, yanatosheleza kuonyesha kuwa Upinzani umekuwa na mchango mkubwa sana katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na ya kusimamia rasilimali za Taifa zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote.

Well said.
 
Dr. Slaa, huoni kuwa kwa kukubali kinadharia kuwa hata kama CCM haitabadilisha Katiba mko tayari kujaribu kushinda kwa kutumia "Katiba Mbaya" mnaondoa kabisa umaana wa Katiba Mbaya? Kama Katiba ni mbaya na haitengenezi mazingira huru na ya usawa kushindana unaweza vipi kushiriki kushindana? Kwa kukubali kushindana kwa kutumia katiba mbaya si kwamba mnaikubali kwamba katiba hiyo mbaya inaweza kutumika kushinda kitu ambacho kimsingi mnakubali ni KATIBU NZURI?

Hivi hii ndiyo imani kwamba njia pekee ya kusababisha mabadiliko ni kutumia sanduku la kura tu? Je hiyo ndiyo njia pekee ya kisiasa ya kulazimisha watawala kubadili mfumo wa utawala wao?

Karibu nchi zote duniani ambazo ziliamua kulazimisha mabadiliko makubwa ya kisiasa zimetumia muunganiko wa njia mbalimbali ambazo kilele chake ni kufanyika kwa uchaguzi huru zaidi na wa haki zaidi. Miongoni mwa njia hizo ni pamoja na maandamano, migomo, civil disobedience (kama kukaa chini mbele majengo ya serikali) n.k

Kwanini Chadema hadi leo hii haijafikiri, kujaribu, wala kutumia njia za kulazimisha serikali na chama tawala kuja kwenye mazungumzo. Hamuoni kuwa Zanzibar wameamka zaidi katika kutumia njia mbalimbali kiasi cha kulazimisha serikali ya mseto sasa?

Kweli kwa kuendelea kujenga hoja kwenye mikutano ya hadhara, na vyombo vya habari tunaweza kweli kuwashawishi CCM waone uzuri wa hoja hizi na hatimaye kutokana na hisani na uungwana wao wakubali kubadilisha mfumo unaowalisha?

Kwanini Chadema isifanye vigumu sana kwa CCM kutawala wapendavyo kwa kutumia njia nyingine za kidemokrasia za kulazimisha kama migomo, maandamano, n.k Yawezekana kwamba uongozi wa Chadema hauko tayari kulala rumande na kutiwa pingu kwa kusababisha vurugu? Yawezekana wengi wao wanaogopa kwenda kukaa mbali na familia zao na kumwagiwa maji ya kuwashwa?

labda kama mkiwapa wananchi uongozi wa kupinga ufisadi kwa maandamano na migomo, kudai Katiba mpya kwa kugomea vikao vya Bunge na hata kufanya sitins, kukataa hoja za serikali kwa kutoka kwenye vikao vya bunge in protest (CUF wamefanya hivyo) na hata ikibidi kugoma kuitambua serikali iliyopo; labda wananchi watabadili fikra zao..na kupata matumaini ya kuchagua wapinzani wengi zaidi?

Duh! wewe ni nabii wa siasa! ningemuuliza kama ulivyouliza japo umeenda deep zaidi, sina la nyongeza.

sure, I see no future through ballot box.

Slaa I adore your hardworking and I do appreciate your braveness in all matters that concern Tz, lakini katika hizi ishu za which approach, I think alichosema MKJJ hapa ndiyo mwisho wa matatizo

Mathalan, kwa nini msiutangazie ulimwengu mwaka huu hamfanyi uchaguzi mpaka katiba ibadilike? tume ya uchaguzi ibadilike? n.k

kitu gani kinachofanya nchi hii ionekane ni ya CCM? serikali ni nani kwani? is it an alien came from venus? kuna damu za watu zinarukaruka na mioyo inavuta pumzi za kimapinduzi we need one crazy leader kuwaamsha watu kwa kidedea! ona Mrema angalau aliweza tena miaka hiyo wakati mzee wetu JKN yu mzima!!

Naomba msifanye uchaguzi mwaka huu mpaka mabadiliko yatokeaa kama kweli unaipenda Tanzania, Tanzania ni ya wote for God sake why Slaa are you sounding like CCM's

Kipi bora kuingia kwenye uchaguzi baada ya kurekebisha mambo na mnakuwa na tumaini 50%-50% ya kushinda au ndiyo hii bora liende kiwa na tumaini la kupata asilimia 2% ya kura za urais!!
 
tatizo lao ni kuwa ati wao wakigoma vyama vidogo vidogo vitashiriki.. well waviache vishiriki wananchi si ndio waamuzi? Sasa siyo kugoma halafu wanajifungia vyumbani; kama wanagoma wanaanzisha maandamano na wao kina Slaa, Zitto, Mbowe, Seif.. wawe wa kwanza kumwagiwa maji ya kuwashawasha.. Vinginevyo wanabakia ni wana mageuzi wa majukwaani na watoa hoja motomoto bungeni lakini they are not challenging the very pillars of corruption on the streets!

Nimesema mahali fulani huko nyuma "kama hatuko tayari kulipa gharama ya mabadiliko tuyatakayo, tusijaribu kuyaanzisha"!
 
Shukurani za dhati kwa Dr.Slaa kwa kuchukua muda na kujibu maswali ya wana JF.

1]Kuna jitihada zozote za wapinzani Tanzania kushirikiana kwa pamoja katika uchaguzi ili kuongeza nguvu za kuing'oa CCM madarakani?Au kila mpinzani anashiriki independently bila ya kushirikiana, ukizingatia budget yenu munayopata kwa uchaguzi ni ndogo kulinganisha na ile ya CCM.

2]Kuna mipango yoyote ya CHADEMA kusimamisha presidential candidate huko Zanzibar?

Nimefurahi sana kuona angalau viongozi wanapata muda wa kujibu maswali yetu...thanks
 
tatizo lao ni kuwa ati wao wakigoma vyama vidogo vidogo vitashiriki.. well waviache vishiriki wananchi si ndio waamuzi? Sasa siyo kugoma halafu wanajifungia vyumbani; kama wanagoma wanaanzisha maandamano na wao kina Slaa, Zitto, Mbowe, Seif.. wawe wa kwanza kumwagiwa maji ya kuwashawasha.. Vinginevyo wanabakia ni wana mageuzi wa majukwaani na watoa hoja motomoto bungeni lakini they are not challenging the very pillars of corruption on the streets!

Nimesema mahali fulani huko nyuma "kama hatuko tayari kulipa gharama ya mabadiliko tuyatakayo, tusijaribu kuyaanzisha"!
Samahani mkuu M.M. Mwnakijiji, kwa heshima kubwa naomba kuwa tofauti na haya maoni na mwelekeo wako. Wewe unaamini katika vurugu wao wanaamini katika majadiliano. CUF walifanya hayo kule Pemba lakini leo ni karibu miaka kumi hali ni ile ile na mwisho wamelazimika kuanza njia ya majadiliano na kuvumiliana.

Katikati ya Maandamano na vurugu za kudai katiba mpya mambo mengi sana yatatokea, wizi, uporaji, ubakaji, ikiwa ni pamoja na viongozi wahusika kupoteza muda mwingi magerezani kisingizio kikiwa ni kudai katiba mpya. Majeraha ya kutumia njia hiyo uliyopendekeza ni makubwa sana kwa taifa na wananchi wake. Utafiti usio rasmi unaonyesha kuwa nchi ikiingia kwenye vurugu ama za wenyewe kwa wenyewe ama za jeshi kuchukua nchi, inachukua miaka kati ya kumi na ano na thelathini kurudia katika hali ya kawaida. sidhani kwamba hayo ndiyo tunayotaka. Haki inaweza kucheleweshwa lakini siku moja itapatikana tu. Muhimu tuelimishe vizazi vyetu ili viendeleze mapambano haya ya kuiondoa nchi yetu mikononi mwa kikundi kidogo cha wezi wa mali ya umma

Mtikila ana kesi mahakamani imechukua zaidi ya miaka kumi, hatima yake kila mmoja anaweza kutabiri. Kwa mtizamo wangu nahisi hii ni njia muafaka zaidi katika kuilazimisha serikali kurekebisha katiba hiyo mbaya kuliko maandamano.

Mara nyingi viongozi wanaoongoza mageuzi ya vurugu huwwacha wafuasi wao wakipigwa virungu na kufungwa jela na wao kukimbilia ugaibuni, NAAMINI NA WEWE UKO UGHAIBUNI. tutakaopata shida kwa sababu ya vurugu za kudai katiba mpya ni sisi ambao hatua kabisa uwezo wa kuipata hiyo hifadhi ya kisiasa hotelini, sana tukifanikiwa kukimbia tutaishia kuishi kwenye mahema na kupoteza kabisa mwelekeo na matumaini ya kimaisha,

Nakupongeza Dr Slaa kwa majibu mazuri. Naomba mada na maswali yaendelee?

Respect
 
asante sana kwanza kwa kuchukua mda wako Mh W.Slaa. Swali langu moja ambalo linanisumbua akili kwani najua bila upinzani kuungana ni sawa sawa na kutwanga maji kwenye kinu inavyofika kwenye uchaguzi.Utengano wa upinzani anaye faidi sana ni CCM.

Swali langu je kuna mpango wowote wa kujaribu kuunganisha vyama upinzani vyote hili mueze kushindana na ccm kwa nguvu zaidi? Kama mkiweza kuungana nadhani itasaidia sana kuwezakupata wabunge wengi zaidi na ndio hapo watanzania nasi tutapata moyo zaidi kwenu kwani tutawaona jinsi gani mnavyo tetea maslahi ya nchi.

Utengano wa upinzani unatukatisha tamaa tunaona kama kila mtu anaangalia zaidi maslahi yake binafsi kuliko ya nchi yetu,kama wote mnaitakia mema nchi yetu na mna nia safi ya uongozi bora kwanini mnashindwa kuungana?

kuna juhudi zozote chama chako kinafanya kuweza hili kufanyika? kama wabunge wachache wa upinzani wanaweza kusumbua akili ccm inamaanisha mkiongeza nguvu pamoja basi nchi yetu itapata mabadiriko makubwa sana.
Wenger,
Wana JF, kwanza naomba radhi kwa kutokuwa jamvini kwa kipindi kirefu kidogo. Kama mnavyofahamu wakati wa Bunge kutokana na uchache wetu (Wapinzani) kazi ni nyingi sana. Kwa wale wasiofahamu tunafanya utafiti wetu wenyewe, tunaandka hotuba zetu wenyewe, na tunasimama wenyewe wakati hoja za Serikali tunazojibu zinafanyiwa kazi na mamia ya watendaji, tena wataalam katika kila eneo. Sisi, hatuna wataalam, na hata kama wachache tunautalaam katika fani chache ni katika fani hizo na zingine hatuna kabisa. Hivyo, kutokana na hali hiyo naomba radhi sikuingia kwenye jamvi kwa muda. Naomba sasa nijibu maswali machache yaliyoelekezwa kwangu tangu nilipojibu mara ya mwisho kama ifuatavyo:-

Nakushukuru sana kwa swala hili ambalo naona linajirudia mara nyingi. Natambua kuwa hili ni hitaji la Watanzania wengi. Natambua pia kuwa hitaji hili linatokana na jinsi watu wengi wasivyojua operations za vyama katika hali halisi. Kwa yeyote anayefuatilia masuala ya kisiasa, na hali halisi ndani ya vyama nadhani majibu ya swala hili yangelikuwa mepesi sana. Kwa kauli za hivi karibuni za Mwenyekiti wa TLP hivi unadhani kuna uwezekano wa vyama vya Upinzani kuungana? Wakati wengi wetu tunaona kwa dhahiri kabisa CCM imeshindwa kutekeleza ahadi zake( either fully or partially), au imewadanganya watanzania kwa kauli Tamu tamu, wakati Serikali leo inakiri kabisa hatutaweza kufikia malengo ya Millenia, wakati Serikali inakiri kuwa pamoja na jitihada nyingi hata mambo machache yaliyofanyika hayakuleta tija iliyotegemewa na wala wananchi kama wananchi hawajanufaika na hayo, lakini wako viongozi wamejitokeza hadharani wakisema, JK ame "dever".

Ni vema tukafanya tafakari ya kina ya vyama vya siasa na kujua misimamo yao, sera zao, ilani zao, mwelekeo wa viongozi wao, vyama gani viko serious katika kutetea na "kufia" maslahi ya umma. Swali ni je, iwapo mwungano haupo kutokana na sababu hizo, vyama makini vichache au hata kimoja viache (kiache) jitihada za kulikomboa Taifa kwa vile hatujaungana. Nadhani tatizo ni la "mind set" zaidi na au linapandikizwa na wachache ili ionekane tu Upinzani hauko makini kwa vile hauungani, jambo ambalo nadhani ni vizuri tukaliangalia kwa umakini zaidi. Kama nilivyosema mara zote, Chadema inapenda sana kuunganisha nguvu, inaelewa falsafa ya "Ummoja ni nguvu" ndiyo maana inatumia sana kauli mbiu ya "Nguvu ya Umma", lakini

Narudia tena Chadema haiko tayari kuungana tu na vyama au chama kwa sababu tu jamii inataka kuona vyama vinaungana. Mwenye kujua kiatu kinavyoumiza ni mvaa viatu, na kwa maana hiyo Chadema ambayo tumeisha kuwaunga wenzetu mara mbili tunaelewa maumivu yanayoweza kutokana na kuungana iwapo hutapata mtu makini wa kuungana naye. Kwa wale walio makini wanaopenda kulikomboa Taifa milango ya Chadema iko wazi, jitihada za chadema kuunganisha vyama is on record, na fursa ya kuungana itakapotokea na "partner" makini hatutaacha kuitumia. Tukikosa fursa hiyo, tutapambana kama Chadema hadi kieleweke, kwani ukombozi si lazima uletwe na utititiri bali na wale wenye dhamira ya kweli.

Nadhani hoja imeeleweka.
 
Mkuu Dr. Slaa.
Nimefuatilia majibu yako ktk hoja zetu mbali mbali hapa jamvini. Ama kuhusu kutoonekana jamvini nakubaliana nawe kwamba mpo wachache na mna wakati mgumu sana huko jumbani ktk kusimamia hoja zenye mantiki kwa wananchi bila kujali itikadi.

Napenda kuuliza au iwe changamoto kwenu chama m-badala. Kwa nini hamna sera za kuandaa viongozi wa kesho yaani wapambanaji wabichi kwani inavyoelekea ni kwamba vyama vingi ninasubiri kudaka wanachama waandamizi wanajiengua kutoka vyama vingine ili kusukuma gurudumu la kiuongozi. Je Chadema mpo ktk mkakati upi wa kuandaa viongozi mbadala?

Napenda pia kufahamu kuwa chadema mmefaidikaje na mtikisiko, mgawanyiko, sarakasi na mpasuko vilivyoko ndani ya ccm? au ndo mnawaombea waungane wawe imara au mpoje ktk hili?
 
Duh! wewe ni nabii wa siasa! ningemuuliza kama ulivyouliza japo umeenda deep zaidi, sina la nyongeza.

sure, I see no future through ballot box.

Slaa I adore your hardworking and I do appreciate your braveness in all matters that concern Tz, lakini katika hizi ishu za which approach, I think alichosema MKJJ hapa ndiyo mwisho wa matatizo

Mathalan, kwa nini msiutangazie ulimwengu mwaka huu hamfanyi uchaguzi mpaka katiba ibadilike? tume ya uchaguzi ibadilike? n.k

kitu gani kinachofanya nchi hii ionekane ni ya CCM? serikali ni nani kwani? is it an alien came from venus? kuna damu za watu zinarukaruka na mioyo inavuta pumzi za kimapinduzi we need one crazy leader kuwaamsha watu kwa kidedea! ona Mrema angalau aliweza tena miaka hiyo wakati mzee wetu JKN yu mzima!!

Naomba msifanye uchaguzi mwaka huu mpaka mabadiliko yatokeaa kama kweli unaipenda Tanzania, Tanzania ni ya wote for God sake why Slaa are you sounding like CCM's

Kipi bora kuingia kwenye uchaguzi baada ya kurekebisha mambo na mnakuwa na tumaini 50%-50% ya kushinda au ndiyo hii bora liende kiwa na tumaini la kupata asilimia 2% ya kura za urais!!
Waberoya,
Nakushukuru sana kuhusu options za kuleta mabadiliko ikiwa ni pamoja na kutokushiriki kwenye uchaguzi mwaka huu ili kushinikiza mabadiliko, kuutangazia ulimwengu wa kimataifa kuwa hakuna demokrasia na kuwa hatutashiriki, na kadhalika. Napenda kusema tu kuwa mapendekezo yako ni mazuri, lakini hayaendani na mazingira ya Tanzania Bara na wala na historical reality katika Tanzania.

i) Nadhani msingi wa hoja ya kushinikiza unatokana zaidi na matokeo ya "Maridhiano ya Zanzibar". Hali hiyo ya Maridhiano ya Zanzibar haijatokea hivi. Kwanza ni mapambano ya muda mrefu Zanzibar kati ya CCM na CUF Zanzibar. Ikumbukwe kuwa katika chaguzi zote tangu 1995, margin ya ushindi wa CCM ni ndogo sana ukilinganisha na CUF ( na Taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa kama kungelikuwa na Fair Play Ground, CUF wangelikuwa washinde, aidha wako wanaoamini CUF walikuwa wakishinda lakini wamekuwa wakipokonywa.

ii) Mapambano hayo, ambayo yalizaa "mwafaka" mara kadhaa ulifikia umwagaji damu 2001 na pia katika historia ya nchi hii, kuzalisha Wakimbizi waliokimbilia Shimoni, Kenya. Tanzania imekuwa na historia ya kupokea Wakimbizi lakini siyo kuzalisha wakimbizi.

iii) Ikumbukwe kuwa historia ya mapambano kati ya CUF na CCM Zanzibar, imekuwa polarized kati ya Pemba na Unguja, ambako Pemba yote ni 99.9 percent CUF na ndiyo maana CCM mara zote imeshindwa ku penetrate isipokuwa wakati ilipozalisha wawakilishi "Maruhani" hivyo ni dhahiri kabisa mazingira ya Tanzania visiwani ni tofauti kabisa na Tanzania Bara na hayawezi kulinganishwa.

iii) Tanzania Bara ni lidudu likubwa, uelewa wa Watanzania ukiunganisha na hali ya umaskini ni kikwazo kikubwa sana katika mapambano dhidi ya utawala mbovu, wananchi hao hao ni wa kwanza kulia na kulalamika, lakini ikifikia kujitetea, kupambana, kupigia kura vyama vya upinzani ni kinyume kabisa (isipokuwa maeneo machache kama Karatu ambayo yana historia ya upinzani toka 1961-wakati huo ikiwa sehemu ya Mbulu, ndiyo maana hata Mbulu Chadema ina madiwani 8 kidogo tu ingelichukua Halmashauri), Tarime, Bariadi na Kigoma( ambayo kwa bahati mbaya iliyumba na kumpoteza Mbunge na kugawana Madiwani na CCM). Hii ndiyo background ya Tanzania Bara.

iv) Vyama vya Upinzani vina malengo yanayotofautiana kabisa ( Tofauti na Pemba ambapo CUF ni chama kimoja pekee kikubwa dhidi ya CCM na kinaweza kutoa shinikizo la kweli kwa CCM, kwa kuwa na wawakilishi wengi na wabunge 32 Bungeni mara tatu ya vyama vingine vyote vilivyoko Bungeni). Hizi ni facts ambazo huwezi kuzi "ignore" katika pendekezo lolote la kutoka kwenye hii "Stale mate" au vicious circle. Ukisusia iwapo vyama vingine 3 au vinne vikienda kwenye uchaguzi, CCM itaendelea na uchaguz, kwa vile hakuna "dominant party" kama ilivyo CUF kule PEMBA. Ndiyo maana Chadema inajenga Chama Mbadala na kuwa Dominant Party ili wakati utakapofika, kama hatutakuwa tumeshinda tuwe na nguvu ya kushinikiza au kwa kushirikiana na chama chochote makini tutakachoshirikiana nacho au hata peke yetu. Lakini bila Dominant Party, dhana ya kushinikiza ni nadharia tu.

v) Historia inaonyesha hata pale vyama viliposhinikiza na kuacha kushiriki uchaguzi, CCM iliendelea na uchaguzi, mathalan uchaguzi wa marudio wa Jiji la Dar-Es-Salaam, ambapo wapinzani tulisusia na CCM ikashangilia na kuendelea na uchaguzi na shinikizo halikuwa na impact yeyote. In my opinion that was a miscalculation, kwa sababu politics is a Game of Timming, na msipopata the correct gear, matokeo yanayotarajiwa hajaji automatically.

Wana JF ni analysis ya aina hiyo, pamoja na jitihada tunzoendelea nazo za kuelimisha Watanzania kupitia operations mbalimbali mathalan Operation Sangara, kuimarisha mtandao wa Chama na strategies mbalimbali ili Watanzania waone na "Waamini" kuwa Tanzania inawezekana bila CCM. Siku tukiwa na proportion kubwa ya watu wanaoamini hivyo, na tukiwa na sehemu kubwa ya Vyama ikakubali kuwa katika alliance ya namna fulani, na au watanzania wakakikubali chama kimoja au ushirikiano wa vyama makini siku hiyo tutafanya mabadiliko makubwa kupitia multiple options za kuleta mabadiliko.

Hata hivyo ninashukuru sana kwa ushauri na mapendekezo na tutaendelea kuyafanyia kazi kwa lengo la kufanikisa mabadiliko ya haraka, ili Taifa lisiendelee kuangamia, wananchi wasiendelee kuumia na demokrasia kuendelea kunyongwa.
 
Wenger,
Wana JF, kwanza naomba radhi kwa kutokuwa jamvini kwa kipindi kirefu kidogo. Kama mnavyofahamu wakati wa Bunge kutokana na uchache wetu (Wapinzani) kazi ni nyingi sana. Kwa wale wasiofahamu tunafanya utafiti wetu wenyewe, tunaandka hotuba zetu wenyewe, na tunasimama wenyewe wakati hoja za Serikali tunazojibu zinafanyiwa kazi na mamia ya watendaji, tena wataalam katika kila eneo. Sisi, hatuna wataalam, na hata kama wachache tunautalaam katika fani chache ni katika fani hizo na zingine hatuna kabisa. Hivyo, kutokana na hali hiyo naomba radhi sikuingia kwenye jamvi kwa muda. Naomba sasa nijibu maswali machache yaliyoelekezwa kwangu tangu nilipojibu mara ya mwisho kama ifuatavyo:-

Nakushukuru sana kwa swala hili ambalo naona linajirudia mara nyingi. Natambua kuwa hili ni hitaji la Watanzania wengi. Natambua pia kuwa hitaji hili linatokana na jinsi watu wengi wasivyojua operations za vyama katika hali halisi. Kwa yeyote anayefuatilia masuala ya kisiasa, na hali halisi ndani ya vyama nadhani majibu ya swala hili yangelikuwa mepesi sana. Kwa kauli za hivi karibuni za Mwenyekiti wa TLP hivi unadhani kuna uwezekano wa vyama vya Upinzani kuungana? Wakati wengi wetu tunaona kwa dhahiri kabisa CCM imeshindwa kutekeleza ahadi zake( either fully or partially), au imewadanganya watanzania kwa kauli Tamu tamu, wakati Serikali leo inakiri kabisa hatutaweza kufikia malengo ya Millenia, wakati Serikali inakiri kuwa pamoja na jitihada nyingi hata mambo machache yaliyofanyika hayakuleta tija iliyotegemewa na wala wananchi kama wananchi hawajanufaika na hayo, lakini wako viongozi wamejitokeza hadharani wakisema, JK ame "dever".

Ni vema tukafanya tafakari ya kina ya vyama vya siasa na kujua misimamo yao, sera zao, ilani zao, mwelekeo wa viongozi wao, vyama gani viko serious katika kutetea na "kufia" maslahi ya umma. Swali ni je, iwapo mwungano haupo kutokana na sababu hizo, vyama makini vichache au hata kimoja viache (kiache) jitihada za kulikomboa Taifa kwa vile hatujaungana. Nadhani tatizo ni la "mind set" zaidi na au linapandikizwa na wachache ili ionekane tu Upinzani hauko makini kwa vile hauungani, jambo ambalo nadhani ni vizuri tukaliangalia kwa umakini zaidi. Kama nilivyosema mara zote, Chadema inapenda sana kuunganisha nguvu, inaelewa falsafa ya "Ummoja ni nguvu" ndiyo maana inatumia sana kauli mbiu ya "Nguvu ya Umma", lakini

Narudia tena Chadema haiko tayari kuungana tu na vyama au chama kwa sababu tu jamii inataka kuona vyama vinaungana. Mwenye kujua kiatu kinavyoumiza ni mvaa viatu, na kwa maana hiyo Chadema ambayo tumeisha kuwaunga wenzetu mara mbili tunaelewa maumivu yanayoweza kutokana na kuungana iwapo hutapata mtu makini wa kuungana naye. Kwa wale walio makini wanaopenda kulikomboa Taifa milango ya Chadema iko wazi, jitihada za chadema kuunganisha vyama is on record, na fursa ya kuungana itakapotokea na "partner" makini hatutaacha kuitumia. Tukikosa fursa hiyo, tutapambana kama Chadema hadi kieleweke, kwani ukombozi si lazima uletwe na utititiri bali na wale wenye dhamira ya kweli.

Nadhani hoja imeeleweka.

Ahsante sana Dr Slaa kwa kutembelea jamvi mara kwa mara. Pia nakupa pole kwa kazi mnayoifanya.

Nakuunga mkono zaidi ya 100%. Hakuna sababu ya kuungana kama vyama au viongozi wana ajenda tofauti vichwani mwao. Suala muhimu siyo kuwa na muungano wa vyama bali kuwa na vyama vichache makini hata kama kuna utitiri wa vyama. Kama kuna chama toka 1992 ulipoanza mfumo wa vyma vingi kimeishia kukaa kwenye rekodi za msajili, je kuna umuhimu wa kuungana nacho? Ni heri kubaki na wabunge wachache kama mlivyo sasa, lakini wenye nia dhabiti na wanaojua wanachokifanya kuliko kuwa na wabunge 100 wanaosinzia bungeni na kutoa pointi za kuchefua.

Kwa maoni yangu, tatizo la upinzani (iwe ni kuunganisha vyama kabla na baada ya upinzani, kuendesha shughuli zake, kuvutia wanachama wapya na viongozi wa kesho n.k) siyo la vyama vyenyewe kwani linasababishwa na mfumo wenye uliowekwa kwa ajili ya kudumisha utukufu wa CCM. Kwa wale mnaoweza kufanya kazi zenu mnastahili pongezi nyingi na kutiwa shime. Tulio wengi hata kama tunayo mawazo ya maana sana na tungependa kufanya hii kazi muhimu ya kuikomboa nchi yetu, tumejikuta hatuwezi kustahimili vimbwanga vya CCM. Inshallah, siku moja tutapata ujasiri wa kuungana nanyi wazi wazi. Kwa sasa bado tupo tupo bado!
 
tatizo lao ni kuwa ati wao wakigoma vyama vidogo vidogo vitashiriki.. well waviache vishiriki wananchi si ndio waamuzi? Sasa siyo kugoma halafu wanajifungia vyumbani; kama wanagoma wanaanzisha maandamano na wao kina Slaa, Zitto, Mbowe, Seif.. wawe wa kwanza kumwagiwa maji ya kuwashawasha.. Vinginevyo wanabakia ni wana mageuzi wa majukwaani na watoa hoja motomoto bungeni lakini they are not challenging the very pillars of corruption on the streets!

Nimesema mahali fulani huko nyuma "kama hatuko tayari kulipa gharama ya mabadiliko tuyatakayo, tusijaribu kuyaanzisha"!
MMJ,
Nimekuelewa. Kwa dhati unaamini kuwa Seif atatokaa barabarani wakati huu, ilhali "Maridhiano" yamekubaliwa na kubarikiwa na NEC jana, na saa hizi wanapanga Serikali Mseto! Sisi tunaoamini mapambano, tunaamini kupambana nao kuliko kuwaachia na watanzania wakituelewa watatupa wabunge wengi na kama siyo ushindi basi kuvunja "monopoly" ya CCM ndani ya Bunge na kuondoa "Dictatorship of the rulling party". Options lazima ziwe applied kufuatana na mazingira, hali halisi iliyoko katika eneo na kama "analysis" na "probability rate" zinaonyesha higher percentage of success katika option unayochukua. At this stage nje ya kuongeza support kwa wananchi na kuongeza wabunge, options zingine zote hazina higher probability rate.
 
Ni kweli Dr Slaa. Tanzania sasa hivi huwezi kutegemea maandamani kufanya mageuzi. Maandamano ya watu wenye hoja na walio makini kama wewe yana uwezekano mdogo wa kupata wafuasi. Ila fisadi mmoja (kama vile mmojawap wa wale 11 uliwataja) akiita maandamano anaweza kukusanya walau 10-20% ya wakazi wote wa Dar na watoto wakiwemo. Upinzani utatoa wapi pesa za kuwalipa watu wuunge mkono kama wanavyofanya mafisadi? Ni bora kwenda taratibu ili watu wafunguke macho. Hakuna haja ya kujiingiza kwenye risky projects kama hiyo anayopendekeza MMJ wakati matokeo yake yako wazi. The price you are paying now by the virtue of being mpizani is far bigger than most of us can comprehend. I am against fruitless options!
 
Ndugu Dr Slaa asante sana kwa kuungana nasi tena humu JF swali langu ni moja tu kwenye bunge lililopita pamoja na wewe kusimama kidete kupinga hoja zilizoletwa na serikali kwamba imeshatekeleza maazimio karibu yote ya bunge kuhusu sakata la Richmond umeweza kujifunza nini kwa vile sula hilo limechukua muda mrefu wa bunge karibu miaka miwili na gharama kubwa imetumika ikiwemo tume ya Mwakyembe mwisho wake limemalizwa kirahisi tu.
 
Back
Top Bottom