Dpp Kuridhia Mashtaka Dhidi Ya Vigogo Kesi Za Pccb?

Nalaila Kiula-chamga la macho
Dr Mlingwa-changa la macho
Prof C Mahalu- changa la macho
Brother Ditto-changa la macho
Na hawa nao-changa la macho
Kwa vyovyote hao wamelazimishwa na Donors na kweli tusitegemee kipya at the end will be braaabraaaabraaaaaa
 
Niliwahi kuweka thread moja hapa kuhusu Mkapa lakini watu hawakuitilia maanani. Nilionyesha jinsi ambavyo Mkapa alivyoshirikiana na Yona kuibia Serikali kwa kujibinafsishia kampuni. Katika hiyo thread nilisisitiza kuwa Mh. Kikwete hasiangalie sura za watu au viuno vyao bali kutenda kazi yake sawasawa kwa mujibu wa sheria. Katika sheria ya Tanzania na baadhi ya nchi, hakuna mtu aliye juu ya sheria. Linapokuja suala la prosecution kwa uvunjaji wa sheria kusiwepo Double Standard kwa upande wowote. Sasa iweje serikali iandae mashitaka juu ya Mramba na Yona na kumuacha Mkapa????? This is Bull Craps. Haki sawa kwa wote, hakuna tofauti ya Rais mwizi na Mwanakijiji mwizi, wote ni wezi mbele ya sheria. Kwa hiyo wote waadhibiwe kwa mujibu wa sheria. Hizi sheria ambazo zimepitwa na wakati lazima ziondolewe. Kama zisipoondolewa nani atamshitaki JK kama na yeye akifuata sera za Mkapa kama atapata kipindi cha PILI????????
 
kama kweli jk anataka kumrithi nyerere na kama anataka watanzania wamsamehe basi afanye kweli ktk kuwashtaki hawa wakuu wa mafisadi maana hawa watu kwa sasa ni chukizo kuu kwa watanzania maana walitufanyia kitu kibaya mno na mungu ndiye anayejua mpaka yule mzee wetu wa south mandela alichukia mno maana nanukuu maneno aliyomuambia bwm "HIVI KWELI KAMA BABA YAKO NYERERE ANGEKUWA HAI UNGEWAFANYIA WATANZANIA MAMBO HAYA!!!NA UTALAANIKA KWA HAYA UNAYOYAFANYA"misho wa kunukuu. na laana yenyewe ndiyo hii inaaza taratiiibu
 
Wanaopaswa kuwawajibisha mafisadi walikuwepo serikalini katika kipindi nchi ikivunwa, waliyafumbia macho na au walinufaika kwa namna moja au nyingine. Kuwashtaki wazito kama BP, YN na BWM sio Tanzania ya sasa ambapo hata viongozi wanaofisadi vyama kama vya mpira tu tunashindwa kuwachukulia hatua. Kiongozi asiyemkubwa sana anaua hadharani na hazichukuliwi hatua stahili, Tume ya kuwajibisha wahusika pale EPA inaundwa na watuhumiwa wa Richmond nk, na wahanga wa ufisadi yaani Watanzania wakijipanga barabarani mchana wa jua kali na vumbi zito kuwashangilia mafisadi wakipita kwenye carpet jekundu walilowatandikia!

Meno hamna, mfupa wa nini? Si bora Uji!
 
kama kweli jk anataka kumrithi nyerere na kama anataka watanzania wamsamehe basi afanye kweli ktk kuwashtaki hawa wakuu wa mafisadi maana hawa watu kwa sasa ni chukizo kuu kwa watanzania maana walitufanyia kitu kibaya mno na mungu ndiye anayejua mpaka yule mzee wetu wa south mandela alichukia mno maana nanukuu maneno aliyomuambia bwm "HIVI KWELI KAMA BABA YAKO NYERERE ANGEKUWA HAI UNGEWAFANYIA WATANZANIA MAMBO HAYA!!!NA UTALAANIKA KWA HAYA UNAYOYAFANYA"misho wa kunukuu. na laana yenyewe ndiyo hii inaaza taratiiibu

Major,
Hii ya Mandela sijawahi kuisikia....ni wapi na ni lini ilitokea?? Tufahamishane, kwani ni moja ya pointi muhimu kuonyesha ubadhirifu uliokithiri, na jinsi Muungwana asivyo pamoja na watanzania kwa kumlea hichi kidudu kibaya sana....
 
Lets be serious!!Hakuna anayeweza kumshitaki Yona wala Mramba, Serikali ina wenyewe na wenyewe ndio hao tuliowataja. Sasa ndugu zangu watawezaje kumshitaki waziri aliyetumwa na Rais bila ya kumshitaki Rais mwenyewe? Mkapa will never have a day in court, and so is yona and Mramba. Beside J.K made it clear on friday in Butiama kwamba waliojichotea mali za uwa hawata taifishiwa mali zao. Yani kwa kifupi ni RUKSA kuwa fisadi kama upo tayari kula hiyo keki ya kifisadi na chama. Kidumu Chama Cha Mapinduzi..
 
Mramba kalamba kila kitu B.OT na amewekeza kwenye mradi wao wa PRECISSION AIRLINE.
ni mali ya mramba na mama MKAPA.
 
Bila kupotoshana, Precision Airlines ni mradi wa Bw. Michael Shirima...mjasirimali mwenye kujituma tangu alipoanzisha hii kampuni kule Arusha miaka ya 1990. Ni mrombo kama Mramba lakini sidhani huu ni mradi wa Mramba na mama Mkapa.

Kinachoniuma wandugu ni kuwa, Mkapa anapata kinga wakati wamachinga wenzake wanaojaribu kupata mkate wa kila siku wanadhalilishwa na mgambo kwa kuvuliwa nguo na mali zao kuporwa. Mnakumbuka sentensi ya mwisho kwenye riwaya ya Shafi Adam Shafi iitwayo "Kuli"? Sentensi hiyo ilisema "yana mwisho haya"!!!!
 
Mkapa, it is only a matter of time, atatinga tu mahakamani na wengine wote hawa, mimi ningekuwa wao ningeanza kujitayarisha either kwa kuzirudisha hela za wizi, au kukimbia nchi!
 
Bila kupotoshana, Precision Airlines ni mradi wa Bw. Michael Shirima...mjasirimali mwenye kujituma tangu alipoanzisha hii kampuni kule Arusha miaka ya 1990. Ni mrombo kama Mramba lakini sidhani huu ni mradi wa Mramba na mama Mkapa.

!!!

Sipendi kuongelea mambo ya ndani ya watu, lakini shares za precision hao watajwa hapo juu wote wanazimiliki.
 
Mkapa, it is only a matter of time, atatinga tu mahakamani na wengine wote hawa, mimi ningekuwa wao ningeanza kujitayarisha either kwa kuzirudisha hela za wizi, au kukimbia nchi!

Mkuu nakuomba sana ufute kauli yako maana humu ndani tunakuheshimu kwa maono na facts za nchi yetu; Unadhani ujio wa Bush ulikuwa kitu kidogo eti? Tanzania is similar to America,when u're off from the office like Jumba jeupe unaingia ktk kundi la watu watakatifu waliowahi kutokea ktk nchi ile. JK knows and u know it 100% kuwa hana cha kujibu mahakamani na kama ilivyokuwa kwa Mwinyi,Julius ,Kawawa,Msuya and malecela. Ukiacha Mkapa unataka tuamini hawa wote walikuwa watu safi 100% na kwanini wasipelekwe mahakamani hata kama wamekufa?
Tunakuheshimu kaka na tusingependa kukuona nawe unaingia ktk group ya wasabato wale wa Kyela.Unayao haki ya kumchukia huyu mzee Ben lakini sidhani kama unajitendea haki kwa kubainisha yasiyowezekana ilihali rohoni mwako unajua ukweli kaka.
Heshima mbele.
 
Mkuu nakuomba sana ufute kauli yako maana humu ndani tunakuheshimu kwa maono na facts za nchi yetu; Unadhani ujio wa Bush ulikuwa kitu kidogo eti? Tanzania is similar to America,when u're off from the office like Jumba jeupe unaingia ktk kundi la watu watakatifu waliowahi kutokea ktk nchi ile. JK knows and u know it 100% kuwa hana cha kujibu mahakamani na kama ilivyokuwa kwa Mwinyi,Julius ,Kawawa,Msuya and malecela. Ukiacha Mkapa unataka tuamini hawa wote walikuwa watu safi 100% na kwanini wasipelekwe mahakamani hata kama wamekufa?
Tunakuheshimu kaka na tusingependa kukuona nawe unaingia ktk group ya wasabato wale wa Kyela.Unayao haki ya kumchukia huyu mzee Ben lakini sidhani kama unajitendea haki kwa kubainisha yasiyowezekana ilihali rohoni mwako unajua ukweli kaka.
Heshima mbele.[/
SIZE]


I mean this is something, mkuu vipi inaonekana usingependa nisimguse Mkapa, maana hii sio mara ya kwanza ninatoa maoni yangu wewe unajaribu kuyasogeza kwenye personal, mkuu I have nothing personal na mkapa, isipokuwa ni taifa tu, hao viongozi uliowataja vipi ukisema uovu wao, maana wa Mkapa sikuusema mimi si unajua kuwa umesemwa kwanza na magazeti ya rafiki yake mpenzi Mengi, na baadaye yamesemwa na kila kona ya nchi yetu, sasa mkuu iweje unirukie mimi?

Aliyetoa hii mada mbona hujamgusa? Na waliotangulia wote mbona hukuwagusa mkuu, why me bro? Kwa hiyo unataka nisitoe maoni yangu kwenye ishus za Mkapa, maana hii sio mara ya kwanza mkuu! Hivi ni nani aliyetegemea kuwa lowassa atatoka u-PM? I mean mkuu nina heshima sana na michango yako hapa JF ila never did I expected this kutoka kwako, maana this is low, eti unashauri nifute kauli yangu ya kutabiri one day sheria kufuata mkondo wake on the charges anazoshutumiwa mkapa? are you serious au unatania mkuu?

Mkuu hiii sio saaa ya kutishana tena, hiii ni saaa ya mabadiliko, tuhuma zote za Mkapa unazijua, basi angalau ungezipinga badala ya kunitishia na vitisho uchwara, hao viongozi uliowataja kina Msuya, Kawawa, Malecela, kama wameiba na unajua si useme mkuu, mimi ninaongelea ya mkapa yaliyosemwa na taifa zima mkuu na kila mwananchi anajua, sasa kama unaaamini kuwa ya yeye hawezi kushitakiwa na hayatawezekana then kwa nini una problem na utabiri wangu kuwa iko siku atatinga mahakamani?

Mkuu unasema maneno ya wasabato wa wapi? What that has anything to do na tuhuma za wizi wa Mkapa? mkuu I am not so sorry kama Mkapa anakuhusu, lakini I have nothing to na yeye personally, ulishwahi kushauri huko nyuma maneno kama haya kuwa ninamchukia, hapana mkuu hujui jinsi nilivyokuwa ninamtetea huko nyuma hasa BCS, mpaka nilipokuja kugundua ujanja wake mwingi ndio nikabadilika, lakini it is up to you kuamini unachotaka, sina tatizo lolote na Mkapa, isipokuwa ni taifa tuu,

sasa ninarudia kuwa ninaaamini kuwa iko siku yeye na mafisadi wenziwe watatinga mahakamani tena sio hata mbali sana kabla haijatokea, maana kabla muungwana hajaingia urais ilikuwa inajulikana na wale wote tunaomjua muungwana na kampeni zake kuwa hiyo ilikuwa agenda yake namba moja, na pili ilikuwa kurudisha nyumba za serikali zilizouzwa na Mkapa, sasa mkuu naomba uniweke kwenye hilo kundi lako la sabato kama ulivyoahidi, na from now acha kuniaminia na mawazo yangu hapa JF, lakini ninajua for a fact kuwa hata mr.Zero wakati wa uchaguzi in private alikuwa akilalamika kuwa muungwana akipewa atawafunga yeye na Mkapa, unafikiri ni kwa nini alikuwa akisema hivyo?.

Ahsante Mkuu!
 
KATIKA BIBLIA IMEANDIKWA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI,
KWAHIYO WATAKULI WALICHOPANDA,ILA WATU MUNGU AWASAMEHE,MAANA BORA MUNGU AKUSAMEHE MAANA MUNGU NDIO ANAIWEZA ROHO MWANA DAMU ANAWEZA MWILI,WAZEE MATUNDA HAYO.
 
"Field Marshal ES"na from now acha kuniaminia na mawazo yangu hapa JF
Mkuu point noted ninadumu ktk subira ila JK asipomfikisha mahakamani nitakuomba tena utuombe radhi hata kama kwa sasa hupendi kukwezwa kwa uhodari wa hoja na vyanzo; Leo naongeza hilo la "maana kabla muungwana hajaingia urais ilikuwa inajulikana na wale wote tunaomjua muungwana na kampeni zake kuwa hiyo ilikuwa agenda yake namba moja, na pili ilikuwa kurudisha nyumba za serikali zilizouzwa na Mkapa, sasa mkuu naomba uniweke kwenye hilo kundi lako la sabato kama ulivyoahidi,"" lakini ninajua for a fact kuwa hata mr.Zero wakati wa uchaguzi in private alikuwa akilalamika kuwa muungwana akipewa atawafunga yeye na Mkapa, unafikiri ni kwa nini alikuwa akisema hivyo?.
" Kaka yangu binafsi naamini ktk haki,sheria na kuheshimiana. Sina uwezo wa kukutishia na si mtu wa namna hiyo,sina undugu na Mkapa wala familia yake,sana sana kinachonisukuma hapa ni kurejea kwangu kwa historia ya nchi yetu, kuna siku nilikuwa na mzee mmoja akawa ananipa historia za watawala wetu, yeye anakiri kuwa Julius alikuwa misimamo yake ambayo ilitegemea sana baadhi ya watu aliowaamini yeye na matokeo yake ni kwamba 1985 alipoondoka aliiacha nchi iko bankrupty na anasema ni ukweli hakukuwa na kitu hazina ila alimuomba Bob Mugabe ambaye alitupatia 10m $ ili mzee mwinyi aanze kazi lakini haikuwa kitu kwani tulikuwa hoi na pumzi ya uchumi ilikuwa kwa mirija O2,kuna mengi ambayo yalijitokeza kutokana na hali hiyo na Mwinyi alipofanya mabadiliko yake yaligundulika madudu mengi ambayo mzee aliamua kuyanyamazia ingawaje kuna hatua zilizochukuliwa zilizoonyesha Mwinyi kukosa imani na Mtangulizi wake kama vile kung'oka kwa Apiyo na watu wa aina yake pale state house na serikalini.
Ally alipoondoka Mkapa alipokea nchi ikiwa choka mbaya lakini tayari ina muamuko wa kijasilimali huko ghalani alikokuwa JK kulikuwa hovyo na pia serikali ni kama ilikuwa likizo,urithi mkubwa aliouacha mzee mwinyi ni umma wenye tumaini la kujikwamua na umaskini hata wa mavazi na lishe-ya ndani yalikuwepo na Warioba alithubutu kunyoshea vidole watu Mkapa akafunika komne na mwanaharamu akapita,mzee anasema hawa waliomtangulia Mkapa hawakuiacha nchi vizuri kiuchumi na serikali ila walichafuliwa na watu waliowaamini sana ktk usaidizi, Mkapa yeye kaiacha nchi ikiwa na angalau na sura ya kiuchumi na utawala na hata hapo hazina wanakubali aliacha mapesa mengi sana licha ya mengine kumegwa ki-EPA epa tatizo ni involvement zake ktk ujasiliamali akiwa madarakani na kukubali kwake kuwa blackmailed na warithi wake ktk nchi.

Kwahiyo alinieleza kuwa Muungwana anafahamu ya Ben lakini pia yeye anajifahamu na kwamba Ben anafahamu yaliyojiri na kutambua kuwa JK ni mwenye nchi,mzee ameeleza kuwa JK na wenziwe wanafahamu kuwa kuna Mkapa's safi na wana uwezo wa kuichukua nchi baada ya yeye kuondoka ,akaniuliza kama watamdhalilisha mahakamani zaidi ya haya ktk magazeti na vijibarazani hawa wafuasi wake watakubali? Nikasema hapana akasema ,ndiyo kwani si rahisi nchi kutawalika kwa wewe kumsakama aliyekuachia madaraka na ukaacha kuishi na kuongoza kwa maono yako na si kuangalia ya nyuma.JK knows that na anafahamu kazi ya Mengi na washirika wake dhidi ya Mkapa imedumu kwa 2 yrs now but watu wamenyamaza kimya,si kama wanafurahia kusoma habari za huyo mzee ila sasa wanajiuliza iweje kila story izunguke imrudie Mkapa au Mengi analipa fadhira kwa Mwinyi pale automatically alipokuwa oustsmarted presidentially na Mkapa ? Watu wanajiuliza sana why Mengi's magazeti? Is it Kilimanjaro Hotel? Masilingi? Nassaco building au nini? NBC au nini? Is it Mwinyi? Or Msuya 1995 race? Ni mengi kaka yangu tunayojiuliza na tungependa sana kufahamu hawa wanaoimba wimbo Mkapa nao tuwafahamu kama hoja ni uzalendo au chini ya kapeti.
Nami naungana na mzee huyu ambaye anashauri na kuelimisha,Msimamo wangu juu Mkapa unasimama ktk ustaafu wake -Ni kweli apumzike lakini kama lipo jambo kama tunavyosikia basi wasaa umefika kuangalia na upande wa pili wa shilingi.Mkuu ,Daima heshima mbele.
 
This time heshima zaidi kwako, angalau umeweka hoja, binafsi I have nothing to na naything zaidi tu ya kukata ishus, ninatabiri mengi sana humu kuna yanayotokea na kuna yasiyotokea ndio maana ya utabiri hasa wa kisiasa,

ukitaka kumsafisha mkapa, unakaribishwa, lakini kunishambulia mimi ambaye nina-react tu kwa ninayoyasoma na kuyafahamu hukunifanyia haki mkuu, Mkapa kama alihusika na ubadhirifu wa mali za taifa letu ninakuhakikishia kuwa iko siku atatinga tu mahakamani na sio yeye peke yake, wote wanatuhumiwa that is my prediction, ukitaka kuni-attack personal just go ahead mkuu, lakini ni haki yangu kama ilivyo yako kutoa maoni kuhusiana na ishu at hand, in the future vipi uki-stick na hoja kwenye ishu kama ulivyofanya this time itakuwa ni bora kwa wananchi wote hapa JF, kulikom personal attack against someone usiyemjue, au?
 
Jamani,

Why shoudl we go on speculating issues wakati vyombo na watu wa kutatua mafumbo haya wapo?Ni swala la bunge tu kuamua sasa no presidential immunity kwa marais matapeli,they remove the immunity and let the law take its course.

Vinginevyo inakuwa sawa tu na minong'ono ya "ghahwa" kwani kila mtu atakuja anadai yeye data zake ndo zina nguvu zaidi.
 
Posted Date::5/31/2008
Mwendesha Mashtaka akamilisha uchunguzi kuhusu Basil Mramba

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

UCHUNGUZI dhidi ya tuhuma za ufisadi dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya tatu, Basil Mramba, umechukua sura mpya, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Eliezer Feleshi kukamilisha kazi yake.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tayari jalada la uchunguzi huo limesharejeshwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa ajili ya kufanyika kazi zaidi.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa, Mramba anachunguzwa kutokana na tuhuma za ufisadi katika misamaha ya kodi ambayo ilitolewa kwa mabilioni ya shilingi kwa wafanyabiashara katika mazingira tata.

Feleshi alilithibitishia Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalumu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa jalada la kesi hiyo lilifikishwa ofisini kwake na amemaliza kulifanyia kazi.

Alisema baada ya kumaliza kulifanyia kazi amewakabidhi Takukuru kwa ajili ya kulifanyia kazi zaidi.

"Tumelirudisha kwao ndiyo wanaojua ambacho wanaendelea nacho, kwa hiyo nini kinafanyika ni bora muwaulize wao," alisema Feleshi.

Alipoulizwa kama ofisi yake imetoa maelekezo ya kufunguliwa mashtaka au kulifanyia kazi zaidi jalada hilo, alisema kwa kawaida taratibu zao haziruhusu kueleza nini ofisi hiyo imeandika katika jalada la uchunguzi.

Feleshi aliongeza kwamba, Takukuru ambao ndiyo wanaochunguza tuhuma hizo ndiyo wenye mamlaka ya kueleza hatua iliyofikiwa.

Mkurugenzi huyo alifafanua kwamba, taratibu za kiutendaji haziruhusu kueleza nini ambacho ofisi hiyo imeandika kwenda kwa mhusika.

Alisema taratibu zote zinazofanyika ikiwamo kama ni mashtaka, mhusika pia anapaswa kupewa taarifa.

"Hakuna kitu kinafanyika kwa siri, hata mhusika (mtuhumiwa) lazima awe anapewa taarifa za mchakato," alisisitiza Feleshi.

Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini zaidi kwamba kuna mipango mbalimbali ya chini kwa chini, inayofanywa na serikali ya kutaka kuwafikisha mahakamani baadhi ya vigogo nchini kwa tuhuma za ufisadi.

Taarifa kutoka ndani ya serikali zinaeleza kwamba, majalada mbalimbali ya uchunguzi yameanza kupelekwa katika ofisi ya DPP.

Alipoulizwa taarifa za majalada ya baadhi ya vigogo wengine kuchunguzwa na kupelekwa ofisini hapo, alisema wingi wa majalada katika ofisi hiyo ni kitu cha kawaida.

Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Lilian Mashaka, alisema pamoja na taarifa hizo kuwa za kweli, hawezi kusema chochote kwa kuwa sio msemaji wa taasisi.

Alishauri gazeti hili kuwasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hosea, kwa maelezo ya kina kuhusiana na suala hilo.

Kauli ya Mashaka ilirudiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa taasisi hiyo, Alex Mfungo, aliyesema kuwa taasisi hiyo ina taratibu zake katika kutoa taarifa na kwamba mkurugenzi mkuu ndiye msemaji.

"Nyie mkitaka taarifa hizo njooni ofisini, mfuate utaratibu, sio kila mtu anasema kila kitu. Msemaji wa taasisi ni mmoja tu," alisema Mfungo.

Hata hivyo, Dk Hosea hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, baada ya simu yake ya mkononi kuita mara kadhaa bila kupokelewa.

Kwa upande wake, Mramba alipotafutwa kwa njia ya simu jana kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kuhusiana na suala hilo, alisema hawezi kuzungumzia mambo yaliyopo katika ofisi za watu wengine bila kufafanua zaidi.

Ikiwa mwanasiasa huyo atafikishwa mahakamani, itakuwa ni mara ya pili kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwashtaki watendaji wake wa zamani ikianzia na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, anayeendelea kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Profesa Mahalu anatuhumiwa kuiibia Serikali Sh 2 bilioni kutokana na kuongeza bei wakati wa mchakato wa ununuzi wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania, mjini Rome.

Pia kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa rasmi kwamba, serikali iko mbioni kuwashtaki watu wanaotajwa kuhusika katika wizi wa mabilioni ya fedha za umma, katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wale waliohusika kuipa zabuni kwa upendeleo Kampuni hewa ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development LLC.

Rais Kikwete alimuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kuongoza timu ya wataalamu akisaidiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema na Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hosea kuchunguza na kuwashtaki watu ambao watabainika kuhusika na wizi wa Sh 133 bilioni kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika BoT.
 
Hurray! kwa mbali mwanga wa mapambazuko waanza kujitokeza taratibu na kuleta marumaini mapya kwa watanzania, wafikishwe maakamani tuone uzalendo wa majaji kwa mafisadi wanaomaliza nchi yetu.
 
Back
Top Bottom