Ikimita
JF-Expert Member
- Oct 23, 2010
- 300
- 21
Valambia hajalipwa, kesi inaendelea, ilianzia kwa wakili Mkono, sasa inashikwa na Dr. Tenga. Malipo ya mawakili yameshapitiliza gharama za deni!, mind well supply ilifanyika 1978 wakati wa vita vya Kagera, more than twenty years now!, mawakili wanaendelea kulipwa!.
Kwa Dowans tutumie mkakati huo huo wa Valambia kuibakiza kesi mahakamani kwa muda mrefu mpaka jamaa wanyooshe mikoni kuwa hilo deni halilipiki. Tuache maamuzi yafanyike zaidi ya miaka 20 ijayo na kiukweli baada ya miaka 20 Tanzania itakuwa na watu wengi wanaoelewa zaidi tofauti na ilivyo sasa.