Dpp Kuridhia Mashtaka Dhidi Ya Vigogo Kesi Za Pccb?

Hakuna Mwenye Ubavu Wa Kuwafikisha Mahakamani Kwani Wanochunguza Na Wanochunguzwa Ni Kitu Kimoja!
 
Serikali yenye vyombo vya dola inatishwa na mafisadi na kufyata mkia!!!! Kweli hapa kuna jambo kubwa sana lililojificha.

Bubu,

Tatizo ni kwamba Rais wetu aliingia Ikulu kwa njia za kifisadi na ndiyo maana hana ubavu wa kupambana na mafisadi. Kesi nyingi zilizotajwa hapo zinatua mgongoni kwa Basil P. Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha wakati huo.

Kesi nyingi zilizotajwa hapo zinamgusa Mramba. Mramba anajua fedha za kampeni za JK zilipatikana namna gani na ndiyo maana JK hana ubavu wa kumfanya lolote. Siku Mramba akifikishwa mahakamani basi na Mkapa nae ataunganishwa kwa kuwa nae ni mshiriki wa huo uchafu. Kwa hiyo hapo Mkapa na Mramba wamejizungushia mabomu, siku mtu akiwagusa tu yatakapolipuka hakuna atakayepona.

Pinda kasema Meremeta, TANGOLD na Deep Green Finance zilikuwa zinahusiana na maswala ya UWT na JWTZ, cha kushangaza ni hapo kwamba kulikuwa na uchunguzi. Kama serikali ilijua kwamba ni ya usalama iweje wairuhusu PCCB ianze kuyachunguza? Hapo ndipo serikali ya JK inapozidi kujichanganya!
 
Tatizo linaonekana ni wengi walishirikiana katika hizi deal sasa inakuwa noma kumfunga paka kengele! za mwizi arobaini zitafika tu!!
 
Bubu,

Tatizo ni kwamba Rais wetu aliingia Ikulu kwa njia za kifisadi na ndiyo maana hana ubavu wa kupambana na mafisadi. Kesi nyingi zilizotajwa hapo zinatua mgongoni kwa Basil P. Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha wakati huo.

Kesi nyingi zilizotajwa hapo zinamgusa Mramba. Mramba anajua fedha za kampeni za JK zilipatikana namna gani na ndiyo maana JK hana ubavu wa kumfanya lolote. Siku Mramba akifikishwa mahakamani basi na Mkapa nae ataunganishwa kwa kuwa nae ni mshiriki wa huo uchafu. Kwa hiyo hapo Mkapa na Mramba wamejizungushia mabomu, siku mtu akiwagusa tu yatakapolipuka hakuna atakayepona.

Pinda kasema Meremeta, TANGOLD na Deep Green Finance zilikuwa zinahusiana na maswala ya UWT na JWTZ, cha kushangaza ni hapo kwamba kulikuwa na uchunguzi. Kama serikali ilijua kwamba ni ya usalama iweje wairuhusu PCCB ianze kuyachunguza? Hapo ndipo serikali ya JK inapozidi kujichanganya!

Tangu lini fisadi akamkamata fisadi? Wanaujua ufisadi wa JK hivyo wanasubiri waguswe tu na hapo ndipo nchi itawaka moto kama walivyosema akina Pinda, Mwanyika na Mkuu wa polisi maana ni serikali yote imejaa mafisadi. Itakuwa ni makosa makubwa kwa Watanzania kumrudisha tena JK madarakani 2010. CCM ni chama cha mafisadi hivyo sitashangaa wakimchagua tena kama mgombea wao pamoja na kuonyesha wazi kwamba hana uwezo kabisa wa kuiongoza nchi na kulinda maslahi ya Watanzania. Aliapa pale alipokuwa anaapishwa January 2006 'nitaitetea Tanzania kwa nguvu zangu zote', kumbe ulikuwa ni usanii tu!!
 
Kuna haja ya kutafuta mkakati hili mafisadi waturudishie nchi yetu wamechukua nchi ikiwa na raslimali za kutosha sasa hivi nchi imechoka kabisa. Sasa angalia baada ya kumaliza raslimimali wanaanza kuwageukia wananchi angalia kodi lukuki zinazomuandama mwananchi wa kawaida. Kuanzia umeme, usafiri, mawasiliano, nafikiri wataongeza hata kodi za kutembea kwa miguu barabarani hili kuongeza mapato nk.

Haya yote ni matunda ya ufisadi. Sasa hivi badala ya kufikiria maswala ya maendeleo kila sehemu wanazungumza ufisadi angalia hata wanafunzi kuanzia msingi, sekondari(Kumbuka ishu ya makamba) mpaka vyuo vikuu kila kukicha wanazungumzia ufisadi.

Ukienda bungeni ni ufisadi, ukienda mahospitalini wanazungumzia ufisadi.

Sasa nafikiri kwa sababu hatuna sheria ya kupambana na ufisadi, hatuna budi kuangalia swala hili kwa makini na kuwaambia wanaotuongoza kwamba baasi tunaomba mturudishie nchi yetu. Hawakupewa kuwa viongozi kwa ajili ya either kulinda wizi au kuiba. Mwisho wa siku tunashangaa kuona wakitembea tu na kuonekana kama hawajui kuwa kuna watu wamevunja sheria za nchi walizohapa kuzilinda.Mwisho wa siku viongozi tuliowaamini wataishia hata kuuza wananchi waliowachagua.

Tunaomba kama nchi yetu waliokabidhiwa imewashinda basi itisheni uchaguzi upya ili tupate viongozi wengine watakao weza kutatua matatizi yanayotukabiri kwa sasa.
 
This does not come to me as a suprise. Niliposikia Pinda ameanza kujiumauma nikajua kuna kubwa litakuwepo. Hiawezekani ofisa wa usalama wa taifa mkubwa kabisa na uwezo wake wote anaogopa mafisadi, haiwezekani hadi leo Rais ahsindwe kutoa orodha ya dawa za kulevya, hawa watu lazima wana nguvu kuliko serikali ya sasa. Inawezekana wao ndio serikalii tu serikali iseme imeshindwa wananchi tufanye kazi yetu
 
Vigogo mafisadi waitisha serikali

Waandishi Wetu Julai 16, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Kesi zao zakwama kufunguliwa

WATUHUMIWA wakubwa wa rushwa na ufisadi, wanaelezwa kupumua baada ya kufanikiwa kuwatisha viongozi na watendaji wa juu wa Serikali ili kesi dhidi yao zisitishwe, Raia Mwema imebaini.

Habari za ndani ya Serikali zinaeleza kwamba uchunguzi wa kesi kadhaa uliokuwa katika hatua za mwisho na hata zile kesi ambazo zimekamilika 'zimegonga mwamba' na watendaji huenda sasa 'wakageuziwa kibao'.

Kwa mujibu wa habari hizo, taarifa zilizovuja na kuwafikia wahusika zilipenyezwa kutoka ndani ya vyombo vya Serikali na hivyo kuwafanya watuhumiwa hao kuanza kupambana kuhakikisha wanajihami kwa nguvu zote.

"Kesi zote kubwa sasa zimegonga mwamba baada ya watendaji na viongozi wa juu wa Serikali kutishwa na watuhumiwa ambao baadhi wana mahusiano nao kikazi ama waliwahi kufanya kazi pamoja," anaeleza ofisa mmoja wa ngazi ya kati serikalini.

Na mwanasheria mmoja mwandamizi ameiambia Raia Mwema wiki hii kwamba, kwa sasa inabidi Serikali iwe makini maana watuhumiwa wameungana kuhakikisha 'wanajibu mapigo' kwa yeyote ambaye anashiriki 'kuwaangamiza'.

Imeelezwa kwamba
hata zile kesi kubwa 10 ambazo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, aliwahi kutamba kwamba ziko katika hatua nzuri, nazo hazitoweza kufikishwa mahakamani na wahusika sasa wanapumua.

Kwa mujibu wa habari hizo, watuhumiwa hao wamefanikiwa kuvivuruga hata vyombo vya dola kwa kuwagawa na kuwachafua watendaji wa vyombo hivyo na sasa wameahidi kutumia nguvu zao zote kupandikiza watu wao ndani ya vyombo hivyo, kimoja kikiwa ni TAKUKURU.

"Hivi sasa wanajitapa kwamba wataweka watu wao TAKUKURU na kwenye vyombo vingine ambavyo wanaamini kwamba kuna watendaji ambao wana nia ya kuwashughulikia, wakidai kwamba watendaji hao wametumwa kuwamaliza," anasema ofisa mwingine ndani ya Serikali aliye karibu na masuala ya kesi hizo.

Hosea alipata kunukuliwa akitangaza hadharani kwamba ofisi yake inachunguza kesi 10 kubwa za ufisadi, akisema kesi tano kati ya hizo ziko katika hatua za mwisho za kufunguliwa mashitaka akiungwa mkono na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ambaye alitaja hata kesi ambazo amekwisha kuzitolea kibali cha kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna hata kesi moja iliyofunguliwa mahakamani na baadhi ya watuhumiwa wamediriki kutamka hadharani kwamba hakuna mwenye 'ubavu' wa kuwafikisha mahakamani.

"Mwaka huu (2008) kufikia Julai tutakuwa tumekamilisha kesi tano za kwanza… hizi ni kesi za rushwa kubwa kubwa. Na tabia ya kesi za rushwa kubwa ni kwamba inakuwa na madhara makubwa kwa uchumi wa nchi, wahusika huwa ni watu wakubwa, kiasi cha rushwa kinachohusishwa ni kikubwa, eneo la uchunguzi wake huvuka mipaka ya ndani na nchi za nje, zinahusisha maandiko mengi, zinahitaji kiasi kikubwa kwa uchunguzi na huvuta hisia za jamii," alinukuliwa Hosea akisema.

Habari zilizochapishwa na vyombo vya habari zimezitaja kesi kumi zinazochunguzwa kuwa kuwa ni pamoja na ile inayohusu mradi wa mgodi wa dhahabu uliopo Kahama wa Buzwagi, kampuni tata za Meremeta, Tangold, Deep Green na Mwananchi Gold ambazo zilichota fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kesi nyingine zilizotajwa ni pamoja na ile inayohusu kampuni ya ukaguzi wa madini ya Alex Stewarts, tuhuma zinazohusu ujenzi wa majengo pacha ya BoT, mradi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, utata katika miradi ya umeme wa dharura na ununuzi wa rada ya kijeshi kutoa kampuni ya BAe Systems ya Uingereza.

Aidha ilipata kuripotiwa kwamba wanasiasa waliopata kushika nafasi za uwaziri wa fedha, walitarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni, taarifa zilizothibitishwa na maelezo ya DPP, Elieza Feleshi aliyenukuliwa akithibitisha kutoa kibali cha mashitaka kuhusiana na mmoja wa wanasiasa, hao lakini hadi sasa hakuna kesi iliyokwisha kufunguliwa mahakamani.

Miongoni mwa kesi zinazotajwa kuwa na ushahidi wa kutosha ni pamoja na ile inayoihusu kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington DC, Marekani iliyopewa kazi ya kukagua mahesabu ya makampuni ya uchimbaji dhahabu.

Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, amewahi kunukuliwa akisema kwamba chini ya mkataba wake na Serikali, kampuni hiyo inalipwa asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya dhahabu.

Dk. Slaa alisema kufuatana na barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, katika mwaka wa fedha 2005/06, Alex Stewart (Assayers) walilipwa shilingi 14,175,753,189.46 kama malipo ya ukaguzi wa mahesabu ya makampuni ya dhahabu, ijapokuwa "hakuna ripoti za ukaguzi zilizowasilishwa na wakaguzi hawa kuhusu ukaguzi uliofanywa katika mwaka 2005/06."

Akimnukuu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Dk. Slaa alisema, "hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa zabuni ya ushindani."

"Kuna taarifa za kuwapo kwa rushwa na/au ufisadi kuhusiana na mkataba kati ya Serikali na Alex Stewart Assayers. Barua pepe iliyoandikwa na Erwin Flores ambaye ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni hiyo ya Novemba 14, 2006 inamtaja mtu mmoja mwenye wadhifa wa Waziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa yeye pamoja na wenzake ambao hawakutajwa wana asilimia 12.5 za hisa kwenye kampuni hiyo na kuwa analipwa na kampuni hiyo," alisema Dk. Slaa.

Sehemu kubwa ye kesi hizo, ni mambo yaliyofanyika katika kipindi cha mwisho cha utawala wa awamu ya tatu ambayo ilijitambulisha kwa maofisa waandamizi serikalini kufanya kazi bila kujali kana kwamba walikuwa wakitarajia kuhama nchi.

Matukio kadhaa ya uhalifu kabambe miaka hiyo ya mwisho wa awamu ya tatu yanaonyesha mtiririko wa wizi wa kughushi, rushwa kabambe na maamuzi yasiyozingatia sheria, kanuni na taratibu za utendaji kazi serikalini.

Udaku.

Bubu, samahani, sio wewe, bali habari yenyewe.

Gazeti limetegemea stori za watu bila substantiation hata moja- udaku. Na hailezi hao Serikali, mpaka waogope, wametishiwa kwa bastola au unga unga ofisi za TUKUKURU!
 
Haya yanajirudia, Mwema alishawahi kusema kuwa mafisadi wameshaiteka nchi. Hatukumwelewa. Lakini naona sasa kauli yake ndio itaanza kueleweka
 
Hii kwa vyovyote vile haitakuwa habari njema kwa wale wanaodhani wenzao hawajui kazi isipokuwa wao tu!!!

Habari kamili bofya hapa

Faraja Mgwabati
Daily News; Monday,July 21, 2008 @18:01

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewasilisha majina ya vigogo watano wanaotuhumiwa kwa kashfa za ufisadi kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili washughulikiwe.

Akikanusha madai kwamba Takukuru imeshindwa kuwapata wala rushwa wakubwa, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hosea alisema kwa idadi hiyo ya kesi zilizopelekwa kwa DPP ni ishara tosha kwamba wanafanya kazi yao bila woga.

Dk. Hosea alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kufungua mafunzo kwa majaji na mahakimu kuhusu maadili katika Mahakama, yaliyofanyika Dar es Salaam. Ingawa hakutaja majina ya watuhumiwa hao wakubwa, lakini Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa Takukuru, Mary Mosha aliliambia HabariLeo kuwa watatangaza majina ya vigogo hao baada ya DPP kuthibitisha kwamba wahusika wana kesi za kujibu.

Alisema mashauri waliyoyapeleka kwa DPP, yatapitiwa na Mkurugenzi huyo wa Mashitaka na ndiye atakayesema watuhumiwa wangapi wanastahili kushitakiwa kulingana na vielelezo vya ushahidi ambavyo Takukuru
wameviwasilisha. “Wakishatuambia tutatangaza majina ya wale tutakaowapeleka mahakamani, lakini kwa sasa hatuwezi kuwaambia ni akina nani,” alisema Mosha.

Dk. Hosea alilaumu jamii kwa kuilaumu taasisi yake badala ya kuipa ushirikiano ili itimize majukumu yake vizuri. Alisema kuitupia lawama taasisi hiyo, hakutasaidia katika juhudi za kupambana na rushwa nchini. “Takukuru ipo na inafanya kazi yake vizuri tunahitaji kuungwa mkono na nyinyi waandishi na wananchi badala ya kutupiga madongo… namna hii hatuwezi kufanikiwa,” alisema Dk. Hosea.

Aliwapongeza waandishi wa habari kwa kufichua ufisadi katika jamii na akataka waendelee kufanya hivyo na waisaidie taasisi yake ili ifanikiwe kuzuia na kupambana na ufisadi. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku mbili, Mosha alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia sana baadhi ya mahakimu na watumishi wa Mahakama kwa vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa maadili.

“Malalamiko ya wananchi dhidi ya rushwa kwenye Mahakama yatakoma kama Kamati za Maadili za majaji na watumishi wa Mahakama watakapoweza kushughulikia tatizo la rushwa na ukiukwaji wa maadili,” alisema Mosha. Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Majaji, Jaji Eusebia Munuo alisema lengo la Kamati hizo ni kuwawezesha majaji na mahakimu kuwa waadilifu ili wasishawishike kupokea rushwa.

Aliwataka wananchi kutowashawishi watoa haki hao kujiingiza kwenye vitendo vya ukiukwaji wa maadili kwa kuwa kufanya hivyo hakutapunguza vita dhidi ya rushwa kwenye Mahakama. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Takukuru kwa lengo la kutoa elimu ya namna ya kuzuia rushwa na uzingatiaji wa maadili kwa majaji na mahakimu ambao ni wajumbe wa Kamati za Maadili katika mfumo wa Mahakama.
 
Nimemsikia sasa hivi Hosea ni mshenzi tuu na mimi ni Thomaso kwa hili, labda nione kweli lowasa, karamagi na mapumbaf wengine wamekamatwa tukawaona kwenye lile karandinga bovu la segerea, shukuru Mungu zimeletwa basi siku hizi. Lakini mengine yote ni sisi tunafungwa macho tusione mbele. Kwani mwataka kusema leo ndio Hosea amejua kuna rushwa kubwa za kushughulikia? wako kwenye wakati mgumu sana, na sisi tuko masikio wazi tusikie watathubutu kumtoa nani sadaka wakati huu, pia tunasubiri kuona kama huyo mwenye kutaka kutolewa sadaka atakubali hivihivi ama la? nilivyosema hapo mimi ni Thomaso, nimemwona akiongea hilo kwenye TV sasa hivi lakini "kithembe" chake kinaonyesha wazi kwamba kazidiwa na anaomba msaada kwamba yeye mwenyewe hawezi. Sio kweli, ujumla wake ni kwamba HAWEZI hata tukimsaidia maana alishasaidiwa na hakuwahi kufanya lolote tangu hapo zaidi ya kutuuza.
 
Nakubaliana na wewe AKILI MTINDI...Swali jingine la kujiuliza pia ni je kati ya hao vigogo watano...ROSTAMA AZIZI YUMO?
 
Hivi Hosea amesoma?

Hivi amefundishwa na watu gani mambo ya sheria?

Bado natafakari kutafuta group lake, Kuna mtu aliniambia amesomea ushahidi wa mazingira. sasa inakuaje hata ashindwe kukamata watu ambao ushahidi unapatikana hapa darajani manzese? badala yake akalie siasa?

Nafikiri inatakiwa asidhalilishe elimu yake kama kweli ameipata inavyotakiwa. vinginevyo tutaamini kuwa amepata elimu yake kwa njia zile zile.
 
Mwaka huu 'watauana sana', guess who is next kupotezwa............
Kana-ka-Nsungu, maneno yako yanachefua. Unasema:mwaka huu "watauana sana", guess who is next kupotezwa...! Unaongea as if wewe huhusiki, wewe ni kaburu fulani umekaa pembeni na kuwasanifu Watanzania wanapofurukuta kuiweka nchi yao sawa. "Watauana sana"! What do you think you are, a by-stander? A foreign observer without genuine feelings for us? Msiigeuze JF kuwa kijiwe kisicho na purpose, kijiwe cha kubwabwaja maneno ya umbeya tu, ubabaishaji na porojo za kupitisha muda. Nilidhani hii ni seriouas forum for information exchange, interaction and struggle for justice, equity, human dignity etc. "Mwaka huu watauana sana"! Hii ni nini kama si upuuzi! I am disappointed, Lazaros
 
Hii cheap talk inamsaidia nani?
Hii ni habari nzito inayodai michango mizito ya uchambuzi na kutaarifiana ili kupata mustakabali wa nchi yetu bayana. Nimesikitishwa na comments za Kana-ka-Nsungu na Mtanzania ambazo zinageuza serious talk tunayoendesha hapa kuwa ya utani utani tu, ya kijiweni au ile nyepesi nyepesi wanayokuwa nayo akina mama wakisukana nywele. Just imagine Kana-ka-Nsungu anasema: Mwaka huu "watauana sana", guess who is next kupotezwa ...! Mtanzania anajibu "vita vya panzi furaha kwa kunguru!" Sasa mimi nawaza, hii forum ina maana gani: kubwabwaja tu lolote au kuchangia taarifa na elimu kupata picha ya kutusaidia? Unaposema "watauana sana", who do you think you are: a by-stander, an unconcerned foreigner laughing at us Africans as we try to cleanse the shit in our midst? "Vita vya panzi furaha kwa kunguru", sasa kunguru huyo ni nani kama si kubwabwaja tu alimradi litoke? Sisi tuko katika mapambano, msituchefue! Disappointed, Lazaros
 
Hii kwa vyovyote vile haitakuwa habari njema kwa wale wanaodhani wenzao hawajui kazi isipokuwa wao tu!!!

Habari kamili bofya hapa

Faraja Mgwabati
Daily News; Monday,July 21, 2008 @18:01

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewasilisha majina ya vigogo watano wanaotuhumiwa kwa kashfa za ufisadi kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili washughulikiwe.

Akikanusha madai kwamba Takukuru imeshindwa kuwapata wala rushwa wakubwa, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hosea alisema kwa idadi hiyo ya kesi zilizopelekwa kwa DPP ni ishara tosha kwamba wanafanya kazi yao bila woga.

Dk. Hosea alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kufungua mafunzo kwa majaji na mahakimu kuhusu maadili katika Mahakama, yaliyofanyika Dar es Salaam. Ingawa hakutaja majina ya watuhumiwa hao wakubwa, lakini Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa Takukuru, Mary Mosha aliliambia HabariLeo kuwa watatangaza majina ya vigogo hao baada ya DPP kuthibitisha kwamba wahusika wana kesi za kujibu.

Alisema mashauri waliyoyapeleka kwa DPP, yatapitiwa na Mkurugenzi huyo wa Mashitaka na ndiye atakayesema watuhumiwa wangapi wanastahili kushitakiwa kulingana na vielelezo vya ushahidi ambavyo Takukuru
wameviwasilisha. “Wakishatuambia tutatangaza majina ya wale tutakaowapeleka mahakamani, lakini kwa sasa hatuwezi kuwaambia ni akina nani,” alisema Mosha.

Dk. Hosea alilaumu jamii kwa kuilaumu taasisi yake badala ya kuipa ushirikiano ili itimize majukumu yake vizuri. Alisema kuitupia lawama taasisi hiyo, hakutasaidia katika juhudi za kupambana na rushwa nchini. “Takukuru ipo na inafanya kazi yake vizuri tunahitaji kuungwa mkono na nyinyi waandishi na wananchi badala ya kutupiga madongo… namna hii hatuwezi kufanikiwa,” alisema Dk. Hosea.

Aliwapongeza waandishi wa habari kwa kufichua ufisadi katika jamii na akataka waendelee kufanya hivyo na waisaidie taasisi yake ili ifanikiwe kuzuia na kupambana na ufisadi. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku mbili, Mosha alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia sana baadhi ya mahakimu na watumishi wa Mahakama kwa vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa maadili.

“Malalamiko ya wananchi dhidi ya rushwa kwenye Mahakama yatakoma kama Kamati za Maadili za majaji na watumishi wa Mahakama watakapoweza kushughulikia tatizo la rushwa na ukiukwaji wa maadili,” alisema Mosha. Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Majaji, Jaji Eusebia Munuo alisema lengo la Kamati hizo ni kuwawezesha majaji na mahakimu kuwa waadilifu ili wasishawishike kupokea rushwa.

Aliwataka wananchi kutowashawishi watoa haki hao kujiingiza kwenye vitendo vya ukiukwaji wa maadili kwa kuwa kufanya hivyo hakutapunguza vita dhidi ya rushwa kwenye Mahakama. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Takukuru kwa lengo la kutoa elimu ya namna ya kuzuia rushwa na uzingatiaji wa maadili kwa majaji na mahakimu ambao ni wajumbe wa Kamati za Maadili katika mfumo wa Mahakama.

Hosea anataka kufa na wengi au vipi???
 
Hakuna lolote hapo! mbona watu wengine wakikutwa wanamakosa ya rushwa wanapelekwa mahakamani siyo kwa DPP? kwani Tanzania zipo gapi jamani. Sheria ya kuundwa kwa TAKUKURU may be bado haijaeleweka. iweje kabwela apelekwe mahakamani na kibosile kwa DPP? sitaki kabisa mambo ya ubaguzi.

huu ni mwendelezo wa usanii ule ule wa watuhumiwa wa madawa ya kulevia, Richmond, EPA, CIS etc.
 
Kwa wanao cite kutomshitaki Mkapa kwa sababu ya presidential immunity.

Presidential immunity ina apply kwa vitu vilivyofanywa katika presidential capacities, siyo personal capacities.

Kwa hiyo presidential immunity ina apply kwa Mkapa kama mtu atataka kumshitaki juu ya mauaji ya January 27 kule Zanzibar, kwa sababu alitoa order kama rais wa Jamhuri ya muungano citing some national security issues.

Lakini kama alichukua Kiwira Mines, in his personal capacity kama Benjamin William Mkapa wakati akiwa rais, presidential immunity hai apply kwa sababu aliyechukua Kiwira pale si President of The United Republic of Tanzania, bali ni Benjamin William Mkapa.

Kwa hiyo katika kumshtaki Mkapa kuhusu ufisadi binafsi hakuna issue ya Presidential immunity.

Well said Pundit!
 
Nimemsikia sasa hivi Hosea ni mshenzi tuu na mimi ni Thomaso kwa hili, labda nione kweli lowasa, karamagi na mapumbaf wengine wamekamatwa tukawaona kwenye lile karandinga bovu la segerea, shukuru Mungu zimeletwa basi siku hizi. Lakini mengine yote ni sisi tunafungwa macho tusione mbele. Kwani mwataka kusema leo ndio Hosea amejua kuna rushwa kubwa za kushughulikia? wako kwenye wakati mgumu sana, na sisi tuko masikio wazi tusikie watathubutu kumtoa nani sadaka wakati huu, pia tunasubiri kuona kama huyo mwenye kutaka kutolewa sadaka atakubali hivihivi ama la? nilivyosema hapo mimi ni Thomaso, nimemwona akiongea hilo kwenye TV sasa hivi lakini "kithembe" chake kinaonyesha wazi kwamba kazidiwa na anaomba msaada kwamba yeye mwenyewe hawezi. Sio kweli, ujumla wake ni kwamba HAWEZI hata tukimsaidia maana alishasaidiwa na hakuwahi kufanya lolote tangu hapo zaidi ya kutuuza.

Yaani wanachotafuta hapa ni kwenda kuwasafisha mafisadi mahakamani. Hawako-serious hawa, lao ni moja.

Hakianani... wasipowahukumu kifungo cha maisha hawa mafisadi basi wajiandae kuona watanzania wakiifanya hiyo kazi kivyao. Watanzania wengi wanakufa hospitalini kwa kukosa huduma kwa sababu ya haya mafisadi. Hatutakubali mpaka kieleweke.
 
Kana-ka-Nsungu, maneno yako yanachefua. Unasema:mwaka huu "watauana sana", guess who is next kupotezwa...! Unaongea as if wewe huhusiki, wewe ni kaburu fulani umekaa pembeni na kuwasanifu Watanzania wanapofurukuta kuiweka nchi yao sawa. "Watauana sana"! What do you think you are, a by-stander? A foreign observer without genuine feelings for us? Msiigeuze JF kuwa kijiwe kisicho na purpose, kijiwe cha kubwabwaja maneno ya umbeya tu, ubabaishaji na porojo za kupitisha muda. Nilidhani hii ni seriouas forum for information exchange, interaction and struggle for justice, equity, human dignity etc. "Mwaka huu watauana sana"! Hii ni nini kama si upuuzi! I am disappointed, Lazaros

Lazaro simtindi,

Nadhani hujamwelewa Kana-ka-Nsungu. Kwa maoni yangu, anaposena mwaka huu watauana sana anamaanisha watapelekana sana kutibiwa katika hospitali za ughaibuni kisha watutangazie fulani kafariki alihali u hai!. Rejea kifo cha Balali na utata wake. Hapo upo mkuu??
 
Back
Top Bottom