DOWANS yaibwaga TANESCO; TZ kulipa gharama na adhabu Bil. 185!

Mafisadi wa tz watuambie kama hakuna hela za kutoa elimu na afya bure kwa walalahoi, hizo hela za kumlipa fisadi zitatoka wapi? Maana kwa hakika mafisadi wamejishisha hii kesi ili walipane.

Ndiyo matokeo ya kutukuza sana politics kuliko technical know how.

Hamna kulia lia hapa inabidi tulipe tu kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi, ni utelekelezaji wa ilani zetu. Chama on top of everything.
 
You can take a donkey to a stream of water but you can't force it to drink. Kama mshitakiwa hakuwa tayari kuandaa utetezi wa nguvu dhidi ya mashitaka juu yake ni wazi kuwa dua na sala zake anaombea kushindwa. Kwani kushindwa huko ndiyo manufaa kwake, more to come kesi zote za kifisadi kuanzia EPA mpaka matumizi mabaya ya madaraka zinalalia mkondo huu huu.

"Kwa kuwa tumeshindwa kufanya maamuzi sasa nchi ikiingia gizani hapo baadae tusilaumiane" - Dr Iddris Rashind Former CEO of TANESCO.

Kwa trend hiyo hiyo ya kutaka kuonesha kuwa tungefuata wanayotaka wao tungekuwa salama ndiyo maana wakafanya maamuzi yanayotufanya leo kujutia kuzuiwa mitambo hiyo. "defeated on arrival to the court"
 
Maana yake mgawo zaidi na bei ya umeme kupanda -kikwete anatupeleka kuzimu -anataka uongozi kwa mabavu wakati hana uwezo wa kuongoza
 
Maana yake mgawo zaidi na bei ya umeme kupanda -kikwete anatupeleka kuzimu -anataka uongozi kwa mabavu wakati hana uwezo wa kuongoza

Jamani hivi kwa nini hamkubali kwamba Uongozi haujaribiwi?
 
Tulichoambiwa ni kwamba tusiponunua mityambo ya Dowans nchi itaingia Kizani - Haikuingia kizani hivyo tusijaribu kutumia utetezi wa Rashid Othman na Zitto.

Tulijua wazi kwamba Tanesco wakitakiwa kulingana na utawala uliopo watashindwa kama vile tunavyojua fika kwamba Uchaguzi huu hakuwa halali na hata kaa Chadema wapewe nafasi ya kwend mahakamani Hawatashinda.

Nini matokeo ya hukumu hii? Hakika bado mko nyuma sana kuelewa mipango ya mafisadi kwani kinatakiwa hasa ni kubinafsishwa kwa shirika hilo na hii ni moja ya hatua za mwanzo kulibana shirika, mwisho wa siku kama uharo itabidi tuachie mapema na salama. Mafisadi wako kazini na safari hii haponi mtu...

Ikiwa swala zima la Richmond limekataliwa kujadiliwa bungeni iweje leo la Dowans lifikishwe mahakamani pasipo kuibua chanzo cha contract hiyo kutoka Richmond wakati ikijulikana wazi kwamba Dowans ndio hao hao Richmond..
 
Naona kuna watu wengi tu mlikuwa hamuujui/hamuuelewi huu MDUARA.................hiyo ilishakula kwetu tokea awali.............ndio maana watu kama akina Dr Idriss et al walitakiwa wawe keko................
 
Mimi nasoma mikono inatetemeka acha nilale kidogo nipate nguvu. Hii kali
 
International Chamber of Commerce, imetoa hukumu yake katika kesi iliyoletwa na Dowans (T) Ltd kupinga uamuzi wa Tanesco kuzuia mitambo ya Dowans.. Hukumu hiyo inaonesha kuwa Tanesco imebwagwa vibaya na kutakiwa kulipa mabilioni ya shilingi kama adhabu pamoja na gharama ya kesi kwa Dowans..

More info to come..

Cha mlevi huliwa na mgema;
Wajinga ndio waliwao;
La kuvunda halina ubani;
Mkataa pema, pabaya panamwita;
Mtoto akilia wembe mpe;
Asiyesikia la mama hufunzwa na ulimwengu;
Nyani ni nyani tu, (siyo ngabu lakini) hageuki kuwa binadamu hata siku moja

Kwa methali hizo sina maana ya kumtukana mtu yeyote bali ninaonyesha kuwa pamoja na mafunzo mengi tuliyoachiwa na mababu zetu, bado watu wetu wana ujinga mwingi sana kiasi cha kutufanya tuwe tunanunua kitumbua kimoja kwa bei ya kununulia Boeing dreamliner 787 kadhaa, ambazo hatuna hata nusu yake. Hata pale ambapo tunaonyeshwa kuwa huo ni wembe utatutakata, bado tumeulilia kucheza nao tena kwa miaka mingine mitano
ijayo ambapo watakuwa hawana haja ya kutuogopa kwa lolote tena.
 
Kana kweli DOWANS inamilikiwa na Rostam Aziz huyo mfadhili mkubwa wa CCM iliyoko madarakani, hakuna kesi iliyoongelewa hapa!!
Hii ni EPA mpya, walitumia sheria fake kurudisha hela zao!!
 
Hawa hawa wanaoponda ndio hawa hawa walikuwa wanashadidia hiyo mitambo isinunuliwe na Tanesco. Hamna nguvu za kufikiri.
 
ndo wakome sasa.maana wanafanya kazi kwa jazba na chuki sasa ndo watajifunza...nchi haina uongozi rais yuko bize kupokea waednesha baiskeli tu hana la maana analowaza stratergically na hayo ndo madhara yake sasa
 
Hili ni jambo ambalo nililiona kabla, rejea post zangu za zamani. Nilijuwa watashinda kwani Dowans hawana kosa walilofanya.

Makosa ni wehu waliokuwa wanashabikia mitambo ile isinunuliwe na serikali Dowans walipotowa offer. Hata Mh. Zitto Kabwe alipigania sana mitambo hii inunuliwe ili kuepusha kesi, gharama na mgao wa umeme.

Leo kikowapi? Mashine tumezikosa, umeme tumekosa, gharama tutazilipia kwa upuuzi wa watu wachache ambao huwa wanajisemea tu bila kuwa na mantiki.

Sasa ndio mtajuwa kuwa Dr. Rashid ni kichwa.

Samahani. Kwani kosa la TANESCO ni kukataa kununua mitambo au vipi? Yaani nikitaka kukuuzia suruwali ukakataa, naweza kukupeleka mahakamani nikashinda? Dr. Rashid anaweza kuwa kichwa lakini ni mwizi/mlafi vile vile. Aende tu akafurahie mgawo wake wa Radar toka kwa Mzee wa Vijisenti.
 
Hapa naona ni mchezo unaochezwa watu wanajilipa hela wao wenyewe yaani kwa kifupi dili limezaa dili jingine ni kama kumkata ng'ombe nyama huku unamkamua maziwa!!
 
Zitto haters chali kwenye swala la Dowans,!!!!

kuna tofauti ya wanaume na watoto wa kiume, mitambo tumekosa, gharama tunalipa zaidi ya zile ambazo tungenunulia, umeme tulikosa!!
 
Zitto haters chali kwenye swala la Dowans,!!!!

kuna tofauti ya wanaume na watoto wa kiume, mitambo tumekosa, gharama tunalipa zaidi ya zile ambazo tungenunulia, umeme tulikosa!!

Mahaba yako kwa zitto yasikupofushe. Unasherekea nini sasa? yani ulitaka sheria ya manunuzi ipindishwe ili kumfurahisha zito na wewe!! hebu wakati mwingine utumie akili zako kidogo unapomtaja zito, manake kwa kuwa mmeamua kumfanya zito mungu wenu mnataka na wengine nao wamsujudie kama ninyi. Hapa hakuna cha zito wala idrisa rashid,huu ni mpango kabambe ulikuwa unatengenezwa ili wajanja wachache watimize malengo yao na wakamtumia zito ili wale mlio na mahaba nae mje kupiga makofi hapa kwamba zito kasema zito kaongea, ni upuuzi tu huu.

Kwa taarifa yako kuna watoto wa kiume wana akili na uwezo kuliko wanaume, kuna wanaume wengine suruali tu, kwahiyo wacha kupiga mayowe na zito wako huyo.
 
dawa hapa ni kufanya kama mwalimu nyerere kutolipa, kwani watatufanya nini? Ndio tutajifunza kujitegemea na kuachana na kuwa omba omba
 
Inasikitisha sana kwamba walipakodi tunatakiwa tuwalipe Dowans (manyang'au) zaidi ya bilioni 180, kampuni ambayo haijawahi kufanya lolote haijawahi kuzalisha hata unit moja ya umeme Tanzania, safari hii hapana wamezidi kutufanya wendawazimu kama serekali italipa ikatafute sehemu nyingine ya kutoa hizo hela ila sio kwa kodi yetu, HAPANA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom