Dr. Asha Rose Migiro: The next president?

Tatizo la tanzania mpaka sasa ni la kimfumo pia na uwezo wa viongozi binafsi

Na mfumo wa kiutawala na kisiasa ndio unaofanya hata kionngozi mwenye uwezo asiweze kufanya mabadiliko yanayotarajiwa

Ni kwa sababu hiyo A R Migiro hawezi kuisaidia nchi hii kwa matatizo tuliyo nayo hata kama atafanikiwa kuchaguliwa

Sitampigia kura!
 
haya siyo maigizo, atoke mbali hasituchefue zaidi ya hapa, hatutaki sera za CCM tena, yeye na chama chake watalamba kwato... raisi wa 2015 anaeleweka ni slaa
 
JK M.kwere...Migiro Mpare..hawa watu wana kitu kinachofanana,tofauti ni jinsia zao tu...changanya na zako.
 
suala si migiro, EL, Makufuli au nani. Suala ni kua rais atatoka nje ya ccm, ambayo ilikufa na nyerere.
 
anavyolegea vile, atatusaidia nini watz? kama wanataka waangukie pua, wamlete huyo ******. kwa habari ya udini, sidhani kama adha rose mingiro ni mwislam, nilikuwa najua ni mkristo...kama kuna mwenye fununu atuelezee vizuri.

Halafu ukishapata uhakika wa dini yake, ndo itakusaidia kufikia uamuzi au?... udini utatumaliza!
 
Naomba niulize, hivi miaka 50 ya kutawaliwa na wanaume kwa maana ya kujitawala, na miaka 100 ya kutawaliwa na wanaume kwa maana ya tukijumlisha na enzi za ukoloni kuna jambo gani kubwa sana la kuonesha?

Hivi watu mnajua kuwa mwaka 1961, sisi Tanzania, South Korea, Singapore, Dubai, Malaysia tulikua ni nchi zinazofanana kiuchumi. Hao wanaume wamefanya nini kwa kipindi chote hicho cha miaka 50 mpaka wenzetu wakapaa kiuchumi, sisi tumebaki tunamark time tu?... Binafsi simfahamu vizuri, ila napinga kumdisqualify mtu just because ya jinsia yake alone.
 
Rekebisha hapo penye bold --Hebu sema ni kwanini muda bado? 50 yrs ya uongozi wa wanaume umetuletea nini?

Wanawake nao wana haki kushiriki uongozi katika ngazi yoyote. Huenda hata ufisadi ukapungua pale tutakapoongeza wanawake kwenye uongozi. Nikisema hivi sina maana kumshabikia ARM bali napinga hiyo kauli kwenye bold. Mwisho wa siku watanzania ndio wataamua wenyewe.
Kama kwa miaka 50 wanaume wameshindwa unategemea wanawake wataweza kwa nguvu ipi wakati bado ni tegemezi wa mfumo dume. Tumewajaribu kwa Spika hatutafanya makosa tena kwa urais, urais haujaribiwi Makinda anawaangusha.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
MIAFRIKA JAMANI?....

Hivi kweli kuna mtuanaweza kunipa sifa za Asha Rose Migiro kama kiongozi?..Kumbukeni tu kwamba Uongozi wa nchi ni kipaji ambacho hakina sifa ya darasa wala ujuzi..Halafu tujiulize - nini msimamo wake kuhusu Mafisadi na Azimio la Zanzibar, Katiba Mpya, Muungano, Uwekezaji, Uhamiaji, madini, Usalama wa Taifa, Umiliki wa Ardhi, Ajira, Elimu, AFYA na Maisha bora kwa wananchi.

Msitake kumpamba mtu kama mlivyofanya wakati wa JK kumbe hakuwa na sifa ya Uongozi.. Je, kuchaguliwa Umoja wa Mataifa ndio sababu kubwa ilowavutia na jina lake? maanake toka awepo hapo UN hakuna lolote la maana kalifanya...Simchukii hata kidogo, she is good people - lakini ucheshi ama uzuri wa sura hakuimpi wala hakuongezi uwezo wake wa kuwa rais wa nchi.. Hizi habari za Usawa na uuwiano ktk hali tuliyopo haiwezi kuwa sababu wala kigezo cha kujivunia...

Toka kaingia yeye na Huyo macho madogo UN imekuwa chombo cha mabepari, wanapelekeshwa kama malaya, vikwezo kwa Syria lakini sio Bahrain. Majeshi ya NATO yanavamia nchi za watu na kuvunja sheria zote za Umoja wa Mataifa kuhusiana na sovereign immunity, jambo ambalo sisi hatuwezi kuwachagulia wao viongozi. Obama amegeuka kuwa mpenda vita kuliko hata Bush..Dunia ya leo vita kila kona duniani kutokana na uvamizi wa uwekezaji kujenga interest zao (Ukoloni mamboleo) - WHAT HAS SHE DONE FOR US LATELY?

Mkuu Mkandara huwa unanishangaza sana ukitumia derogatory names kwa watu!

Naamini unajua utaifa wa Ban Ki Moon kama ulitaka urejelee utaifa wake hukuwa na sababu ya kumwita "macho madogo"

Mtendee mwenzako kile unachopenda wewe kutendewa, sidhani Kama yupo atakae furahi Migiro akiitwa "ngozi nyeusi" kwa mfano
 
Dada yake anaitwa R.msuya ..ni godoro la muda mrefu la JK....ALL In all sikatai namheshimu sana ASHA ROSE......Lakini bado nina mashaka na mfumu dume uliotawala Tanzania..hasa sehemu za vijijini...wengi hawaamini kuwa mwanamke anaweza!!....na utendaje wa SPIKA wetu Anna Makinda utatoa mwelekeo wa mwanamke kwenye uongozi wa nchi...maana kabla tulimfikiria Getrude Mongela .....lakini alichoenda kutufanyia kule AU kama spika wa bunge la afrika ..hakielezeki....sijui alipata kijana akamdanganya au nini maana sio Mongela tuliyemjuwa.....

Natoa tu onyo ccm wasijaribu kutumia hoja ya uwanamke wa ASHA kama njia ya kuwaengua wagombea wengine watakaojitokeza kwa hoja kuwa "safari hii tuwaachie wanawake"..kuna kazi nyingi za majaribio nchini...hata uspika cheo cha nne kwa mamlaka nchini wamefanya cha majaribio .........lakini kwamwe URAIS wa majaribio kwa miaka 10 mingine ..HAPANA!!
 
Kwenye bold kweli mmejipanga kama mtoa hoja alivyosema(sio kawaida yenu), lakini ni ndoto kusema eti kambi mbili za mahasimu zinamkubali hiyo labda jaribu kuja vingine tifu tifu lenyewe bado ndiyo linatoa vumbi wewe unakuja na conclusion hapana.

On the red: What makes you say kambi mbili ni ndoto?
 
naomba niulize, hivi miaka 50 ya kutawaliwa na wanaume kwa maana ya kujitawala, na miaka 100 ya kutawaliwa na wanaume kwa maana ya tukijumlisha na enzi za ukoloni kuna jambo gani kubwa sana la kuonesha?

Hivi watu mnajua kuwa mwaka 1961, sisi tanzania, south korea, singapore, dubai, malaysia tulikua ni nchi zinazofanana kiuchumi. Hao wanaume wamefanya nini kwa kipindi chote hicho cha miaka 50 mpaka wenzetu wakapaa kiuchumi, sisi tumebaki tunamark time tu?... Binafsi simfahamu vizuri, ila napinga kumdisqualify mtu just because ya jinsia yake alone.

kumbe tunadandia ajenda za watu.....
 
Naomba niulize, hivi miaka 50 ya kutawaliwa na wanaume kwa maana ya kujitawala, na miaka 100 ya kutawaliwa na wanaume kwa maana ya tukijumlisha na enzi za ukoloni kuna jambo gani kubwa sana la kuonesha?

Hivi watu mnajua kuwa mwaka 1961, sisi Tanzania, South Korea, Singapore, Dubai, Malaysia tulikua ni nchi zinazofanana kiuchumi. Hao wanaume wamefanya nini kwa kipindi chote hicho cha miaka 50 mpaka wenzetu wakapaa kiuchumi, sisi tumebaki tunamark time tu?... Binafsi simfahamu vizuri, ila napinga kumdisqualify mtu just because ya jinsia yake alone.
Na pia huwezi kumpa mtu sifa ya Kutawala kwa sababu ni mwanamke.
.
Kisha huwezi kutupa nchi hata moja ilofanikiwa kwa sababu kiongozi wake ni mwanamke, nadhani hapa ndipo tunapokosea kupinga kitu, kisha ukatumia sababu hizo hizo kupitisha kingine. Asha Rose Migiro hana sifa yoyote ya Uongozi zaidi ya kuwa ametengenezwa na kujulikana sana toka ujio wa JK na alikuwa mtu wa karibu...
 
hii nchi tutampa MAGUFULI ..Tosha.....hatutaki majaribio hapa!....tunahitaji rais mkali na madhubuti!

TUnazo taarifa za siri za ASHA ROSE projec ...na ziara zake za kujipitisha tunazielewa>>
 
Mkuu Mkandara huwa unanishangaza sana ukitumia derogatory names kwa watu!

Naamini unajua utaifa wa Ban Ki Moon kama ulitaka urejelee utaifa wake hukuwa na sababu ya kumwita "macho madogo"

Mtendee mwenzako kile unachopenda wewe kutendewa, sidhani Kama yupo atakae furahi Migiro akiitwa "ngozi nyeusi" kwa mfano
Mkuu wangu mimi Mtanzania na nazungumza na Watanzania. Siwezi kuiga ya wazungu kutaka kuleta au kupangiwa jinsi ya kusema. Mzungu akiniiita mimi ngozi nyeusi sina tatizo hata kidogo na wanafanya hivyo..maadam yeye atakubali nikimwita ngozi nyeupe. Wachina tunawaita macho madogo pale tunapozungumzia maswala yanayochukiza. I don't like the guy ni Kibaraka, hivyo matumizi yangu ktk vitu hivi yanatokana na Utanzania wangu. Jinsi nilivyokua kiasi kwamba naweza kumwita JK - m.k.w.e.r.e iwe maana mbaya kwenu lakini isiwe na maana mbaya mimi kuitwa Mkerewe!

Na tazama hata hapa JF ukiandika kabila la rais ni tusi lakini sio la Mbowe au Mkandara! Hata hivyo nadhani umeona sehemu nyingi sana najivunia Ukerewe wangu jambo ambalo sijawahi kukuona wewe ukijisifia kwa kabila ama rangi yako isipokuwa ni ile inferiority complex inawafunga akili..
 
Mkuu wangu mimi Mtanzania na nazungumza na Watanzania. Siwezi kuiga ya wazungu kutaka kuleta au kupangiwa jinsi ya kusema. Mzungu akiniiita mimi ngozi nyeusi sina tatizo kwani hata kidogo maadam yeye atakubali nikimwita ngozi nyeupe. Wachina tunawaita macho madogo pale tunapozungumzia maswala yanayochukiza. I don't like the guy ni Kibaraka, hivyo matumizi yangu ktk vitu hivi yanatokana na Utanzania wangu. Jinsi nilivyokua kiasi kwamba naweza kumwita JK m.k.w.e.r.e iwe maana mbaya kwenu lakini isiwe na maana mbaya mimi kuitwa Mkerewe!

Na tazama hata hapa JF ukiandika kabila la rais ni tusi lakini sio la Mbowe au Mkandara! Hata hivyo nadhani umeona sehemu nyingi sana najivunia Ukerewe wangu jambo ambalo sijawahi kukuona wewe ukijisifia kwa kabila ama rangi yako isipokuwa ni ile inferiority complex inawafunga akili..

To keep the record straight, Ban Ki Moon is not Chinese, he is Korean, South Korea by nationality

Kwa ufupi ni kuwa unahalalisha udhalilishaji wa maumbile ya watu kwa kutumia karata ya Utanzania wako.

Umeeleweka. Kumbuka tu unachofundisha wengine pia ni kuendelea kudharau/bagua wengine kwa visingizio kama hivyo vya Utanzania, Ukabila, Ukanda, Udini,n.k

Hiyo ya kuwa wewe unajisifia kabila lako wengine hawajinadi rangi zao au kabila hapa JF is totally beside the point of discussion here.
 
Mkuu wangu uitaka haya ya South Korea nenda CNN au BBC tupo Jamii forums hapa. Watanzania wote tunawaita jamii hiyo Wachina awe Mkorea, M Laos au Vietnam wote ni asili moja ya WACHINA... Nahalalisha kitu gani? mbona huelewi wewe! dah wewe na huyo Moon kuna kipi kinaendelea..Hii ni sehemu yetu sisi watanzania na tutatumia lugha zetu kwa jinsi tunavyojisikia hakuna mtu wa kunichagulia maneno...Siwatukani ndivyo walivyoumbwa na macho madogo, na ni moja ya kitambulisho chao! kama vile sisi wabantu wenye mipua mikubwa ukisema ni tusi lakini tukisifiwa ukubwa wa sehemu za siri inakubalika..(samahani lakini) -Acha kujishusha mkuu wangu.
 
Rekebisha hapo penye bold --Hebu sema ni kwanini muda bado? 50 yrs ya uongozi wa wanaume umetuletea nini?

Wanawake nao wana haki kushiriki uongozi katika ngazi yoyote. Huenda hata ufisadi ukapungua pale tutakapoongeza wanawake kwenye uongozi. Nikisema hivi sina maana kumshabikia ARM bali napinga hiyo kauli kwenye bold. Mwisho wa siku watanzania ndio wataamua wenyewe.
ukweli ni kwamba muda wa kuongozwa na mwanamke umefika lakini Asha Mtengeti sio mwenyewe

Wajipange upya

Nchi si sawa dawati la UN
 
Mkuu wangu uitaka haya ya South Korea nenda CNN au BBC tupo Jamii forums hapa. Watanzania wote tunawaita jamii hiyo Wachina awe Mkorea, M Laos au Vietnam wote ni asili moja ya WACHINA... Nahalalisha kitu gani? mbona huelewi wewe! dah wewe na huyo Moon kuna kipi kinaendelea..Hii ni sehemu yetu sisi watanzania na tutatumia lugha zetu kwa jinsi tunavyojisikia hakuna mtu wa kunichagulia maneno...Siwatukani ndivyo walivyoumbwa na macho madogo, na ni moja ya kitambulisho chao! kama vile sisi wabantu wenye mipua mikubwa ukisema ni tusi lakini tukisifiwa ukubwa wa sehemu za siri inakubalika..(samahani lakini) -Acha kujishusha mkuu wangu.

Hakuchagulii mtu maneno ya kutumia, lakini haki ile ile inayokuruhusu wewe kusema utakacho iwe tusi au si tusi, ndio ile ile inayoniruhusu mimi kutathmini na kusema kuwa ni tusi, udhalilishaji au vyenginevyo

Kwa hiyo endelea na uhuru huo nami naendelea na wangu, haijalishi kama itaonekana ni kujishusha, kwa kuwa naamini huwezi kujishusha zaidi ya kisingizio cha Utanzania kuhalalisha dharau au tusi
 
Huyu Migiro keshaonyesha uongozi kwenye nini kiasi watu wamfikirie kwenye nafasi ya uraisi? Au watu wanazuzuka kwa vile yeye ni Dr?
Mkuu nadhani watanzania tuna shida kubwa sana ya kujua kiongozi

Asha hajafanya chochote cha kustahili kuongoza nchi hii... kibaya zaidi she is out of touch

Kama shida yetu ni mwanamke.. bsi tujipange upya and if CCM pick Asha, itakua mbaya sana aisee.... she is nobody, they will have to do alot to sell this product, it is not known hapa

Nasikia role yake kule nayo inamnyima nafasi ya innovation zaidi ya kuwa kama desk officer, sijui ni kewli?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom