DOWANS yaibwaga TANESCO; TZ kulipa gharama na adhabu Bil. 185!

sema wewe MTANZANIA umewatakia nini DOWANS, mliwachokoza wenyewe na kusaign mikataba na mikataba ndiyo INATUUA sasa! hawana kosa makosa ni UFISADI!
 
Nitacheka nikiona viongozi wa upinzani wanaitisha mikutano ya waandishi wa habari na kutoa tamko wakiitaka "serikali kutoa maelezo"; nitacheka na kusikitika.
nakuheshimi sana mkuu sasa kitakachokuchekesha ni nini? na kitakachokusikitisha?
 
Lets say no, individually and as a nation.
Tukatae kulipa just like that tuwaambie point blank,
After all watatufanya nini? Kwani ICC inaweza kuchukua hatua yoyote (coercive) dhidi
yetu?
Tumechoka sasa, hawahawa walisema tulipe hela za IPTL, wanajua kabisa deni halijaisha na umeme hatupati na sasa wanasema tulipe za Dowans wanatuona sisi mafala sana tukikubali kampuni nyingine itenda kubai wameshaona tanzania ni shamba la bibi
 
Mitambo ile waliizuia ili wainunue kwa bei ya kutisha sasa iliposhindikana yaliyofuata yalijulikana.........Tatizo hapa hakuna atakayewajibika.............Hakukuwa na sababu ya Tanesco kuzuia mitambo ya Dowans waliokuwa na sababu walikuwa ni TRA kwa kutolipwa kodi.....................This country is run by cursed people to put it mildly............
Waombewe ili laana iwakimbie
 
Lets say no, individually and as a nation.
Tukatae kulipa just like that tuwaambie point blank,
After all watatufanya nini? Kwani ICC inaweza kuchukua hatua yoyote (coercive) dhidi
yetu?
Tumechoka sasa, hawahawa walisema tulipe hela za IPTL, wanajua kabisa deni halijaisha na umeme hatupati na sasa wanasema tulipe za Dowans wanatuona sisi mafala sana tukikubali kampuni nyingine itenda kudai wameshaona tanzania ni shamba la bibi
 
ingetumika sharia yoyote atakaethibitika kushiriki ufisadi na kuligharimu taifa apigwe mawe mpk afe kila cku watu wanatutenda tunabaki tukilialia kabla hatujanyamaza wanatutenda tena sasa tupaze sauti zetu hivi haiwezekani siku ya kusheherekea uhuru wa Tanganyika tukabeba mabango maeneo yote ya nchi kupinga ufisadi?
 
Mitambo ile waliizuia ili wainunue kwa bei ya kutisha sasa iliposhindikana yaliyofuata yalijulikana.........Tatizo hapa hakuna atakayewajibika.............Hakukuwa na sababu ya Tanesco kuzuia mitambo ya Dowans waliokuwa na sababu walikuwa ni TRA kwa kutolipwa kodi.....................This country is run by cursed people to put it mildly............

is a longterm strategy to find money for next election the fisadis have vision what to do whare and how they have united than ever mtaona meeengi tulieni UMA UTAAMUA....How mimi sijui!
 
Hii ndiyo matokeo ya kuendesha idara za serikali kupitia magazeti. The whole decision making process ya Dowans kuanzia mwanzo pmpaka mwisho ilikuwa politicized rather than technical.
 
Hili ni jambo ambalo nililiona kabla, rejea post zangu za zamani. Nilijuwa watashinda kwani Dowans hawana kosa walilofanya.

Makosa ni wehu waliokuwa wanashabikia mitambo ile isinunuliwe na serikali Dowans walipotowa offer. Hata Mh. Zitto Kabwe alipigania sana mitambo hii inunuliwe ili kuepusha kesi, gharama na mgao wa umeme.

Leo kikowapi? Mashine tumezikosa, umeme tumekosa, gharama tutazilipia kwa upuuzi wa watu wachache ambao huwa wanajisemea tu bila kuwa na mantiki.

Sasa ndio mtajuwa kuwa Dr. Rashid ni kichwa.

tutanunuaje used mkuu!
 
ingetumika sharia yoyote atakaethibitika kushiriki ufisadi na kuligharimu taifa apigwe mawe mpk afe kila cku watu wanatutenda tunabaki tukilialia kabla hatujanyamaza wanatutenda tena sasa tupaze sauti zetu hivi haiwezekani siku ya kusheherekea uhuru wa Tanganyika tukabeba mabango maeneo yote ya nchi kupinga ufisadi?


unaona umuhimu wa ile mahakama eeh
 
Nitacheka nikiona viongozi wa upinzani wanaitisha mikutano ya waandishi wa habari na kutoa tamko wakiitaka "serikali kutoa maelezo"; nitacheka na kusikitika.

swala hapa mkuu sio viongozi wa upinzani ni swala la kila mwananchi mzalendo kuihoji serekali na michezo yake ya ajabu ajabu ni jukumu la kila mtu sasa maana ni kodi zetu ndo zinahusika hapa, hayo mabilioni si yangetumika kwa huduma nyingine nyingi za kijamii? kwa nini wametufikisha hapo pa kuwalipa dowans?
 
Hivi ni nani aliyeishtaki TANESCO? Nakumbuka kuna wakati kampuni hiyo DOWANS ilikuwa kama haina mwenyewe. Yule Valambhia (Not sure of spelling) aliyekuwa anaidai serikali baada ya kusuply vifaa vya jeshi alilipwa????? Just curious?
Valambia hajalipwa, kesi inaendelea, ilianzia kwa wakili Mkono, sasa inashikwa na Dr. Tenga. Malipo ya mawakili yameshapitiliza gharama za deni!, mind well supply ilifanyika 1978 wakati wa vita vya Kagera, more than twenty years now!, mawakili wanaendelea kulipwa!.
 
Nini matokeo ya hukumu hii? Hakika bado mko nyuma sana kuelewa mipango ya mafisadi kwani kinatakiwa hasa ni kubinafsishwa kwa shirika hilo na hii ni moja ya hatua za mwanzo kulibana shirika, mwisho wa siku kama uharo itabidi tuachie mapema na salama. Mafisadi wako kazini na safari hii haponi mtu..
Mkuu Mkandara, nadhani ni maneno ya unabii!.
 
Lets say no, individually and as a nation.
Tukatae kulipa just like that tuwaambie point blank,
After all watatufanya nini? Kwani ICC inaweza kuchukua hatua yoyote (coercive) dhidi
yetu?
Tumechoka sasa, hawahawa walisema tulipe hela za IPTL, wanajua kabisa deni halijaisha na umeme hatupati na sasa wanasema tulipe za Dowans wanatuona sisi mafala sana tukikubali kampuni nyingine itenda kudai wameshaona tanzania ni shamba la bibi

umetoa wazo zuri lakini wizara ya sheria Wya pesa na hazina wanawaza kama umma wa TZ hapo ndipo penye tatizo ndio hasa inapo takiwa mkutano wa katiba ili muajiri awe na haki bayana ya kumwajibisha/kuwajibika kwa kiongozi mzembeaji la sivyo tunatwanga maji kwa huu utaratibu/katiba Ulivyo usivyo kidhi haja hiyo mwanangu iishi TANGANYIKA WAISHI WATANGANYIKA
 
Chadema na wapenzi wa Chadema ndio walishikilia bango hili la kuwakataa Dowans. Wakati ni wazi Dowans ndio wali save the whole situation, wakaleta mitambo mipya, mkaanza kulumbana na mwisho wakatoa offer ya kuwauzia kama hamtaki kuikodi na still mkaleta tafarani. Sasa, msiilaumu serikali wala watendaji wake. Dr. Rashid alikuwa tayari kuinunuwa, wapingaji wakubwa walikuwa nani? Na Zitto aliposhauri inunuliwe, nyie wapenzi wa Chadema mkamshutumu na kusema kisha nunuliwa. Leo mnataka kumlaumu nani?

Mimi, binafsi yangu, nililiona hili na nikabishana sana na watu kwenye hiki kijiwe, hakuna alietaka kuelewa, nangoja nipate wasaa, nizitafute zile posts nizikandamize hapa. Tutawaona wanafik wanao ishutumu serikali sasa hivi, nna uhakika wao ndio walikuwa wa kwanza kupinga isinunuliwe, ooh, Dowans mafisadi, sasa waambieni na hiyo mahakama iliyotowa maamuzi kuwa ni mafisadi. Pambaaf
 
SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limeamriwa kulipa fidia ya Sh106 bilioni kwa kampuni ya ufuaji umeme ya Dowans Tanzania Limited baada ya kuvunja mkataba.Uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), Novemba 15, mwaka huu chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali, Jonathan Parker uliamuru Tanesco iilipe Dowans kiasi hicho cha fidia.

"Jopo la wasuluhishi limeamuru zaidi ya Sh36bilioni (dola za Marekani 24,168,343) na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya Sh 26bilioni (dola za Marekani 19,995,626) tangu Juni 15, 2010 hadi fidia hiyo itakapolipwa,' imeeleza sehemu ya uamuzi huo.

Pia jopo hilo la wasuluhishi wa migogoro ya kibiashara liliamuru Sh60bilioni (sawa na dola za kimarekani 39,935,765) na riba ya kiasi cha asilimia 7.5 ambayo ni sawa na Sh 55bilioni (dola za Marekani 36,705,013.94) zilipwe kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.

Jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi na za utawala Sh1bilioni (dola za Marekani 750,000) kwa wasuluhishi wa ICC zinatakiwa zilipwe na pande zote husika.

"Tanesco wanatakiwa kumlipa mdai (mlalamikaji) Sh3bilioni (dola 1,708, 521) ikiwa ni gharama za uendeshaji wa kesi na gharama zingine na kwamba madai mengine yaliyotolewa na pande zote katika kesi hiyo yanatupwa.

Mpango wa kuuza mitambo hiyo uliwahi kuibua mjadala mzito nchini huku baadhi ya wabunge akiwemo mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe wakikubaliana na dhamira hiyo jambo lililosababisha serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kutangaza rasmi kuwa haina mpango wa kununua mitambo hiyo.

Kufuatia uamuzi huo Dowans iliamua kutangaza kuiuza mitambo yao nje ya nchi jambo lilosababisha serikali kuiwekea pingamizi katika Mahakama ya Biashara ikitaka wamalize kwanza masuala ya mikataba.

Siku chache baadaye Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), iliikamata mitambo hiyo kwa madai kuwa ilikuwa ikidaiwa ushuru.

Hatua ya kuiwekea pingamizi ili mitambo hiyo isiuzwe ilipigwa vikali na Dowans na kuamua kukimbilia katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court) iliyopo nchini Ufaransa ili kuhakikisha mitambo hiyo inaweza kuuzwa.

Lakini taarifa iliyotolewa na Dowans jana ilionyesha kuwa mgogoro huo umepatiwa ufumbuzi na kwamba kampuni hiyo na Tanesco sasa wamekubaliana baada ya mahakama hiyo kuketi.

"Jopo la waamuzi uliojumuisha waamuzi watatu chini ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), limetoa tunzo kuhusu mgogoro baina ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Limited (kwa pamoja ‘Dowans'), kwa upande mmoja dhidi ya Tanesco kwa upande mwingine.

"Dowans wameridhika na tunzo iliyotolewa na jopo hilo na kwa matokeo hayo wanayo furaha kuutangazia umma kuwa mgogoro baina yetu na Tanesco sasa umekwisha,"alisema sehemu ya taarifa hiyo.

Akizungumzia uamuzi wa kumaliza mgogoro huo baina ya Tanesco na Dowans, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja alisema hajapata taarifa hiyo rasmi wala maamuzi yaliofikia katika mahakama hiyo.

"Kwa sasa nipo nje ya ofisi kama ni kweli Mahakama hiyo imeweza kuwasuluhisha ni lazima nitaletewa taarifa na kuweza kusoma rasmi ili kujua iwapo katika makubaliano hayo suala la kuuza mitambo hiyo nalo wamekubaliana nalo au la ndio nitaweza kuzungumza chochote,"alisisitiza Waziri Ngeleja.

Waziri Ngeleja alisema kuwa anachojua yeye pingamizi la serikali lipo mahakamani na kwamba hakuna mabadiliko yoyote.

Kwa upande wa Tanesco, Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alipoulizwa alisema kwa sasa Tanesco hawezi kusema chochote watatoa taarifa mara baada ya uongozi wa Tanesco kukutana.

Mara ya kwanza dhamira hiyo ya serikali kupitia Tanesco kutaka kununua mitambo ya Dowans, iliibua mjadala mkali miongoni mwa Watanzania, huku wakionyesha shaka kuhusu uamuzi huo.

Mjadala huo ulitokana na malumbano ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini inayoongozwa na Shellukindo na ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma, iliyokuwa chini ya Zitto (Chadema). Kati Kamati ya Shellukindo ikisisitiza kutokuwepo umuhimu kwa Tanesco kununua mitambo hiyo.

Mvutano wa kamati hizo ulikuwa mkubwa, baada ya Zitto kusisitiza kuwa atamuomba Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuitisha mkutano wa kamati hizo mbili ili kujadili upya suala hilo na kwamba utetezi wake wa kununua mitambo hiyo unatokana na kuweka mbele maslahi ya taifa.

Wakati huo, Watanzania wengi ambao walikuwa wakitoa maoni yao kwa gazeti hili kwa njia ya simu za mkononi na katika mitandao ya ‘internet', walionyesha kupingana katika suala hilo, jambo linaloonyesha kuwapo kwa mgawanyiko wa wazi kuhusu kununuliwa au kutonunuliwa kwa mitambo hiyo.

Kutokana na mjadala huo uliochukua mwelekeo wa kupinga ununuzi wa mitambo hiyo, hatimaye Tanesco ilitangaza kuondoa nia yake hiyo kwa kile ilichoeleza kuwa mjadala wake umechukua sura ya kisiasa kuliko kuzingatia utaalamu.

Shirika hilo lilichukua uamuzi huo siku chache baada ya Spika Sitta, kutoa mwongozo na ushauri wa kupinga nia hiyo ya Tanesco iliyopigiwa chapuo na serikali ambapo msimamo wa Tanesco ulitangazwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wake, Dk Idris Rashid, katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema wameamua kuondoa nia hiyo kwa kuwa mwelekeo wa ununuzi wa mitambo ya Dowans, unalipeleka shirika hilo kwenye ugomvi wa wanasiasa, jukwaa ambalo alidai hawana mamlaka nalo.

Alisema Tanesco itaandika barua serikalini kwa Waziri wa Nishati na Madini, kumfahamisha kuhusu maamuzi hayo, ambayo yalionyesha dhahiri kuchukuliwa kwa shingo upande.

Akifafanua zaidi kuhusu mahitaji halisi ya umeme nchini na mazingira yaliyoifanya Tanesco kutaka kununua mitambo ya Dowans ili izalishe umeme wa dharura, alisema shirika hilo liliwasilisha tathmini ya hali halisi ya uzalishaji wa umeme nchini kwa wakati huo na matarajio ya uzalishaji wa umeme kwa muda wa kati na mrefu na pia mahitaji.

Alisema, Tanesco iliwasilisha taarifa kwamba hali ya ukuaji uchumi inafanya mahitaji ya umeme yaongezeke kwa megawati 75 kila mwaka na kwamba kulingana na tathmini hiyo, hivi sasa nakisi ya mahitaji ikilinganishwa na uzalishaji ni megawati 150.

Mkurugenzi huyo alibainisha ifikapo mwezi Desemba, nakisi hiyo itakuwa ni megawati 225 kwa uchache, ikiwa hapatakuwa na ongezeko lolote la uzalishaji wa umeme.

Alisisitiza pia kuwa shirika lake ilizingatia kuwa, ongezeko la uzalishaji uliotarajiwa kutoka vyanzo vya Kiwira na Tegeta, lisingesaidia kwani vyanzo hivyo visingeingia kwenye mtandao kwa muda uliokuwa umepangwa, kwa sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wa Tanesco.

Dowans ilirithishwa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura mwaka 2006 baada ya kampuni iliyoshinda zabuni hiyo, Richmond Development Company LLC kushindwa kuleta mitambo hiyo na baadaye kukumbwa na kashfa ya ushindi wa zabuni hiyo uliosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wake na baadaye kufuatiwa na mawaziri wawili, Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi.

Jenereta hizo za kufufua umeme ambazo zinatumia gesi asilia zilitangazwa kuuzwa nje ya nchi kwa zaidi ya Sh101 bilioni ingawa bishara hiyo ilishindwa kufanyika baada ya serikali kuiwekea pingamizi mahakamani kampuni hiyo isiuze mitambo hiyo.
 
... hawako peke yao. Leo natumia lugha mbaya kidogo, that:
1: Watanzania wengi ni SPINELESS COWARDS!
2: Watanzania wengi, hususan wapenzi wa chama flani ni watu WAPUMBAVU kupindukia na hapa natoa mfano: Changanya waumini wa MLINGOTINI, wehu kama kina Sophia mpayukaji, kina Yusuphu Kambanyingi na wengine wengi tu wenye madaraka ukichanganya na wale wanaowaweka watu kama watu hawa madarakani
3: Watanzania wengi wana akili za zamadamu! Ni adui wa maendeleo. Kazi kubwa ni kupiga domo tu kuendeleza imani za kishirikina. Mauaji ya ALBINO na imani za hayo mambo toka vijijini maporini hadi mijini zipo. Angalia kwenye soka...mambo ya Msimbazi na Jangwani.... wametoa kafara ngapi za albino pale.??... huu upuuzi unaaaminika na Watanzania wengi tu...kwamba UCHAWI una miujiza hiyo ya kuleta solutions. UJINGA mtupu!
4: Kwa hiyo hata hao VIONGOZI ni product, offspin ya upuuzi iliokithiri kwa wingi tu Tanzania. A very dark country!! Uswahilini.

How long it takes to achieve real progress is directly proportional to shedding off COWARDNESS and I dare say, USWAHILI.
Apologies to whomsoever gets insulted.

Mmmh.........., you must be angry.
 
huuuuuuuuuuuwiiiiiiiiiiiii, yametimia ya RA kutuumiza kwa njia nyingine, kweli fisadi ana mbinu nyingi ingawaje Mheshiwa mteule Speake hajui maana ya fisadi labda tutafute jina mbadala huyu fisadi Papa kweli katuumiza kama ni ubaguzi sasa naanzia kwa huyu Bagacholi RA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom