MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Inaelekea Shein ni mkimya sana. Makamo wetu wa raisi huyu kwangu mimi ndiye ninayeona anayefaa kuongoza nchi 2015. Hayupo kwenye spotlight sana kama viongozi wengine wakuu. Katika viongozi tulionao mimi naona huyu mzee ni moja kati ya waliyo bora maana haendekezi siasa za jukwaani. Sijui kwa nini yeye hatajwi kati ya moja ya watu wanaoweza kumrithi JK, labda mwenyewe hautaki uraisi. Ukilinganisha na viongozi wengine wanao tajwa tajwa sasa mimi naona so far namsupport Shein for 2015.
Sababu zangu ni zifuatazo.
1.Hajaonyesha tamaa wala uchu wa madaraka.
2.Hana skendo yoyote kubwa anayo tajwa kuhusika.
3.Haelekei kuwa na makundi
4.Ni mpole na hapendi spotlight kitu ambacho kinaweza kuashiria he is all action and no talk.
5.Tetesi niliyo sikiaga ni kwamba 2005 Kikwete alikua na mgombea mwenza wake mwenyewe lakini baada ya majadiliano wakaona kwamba Shein ndiyo anafaa kuwa kwenye tiketi ya chama.
Sijui kama mwenyewe ana ndoto za 2015 lakini kwenye kundi la sasa yeye anaonekana kufaa kuliko wenzie. Wanaweza kutokea wengine wanaofaa kabla ya 2015 ila kwa sasa nimemuona huyu. Haya ni maoni yangu tu wakuu sijui nyie mna semaje.