Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,552
- 19,420
Nauliza huyu mgombea wa chadema dkt,Slaa kasomea wapi na kasomea nini?
Hii ni muhimu kujua kwani taifa letu kwa sasa linahitaji msomi wa fani kama za kiuchumi kutokana na shida za maisha tulizonazo na kuwa nyuma kimaendeleo.
Nimesikia tetesi eti fani yako ni katika theolojia ya kikatoliki tu.Hivi mkutano mkuu wa chadema waliompitisha walifanya hivyo wakiwa wamelewa au walikusudia nini?
Mimi nilitaka kuchukua fomu lakini nikajuwa katika nchi ambayo elimu kama ya kwangu haithaminiwi na itahojiwa nikaamua kukaa kimya. Au tuseme elimu za dini sasa si tatizo tena?
Hapana hawasomi theology tu; wana elimu kubwa sana kuliko unavyodhani.
Kwanza, elimu ya seminary za kikatoliki ni kama elimu nyingine ila inatolewa kwa ubora wa hali ya juu duniani kote, ndiyo maana miaka yote hapa Tanzania mitihani ya form 4 na form 6 huongozwa na seminari za kikatoliki tu. Hata marekani ambako nimewahi kuishi kwa muda mrefu sana, ninajua kuwa shule za kikatoliki zinaongoza sana.
Baada ya kumaliza form 6 seminari, huwa ama wanaingia chuo kikuu kama wanafunzi wengine wa kitanzania au wanakwenda kusomea filosofi kwa miaka miwili kabla hawajaenda kusoma kule seminari kuu ya Kipalapala Tabora ambapo masomo wanayosoma ni pamoja na Theology, Sociology, Psychology, Islamic Studies, New Testament, Old Testament, Anthropology, Family Law na mengineyo.
At least ungepima pia uwezo wake wa kuchambua mambo ambacho ndicho kipimo kikubwa sana cha elimu kuliko kutilia shaka elimu yake bila msingi wowote wa maana.