Dr.Slaa ajiandikisha rasmi kuwa member JF.

Status
Not open for further replies.
Mh. Dr. Slaa karibu sana. Nimeguswa na maelezo yako ukimjibu FMES kuwa vyama ni jambo la mwisho kabisa - kwanza ni utaifa. Ina fariji sana kuona hata viongozi wa vyama wanawaza sawa na tusio na vyama. Mimi nami naamini chama kinafuata baada ya nchi na naamini haya ni mawazo ya watanzania walio wengi, isipokuwa watu walio na maslahi na CCM (hii haiwahusu wanachama wa kawaida wa CCM).

Pamoja na kwamba vyama si muhimu kuliko utaifa wetu, itabidi tusijidanganye kwamba na viongozi wa CCM wanawaza hivyo. Kwa hiyo ni lazina katika huu mkakati wa kujenga nchi yetu tujue tuna changamot ya kubadilisha mindset za baadhi ya watanzania wenzetu. Kama si kuzibadilisha mindset basi kuwaweka pembeni katika uongozi wa nchi yetu (yenye asali na maziwa). Hili la mindset (kama sio mindset basi ni ulafi) inajionyesha wazi sana ndani ya bunge letu. Pamoja na kuwa bunge letu lina watu wasomi na ambao akili ya kawaida ingewaona ni watu wenye uelewa mkubwa, lakini unakuta mtu ameng'ang'ania kutetea maovu kwa sababu tu kusema vinginevyo kuta-undermine image ya chama! Mifano ya akina mzee kingunge na akina Anna Abdallah inaweza kutosha kukazia point yangu! Wakati mwingine mtu unaanza kuwaza hivi kweli elimu ya uzalendo (labda na uraia) inatakiwa ipelekwe vijijini kwa watu wasio na ufahamu mkubwa wa dunia ya sasa au uanzie kwa wabunge wa CCM!!!! Maana hawa wabunge hawajaelimika na pia kwa sababu ya uwingi wao wanapotosha jamii kubwa ya vijijini. Kwa kweli kazi ni kubwa sana, lakini inabidi tuifanya kwa juhudi kubwa. Mafanikio yatapatikana, maana hii ni vita ya kupigania taifa letu na jeshi lake ni la wazalendo. Mungu yupo upande wa wenye haki, tutashinda.

Mimi binafsi nakupongeza sana kwa courage yako na uzalendo uliouonyesha mpaka hapa tulipo. Natamka kwa moyo wangu wote kwamba 'You are one of the brilliant Tanzanians'

Keep going (flying) we and God are with you.

Karibu sana.

Samwel Chitalilo ni mfano sahihi hapa!
 
....mimi mbunge wangu sijawahi hata siku moja kumsikia akizungumza bungeni au chochote kwa maslahi ya wilaya yetu au Taifa jamaa ni zero kabisa,dawa ni kwenda kumng'oa tuu...check/sauti yangu itakuwa wazi kwa yeyote atakayesimama kumpinga hata kama naye ni zero,bora kubadili zero kwa zero kuliko kuendelea na zero ya zamani!
 
Haya Mkuu Dr. Slaa,

Ki honeymoon cha ukaribisho naona ndio kimekwisha tena.

Wadau wa nchi wamerudi kazini.

Habari na kazi na maswali na hoja na vioja na majibu na kosoa na mawazo na mapendekezo yameanza.

Watu wamekupa hilo 'jiwe' dogo kwanza, tuone unadili nalo vipi.

Karibu jamvini.


....sio jiwe nilitaka kumweka kwenye WIKIPEDIA maana ametusaidia sana kwenye vita vya ufisadi.
 
Field Marshal ES,
Thanks a lot. Kimsingi, kinachotusukuma ni uzalendo kwa nchi yetu. Kwangu mimi siasa ya vyama inachukua namba ya mwisho. Kwanza sisi ni Watanzania, na watanzania wawe walalahoi kama wanavyoitwa, au wa ngazi ya juu sana (japo naamini binadamu wote sawa) wote wana mchango katika kuijenga, kuilinda na kuitetea nchi yao. Hakuna mwenye ukiritimba wala hati miliki ya nchi. Hivyo nadhani mchango wa kila mmoja nitauheshimu sana na utaheshimiwa na kila mmoja wetu. Ni kweli JF mimi si mgeni, hivyo kipya ni kujisajili upya. Thanks for the warm welcome.

Nimefurahi kusikia ukiwa na mwelekeo wa kitaifa zaidi kuliko kichama. Ugonjwa sugu wa kutetea maslahi ya chama kwanza kwa wabunge wa CCM ndio uliotufikisha hapo kwenye matatizo sugu pia kama ya UFISADI na RUSHWA iliyokithiri ndani ya serikali. Kwani wabunge wa CCM amabo ndio wengi bungeni wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha mapambano dhidi ya ubadhirifu unaofanywa na serikali yao. Kwa maoni yangu, ni busara zaidi kuwaondoa CCM haraka iwezekanavyo ili kuikomboa nchi na janga hili. Swali langu kwako Mh. Slaa ni je, una maoni gani kuhusu maandalizi ya kambi ya upinzani (vyama vya upinzani kwa ujumla wake) katika uchaguzi ujao? Wasi wasi wangu ni kwamba sioni jitihada za wazi kutoka vyama hivi katika kuwafikia WAPIGA KURA WALIO WENGI HUKO VIJIJINI NA KUJARIBU KUWAELIMISHA na kuwapa update za hali halisi ya siasa nchini ilivyo kwa sasa. Ninaamini CCM inatumia wapiga kura hawa kama msingi muhimu wa ushindi katika uchaguzi wakitumia advantage ya kujulikana kwao miaka mingi huko vijijini na ukweli kwamba wananchi hawa hawana uelewa na mwamko wa kisiasa. Tafadhali waelimisheni ndugu zetu hawa mapema ili waweze kujiunga nasi katika mapambano haya ya ukombozi wa nchi kutoka katika UKOLONI MAMBOSASA (yaani UFISADI).
 
Tafadhali waelimisheni ndugu zetu hawa mapema ili waweze kujiunga nasi katika mapambano haya ya ukombozi wa nchi kutoka katika UKOLONI MAMBOSASA (yaani UFISADI).

Mkuu Heshima Mbele,

Ni sisi sasa ndio wa kuwaelimisha wananchi, maana mbunge kama huyu Dr. Slaa, ameshafanya kazi kubwa sana kwenye jimbo lake la kuwaelimisha wananchi mpaka wakamchagua, sasa iliyobaki ni kazi yetu sisi wananchi kuelimisha wananchi wengine waliobaki.
 
Nashukuru wana JF. Nchi ni yetu tushirikiane kuijenga.

Mheshimiwa Dr. W. Slaa,

Nimewahi kusema hapo nyuma kuwa katika mila na desturi zetu tulikuwa na vigezo viwili tu vya kumpata KIONGOZI. Either alirithi au alitia fora kwenye mapambano mpaka akakubalika. Lililotakiwa kwa hawa wote ni kuwa wawe shupavu na wasiwe waoga. Ukiacha Hayati Mwl. J. Nyerere hatujaweza kumpata kiongozi mwingine yeyote mwenye sifa kwa mojawapo ya vigezo nilivyovitaja.

JF ni uwanja wa majadiliano wa jinsi ya kulinda na kutetea maslahi ya Taifa letu bila kujali rangi, kabila, jinsia, chama wala elimu kwani kwa JF - ni nchi kwanza. Ukweli ni kwamba nchi iko njia panda na kiongozi shupavu anatakiwa. Tuungane tuiokoe Tanzania. Karibu Mheshimiwa.
 
Sijui niseme jina langu?Shida hamta niamini.Ila naunga mkono siku moja tuseme majina yetu mtashtuka.Wengine mtapata heart attack.

Nani Mwenzetu? JK...:) Hatutapata heart attack bali tutakupongeza sana kwa kujiunga na Watanzania wenzako kujadili matatizo mbali mbali yanayoikabili nchi yetu hasa kuhusiana na ufisadi na pia kutokuwa na maslahi yoyote kutoka kwenye rasilimali zetu ambao 'wachukuaji' na mashareholders wao wanapata faida kubwa na kutajirika lakini Watanzania hatufaidiki na chochote. Ukiyachukua mawazo yaliyomo hapa ukumbini ambayo yanachangiwa na Watanzania mbali mbali wafuasi wa vyama na wasiokuwa na kuyafanyia kazi basi unaweza kuyapunguza matatizo makubwa ya nchi yetu kwa asilimia kubwa sana. Karibu Mzee tufahamishe na tutakupokea kwa mikono miwili
 
Mkuu Heshima Mbele,

Ni sisi sasa ndio wa kuwaelimisha wananchi, maana mbunge kama huyu Dr. Slaa, ameshafanya kazi kubwa sana kwenye jimbo lake la kuwaelimisha wananchi mpaka wakamchagua, sasa iliyobaki ni kazi yetu sisi wananchi kuelimisha wananchi wengine waliobaki.

Heshima mbele kamanda FMES
Najua ni jukumu letu sote kusaidia katika kutoa elimu kwa wananchi, na nimekuwa nikifanya hivyo pindi ninapopata nafasi ya kuwa huko nyumbani. Lakini pia kumbuka kwamba uzito wanaobeba viongozi wa juu (including wabunge) wa vyama vya siasa ni muhimu sana katika mpokeo ya elimu yenyewe.
 
....sio jiwe nilitaka kumweka kwenye WIKIPEDIA maana ametusaidia sana kwenye vita vya ufisadi.

Ni kweli Mzee Slaa ni mpiganaji.

Nilisema swali la bio ni 'jiwe dogo' nikimaanisha anaweza kuona ugumu kujadili bio yake hapa. Nikataka kuona ata handle vipi swali kama hilo.

Hata mimi ningetaka kujua bio, hususan professional background, ya viongozi na wanasiasa wetu. Hakuna anaejua chochote kuliko yoyote. Kuna mtu anajua background ya Mtikila? Au mtu kama Jaji Ramadhani? Nataka kujua lini alitoka jeshini, kabla au baada ya kuwa Jaji Mkuu.

Au kwa mfano, siku Pinda alipoteuliwa, tuliambiwa ana proffesional distinction gani Rais aliyo ipenda? Uchapa kazi peke yake sio distinction, maana tunaambiwa kutoka mbinguni - au sijui chini ardhini - kwamba shetani nae ni mchapa kazi, halali usiku. Pinda ana juhudi ya kazi, je ana maarifa?

For all I know Pinda alikuwa kafungiwa Ikulu toka atoke Wizara ya Sheria in the 60's sijui huko. Hapo Ikulu hapo Pinda aliwahi ku advise Marais nini cha maana, au alifanya nini chochote kile humo walimo mfungia dikedi na dikedi kabla hawajamuibua juzi?

Back to Mzee Slaa, kuna CV kwenye website ya Bunge. Naiangalia sielewi alipata vipi PhD ndani ya miaka 4 wakati hakuwa na bachelors wala masters.
 
Bachelors na Masters zinaweza kuchukua miaka mitano kwa ujumla.
HOWEVER inawezekana kumaliza bachelors kwa miaka mitatu.
Na masters mmoja.Jumla ni minne.
Ninaweza nikawa wrong...Ila if thats the case...Then naomba murekebishe kwani ndio kazi zetu wana jf kurekebishana.
 
Mheshimiwa dr. Slaa karibu sana! tupo mjini JF na hakika mjini ndio kwenye visa vyote...Karibu sana ila angalia sana unapokanyaga pamoja na kwamba hakuna nyoka mjini!...
 
Bachelors na Masters zinaweza kuchukua miaka mitano kwa ujumla.
HOWEVER inawezekana kumaliza bachelors kwa miaka mitatu.
Na masters mmoja.Jumla ni minne.
Ninaweza nikawa wrong...Ila if thats the case...Then naomba murekebishe kwani ndio kazi zetu wana jf kurekebishana.

Na PhD hujaijumuisha hapo.

Tunaongelea PhD ndani ya miaka minne bila kuwa na bachelors wala masters. Ina maana PhD yake ilimeza bachelors na masters. Sawa. Kwa mtaji huo nilitegemea ingechukua zaidi ya miaka 4.

Au?
 
Ili kuwa na phd lazima uwe na masters.
Masters yaweza kupatikana kwa mwaka.
Na bachelors yaweza kupatikana kwa miaka mitatu.
Jumla yaweza kuwa miaka minne which therefore makes a phd in 4yrs?
Au?
 
Kuhani, inabidi ujifunze kidogo juu ya elimu ya mapadre wakatoliki. Kabla hawajapata Udaktari huwa wamepitia miaka karibu saba ya digrii za kwanza. Falsafa inachukua miaka 2, na Theolojia inachukua miaka 4 (wanapomaliza kutegemea na upadre wao wa jimbo au utawa) wanapata elimu ambayo ni sawa na shahada, baadhi ya Seminari siku hizi wanakupa shahada kabisa. Padre wakikatoliki anapotoka Seminari huwa na angalau shahada moja.

Nikuoneshe kitu kwenye CV ya Dr. Slaa:

Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974 1977 CERTIFICATE (ni certificate gani inachukua miaka mitatu)
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972 1973 CERTIFICATE

Utaona kaingia seminari baada ya kidato cha sita na kutumia kuanzia 1972-1977 (miaka mitano) kusomea certificate. Wakati ule (na sitoshangaa hata sasa) mapadre wengi wa jimbo wakihitimu hawapewi shahada bali vyeti tu. Siku hizi hasa US na nchi nyingine wamebadili kwamba ukimalizia mwaka wa Falsafa unapata BA in Philosophy na ukienda Theolojia unaweza ukamaliza na MA.

Ni kwa sababu hiyo basi alipomaliza Seminari ya Juu aliweza kuapply kwenye Chuo cha Kipapa cha St. Urban mojawapo ya vyuo vikuu vya zamani zaidi duniani (est 1627). Ingawa hili ni off topic ni kuwa mojawapo ya matatizo ya mapadre au vijana walioacha seminari baadaya theolojia tu walijikuta hawana vyeti vya kuonesha kuwa wana digrii isipokuwa stashahada tu na wakati mwingine inakuwa ngumu sana kwa wao kupata kazi "uraiani". Ndio maana wale ambao walipata nafasi ya kujiendeleza kwenye Vyuo Vikuu kama Dr. Slaa hupata heshima ya pekee kwani kama ni elimu wameisotea sana.

Hivyo utaona kuwa kuanzia 1972-1981 Dr. Slaa alikuwa anakula kitabu cha nguvu.. so ile miaka ya mwisho ya udaktari make sense...
Natumaini nitakuwa nimesaidia kidogo hapo.
 
Ili kuwa na phd lazima uwe na masters.
Masters yaweza kupatikana kwa mwaka.
Na bachelors yaweza kupatikana kwa miaka mitatu.
Jumla yaweza kuwa miaka minne which therefore makes a phd in 4yrs?
Au?

Mushi,

Kwenye hesabu zako hujumuishi PhD, why?

3 + 1 = 4 (bachelors and masters for a very smart guy)

ph = ?

Mkuu ana kila kitu ndani ya mvua nne tu.

Ushaelewa?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom