DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?

Hakika mkuu, ila serekali isikae kimya itoe ufafanuzi


 
Lengo la mama ni zuri lakufanya bandari yetu ifanye kazi kwa manufaa ya watanzania wote na sisi wanainchi wakawaida tunaomba wale wenye profetiona zao za sheria washirikishwe kwa kiwango kikubwa kuepusha sintofahamu iliyotanda.
Anayetakiwa kuwashirikisha ni nani waziri Mkuu au spika au waandishi wa habari
 
Duh! Sasa waliofuata hawakujifunza kutokana na hili na Bungee letu pia na Mwana Sheria wetu Mkuu ambao wengeni ni majaji. Na waandishi wetu wa habari ndio makajanja
Miaka ya nyuma Loliondo ilipigiwa kelele lakini wapi.

Wale wana hadi ka uwanja wao wa ndege.

Ukijichanganya ukaingia maeneo yao umekwisha.
Wanyama wanajichagulia na usisahau kuwa Loliondo imeungana na Serengeti na ina gate la kuingilia linaitwa Klains gate, nimepitia mara kadhaa
 
Hii nchi ukiwa mgeni ni rahisi kufikiri kwamba hao DP World watakuwa msaada sana hapo bandarini ila kimsingi kwa ambao tuna uzoefu na shuhuda za mambo yanayotokeaga ni kwamba hapo itakuwa ni mfumo wa kubadilisha walaji tu.
Yani kundi lililokuwa linanufaika linaporwa tonge wanaingia wengine kula keki kupitia mkataba na DP World. Nina hakika bila huo mkataba kuvuja hii ishu ingepigwa kimya kimya tu ni kwamba kuna mtu hakupewa mgao wake akachomesha.
😂😂😂 let's wait to see mkuu.
 
"Kwenye hili la DPW na Bandari, kiukweli kabisa, Rais Samia anastahili pongezi za dhati na sio lawama" Usipongeze sana ubora wa fundi mkuu bado panavuja tena sana.
 
Nani katika huu uzi huu anafahamu kuwa MoU 36 zilisainiwa Dubai wakati wa Expo 2020 mwaka mmoja kabla mwendazake hajaenda zake, mama Samia akasifiwa sana wakati huo kwa ushindi huo. Mpaka Mataifa ya nje yoe yakawa yanajiuliza huyu mama kaweza vipi?

Mwendazake mwenyewe alipotumiwa kopi kabla hazijasainiwa MoU akapiga simu akauliza Dada Samia, umewezaje waliposhindwa wenhgine? Hawa wajomba zako wanakuheshimu sana, hapo hapo akaongea na watu wengine huku anajisifu, sasa mlitaka nimpeleke mmakonde kwa Waarabu? akimaanisha Majaliwa? "nimempeleka Mwarabu mwenzao wanaongea lugha moja. Dah lakini wamemheshimu sana, MoU 36 siku moja? Msichelewe zipitieni haaraka wasaini, hawa Waarabu hawapendi mambo ya kuchelewachelewa.


Huyo ndiye Mama Samia na huko ndipo palipoanzia mkataba huu t-unaozungumzwa sa, huu ni Bashraf tu, mziki kamili haujaanza, ndiyo maana mama kimya, anawaona wajinga tu wanaopigapiga kelele hovyo.
 
Unaanza wapi kumpongeza Raisi kwenye hili?

Akubali kulaumiwa kama anavyokubali kupongezwa.

Mkataba huu hauna tija katika Karne hii. Zilch.
 
"Maliasili zetu Watanzania zinachukuliwa bure haya ni maajabu,sitaruhusu hilo" Hayati Rais John Pombe Magufuli.
 

Attachments

  • VID-20230715-WA0734.mp4
    9.5 MB
Back
Top Bottom