Na wewe ni sehemu ya wapotoshaji, mwanzo nchi yetu ilikuwa inaitwa German East Africa, na baada ya Waingereza kuichukuwa na kuwa koloni lao ndio wakabadili jina na kuiita Tanganyika.
Na wewe acha kupotosha German East Africa au Deutsche Ostafrica ilijumuisha pia nchi za sasa za Burundi na Rwanda, na baada ya Ujerumani kushindwa vita vikuu vya pili vya dunia iligawanywa na Tanganyika kuwa chini ya Uingereza, huku Burundi na Rwanda zikiwa makoloni ya Ubelgiji. Kwa hiyo, German East Africa sio Tanganyika ya sasa pekee, naomba kabla ya kupost tufanyie utafiti kidogo wa kile tunachoandika.
Kwa kweli hata mimi natamani sasa jina la Tanzania Bara life na lirudi jina letu la Tanganyika; mjadala huu unanipa matumaini kwamba wakati huo upo na hauko mbali. Kama uhuni wa Mobutu Wacongo wamekuja kuutaa na kurudisha jina la nchi yao iliyobatizwa kiharamu na kuitwa Zaire; our beloved Tanganyika is on the way to resurface and assume its due status.
Wakuu, wengine mnakurupuka tu na kutoka mapovu. Jiulize ni Tanzania au Tanganyika ndio iliyopata uhuru 1961? Ukipata jibu utajua kama Prof au mchangiaji ndio mpuuzi. Watu milioni 1 bado wanajiita Wazanzibar na wimbo wao wa Taifa, Bunge na Bendera yao. Kwanini isiwe hivyo kwa upande wa pili/Tanganyika? Acheni utumwa wa mawazo kwa kuwa amesema mtu eti kwa sababu ni Dk. ama Prof. huo ndio upuuzi kupita wa huyo mzee mimi nathubutu kumwita mamluki.
Tananyika iko replaced na Tanzania bara,Kwa mfano kabla hujaolewa uliitwa Jane John,baada ya kuolewa ukabadili jina unaitwa Jane Mushi,unapofanya birthday si unasherekea siku ile ile even if you are no longer Jane John but you are Jane Mushi.
Swali lako zuri sana lakini nakuomba pia unijibu moja.. Kwa nini katika ramani hiyo hiyo Utaona TANZANIA imewekwa ktk eneo la Bara na ZANZIBAR imewekwa visiwani?..Je ndio kusema bara imekuwa Tanzania na Zanzibar imebakia kuwa Zanzibar maana kama limeandikwa jina la Tanzania haikutakiwa Zanzibar ioneshwe ktk ramani.. Kwa mtu yeyote asiyejua nchi hizi akiona ramani ataelewa kwamba Tanzania ni bara na Zanzibar ni visiwa vipo mashariki ya Tanzania...Kwa nini makosa haya hutumika?Hio nchi ya Tanzania Bara wanayosema ipo kwnye ramani ipi ya dunia? mbona mie sijawahi kuiona?
Angalia ramani zote utakuta Tanzania na kule baharini Zanzibar.
Au Hio Tanzania bara imekua kama Mamlaka ya ndani ya palestina?
1. NIkikubaliana na nyier mnaotaka tuseme Tanzania Bara, sawa. Sasa si inabodo siku ya Uhuru wa nchi ya Tanzania Bara Tupandishe bendera yake na tuimbe wimbo wake wa Taifa? hivi vitu vipo? kwa sababu mojawapo ya ID ya nchi ni BENDERA NA WIMBO.
2. Tena rais wenu wa Tanzania Bara ni nani kama Tanzania visiwan inayo rais wake?
Kama majibu hayo hayapo vema inavotakiwa kuwepo, NI KWAMBA HAKUNA NCHI YA TANZANIA BARA.
MNADANGANYWA NA WANASIASA WAJINGA KWA MASLAHI YAO NA UOGA ULIOWATAWALLA JUU YA SUALA LA MUUNGANO.
LWAITAMA anatumiwa yule
Tanzania bara mna jeshi?
bendera?
wimbo?
rais?
serikali?
kama hamna vyote ivyo mnachezewa shere tu kuambiwa miaka 50 ya tanzania
Dr Azavel Lwaitama has been right in many discussions on this country's politics. In this issue of Tanganyika I believe that he is wrong. The songs of Tanzania bara and Tanzania visiwani has been buried by Zanzibaries. Let's all now sing the new songs Of Tanganyika and ZanzibarKwa hilo si jina kama CRDB ya zamani na CRDB yaleo je maana ni ileile??funguka Azavel Lwaitama hawezi kuwa mpuuzi kwawatu wenye uwezo kiakili ni mmoja wapo!!wewe ndo unawezakuwa mpuuzi watu wanaomjua Azavel lwaitama na hii thread yako haiitaji kuwa jiniasi!!!dairekiti wewe ndiye mpuuzi!!!
Na mimi ningekushauri siku nyingine usome vizuri kabla ya kuchangia, kumbuka hii thread niliianzisha kwa mtindo wa live coverage ili waliokuwa wanasikiliza BBC kwa wakati ule nao watoe maoni yao na ambao walikuwa hawasikilizi ilikuwa ni taarifa watune BBC swahili kwani inapatikana online.Uwezo wa kufikiri wa Dr. Lwaitama ni mkubwa na ni mmoja kati ya watz ambao wananyadhifa katika jamii na wanatenda wanachokiamini tu. Jamaa hana unafiki wala woga wa kuwatii watawala ktk historia yake. Heshima kwa Dr. Lwaitama, mleta maada inawezekana ameshindwa kudadavua kwa undani sababu zilizotolewa kwa sababu Dr. ni mtu wa falsafa hivyo kumwelewa inahitaji kichwa kiwe vizuri.
Siku nyingine kwa ushauri ukileta maada sema kabisa maneno yote au toa sababu alizozitoa wakati ametoa kauli yake tukusaidie kudadavua.