Dr.Slaa ajiandikisha rasmi kuwa member JF.

Status
Not open for further replies.
Mheshimiwa Dr. Slaa,

1. Karibu rasmi mkuu hapa JF, ninasema rasmi kwa sababu kwa njia zangu za pembeni ninafahamu kwamba umekuwepo hapa kwa muda mrefu sana, lakini kwa pembeni, ila sasa umeamua kuyavulia nguo maji rasmi, kwa hilo ubarikiwe mheshimiwa sana maana sio viongozi wote wenye huo ubavu wa kuweza kujitoa mhanga na kusema wazi, maana ninawajua viongozi wengi waliopo hapa kibubu, lakini wako ni mfano wa kuigwa na taifa zima kwa upande wa viongozi wetu.

2. Kwa maoni yangu ni kwamba unaifahamu vizuri sana hii forum, ina waananchi wengi na wenye nia nyingi sana, lakini karibu wote hapa tunakubaliana kuwa tupo hapa kwa ajili ya uchungu wa taifa letu Tanzania. Baadhi yetu tuliacha kabisa kupoteza muda na siasa za vyama, lakini wengi hapa tumejikita katika siasa za taifa, ndio maana hata ishu ya Wangwe, tumesema ni ishu ya ndani ya Chadema, sio ya taifa ingawa pia kwa sababu ilifika hapa basi tukasema kuwa Chadema wangetafuta njia bora zaidi kama chama kui-handle hiyo ishu kuliko ilivyokuwa handled kwa sababu imeleta hisia nyingi sana ambazo sio nzuri kwa Chadema as chama cha siasa cha taifa na chenye nguvu kuliko vingine vya upinzani hasa kwa upande wa Bara, na hasa katika kipindi hiki kigumu ambacho baadhi yetu sisi wananchi tunawaunga mkono wewe na wabunge wengine wa Chadema na baadhi wa ccm katika kujaribu kuleta mabadiliko ya the way we do our things katika serikali yetu.

3. Forum ni ile ile haijabadilika, kilichobadilika ni kuongezeaka kwako na the fact kwamba sasa tutayajadili matatizo yetu kitaifa politically, katika level nyingne kabisaa, ninaomba pia nitoe heshima zangu kwa Mheshimiwa Zitto, ambaye amekuwa member hapa wa wazi kwa muda mrefu sana, ninaamini kuwa tukijumuika wote hapa, yaani nyinyi wabunge wa Chadema na wananchi wengine wa kawaida, tutafanikiwa kuzidisha ukali wa hoja za kuweza kuwasaidia na kuwakosoa viongozi wetu wa taifa na vyama vyetu pia vya siasa, kuanzia Chadema, mpaka CCM, na vym,a vyote vingine vya siasa nchini.

Kwa hayo machache, ninaomba kukukaribisha kwa mikono miwili, na ninategemea kuwa kiongozi wa aina yako, ana sifa nyingi sana za uongozi, uvumilivu na unyenyekevu kwa wananchi zitakuwa ni moja wapo, kwa sababu taifa kama letu halkitengenezwi na wananchi wenye akili za aina moja, nitakupa mfano mdogo hapa, siku moja niliwahi kumuuliza mkapa akiwa rais maswali magumu sana, aliposhindwa kuyajibu kwa hasira na uchungu mkali sana alimfokea balozi wetu aliyetayarisha ule mkutano kuwa ni kwa nini aliniruhusu niwepo pale kwenye mkutano huku alijua mapema kuwa mimi ni upinzani, alimaliza mkutano hapo hapo, na kuondoka bila hata kula chakula alichotayarishiwa.

My point ni kwamba hapa kuna vichwa vingi sana, lakini ni wananchi na ni haki yao kuuliza na kutoa maoni, wengine ni wagumu sana kuelewa, wengine ni wepesi kuelewa, ninaamini hata huko bungeni wapo hawa wananchi wa namna hii, kwa hiyo ninakutakia mafanikio makubwa huko bungeni na hapa pia yaani JF, kwamba cheche za moto unazowasha huko bungeni, utazihamisha na hapa pia ili wananchi tujue ukweli wa kinachoendelea, badala ya kumsubiri Salva Rweyemamu, kukiwa na mpya huko tupenyezeee huku wananchi,

Karibu sana, Mheshimiwa Shujaa Wa Taifa Dr. Slaaa, ninaamini kuwa huu ni mwanzo wa wabunge na viongozi wengine wengi kuja hapa, niliwahi kutabiri mwaka jana nilipofikisha michango 2000, kuwa ninaamini kuwa kuna siku JF kitakuwa ni chombo kikubwa na muhimu sana kwa taifa letu, kwamba hakuna ishu ya siasa ya taifa itapitishwa bila kukubaliwa hapa kwanza, ninaamini pole pole ndoto inaelekea kuwa kweli, kwa sababu sasa hatutarudi nyuma tena ni kuangalia mbele tu!

Mungu Aibariki Tanzania!
 
mzee, u r warmly welcome! Let us join hands to discuss the future and presents of our lovely country!
 
Pia ingekuwa ni muhimu wananchi wote huko TANZANIA WAPEWE INTANETI NA WAJIUNGE NA JF MARA MOJA KABLA HAWAJAPIGA KURA ZAO.
 
Field Marshal ES,
Thanks a lot. Kimsingi, kinachotusukuma ni uzalendo kwa nchi yetu. Kwangu mimi siasa ya vyama inachukua namba ya mwisho. Kwanza sisi ni Watanzania, na watanzania wawe walalahoi kama wanavyoitwa, au wa ngazi ya juu sana (japo naamini binadamu wote sawa) wote wana mchango katika kuijenga, kuilinda na kuitetea nchi yao. Hakuna mwenye ukiritimba wala hati miliki ya nchi. Hivyo nadhani mchango wa kila mmoja nitauheshimu sana na utaheshimiwa na kila mmoja wetu. Ni kweli JF mimi si mgeni, hivyo kipya ni kujisajili upya. Thanks for the warm welcome.
 
Kuna mtu yeyote ana BIO ya DR Slaa,nataka kumjua huyu mpiganaji maana namsikia tuu!

...Slaa hii mbona unaipita bila jibu? tunataka kujua viongozi wetu!

Haya Mkuu Dr. Slaa,

Ki honeymoon cha ukaribisho naona ndio kimekwisha tena.

Wadau wa nchi wamerudi kazini.

Habari na kazi na maswali na hoja na vioja na majibu na kosoa na mawazo na mapendekezo yameanza.

Watu wamekupa hilo 'jiwe' dogo kwanza, tuone unadili nalo vipi.

Karibu jamvini.
 
Kabla hujafa hujaumbika, JF siku zote ipo mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya Watanzania bila kujali wanatoka chama gani. Kumkoma nyani hadi giladi ili walalahoi waweze kuona faida na matunda ya jasho lao.

Karibu sana mbunge wetu ... ....
 
Quote:- Dr.W.Slaa

Dr.W.Slaa has no status. Junior Member Join Date: Tue Jul 2008

Re: Dr.Slaa ajiandikisha rasmi kuwa member JF.

Field Marshal ES,

Thanks a lot. Kimsingi, kinachotusukuma ni uzalendo kwa nchi yetu. Kwangu mimi siasa ya vyama inachukua namba ya mwisho. Kwanza sisi ni Watanzania, na watanzania wawe walalahoi kama wanavyoitwa, au wa ngazi ya juu sana (japo naamini binadamu wote sawa) wote wana mchango katika kuijenga, kuilinda na kuitetea nchi yao. Hakuna mwenye ukiritimba wala hati miliki ya nchi. Hivyo nadhani mchango wa kila mmoja nitauheshimu sana na utaheshimiwa na kila mmoja wetu. Ni kweli JF mimi si mgeni, hivyo kipya ni kujisajili upya. Thanks for the warm welcome.

Mheshimiwa Sana Dr. Slaa, ahsante kwa kunitambua na I am humbled, na JF idumu zaidi where we dare kumkoma nyani mchana, tena kweupeee! Hapa ni hoja tu, haya turudi kukata ishus taifa liko njia panda hili!
 
Mh. Dr. Slaa karibu sana. Nimeguswa na maelezo yako ukimjibu FMES kuwa vyama ni jambo la mwisho kabisa - kwanza ni utaifa. Ina fariji sana kuona hata viongozi wa vyama wanawaza sawa na tusio na vyama. Mimi nami naamini chama kinafuata baada ya nchi na naamini haya ni mawazo ya watanzania walio wengi, isipokuwa watu walio na maslahi na CCM (hii haiwahusu wanachama wa kawaida wa CCM).

Pamoja na kwamba vyama si muhimu kuliko utaifa wetu, itabidi tusijidanganye kwamba na viongozi wa CCM wanawaza hivyo. Kwa hiyo ni lazina katika huu mkakati wa kujenga nchi yetu tujue tuna changamot ya kubadilisha mindset za baadhi ya watanzania wenzetu. Kama si kuzibadilisha mindset basi kuwaweka pembeni katika uongozi wa nchi yetu (yenye asali na maziwa). Hili la mindset (kama sio mindset basi ni ulafi) inajionyesha wazi sana ndani ya bunge letu. Pamoja na kuwa bunge letu lina watu wasomi na ambao akili ya kawaida ingewaona ni watu wenye uelewa mkubwa, lakini unakuta mtu ameng'ang'ania kutetea maovu kwa sababu tu kusema vinginevyo kuta-undermine image ya chama! Mifano ya akina mzee kingunge na akina Anna Abdallah inaweza kutosha kukazia point yangu! Wakati mwingine mtu unaanza kuwaza hivi kweli elimu ya uzalendo (labda na uraia) inatakiwa ipelekwe vijijini kwa watu wasio na ufahamu mkubwa wa dunia ya sasa au uanzie kwa wabunge wa CCM!!!! Maana hawa wabunge hawajaelimika na pia kwa sababu ya uwingi wao wanapotosha jamii kubwa ya vijijini. Kwa kweli kazi ni kubwa sana, lakini inabidi tuifanya kwa juhudi kubwa. Mafanikio yatapatikana, maana hii ni vita ya kupigania taifa letu na jeshi lake ni la wazalendo. Mungu yupo upande wa wenye haki, tutashinda.

Mimi binafsi nakupongeza sana kwa courage yako na uzalendo uliouonyesha mpaka hapa tulipo. Natamka kwa moyo wangu wote kwamba 'You are one of the brilliant Tanzanians'

Keep going (flying) we and God are with you.

Karibu sana.
 
Hata mzimu wa Mwalim Julius Kambarage Nyerere inasemekana upo ,na kinachochomshughulisha ni lini Watanzania kwa asilimia kubwa wataweza kuelimika kwa mtandao huu wa utandawazi. na hata ikiwezekana ziwepo sehemu huru ambazo zitamilikiwa na vyama vya upinzani kwa kila mkoa ili kuweza kuruhusu wananchi wa miji mikuu ya wilaya kuweza kupata na kujisomea moja kwa moja nakala zipatikanazo hapa JF.
Yaani kila wilaya iweze kutoa kituo kimoja cha kupata habari kupitia mitandao.Na hata kuruhusiwa kupata nakala za siri kwa kutoa ronyo ili waliko vijijini wapatiwe habari muhimu za yapitayo hapa Tanzania badala ya kungojea magazeti yenye habari za kufikirika
.
yokwenda.

Pamoja na kazi yote alifanya Mwalimu JK Nyerere, hawezi kabisa kukwepa lawana za kuwaacha kwa makusudi kabisa watanzania wengi wakiwa wajinga wasio na elimu wala uelewa wa jinsi nchi inavyoendeshwa. Lengo hasa lilikuwa ni kutoa mwanya wa kutawala kirahisi bila upinzani kutoka kwa watu wenye upeo. Tatizo hili limeendelea kutusumbua tangu uhuru na litaendelea kwa muda mrefu kuzingatiana na mazingira ya elimu nchini. This's probably the main drawback of Nyerere regime!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom