Dr.Slaa ajiandikisha rasmi kuwa member JF.

Status
Not open for further replies.
Naona hii ya kuvushwa ina utata na pia ni kuingilia uongozi wa JF ,wao ndio wenye namna ya kuweza kumvusha mtu na kumpa high grade ,nasema sioni ubaya wowote ,ila mimi naona ikiwa mamlaka husika itapenda kuwapa daraja maalum basi ikithitika na kuthibitishwa kuwa baadhi ya vigogo wa siasa Tanzania ni wanachama na mamlaka ya udhibiti JF inaweza kumshauri mkuu mwenyewe kama wanataka kumpandisha grade au mwenyewe awachwe na apande kama wengine ni heshima tu maana waTz tunamsemo kuwa Heshima kitu cha Bure.
Ila jambo la busara ninaonelea kwa usalama wao watu hawa waonekane offline japo wapo online ikiwa ni vigogo wa CCM au vyama vyengine na hili pia washauriwe au liwe ni kitu cha lazima. Kwani mienendo ya watu hawa huwa mara nyingi inajulikana wapo wapi na wanafanya nini ,sasa isije kuwa mtu amejibanza na usalama wa mafisadi anachunguza kwenye line anaona jamaa yupo online ,natumai imefahamika ni wazo tu.
 
Ahsante sana Dr. Wilbroad Slaa kujiunga hapa ndani ya JF wewe ni Presidential material, nadhani hii iwe changamoto kwa viongozi vichwa maji wa CCM nao waje kujiunga na kupata nondoz hapa..
 
Karibu sana Dr.Slaa.

Tunaheshimu sana mchango wako kwa Taifa letu.

Tuko na tutakuwa pamoja nawe katika vita hivi.

Hatutaogopa,hatutakuacha peke yako!

Mungu ibariki Tanzania.



-Wembemkali
 
Nashukuru wana JF. Nchi ni yetu tushirikiane kuijenga.

Du, hivi kumbe ni kweli.

Dr. Slaa nachukua nafasi hii kushangilia kuwa umekuwa mwanachama mwenzetu. Wewe ndiwe Kiongozi halisi wa watanzania unawakilisha maslahi ya watanzania huko Bungeni. Nchi yetu imebaki na viongozi wachache sana wa aina yako: waliobaki wengi, hasa huko CCM, ni nyang'au tu.
 
Nashukuru wana JF. Nchi ni yetu tushirikiane kuijenga.

Kweli JF ni ya wanajamii. be part of it.... Karibu Dr. Slaa...

By the way kauli mbiu ... "Where We dare to Talk Openly!" imerudi... kazi kweli kweli

Je mshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri yupo...


By the way utaacha wenzako wapunguze muda wa kwenda kwenye kuku choma wakitaka nao wao wajifunze kubofya...

Munampelekesha puta Makamba na Wenzake... kwa kasi ya kutisha!!!
 
Koba mie kwa upande wangu siihamu wala sina bio ya Dr. Slaa, nafikiri member wanaweza kujitokeza nayo vuta subira kidogo!
 
maana yake "Vita vikienda, pambana hadi East"...lol

on a serious note kilatini changu kinanikimbia but has to do with

Maisha ni zaidi ya kuwa hai... or something like that.



Umejitahidi Mkuu, tafsiri ya: vita vivenda non vitanda est = Life has to be lived and not be avoided!

Daktari Slaa naomba endeleza hapa kifalsafa...
 
Nashukuru wana JF. Nchi ni yetu tushirikiane kuijenga.

Belated is better than never, Karibu sana Mheshimiwa Dr Slaa ingawa na mie bado mgeni humu.
Kudos kwa uwakilishi wako uliotukuka huko bungeni, Mungu akuongoze kwenye mapambano haya magumu dhidi ya ufisadi. Tuko pamoja
 
I doubt whether he's "the real Dr Slaa"!

sioni kama ni tatizo, au mwenyewe au fake, sisi tuendelee na vita kama ilivyo, kama ni fake tutajua huko mbeleni kma ni original pia tutafahamu pia. Ila mesage atakuwa anazipata whoever is he...... isitupe headache kwa sasa.
 
Si umesema SLAA uko naye hapo DODOMA?
Amesemaje?

Samahani kwa kuchelewesha taarifa, nilikuwa ndani ya ukumbi na ndo tumemaliza punde, Kweli ni yeye mwenyewe, Dk Slaa original. Ameniambia kuwa alijireegister zamani lakini akapoteza pasword. Akawa anaacess kama mgeni na ameamua kujiunga upya. Anasema anaizimia sana JF kwa sababu anapata mambo mengi hapa. Kwa hiyo, tuendelee kushirikiana naye, anaweza kutusaidia kupaza sauti kule tusikofika moja kwa moja
 
Samahani kwa kuchelewesha taarifa, nilikuwa ndani ya ukumbi na ndo tumemaliza punde, Kweli ni yeye mwenyewe, Dk Slaa original. Ameniambia kuwa alijireegister zamani lakini akapoteza pasword. Akawa anaacess kama mgeni na ameamua kujiunga upya. Anasema anaizimia sana JF kwa sababu anapata mambo mengi hapa. Kwa hiyo, tuendelee kushirikiana naye, anaweza kutusaidia kupaza sauti kule tusikofika moja kwa moja

karibu sana Dr Slaa, utakutana na wabezaji hata hapa JF ila wewe vidharau na kuviacha viroja vyao maana havina malengo ya kujenga nchi yetu.
 
DR karibu sana,,usishtuke na jina langu maana ni ushabiki tu wa enzi zile lakini kimtazamo tuko pamoja
 
Ushauri wa kwanza kabisa kwa DK SLAA kama mkichukua nchi.
Mujaribu kuujenga mfumo wa UCHUMI kwa kuangalia mfano KAMA WA TAIFA LA JAPAN.
Ni mfumo wa UCHUMI wenye kuzingatia maslahi ya MJAPAN na si vinginevyo.
Ahsante.
 



Comments ni nyingi zenye sura mbalimbali ila hii imenigusa zaidi.
Asante mkuu - mfano wako ni wa kuigwa.


Ahsante mkuu, tunataka mabadiliko ambayo ni transparent, shirikishi na ya kweli. Na vita kama hii itafanikiwa kama kutakuwa na precise and consulted efforts, hakuna kujaribu ni kufanya kweli coz nchii hii ni yetu wote mpaka tufike huko tunakopenda.
 
This is fantastic! Uamuzi wa Dr Slaa kuingia hapa umeipeleka JF to the next level. Ahsante sana kwa unyenyekevu na utumishi wako kwa nchi yetu.
 
This is fantastic! Uamuzi wa Dr Slaa kuingia hapa umeipeleka JF to the next level. Ahsante sana kwa unyenyekevu na utumishi wako kwa nchi yetu.

Kitila nadhani JF ilikuwa tayari iko kwenye "next level".. kujiunga rasmi kwa Dr. Slaa au wabunge wengine na viongozi wengine wanathibitisha tu kuwa we are a force to reckon with and place where if you are anybody in Tanzania, then you can can be somebody hapa JF.

Binafsi, kujiunga rasmi kwa Dr. Slaa ni uthibitisho kuwa we are on the right track na lazima tulinde nafasi yetu hiyo.
 
habari kubwa hiyo! humu ndani itabidi siku moja tujitambulishe kwa majina yetu halisi, nina uhakika hata Makamba yupo huku JF!! na tena usikute ndio huyu "Antsadism" na propaganda zake za CCM!

..wengi wamo humu,ila unalolifikiria ndilo, sio!

..halafu,wengi hawamo vile vile!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom