Dr.Slaa ajibu hoja mbalimbali na kueleza Sera za CHADEMA hapa JF

Dr Slaa je unakubaliana na mimi kuwa huenda tukahitaji sheria ya kudhibiti idadi ya vyama vya siasa, labda vibaki viwili tu ili kweli kuleta maana na tija, hasa kwa wananchi?

Na ningetaka kujua, kwa kutizama namna ambavyo mfumo wa siasa ulivyobadilika hapa nchini toka chama kimoja na sasa vyama vingi, ikiwa siasa inachukua sehemu kubwa sana katika kuelezea maendeleo ya nchi na wananchi, je nipe mtizamo wako, are we better off now au before tulipokuwa na chama kimoja?

Does this so called multiparty democracy deliver what it was meant to deliver
Recta,

Asante kwa kusisitiza maswali yako yote yajibiwa.

i) Sikutaka kujibu swali kuhusu malumbano ya CCM kwa kumsingi inawahusu wao. Kwa sasa kuna vikao vinaendelea ikiwa ni vikao vya kupokea Taarifa ya Mwinyi. Nisingependa kutolea kauli jambo ambalo silifahamu, sina information inayonifanya niwe na informed opinion. Vinginevyo, nitakuwa ninatoa hisia tu, ninaona hatari sana kujenga Taifa linalojijenga kwenye misingi ya Hisia. Sitaki "indovination" pia kwa kuwa inatuingiza katika ulimwengu wa "Political Utopia" ambao hauna manufaa kwa Taifa wala kwa mchakato wa siasa. Subira yavuta heri, na punde mambo yatakuwa hadharani, wakati huo tutayatolea opinion. Kwa wote pia iwe indicator ninapoacha kujibu hoja ni kwa sababu I may not have the inclination at the material time for lack of adequate information.

ii) Swala la kuweka Wagombea kwa kuachiana niliisha kulijibu awali. Msimamo wangu bado ni huo huo.

iii) Swala la Katiba, nimeisha kulijibu. Mabadiliko ya Katiba yatawezekana tu tukiwa na uwiano mzuri wa Wabunge wa Upinzani na wa Chama Tawala ndani ya Bunge. Mabadiliko ya Katiba yanatawailiwa na Katiba yenyewe, na unahitaji theluthini mbili siyo ya Wabunge wote, bali ya kila Upande wa Mwungano separately. Huu ni mchakato ambao kwa mazingira ya sasa haiwezekana, na ndani ya Bunge Serikali imeisha kusema Katiba "haitaandikwa upya". Lakini nikasema tusilie lie wala kuomboleza. Let us be proactive. Tunaweza kushinda na Katiba hiyo hiyo mbovu. Ushahidi ni maeneo tuliyoshinda sasa, hatukuwa na Katiba nyingine bali hii hii mbovu. Tunachohitaji ni "determination", kujipanga vizuri na kuwa na mikakati thabiti. Full stop. Tutaishinda ccm tukiamua na Watanzania wakituelewa vizuri wakatuunga mkono.
 
Mh Slaa, samahani naona kama umekosea umechukua maswali yangu halafu majibu ukawa unalenga kumjibu Recta. Pole najua its too much hasa kwakuwa unatakiwa kuandika sio kusema
 
Dr. Slaa, mimi nina maswali mawili tu;

1) Nizipi sera za chadema kuhusu Qadhi Court na Tanzania kujiunga na OIC?

2) Chadema kinajulikana kama chama cha kichanga, mmefanya nini kubadilisha image ya chadema kuhusu ukabila? Respect
 
Dr Slaa je unakubaliana na mimi kuwa huenda tukahitaji sheria ya kudhibiti idadi ya vyama vya siasa, labda vibaki viwili tu ili kweli kuleta maana na tija, hasa kwa wananchi?

Na ningetaka kujua, kwa kutizama namna ambavyo mfumo wa siasa ulivyobadilika hapa nchini toka chama kimoja na sasa vyama vingi, ikiwa siasa inachukua sehemu kubwa sana katika kuelezea maendeleo ya nchi na wananchi, je nipe mtizamo wako, are we better off now au before tulipokuwa na chama kimoja?

Does this so called multiparty democracy deliver what it was meant to deliver
Generation -Y,

Kwanza nisema tu bila Multiparty politics, hata demokrasia ya kujadiliana hapa, pamoja na kuwa inakuwa threatened mara kwa mara tusingekuwa nayo. Matunda ya Multipartysysm nadhani si swala la mjadala tena. Ni wazi kuna maeneo yamepata matunda hayo kuliko mengine. Karatu ni ushahidi wa wazi. Tumemfungia Mkurugenzi Mtendaji (W) nje, na wala hatukushitakiwa.

Tunavyoandikiana hapa leo wananchi kutoka kwenye mkutano wa hadhara wameenda kutengua kinachoonekana mgawo mbovu wa ardhi, (baada ya hatua zote kufuatwa na uchafu kuelekea kufumbiwa macho). Japo si vema wananchi kujichukuliwa sheria mikononi mwao, lakini system inapo collapse hicho ndicho kinachotokea. Mifano iko mingine na kwingineko japo kwa degree tofauti.

Pili, Hakuna haja ya kutunga sheria ya kuwa na vyama vichache au kupunguza utitiri. It is a question of demand and supply. Vyama kama havi perform vitajifuta vyenyewe, au vitabaki kwenye vitabu, kama baadhi ya vyama vinavyoonekana sasa. Kitu kikubwa ni kuwa na parameters, chama gani kifanye nini katika nchi bila kuwa mzigo wa lazima kwa walipa kodi. Kwa mfano Katiba na Sheria ya uchaguzi 1985 (RE), zinaweka wazi "threshold ya 5%". chama ambacho hakijapata asilimia 5 katika uchaguzi mkuu hakipati ruzuku, hakina wabunge wa viti maalum, na kadhalika. Msajili kwa Sheria na 5 ya 1992 naye ana mamlaka ya kufuta vyama ambavyo havitekelezi malengo yaliyoainishwa ndani ya Katiba zao.

Inawezekana tunahitaji kutazama upya Sheria hizi, na kuwa vigezo vilivyo wazi zaidi, ili chama ambacho hakifikii vigezo hivyo, mathalan kinashindwa kufanya mkutano wa hadhara hata kwenye mtaa au kitongoji ambapo mwenyekiti wa Taifa yupo, hakina sababu ya kuendelea kuwepo kwenye vitabu vya Msajili, that sort of thing. Sheria ya namna hiyo itasukuma vyama kufanya kazi na ushindani, hata kutoka vyama dhaifu daima unamnufaisha mwananchi wa kawaida. We need to be also more serious katika kusimamia Sheria zilizoko badala hata ya kufikiria kutunga sheria mpya.
Hivyo, nadhani majibu haya yanajieleza, hasa kuhusu kama vyama vya siasa pamoja na utitiri wao vimetoa mchango wa kubadilisha mazingiria ya kisiasa Tanzania.

Leo Tanzania ina magazeti zaidi ya 50, na yanaendelea kuchipua hata tunaanza kufikiria kuwa labda demokrasia katika uwanja huo umepitiliza. Miaka michache tu iliyopita hatukuwa na TV, leo sijui hata idadi ya TV stations. Hata mikoani nako zinachipuka kila siku. Haya yote ni matokeo ya Demokrasia iliyochangiwa sana na kufungua milango kwa vyama vingi, ambayo nayo ikafungua milango kwenye uchumi huria na wa soko. Haya mambo yote yanategemeana na kufungamana na huwezi kuyatenganisha bila madhara kwa mwingine.

Nadhani hoja imejibiwa vya kutosha.
 
Dr. Slaa, mimi nina maswali mawili tu;

1) Nizipi sera za chadema kuhusu Qadhi Court na Tanzania kujiunga na OIC?

2) Chadema kinajulikana kama chama cha kichanga, mmefanya nini kubadilisha image ya chadema kuhusu ukabila? Respect
Bull,
Asante sana. Ningeomba kabla ya kuuliza swali tujaribu kusoma mtiririko mzima kwenye thread. Vinginevyo kila anayeingia akiuliza anachofikiria tutazunguka hapo hapo kama pia bila kusonga.

1) Bull swala la Image ya Kichaga nimelijibu hapo awali, ikiwa ni pamoja na swala la kama kuna udini ndani ya chadema. Naomba rejea maelezo yote ya awali. Kwa kifupi, mimi mwenyewe nimetoa listi ya viongozi wote wa Kitaifa, wajumbe wa Kamati Kuu, wakurugenzi wa Makao Makuu. Kama kuna mtu bado ana hoja ya Ukabila na Uchaga ndani ya Chadema, basi ninatoa challenge yeye sasa atoe ushahidi. Kwa sababu tumetoa elimu vyombo kupitia vyombo vya habari, kwenye mikutano ya hadhara, operation Sangara. Sijui kama kuna njia nyingine zaidi ya hiyo. Iwapo mtu ameamua kung'ang'ania kwa sababu anazojua, basi, huyo ni wa kumpuuza tu, kwa kuwa ana lake jambo na huwezi kumbadilisha. Unachofanya katika hali hiyo, ni kwenda kwa umma na umma ukikuelewa, yeye mwache aendelee kupiga kelele. Atachoka mwenyewe, na hoja hiyo itafulia.

2) Kuhusu Sera za Chadema kuhusu Kadhi's Court na OIC, labda katika hatua hii niseme tu, kuwa "SERA" hiyo iliingia kwenye Ilani ya CCM kwa kutaka kuteka Kura za Waislamu. Udanganyifu wao sasa umewatoka puani. Waache kwanza waanguke Chadema hatuna sababu ya kununua kesi ambayo hatukuianzisha na tungeliianzisha nina hakika tungelijiandaa vizuri na bila hila wala udanganyifu wowote. Wakati utakapofika Chadema itatoa msimamo wake katika swala la Kadhi na OIC na ni dhahiri si swala ambalo Dr. Slaa anaweza kulijibu bila kufanyiwa uamuzi na vyombo vya maamuzi vya Chadema. Sera ni swala la Chama siyo mapenzi wala matakwa ya Mtu. Chadema ni chama cha Wanachama, wakiwemo waislamu na wakristu, ipo bara na visiwani hivyo, ninahakika wakati utakapofika kama ilivyo kwa Sera zote za Chadema msimamo wa chama utawekwa hadharani.
 
Dr. Slaa, mimi nina maswali mawili tu;

1) Nizipi sera za chadema kuhusu Qadhi Court na Tanzania kujiunga na OIC?

2) Chadema kinajulikana kama chama cha kichanga, mmefanya nini kubadilisha image ya chadema kuhusu ukabila? Respect
Bull,
Asante sana. Ningeomba kabla ya kuuliza swali tujaribu kusoma mtiririko mzima kwenye thread. Vinginevyo kila anayeingia akiuliza anachofikiria tutazunguka hapo hapo kama pia bila kusonga.
i) Bull swala la Image ya Kichaga nimelijibu hapo awali, ikiwa ni pamoja na swala la kama kuna udini ndani ya chadema. Naomba rejea maelezo yote ya awali. Kwa kifupi, mimi mwenyewe nimetoa listi ya viongozi wote wa Kitaifa, wajumbe wa Kamati Kuu, wakurugenzi wa Makao Makuu. Kama kuna mtu bado ana hoja ya Ukabila na Uchaga ndani ya Chadema, basi ninatoa challenge yeye sasa atoe ushahidi. Kwa sababu tumetoa elimu vyombo kupitia vyombo vya habari, kwenye mikutano ya hadhara, operation Sangara. Sijui kama kuna njia nyingine zaidi ya hiyo. Iwapo mtu ameamua kung'ang'ania kwa sababu anazojua, basi, huyo ni wa kumpuuza tu, kwa kuwa ana lake jambo na huwezi kumbadilisha. Unachofanya katika hali hiyo, ni kwenda kwa umma na umma ukikuelewa, yeye mwache aendelee kupiga kelele. Atachoka mwenyewe, na hoja hiyo itafulia.

2) Kuhusu Sera za Chadema kuhusu Kadhi's Court na OIC, labda katika hatua hii niseme tu, kuwa "SERA" hiyo iliingia kwenye Ilani ya CCM kwa kutaka kuteka Kura za Waislamu. Udanganyifu wao sasa umewatoka puani. Waache kwanza waanguke Chadema hatuna sababu ya kununua kesi ambayo hatukuianzisha na tungeliianzisha nina hakika tungelijiandaa vizuri na bila hila wala udanganyifu wowote. Wakati utakapofika Chadema itatoa msimamo wake katika swala la Kadhi na OIC na ni dhahiri si swala ambalo Dr. Slaa anaweza kulijibu bila kufanyiwa uamuzi na vyombo vya maamuzi vya Chadema. Sera ni swala la Chama siyo mapenzi wala matakwa ya Mtu. Chadema ni chama cha Wanachama, wakiwemo waislamu na wakristu, ipo bara na visiwani hivyo, ninahakika wakati utakapofika kama ilivyo kwa Sera zote za Chadema msimamo wa chama utawekwa hadharani.
 
Mheshimiwa Slaa nashukuru kwa kujibu swali langu moja je mengine mawili niliyouliza naomba majibu
 
Asante sana, nimefuraishwa na jibu la swali la kwanza, Lakini swali la Qadhi court bado sijaridhika kwa sababu;

Qadhi court na OIC waislam waliliomba muda mrefu, ni TLP ya mrema aliliweka bayana kwenye sera zake miaka mingi iliyopita, na CCM baada ya kuona watanzania wengi waislam ni jambo wanalihitaji nao wakaliweka kwenye sera na waislam wengi wakatoa kura zao.
Kama waislam wamedanganywa na ccm, hii itakua hasara kwao hao ccm kwa sababu sidhani kama waliowadanganya watawapa tena kura

Chakushangaza kwa nyie Chadema, Swala la Qadhi na OIC limewakera watu kwa muda mrefu, kama hamna sera nalo mpaka sasa mnanipa wasiwasi kuhusu umakini na jinsi msivyoelewa kero za wananchi.

Ushauri wa bure; muweke wazi mapema iwezekananvy msimamo wenu kuhusu maswala haya, vinginevyo mnaonekana kukimbia maswala mazito
 
Generation -Y,
Kwanza nisema tu bila Multiparty politics, hata demokrasia ya kujadiliana hapa, pamoja na kuwa inakuwa threatened mara kwa mara tusingekuwa nayo. Matunda ya Multipartysysm nadhani si swala la mjadala tena. Ni wazi kuna maeneo yamepata matunda hayo kuliko mengine. Karatu ni ushahidi wa wazi. Tumemfungia Mkurugenzi Mtendaji (W) nje, na wala hatukushitakiwa. Tunavyoandikiana hapa leo wananchi kutoka kwenye mkutano wa hadhara wameenda kutengua kinachoonekana mgawo mbovu wa ardhi, (baada ya hatua zote kufuatwa na uchafu kuelekea kufumbiwa macho). Japo si vema wananchi kujichukuliwa sheria mikononi mwao, lakini system inapo collapse hicho ndicho kinachotokea. Mifano iko mingine na kwingineko japo kwa degree tofauti. (Naomba kidogo nilitazame hili kwa mapana kwa baadhi ya mambo. Kuhusu uhuru wa kuongea, hili Dr Slaa sio suala la kikatiba na lilikuwepo kwenye katiba hata wakati wa chama kimoja? Unataka kusema kuwa uhuru huu wa kikatiba umewezeshwa na vyama vingi? Yanayotokea karatu huenda yanachochewa sana na historia na asili ya watu wa mkoa ule, kwani hata wakati wa chama kimoja, tena wakati wa Nyerere bado aggresiveness yao ilishapata kuonekana. Tukumbuke suala la yule bwana (sikumbuki vizuri ni Amri Dodo ama) aliyeamua kugombea ubunge kama mgombea binafsi na akashinda. Nachelea kusema tusije kuchanganya dalili za udikteta na mfumo wa chama kimoja, na tuna mifano ya namna hiyo hata sasa hapa Afrika

Pili, Hakuna haja ya kutunga sheria ya kuwa na vyama vichache au kupunguza utitiri. It is a question of demand and supply. Vyama kama havi perform vitajifuta vyenyewe, au vitabaki kwenye vitabu, kama baadhi ya vyama vinavyoonekana sasa. Kitu kikubwa ni kuwa na parameters, chama gani kifanye nini katika nchi bila kuwa mzigo wa lazima kwa walipa kodi. Kwa mfano Katiba na Sheria ya uchaguzi 1985 (RE), zinaweka wazi "threshold ya 5%". chama ambacho hakijapata asilimia 5 katika uchaguzi mkuu hakipati ruzuku, hakina wabunge wa viti maalum, na kadhalika. Msajili kwa Sheria na 5 ya 1992 naye ana mamlaka ya kufuta vyama ambavyo havitekelezi malengo yaliyoainishwa ndani ya Katiba zao.
Inawezekana tunahitaji kutazama upya Sheria hizi, na kuwa vigezo vilivyo wazi zaidi, ili chama ambacho hakifikii vigezo hivyo, mathalan kinashindwa kufanya mkutano wa hadhara hata kwenye mtaa au kitongoji ambapo mwenyekiti wa Taifa yupo, hakina sababu ya kuendelea kuwepo kwenye vitabu vya Msajili, that sort of thing. Sheria ya namna hiyo itasukuma vyama kufanya kazi na ushindani, hata kutoka vyama dhaifu daima unamnufaisha mwananchi wa kawaida. We need to be also more serious katika kusimamia Sheria zilizoko badala hata ya kufikiria kutunga sheria mpya. (Nimekuelewa asante sana, lakini, wakati mwingine ni ngumu hata hilo unalolisema hasa kwa kuwa sio vyama vyote vinavyoanzishwa hua ni vipya, vingine hua ni mgawanyiko tu wa chama kimoja. Katika hali kama hii wakati mwingine kila chama kinaweza kutimiza vigezo vya msajili, lakini visiwe na tija kwa umma. Ingawa tunaweza kuliweka hili katika mfumo wa demand and supply, lakini utitiri huu wa vyama na hasa ule urahisi wa hiki kikifutwa walewale wanabadili kidogo katiba na jina na kurudi tena kwa msajili, bado equilibrium itachukua miaka na miaka kufikiwa. Unless tuseme katika ilani zetu za uchaguzi kuwa vyama vya siasa navyo ni chanzo mojawapo wa ajira)

Hivyo, nadhani majibu haya yanajieleza, hasa kuhusu kama vyama vya siasa pamoja na utitiri wao vimetoa mchango wa kubadilisha mazingiria ya kisiasa Tanzania. Leo Tanzania ina magazeti zaidi ya 50, na yanaendelea kuchipua hata tunaanza kufikiria kuwa labda demokrasia katika uwanja huo umepitiliza. Miaka michache tu iliyopita hatukuwa na TV, leo sijui hata idadi ya TV stations. Hata mikoani nako zinachipuka kila siku. Haya yote ni matokeo ya Demokrasia iliyochangiwa sana na kufungua milango kwa vyama vingi, ambayo nayo ikafungua milango kwenye uchumi huria na wa soko. Haya mambo yote yanategemeana na kufungamana na huwezi kuyatenganisha bila madhara kwa mwingine. Nadhani hoja imejibiwa vya kutosha.
. (hili labda ulitazame kwa mapana yake. Sehemu kubwa na mafanikio ya mfumo wa vyama vingi unaielezewa kupitia uhuru wa kupata habari, uhuru wa kutoa maoni, na mambo kama hayo, ambayo bado nilikuwa nadhani ni uhuru wa kikatiba ambao kwa hapa kwetu haijalishi ni mfumo gani wa siasa tunafuata. Ninapolitazama hili natazama ni kipi hasa amabacho watu wa upinzani wameweza kukifanya katika kuleta maendeleo ya nchi hii. Kwa wanaotazama misingi, wengi bado wanaona kama wakati wa chama kimoja, concentration kubwa ya chama na serikali yake ilikuwa kwa wananchi. Lakini leo concentration imehama toka huko na kuwa labda nusu nusu, kati ya wananchi na pia wapinzani. Serikali inatumia muda mwingi kudeal na wapinzani kuliko wananchi na maendeleo. Hilo ni moja. Lakini pili, hata lile ambalo lingetegemewa lifanywe na upinzani, bado kwa kiasi kikubwa kinafanya na chama tawala. Mfano mzuri ni pale ambapo nyie bado mmeweza tu kuibua hoja za ufisadi, lakini ni wabunge wa CCM ambao wameweza kuifanyia kazi hiyo na kuiadabisha serikali. labda mtu anaweza kuhisi kuwa huenda pia hata hizo hoja mnapewa na wabunge wa CCM ili m-bweke tu, halafu wao watoke na kumkamata mwizi. unasemaje kuhusu hili la uwezo wa upinzani kuleta mabadiliko makubwa kwa maendeleo ya nchi?)
 
Dr Slaa,mie sina swali bali nina maombi/ushauri

Kwanza,kwa vile jitihada zenu za kuwafichua mafisadi zimekuwa zikikazwa na taasisi kama TAKUKURU,DPP,nk ushauri wangu kwenu ni kuhamasisha wanasheria/taasisi za kisheria (na mna mwanasheria mahiri Ndg Lissu) kufungua kesi dhidi ya watuhumiwa.Japo mie si mwanasheria lakini nadhani upo uwezekano wa kisheria wa kufanya hivyo.Vinginevyo,kazi nzuri mnayoifanya itaishia kuwa kazi nzuri tu pasipo matunda yanayokusudiwa.Na wazo la kutarajia hukumu ya wapiga kura (japo natambua kuwa the court of public opinion is more puwerful than "the usual court") lakini kwa vile idadi ya wapiga kura wengi ni maskini,ni rahisi kwao kununuliwa kwa tsheti,kilo za mchele na sukari,na trkima kama hizo na kusahau "hukumu" wanayopaswa kutoa kwa mafisadi.

Pili,nashauri mhamasishe recruitment drive ya wanachama nje ya Tanzania kama ilivyo ndani ya nchi yetu.Kuna umuhimu wa the likes of operesheni Sangara kutanuliwa hadi nje ya mipaka ya nchi.Correct me if I'm wrong,like kwa takriban muongo mzima niliokaa hapa Uingereza sijawahi kusikia kiongozi wa Chadema amekuja na kufanya maongezi na Watanzania.CCM wanafungua matawi yao hadi huku (sana sana kwa wanaotarajia kuingia kwenye mfumo fisadi),CUF pia walikuwa active sana siku za nyuma (pengine kutokana na idadi ya kutosha ya Wazanzibari waliokuja hapa kama "wakimbizi").It's high time kwa Chadema kuangalia umuhimu wa ku-consolidate support nje ya mipaka ya nchi kama ilivyo kwa ndani ya mipaka.

Ni hayo tu.
 
Kifaru,
Asante kwa swali zuri, nadhani watu wengi wanaingia kwenye mtego kama wa kwako. Si kazi ya vyama vya siasa kufanya au kutekeleza kazi au shughuli za maendeleo. Falsafa yake ni nyepesi sana. Aliyeshinda uchaguzi ndiye aliyepewa Tools za kuleta maendeleo: a) ndiye anayekusanya kodi b) Ndiye, kwa kutumia kodi hizo anaweka mfumo wa kutekeleza mipango aliyoidhinishiwa kutekeleza kupitia Bajeti, na kwa kuajiri civil service- vyama vya siasa havina civil service

Mheshimiwa Slaa naomba kutofautiana nawe hapa. Suala la shughuli za kimaendeleo sio suala la kusubiri kushinda uchaguzi tu. Hata chama kisichokua na uwezo wa kukusanya kodi kinaweza kuwa na mikakati ya kuanzisha, kutekeleza na hata kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo. Ama iwe ni ile ya kuanzishwa na wananchi wenyewe, ama inayoanzishwa na serikali ili madarakani ama itakayoanzishwa na wanachama wa vyama hivi ama chama chenyewe.

Tatizo linakuja pale vyama vinapochukulia FEDHA kuwa msingi mkuu wa maendeleo hivyo kupima uzito wa jukumu hilo kwa mizania ya uwezo wa kifedha. Kuna miradi mingi ya maendeleo ambayo inaweza kutekelezeka kwa kiasi kidogo cha fedha ambacho mnaweza kuchangishana wanachama ama hata vongozi tu wa chama na kushirikiana na wananchi kutekeleza miradi hiyo haswa ile inayoweza kutatua changamoto ndogondogo zinazowakumba wananchi katika maeneo yao.

Hili ni muhimu kwa chama chochote kuweza kujenga imani ya kuwa ni mbadala makini machoni mwa watanzania. Lakini pia ni nafasi muhimu ya wanachama wenu kujijengea uwezo wa kuongoza miradi ya maendeleo kama matayarisho ya kuingia madarakani.

Vyama vya siasa vinashinda kuuza Sera zao na Ilani. Ukishinda unatakiwa kutekeleza ahadi kwa kuwa umeshinda kutokana na ahadi hizo. Tatizo mara nyingi "washindi" huweka ahadi zisizotekelezeka au wanazojua kabisa kuwa hazitekelezeki. Mathalan " Maisha Bora kwa kila Mtanzania". Leo ukiwa uliza walioshinda kwa kauli hiyo jibu lao ni "kila mmoja atajiletea maendeleo na maisha bora" Lakini ulishinda kwa ahadi ambayo wapiga kura, au naively au kwa kuamini kweli walikupa kura. Hivyo ushindi wa aina hiyo ni wa udanganyifu.
Mheshimiwa Slaa kutolea mfano kauli mbiu ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA kama moja ya ahadi zisizoweza kutekelezeka sidhani kama unakuwa sawa. Ina maana kwako wewe ama kwa chama chako hamuamini kuwa MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA yanawezekana? Kwa upande wangu nadhani kuwa ahadi hiyo sio kuwa ni ahadi isiyoweza kutekelezeka bali ni ahadi inayohitaji maandalizi makini yenye kuhakikisha kujenga taifa na uongozi wenye nidhamu na unaojali ufanisi na kuweka mbele maslahi ya watu, yaani watanzania.

Tatizo linakuja pale ambapo ahadi hizo zinatolewa wakati kunakosekana niathabiti ya kujenga mazingira muhimu ya utekelezji wake. Kwa utawala huu naamini ahadi hiyo imeshindwa kutekelezeka kutokana na mazingira hasi yaliyojengwa na wagombea na makundi yao ndani ya chama tawala wakati wa kinyang'anyiro cha uteuzi wa ndani wa Urais na Ubunge. Harakati zile na hali ya ndani ya chama tawala, imelazimisha serikali iliyopaswa kutekeleza ahadi hiyo kutumia muda mwingi hivi sasa kushughulikia masuala mengi yasiyotowa tija katika juhudi za kujenga maisha bora kwa kila mtanzania.

Makosa yaliyofanyika na yanayoendela kufanyika ili kupata/kulinda hadhi ya Chama Tawala na uhodhi wa MADARAKA YA SERIKALI ndio yamekuwa kikwazo cha kutekeleza ahadi ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA na sio kuwa hiyo ni ahadi isiyotekelezeka.

Naamini mkiliangalia suala hilo kwa mtazamo huo na mkawa tayari kujisahihisha nanyi hamtaendelea kuiga makosa waliyoyafanya na wanayoendelea kuyafanya wapinzani wenu katika harakati zenu za kuchukua madaraka, hasa katika suala la DEMOKRASIA NA UWAJIBIKAJI..Na hata mkaweza kutekeleza ahadi ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ambayo wenzenu wanaelekea kushindwa kuitekeleza.

omarilyas
 
Dr. Slaa issue ya mabadiliko ya katiba, tume ya uchaguzi na serikali ya umoja wa kitaifa CHADEMA ina msimamo gani? mmefikia wapi kudai hayo mambo na je kuna tumaini lolote, what about timeline??just imagine mnapata kura 50% ya urais mnafikiri ni vyema kupoteza nafasi ya angalau hata ya kuwa na wizara 5!!
 
Bull,
i) Bull swala la Image ya Kichaga nimelijibu hapo awali, ikiwa ni pamoja na swala la kama kuna udini ndani ya chadema. Naomba rejea maelezo yote ya awali. Kwa kifupi, mimi mwenyewe nimetoa listi ya viongozi wote wa Kitaifa, wajumbe wa Kamati Kuu, wakurugenzi wa Makao Makuu. Kama kuna mtu bado ana hoja ya Ukabila na Uchaga ndani ya Chadema, basi ninatoa challenge yeye sasa atoe ushahidi. Kwa sababu tumetoa elimu vyombo kupitia vyombo vya habari, kwenye mikutano ya hadhara, operation Sangara. Sijui kama kuna njia nyingine zaidi ya hiyo. Iwapo mtu ameamua kung'ang'ania kwa sababu anazojua, basi, huyo ni wa kumpuuza tu, kwa kuwa ana lake jambo na huwezi kumbadilisha. Unachofanya katika hali hiyo, ni kwenda kwa umma na umma ukikuelewa, yeye mwache aendelee kupiga kelele. Atachoka mwenyewe, na hoja hiyo itafulia.

Mheshimiwa Slaa, Mimi ka niijuavyo CHADEMA naweza kukuunga mkono kabisa kuwa CHADEMA kama chama hakina sera za udini wala ukabila. Hata hivyo ni muhimu kutambua na kukubali kuwa yawezekana kichama hilo halipo lakini kwa kuwa chama kinajengwa na watu na katika siasa umuhimu wa watu ni fikira zao kuhusu masuala kadhaa, basi likaonekana kuwepo.

Tunapokuja katika watu, iwe wanachama ama viongozi, kama ilivyo katika vyama vingine, ni muhimu kujiangalia wenyewe ndani ya roho zenu kama yote mnayoyafanya, mnayoyatamka na mnayochagua kuyapigania hayana chembe ya utetezi wa maslahi ya kimakundi jamii kama vile dini na kabila.

Hivi Mheshimiwa Slaa ndani ya chama chako, hata miongoni mwa viongozi wako hakuna watu wenye kuona na kutoa misimamo ya kuwa hamuwezi kushirikiana na CUF kwa kuwa ni chama chama Waislamu?

Hivi katika suala hili la mahakama ya kadhi, mmepima na kujihakikishia kuwa sababu halisi ya CHADEMA kukaa kando nalo ni kwa kuwa tu linakwenda kinyume na katiba na sio wapo baadhi yenu (viongozi na washawishi) wanaona kuwa haliandani na maslahi ama hata "kutishia" maslahi ya kile mnachoamini kuwa ndiyo POLITICAL BASE ya chama chenu?

Hivi ndani ya chama chenu, viongozi wa dini fulani ama wanaotoka katika makabila fulani wanachukuliwa kama wenzetu ama wakuja?

Hivi maamuzi, matamshi na misimamo ya viongozi wa chama ambayo huchukuliwa kama misimamo ya chama huwa inakuwa na umakini gani katika kutambua maslahi na hali ya unyeti wa kimakundi iwe ya kidini ama kikabila?

Mheshimiwa Slaa, nayasema haya sio kwa kuwa eti nami ni mpuuzi ama ninadanganyika kirahisi na propaganda za wapinzani wenu, isipokuwa tu nina wasiwasi kuwa mnachukulia propaganda ama tuhuma hizi kirahisirahisi sana tofauti na mnavyotakiwa.

Ni muhimu kutambua kuwa katika siasa haswa katika nchi kama yetu,suala la PERCEPTIONS ni muhimu na nyeti sana. Hivyo ni muhimu kuwa waangalifu kwa kila mlifanyalo na mlisemalo linajenga perception gani kwa jamii haswa kama yetu ambayo imejengwa na fikira potofu dhidi ya kundi moja na lingine, ingawa misingi ya nchi yetu inasema tofauti na hivyo.

Omarilyas
 
Tutaishinda ccm tukiamua na Watanzania wakituelewa vizuri wakatuunga mkono.

hapo pamenigusa dr nakubaliana nawe mia kwa mia.

nina maswali mawili. la kwanza ni kuhusu sera ya majimbo. sera hii imehusishwa sana na ubaguzi wa kikabila vilevile inasemekana itaigawa nchi kwa kuwa kuna majimbo yatakayonufaika zaidi kwa vile yana rasilimali nyingi kuliko mengine. naomba ulifafanue hili.

pili tumesikia makelele kuhusu muswada mpya wa sheria ya uchaguzi. huu muswada umelenga katika kuvidhoofisha vyama vya upinzani. na kwa kuwa bunge ni la chama kimoja ni mategemeo yetu kwamba muswada huu utapita na utakuwa sheria kabla ya uchaguzi mwaka huu. je ni nini hatima ya vyama vya upinzani?
 
Omar,
Mkuu hapa umeweza kupambanua vya kutosha kwani sisi sote tunaamini kwamba Tanzania ni nchi isiyokuwa na dini isipokuwa raia wake wanazo dini zao na ndo wanaojenga jamii...hivyo hivyo ifahamike kwamba Chadema yaweza kuwa sii chama cha kidini ila wanachama wake wanazo dini..
Sheria,ilani, mwongozo na mambo yote yanayohusu vyama huzingatia pia Imani ya wahusika kwani watunzi wa yote haya hufuata bila kuvunja ibada za imani zao za dini..Na mara nyingi hupinga ama kuunga mkono yanayohusu imani zao...
Jiulizeni kwa nini watu wapinge ama waunge mkono Mahakama ya kadhi/OIC - Ukatoliki n.k... kulingana na imani zao za dini?
Je, chama kitakacho pinga ama kuunga mkono hakiwezi kuwa influenced na imani ya wanachama wake! (walio wengi)..
 
Dr Slaa,
Bunge letu ni kubwa mno. Uchumi wa Nchi yetu hauwezi kulibeba Bunge kubwa namna hii. Na bado kuna mipango ya kuongeza idadi ya wanawake humo sielewi ni kwa manufaa ya nani. Naomba uangalie uwezekano wa kulisemea hili kama ulivyosemea mishahara yenu. Kila HALMASHAURI/MANISPAA ingekuwa na Mbunge mmoja tu kama wewe ulivyo Karatu na umetosha sana.
Serikali yetu pia ni kubwa sana. Baraza la Mawaziri ni kubwa sana bila sababu. Angalia uwezekano wa kuzitaja wizara hizi kwenye KATIBA yetu ili Rais asijiundie wizara kulingana na idadi ya marafiki/washikaji/wapambe/wafadhili alionao kama ilivyotokea 2005. Uchumi wetu umeelemewa sana na mizigo hii miwili ya kisiasa. Matokeo yake huduma nyingi muhimu kwa Watanzania hazipo au zimedorora kwelikweli.
Najua utapingwa sana ukiyasema haya. Sababu ni kwamba siasa imegeuzwa kuwa uwekezaji na ajira.
Sheria ya kupambana na kuzuia rushwa haipewi tafsiri sahihi. Hatuwezi na wala sijasikia mtu kasimamishwa mahakamani kueleza jinsi alivyopata mali alizonazo. Mara kwa mara tunawapeleka watu mahakamani kwa kusababisha hasara ya mamilioni ambayo ni ngumu mno kuithibitisha. Tusaidie kupata tafsiri sahihi ya sheria hii. Vinginevyo tuendelee na kesi za kisanii kwenye mahakama zetu na kufunga wanaopokea hongo za shilingi elfu 10!
 
Mh Slaa, samahani naona kama umekosea umechukua maswali yangu halafu majibu ukawa unalenga kumjibu Recta. Pole najua its too much hasa kwakuwa unatakiwa kuandika sio kusema
Generation -Y,
Naomba radhi kama nilichanganya. Nisamehe sana, ni kweli unavyosema unapojibu maswali mengi yaliyolundikana ni tatizo kwa kuwa kila mara lazima urudi nyuma. Naomba radhi nadhani maswali yako pia katika ujumla wake yamejibiwa.
 
Asante sana, nimefuraishwa na jibu la swali la kwanza, Lakini swali la Qadhi court bado sijaridhika kwa sababu;

Qadhi court na OIC waislam waliliomba muda mrefu, ni TLP ya mrema aliliweka bayana kwenye sera zake miaka mingi iliyopita, na CCM baada ya kuona watanzania wengi waislam ni jambo wanalihitaji nao wakaliweka kwenye sera na waislam wengi wakatoa kura zao.
Kama waislam wamedanganywa na ccm, hii itakua hasara kwao hao ccm kwa sababu sidhani kama waliowadanganya watawapa tena kura

Chakushangaza kwa nyie Chadema, Swala la Qadhi na OIC limewakera watu kwa muda mrefu, kama hamna sera nalo mpaka sasa mnanipa wasiwasi kuhusu umakini na jinsi msivyoelewa kero za wananchi.

Ushauri wa bure; muweke wazi mapema iwezekananvy msimamo wenu kuhusu maswala haya, vinginevyo mnaonekana kukimbia maswala mazito
Bull,
Thanks. Concerns noted re Kadhi Courts and OIC. Kama nilivyosema awali, tuko kwenye hatua ya kuandaa Review ya Sera zetu pamoja na kuandaa Platform (Ilani) kwa uchaguzi Mkuu. Ushauri wako utazingatiwa wakati huo.
 
Dk W Slaa naomba utuwekee Muswada wa Baraza la Usalama wa Taifa ili tujue abc zake! Pia mshaurini Spika aweke Miswada na Acts mapema kwenye Parliamentary Website kama wanavyofanya kwa upande wa Order Papers na Hansards! Please, help us, thanks in advance!
 
. (hili labda ulitazame kwa mapana yake. Sehemu kubwa na mafanikio ya mfumo wa vyama vingi unaielezewa kupitia uhuru wa kupata habari, uhuru wa kutoa maoni, na mambo kama hayo, ambayo bado nilikuwa nadhani ni uhuru wa kikatiba ambao kwa hapa kwetu haijalishi ni mfumo gani wa siasa tunafuata. Ninapolitazama hili natazama ni kipi hasa amabacho watu wa upinzani wameweza kukifanya katika kuleta maendeleo ya nchi hii. Kwa wanaotazama misingi, wengi bado wanaona kama wakati wa chama kimoja, concentration kubwa ya chama na serikali yake ilikuwa kwa wananchi. Lakini leo concentration imehama toka huko na kuwa labda nusu nusu, kati ya wananchi na pia wapinzani. Serikali inatumia muda mwingi kudeal na wapinzani kuliko wananchi na maendeleo. Hilo ni moja. Lakini pili, hata lile ambalo lingetegemewa lifanywe na upinzani, bado kwa kiasi kikubwa kinafanya na chama tawala. Mfano mzuri ni pale ambapo nyie bado mmeweza tu kuibua hoja za ufisadi, lakini ni wabunge wa CCM ambao wameweza kuifanyia kazi hiyo na kuiadabisha serikali. labda mtu anaweza kuhisi kuwa huenda pia hata hizo hoja mnapewa na wabunge wa CCM ili m-bweke tu, halafu wao watoke na kumkamata mwizi. unasemaje kuhusu hili la uwezo wa upinzani kuleta mabadiliko makubwa kwa maendeleo ya nchi?)
Generation-Y,

1) Ni kweli mengi uliyosema, nakubaliana nayo. Lakini, nadhani tukubaliane kuwa kwa wale walioenda vijijini kabla ya 2004 na wale wanoenda leo mabadiliko ni makubwa sana na ninatoa mfano:-

a) Inawezekana wengi wanaandika hapa hawajui mapambano tuliyonayo kama wapinzani. Tulipoanza awamu ya pili ya mzunguko wa vijijini (Mzee Mtei na Timu yake walifanya awamu ya kwanza na wakati ule msukumo ulikuwa zaidi katika kupata wanachama 200 kwa kila mkoa na baadaye kuanzisha matawi. Zoezi hilo kwa bahati mbaya halikuendelea hadi 2004).

CCM ilipogundua kuwa sasa tuko makini na tunaenda vijijini ambako ndio nguzo zao, kila mbinu ya kutuhujumu ilifanyika. Guest hatukupokelewa( nakumbuka Kilwa tulilala kwenye nyumba ambayo haijaezekwa), chakula hatukuweza kupatiwa kwenye hoteli na migahawa tukawajibika kutembea na vyakula vyetu kwenye magari. Ilikuwa kipindi kigumu sana. Wananchi nao walikuwa wanatishiwa sana na hawakuwa wakijitokeza kwenye mikutano ( mfano extreme ni Mufindi ambapo jioni tuliingia wananchi wakatushangilia. Asubuhi tulipoamka kila nyumba imetundikwa bendera mpya ya ccm-mtindo wa zile zinazowekwa kwa mabalozi wao). Tulipoweka uwanjani Sound system na kuweka muziki hata watoto hawakutokea. Tukaamua kujihutubia wenyewe (tulikuwa na msafara wa watu kama 30), ndipo kwa nguvu za Spika tulizokuwa nazo tukawahutubia manyumbani mwao na kuwaondoa hofu. Saa 12 jioni uwanja ukafurika na kuishia kugawa kadi za Chadema kwa wanachama wapya zaidi ya 1,500 kazi iliyoendelea hadi saa 5 usiku. Hivyo, niliweka mkazo kwenye uhuru wa habari na uhuru wa wananchi kwa kuwa wengi inawezekana hawafahamu kabisa vikwazo tulivyokumbana navyo. Unafika jukwaani, hata VEO au WEO tu anakuwa na ujasiri wa kuja kukushusha Jukwaani. Hali hii pole pole imeondoka. Nakumbuka Chunya tulizuiwa kufanya mkutano kwa kisingizio cha mwenyekiti wa Halmashauri kuwa na mkutano wa maendeleo siku hiyo( ulitangazwa usiku kama mbinu ya kuzuia wa kwetu). Tulifika mahali tukamwambia DC na OCD wake watupeleke kwenye Cello(Lupango) yao ndipo tukiona siyo hadhi yetu tutaacha kufanya mkutano. Wakadhani utani wakatupeleka kweli. Tulipopaona tukawaambia mkutano utafanyika na wakitaka watupeleke lupango kwani ni size yetu ndipo wakaogopa kutushusha jukwaani.

Hivyo, kazi kubwa ilikuwa kujenga imani kwa wananchi lakini pia kwa viongozi mbalimbali waliojigeuza kuwa makada kwelikweli wa ccm kuwa na sisi tumesajiliwa kama CCM na hivyo tuna hadhi sawa. Kwa mtu ambaye hajapitia haya, ni vigumu kuelewa hatua tuliyopiga katika eneo hilo, hatua ambayo ilikuwa muhimu kabla hujafanya lolote. Demokrasia mliyokuwa mnasikia ilikuwa zaidi ya vitabuni, na wote mnajua Agustino Lyatonga alivyokuwa anapiga mabomu misafara ya Upinzani, alikuja kugundua ubaya wake baada ya yeye mwenyewe kujikuta upinzani.

b) Ziara nilizoeleza katika a) zilifanya kazi ya kuelimisha umma, kuondoa hofu kwa umma, kuanzisha matawi, lakini hata tulipoondoka bado walitishwa na viongozi wetu wengi siyo tu walinunuliwa, bali walibambikizwa kesi za mauaji, na au ujambazi ambazo nyingi hazikuwa na mdhamana. Mtu yeyote anayehukumu kama upinzani umeleta maendeleo yeyote, ni vyema akawa na msingi huu, ndipo akafanya judgment fair. Swala la Fair Play Ground tunalolilia hadi leo lilikuwa baya zaidi huko nyuma. Mimi mwenyewe, hadi 2000 Wilayani Karatu ambako mimi ni mbunge nilikuwa naachwa Ofisini na DED na wakuu wake wa Idara, sasa kama Mimi Mbunge nilikuwa ninahujumiwa kiasi hicho, je kwa viongozi wetu wengi ambao kwa wakati huo walikuwa ni watu wa kawaida kwa vile wasomi wote walizuiwa kabisa kujiunga na upinzani (japo walikuwa wakigombea kupitia ccm bila kuathiriwa) wasingeliweza kuhimili mikiki ya kudhibiti mapato na matumizi kama unavyosema. Ndiyo maana nimeona ni vema kueleza historia hii kwa kina ili wana JF muelewe mnayosoma kwenye vitabu na hali halisi havifanani sana on the ground. Hayo yamenitokea mimi kama mbunge, kama Katibu Mkuu wa chama katika ziara ya kuzunguka wilaya mbalimbali, na siyo nadharia. Ni mapambano tu ndiyo yametuwezesha kufikia hapa, na wengi mtakumbuka Karatu, tulimpomfungia Mkurugenzi Mtendaji(W) nje ya Ofisi yake kwa siku saba hadi masharti yetu yalipotimizwa na Serikali, jambo ambalo katika Historia ya Tanzania lilikuwa halijawahi kutokea. Unachokisema ni sawa na kumtaka mtoto wa siku 7 aanze kukimbia, political growth is a process and at times a very slow and tedious one. Tusione kuwa CCM imejikita leo, mazingira ya kukua ccm na ya vyama vya upinzani 1992 ni tofauti sana.

c) Kwa hatua tuliyofikia leo, ndiyo maana unasikia kila kona ya nchi kuna kelele za ubadhirifu, ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za wananchi. Juzi nilikuwa na Kamati yangu ya LAAC. Tukapelekwa kwenye nyumba ya Daktari, tukadanganywa na maofisa wa Serikali. Lakini wananchi walisema kidete na kusema " hata senti mmoja ya Serikali haiko katika jengo hilo, imejengwa kwa nguvu ya wananchi". Huu ndio mchango mkubwa kuwa watu leo wako huru. Ingelikuwa miaka ya nyuma wangeliswekwa ndani au kufanyiwa hujuma ya aina yeyote ile. Na ndio maana hata Wenyeviti wa Oversight Committees ni kutoka Upinzani ( kama ilivyo kwa kamati yangu ya LAAC). Wananchi wakielewa majukumu yao vizuri, wakasaidiwa kusimamia maendeleo yatakwenda haraka kwa vile hakutakuwa na uwezekano wa kuficha tena. Serikali ya kijiji itakuwa na Matawi ya vyama ambayo nayo yataa act kama Shadow government katika level hiyo ( jambo ambalo tayari linafanyika maeneo mengi).

2) Generation-Y inawezekana hujafuatilia vizuri chimbuko la Hoja ya Ufisadi. Ukitaka rudi nyuma, 2007 wakati naibua hoja hiyo. Nilizuiliwa(kwa kupigwa point of order wakati nawasilisha hoja ya Upinzani kwa ofisi ya Waziri Mkuu) na mawaziri, wabunge wa ccm kati yao wakiwemo kati yao hao hao ambao leo wanaonekana kinara wa kupiga vita ufisadi. Nadhani umekwisha kuona kauli zetu mara nyingi tukiwaita "wanafiki" kwa kuwa wako wepesi kupiga kelele kama sisis. Wabunge wa ccm hawatakiwi kupiga kelele. Kwa uwingi wao wanayoturufu ndani ya Bunge, na wangelikuwa na ujasiri hoja zote leo zingelikuwa zimefungwa, kwa sababu Bunge linauwezo kwa kupitisha "Azimio". Mara ngapi tukifika kwenye maazimio wanarudi nyuma na kuunga hoja ya upande wa Serikali. Nadhani mnahitaji kufanya utafiti wa kina kujua hoja hii imechumbuka wapi, kwanini iko hai hadi leo. Kama si kwenda kwa Wananchi Hoja zote zingelikuwa zimekwisha kufungwa. Ni baada ya kuona wanazomewa katika majimbo yao ndio wamerudi kuungana nasi hasa baada ya kuona pia kuwa hii ndiyo hoja yenye mshiko.

Hivyo, nadhani kimsingi maelezo yangu, yakichukuliwa pamoja na haya, yanatosheleza kuonyesha kuwa Upinzani umekuwa na mchango mkubwa sana katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na ya kusimamia rasilimali za Taifa zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote.
 
Back
Top Bottom