Dr. Slaa adaiwa kumwandikia meseji ya vitisho IGP

Nchimbi ameunda tume,
IGP meunda tume
Waandishi wa habari wameunda tume independent

Sasa tuone kila tume itakuja na matokeo gani. Inasikitisha lakini inachekesha kama movie vile
 
Nani alitoa order ya kutumia live bullets?kila siku nauliza jamani hivi hapa kwetu hatuna rubber bullets? Alafu nishagundua police wetu ni triger happy sanag,kitu kidogo cha kukabiliana nalo kitaaluma zaid wao wanatumia nguvu chingi sana.khaa
 
IGP Mwema anateuliwa na Rais ambaye ni shemeji, na Dr. Nchimbi anateuliwa na Rais ambaye ni best friend na mkampeni wake mkuu 2005. Sasa ni nani zaidi kati ya hawa wawili? For a fair game, wote waondoke!!

Wote dhaifu tu maana kitendo cha kumkamata Dr Slaa kwa sababu za kijinga kama hizo zingezalisha vifo zaidi! wote hawa ni dhaifu kama aliyewateua alivyo dhaifu!
 
Tutamshukuru IGP maana atakuwa ameturahisishia kazi ya kuwang'oa manyang'au CCM.
Akamatwe sasa tujibu mapigo.
 
mkuu hata mimi nimeshindwa kuamini inawezekana huko wizarani kuna tatizo kubwa.! Halafu Nchimbi inaonekana mwepesi sana.!

Ni kweli hayo maneno ni 80% Nchimbi kayasema,nimesikia clouds fm kwa kauli yake mwenyewe na si kuwekewa maneno
 
Nchimbi ameunda tume,
IGP meunda tume
Waandishi wa habari wameunda tume independent

Sasa tuone kila tume itakuja na matokeo gani. Inasikitisha lakini inachekesha kama movie vile

Hapa ndio naona kama huko wizarani hawaelewani maana nilitegemea kuona IGP na NCHIMBI wanaunda tume moja sasa wameunda tofauti, hapo kati ya tume ya IGP na NCHIMBI naona kuna dalili za kukomoana hapo...
 
Ni kweli hayo maneno ni 80% Nchimbi kayasema,nimesikia clouds fm kwa kauli yake mwenyewe na si kuwekewa maneno

Asante sana mkuu, basi kumeweka wenyewe kwa wenyewe raha sana wacha wavurugane tu
 
Nchimbi ameunda tume,
IGP meunda tume
Waandishi wa habari wameunda tume independent

Sasa tuone kila tume itakuja na matokeo gani. Inasikitisha lakini inachekesha kama movie vile

Hizo tume mbili za kwanza katika orodha zisipewe ushirikiano maana zinapoteza muda tu.

Watuhumiwa hawawezi kujichunguza.

Ni usanii tunaouona kila wanapoua watu wanakula pesa yetu kupitia hizi tume zao za k.i.p.u.m.bavu
 
Bado watashangaana sana, kila mmoja ataunda tume yake sasa sijui ni majibu ya tume ipi yatakuwa sahihi!!
 
Huyu NCHIMBI anafikiri polisi nayo inatenda kazi kisiasa kwa kuongea hadharani tu. Inawezekana IGP amechanganyikiwa na maelekezo ya kipuuzi anayopewa na viongozi wake wa kisiasa serikalini huku akijua ni kinyume cha taratibu za jeshi la polisi.

Very true. Na inawezekana pia kuna mtu ana-play behind them; anawapa conflicting orders. Kama kawaida JK ameshaanza kung'ata na kupuliza sasa atawaacha wagombane wenyewe yeye aah hahusiki. Ndio yale ya Lowassa nakujivua gamba; na ndio yale ya Nape na Mukama. Hivi waziri atasemaje IGP ni dhaifu kwenye vyombo vya habari? Yaani kweli ina maana wameshindwa kufanya kazi pamoja na ku-control conflict zao behind the scene?
 
Nafikiri Nchimbi ameona kabisa imani kwa jeshi la polisi hakuna tena na hasira za wananchi sasa zimefikia pabaya,na pia nchi mbalimbali duniani zimeanza kulitupia macho jeshi la polisi Tanzania kwa udhalimu wake,so ameona wazi hawezi tena kukumbatia uozo unaonuka ni bora amlipua Mwema,hata hvyo sioni kama Dr Slaa angekamatwa ndio ingezuia mauaji haya,kikubwa walitakiwa wayafanyie kazi mawazo yake na kuomba ushirikiano wake!
 
Waziri wa mambo ya Ndani Dr. Nchimbi, Amshangaa IGP kwann mpaka sasa Dr. Slaa hajakamatwa kwa uchochezi mara baada ya kumtumia IGP mwema sms anazoziita za uchochezi na mpaka sasa Dr.Slaa anaendelea kuranda randa mjini na IGP kakaa kimya na amedai anamashaka na itendaji wake wa kazi kama kiongozi wa jeshi la polisi.

Ameendelea kusema haiwezekani wasababishe mauwaji na waendelee kufanya mazungumzo na amesema kaunda tume na wananchi watarajie kufanyiwa kazi ripoti itakayotolewa.

Wakati huo huo Mh John Mnyika kadai kama wa kukamatwa ni Dr. Bilali aliyekwenda kufanya kampeni wakati wao Chadema walikutana katika shughuri za kichama na kufungua tawi

Nchimbi anaugua ugonjwa gani? Hapo kwenye red it is obvious tayari ana conclusion sasa tume ya nini? Kwa nini anatumia kodi ya wananchi kufanya kazi ambayo tayari ana majibu?
 
Nchimbi anaugua ugonjwa gani? Hapo kwenye red it is obvious tayari ana conclusion sasa tume ya nini? Kwa nini anatumia kodi ya wananchi kufanya kazi ambayo tayari ana majibu?

Amepatwa na ugonjwa wa kuweweseka maana anajua kuwa yeye ndiye anatakiwa kuachia ngazi.
He is diverting the truth for a short while.
It will backfire for sure
 
Amepatwa na ugonjwa wa kuweweseka maana anajua kuwa yeye ndiye anatakiwa kuachia ngazi.
He is diverting the truth for a short while.
It will backfire for sure

Wanatupiana mpira now kazi ipo sio kidogo
 
Huyo Nchimbi ni mbumbumbu tu hajui lolote, sheria za nchi na kanuni zake, wala weledi hana. Miezi michache iliyopita alikwenda New Habari ku-officiate zoezi la kuchagua mshindi wa Shindano la Mchongo gazeti la Bingwa.

Alifika pale na kuanza kuokota coupon bila ya kuuliza iwapo afisa kutoka Gaming Board alikuwapo au la maana kuwapo afisa wa Board hiyo ni lazima katika shughuli ya aina hii. Kulikuwa hakuna afisa kutoka Gaming Board.

Kilichotokea ni vurugu tupu -- zawadi ya gari iligombewa na watu wawili kwani angekuwapo mwakilishi wa Gaming Board misunderstanding hiyo usingotokea.
 
Back
Top Bottom