Dr. Slaa adaiwa kumwandikia meseji ya vitisho IGP

Anazingua tu,kwani mara ya kwanza walipo ua morogoro mbona hakulalama...............siku zao zinahesabika.
 
nakumbuka kwenye biblia wale jamaa waliotaka kujenga mnara mrefu(babeli) mpaka wamfikie mungu walipochanyikiwa kwa kila mtu kuanza kuzungumza kwa lugha yake hivyo zoezi likashindikana...mungu hajaribiwi na tunachokiona miongoni mwa viongozi wa ccm kwa kila mtu kuzungumza kama vile hawako serikali moja ni mpango wa mungu na hakika anguko lao kuu li karibu...
 
Ni kweli maneno hayo yote waziri kasema au mtoa mada kadondoshea chumvi kidogo?

Kama ni kweli, tatizo zito hapo.
 
Kitendo cha Nchimbi kuunda tume wakati IGP kashaunda ya kwake na inasimamiwa na DCI ni dalili kuwa wizarani kunawaka moto tena mkubwa sana , sasa kwa kauli hii inaonyesha wazi kuwa kuna tatizo.
 
nchimbi ni mwana siasa, wala simshangai kwa hilo.
igp ni mwana taaluma na mtu makini, hafanyi kazi kisiasa.
Hilo ndio nchimbi anashindwa kuelewa.
 
Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameelezea kushangazwa kwake na ukimya wa mkuu wa jeshi la polisi nchini juu ya sakata la kuuwawa kwa mwandishi wa habari mkoani Iringa.
Waziri Nchimbi amedai kuwa siku moja kabla ya Chadema kufanya mikutano na ufunguzi wa ofisi za chama wilayani Mufindi Dr. Slaa alimtumia 'sms' mkuu huyo wa jeshi la polisi nchini akimtaka ampigie simu haraka pia vinginevyo aandae risasi za kutosha kwa ajili ya kuwaua kwani hawangekuwa tayari kuvumilia uonevu na ukandamizaji unaofanywa na jeshi lake.
Waziri Nchimbi anadai kitendo cha IGP kuendelea kukaa kimya bila kutoa tamko lolote kufuatia kifo cha Mwangosi siku moja baada ya kupokea 'sms' toka kwa Dr. Slaa, na kitendo cha jeshi la polisi kushindwa kumkamata Dr. Slaa kinamuonyesha kwamba yeye (IGP) ni dhaifu sana, ama hajui wajibu wake, na iwapo huko mbeleni Dr. Slaa atakuwa raisi wa nchi atampuuza na kumdharau sana.

MYTAKE:
Kauli ya Waziri Nchimbi dhidi ya IGP Mwema hadharani inaonyesha kuna kutokuelewana baina yao!?
Mkuu Mwita,heshima yako.
Napenda kujua haya kayasema wapi na lini.
This is great contradiction and hypocricy.
 
Kuna uwezekano amri ya kuuwa ilitokea kundi A wakati nchimbi kundi B. Ngoja tuone mwisho wake.
 
Ndugu zangu hawa jamaa IGP na Nchimbi wanaelewa kuwa Tz haiko kisiwani. Wameanza kugombana wengine kwa aibu ya ndani na nje wanaoiona mbele. Kusema Dr Slaa alim sms IGP na matokeo ya kifo cha Mwangosi ni indicator ya kutekelezwa kwa tahadhari aliyoisema Dr Slaa.
 
Ni kweli maneno hayo yote waziri kasema au mtoa mada kadondoshea chumvi kidogo?

Kama ni kweli, tatizo zito hapo.

mkuu hata mimi nimeshindwa kuamini inawezekana huko wizarani kuna tatizo kubwa.! Halafu Nchimbi inaonekana mwepesi sana.!
 
Waziri wa mambo ya Ndani Dr. Nchimbi, Amshangaa IGP kwann mpaka sasa Dr. Slaa hajakamatwa kwa uchochezi mara baada ya kumtumia IGP mwema sms anazoziita za uchochezi na mpaka sasa Dr.Slaa anaendelea kuranda randa mjini na IGP kakaa kimya na amedai anamashaka na itendaji wake wa kazi kama kiongozi wa jeshi la polisi.

Ameendelea kusema haiwezekani wasababishe mauwaji na waendelee kufanya mazungumzo na amesema kaunda tume na wananchi watarajie kufanyiwa kazi ripoti itakayotolewa.

Wakati huo huo Mh John Mnyika kadai kama wa kukamatwa ni Dr. Bilali aliyekwenda kufanya kampeni wakati wao Chadema walikutana katika shughuri za kichama na kufungua tawi
 
nchimbi ni mwana siasa, wala simshangai kwa hilo.
igp ni mwana taaluma na mtu makini, hafanyi kazi kisiasa.
Hilo ndio nchimbi anashindwa kuelewa.

Angekuwa ni mwana taaluma na mtu makini na aciefanya kazi kisiasa acingeyazuia maandamano ya CDM Arusha ambayo tayari yalikuwa yamesharuhuciwa na RPC Andengenye.. Matokeo yake Polisi wakawaua watu watatu..! Alitumika wakati ule na ataendelea kutumika..

Sent from Homms..
 
Back
Top Bottom